In Edward Lowassa, I trust...

In Edward Lowassa, I trust...

Mimi nilimuona kuwa anafaa ni pale alipoelezwa kosa akaachia ngazi maramoja,
Nilimuheshimu sana nakumuona kuwa ni kiongozi baada ya kugundua kuwa kosa limefanyika japo sio yeye ila yeye ndio mkuu,
Tumezoea kuona vitu kama hivyo wakifanywa na wazungu tu! ila yeye anafahamu uongozi nini kwanini hawa wengine hawajiuzulu?
Kwani hawafanyi makosa?
unajua gharama za kujiuzulu?
Kama ilivyomuuma makosa yalipo fanyika nchini mpaka akaamua yeye mwenyewe bila kushinikizwa na wananchi kwamba ajiuzulu ndivyo itakavyokuwa vigumu kufanya kosa tena ili ajiuzulu tena utake usitake................
Kiongozi ni razima awe mwoga na inabidi aumie pindi kosa linapofanywa na watu wake,
Mwingine kama kweli ana roho ya uongozi likifanyika kosa au hasara wengine wanajiua.
Lakini unakuta kiongozi anafanya kosa au linafanyika kosa chini yake ata hachanganyikiwi

REV...... nakuunga mkono upo sahihi kwa mtu ambaye awezi kuwazua hatokaa akaelewa.
 
Mh kama unampenda "Kampikie Chai"hii ndio Tanzania bana Mijizi inaabudiwa,na inajifanya michapa kazi kweli kweli,Uchapakazi wa kutuibia hauna tija na unakuwa kisingizio mbele ya watu kuonekana ''watu wema kumbe si watu"pole bw mdogo TP
 
Knowing Rev. Kishoka very well I make the following observation::

Rev. Is trying to invoke debate so we can discuss who is capable of leading TZ.

He picked EL knowing very well this will make the most bang and will force people to really question the crisis in leadership we are facing in Dar and what needs to be done in 2010 and 2015.

Binafsi, nasema EL is a no no lakini swala je huyu Jk naye vipi?? Nani mwingine ambaye anaweza kutuongoza watanzania tukatoka kwenye hili giza nene la umaskini, magonjwa na matatizo lukuki???[/QUOTE]

Yale yale....kuzungumzia watu badala ya sifa...hata Idd Amini alikuwa mtendaji, lakini kwa faida gani? Acheni kutaja majina, semeni sifa za viongozi. Endapo mtu atatokea kuomba kama Shibuda alivyodhamiria, then tuanze kumjadili kwa vigezo tunavyoamini vinatahili. Lowasa is Gone , just bury the bug!
 
alitumia nguvu na madaraka ovyo kuliko busara..alishindwa hata kujitetea bungeni na kubaki kununa tu wacha ile kwake.
 
Duh!!! Bado siamini. Haya ni yakuzungumzia chumbani kwako, sio kwa watu wanaomjua Lowasa.

Ni mchapakazi, mfuatiliaji na mkali asiye na masikhara na walioko chini yake si kuwa wanamheshimu tuu, wanaogopa kushukiwa na zali kutokana na ukali na ufuatiliaji wake.

Kwa usanii

Kila kazi aliyopewa, kaifanya kwa bidii na kwa ufanisi. Kuna tofauti kubwa sana za kiutendaji kati yake na wenzake walioshika nafasi za uongozi ambazo alizishikilia.
Kazi ipi alipewa na ikafanyika bila hila

Naamini kwa dhati kuwa ili Tanzania iweze kuamka na kurudi katika mstari ulionyooka wa kujituma, kufanya kazi kwa bidii na maarifa bora na la zaidi kwa nidhamu ili tuendelee vyema na safari yetu ya kujijenga kiuchumi na kijamii ili kuleta maendeleo ya kweli, basi hakuna mwingine zaidi ya Lowassa!
This is a joke!!!!! Think twice, out of 40m Tanzania there are many for sure.
 
Rev. unaturudisha nyuma mkubwa, with all much respect i have for you...but i will need to differ with you on this...EL yes he is strict and commited to his work but lack integrity because of his greedy....do u know how f***k rich he is????? and it is not bout his wealth but the ways he got it....ni bora huyu mkerewe aendelee kuuza sura tu kuliko kumrudisha EL
 
Mh kama unampenda "Kampikie Chai"hii ndio Tanzania bana Mijizi inaabudiwa,na inajifanya michapa kazi kweli kweli,Uchapakazi wa kutuibia hauna tija na unakuwa kisingizio mbele ya watu kuonekana ''watu wema kumbe si watu"pole bw mdogo TP

Jamani sasa nani atafaa?
lakini Rev kasema huyo na mimi namuunga mkono ,sasa let say tumemkataa sasa yupi atafaa?
 
John Pombe Magufuli anaweza kutuweka sawa... Hana makashafa kila leo kama huyo ambaye ni muasisi wa falsafa ya UFISADI KUPITIA UONGOZI.

Appetite ya kujilimbikizia mali ya muasisi wa UFISADI KUPITIA UONGOZI ni insatiable. Jamaa hata leo hii apewe migodi yote ya dhahabu iwe anaimilkika na familia yake. Ikitokea kuna kuibinafsisha Tanesco, atafanya hila aimiliki yeye, akijua kuna account ingine design ya EPA pale BoT, atachora mpaka waichote... Jamaa imefikia mahali ni kama ana ugonjwa wa akili when it comes to opportunity ya ufisadi inapomtokea.

Ukitazama estates zake Dar es Salaam na Arusha, Ranchi kubwa za taifa za NARCO alizokomba wakati yupo maji na mifugo, investment ya Vodacom, investment ya Safaricom Kenya, Ardhi ya General Tyre Arusha anayoizungukia kila kukicha(na hapo ana ardhi nyingi tu), no wonder kile kiwanda kinakufa sababu watu wanataka wagawane properties. Yani the list is endless...Na miaka yote hiyo tangu ujana wake ni mtumishi wa umma.

Mwenyewe kama kweli ni mcha mungu kama anavyopenda kujiportray, basi nafsi yake itakua inamsuta kama bado anataka uongozi wa nchi hii ya watu masikini wa hali na akili.
 
I concur Pastor. That guy was keeping us on our toes. And we were also keeping him in his toes. This dialectical relationship between 'us' and 'him' would have propelled our development much further. Uchumi wetu ungeendelea kupaa badala ya kutua. I say better fight the devil you know - Bring him back on board!

"Tupo Tumejaa Tele" - Edward Lowassa, the then PM

Huo uchumi WETU unaosema utapaa ni wa nani na nani?wewe na yeye ama? Maana kama ni wetu alikuwepo na haikupaa ... sana sana aliupeperusha tu,hebu kuweni serious you people!!
 
'Sitaki Longolongo!'

'Udini Mwiko'

'Najali Muungano'

'Siogopi Kuwajibishwa'

'Navutia wawekezaji'

'Nina ushawishi'

'Naona mbali'

'Nachapa kazi'

'Najali wananchi'

'Nasaidia maskini'

'Sitaki mchezo'

'Nazingatia elimu'

'Nahamasisha maendeleo'

'Natumia mamlaka'

'Ndio nitawaongoza'

'Nitakuwa Rais'

'Sitacheka cheka'

'Nitailinda Katiba'

'Nitaleta mvua'

'Nitaondoa njaa'

'Mgao utaisha'

'Nitapaisha uchumi'

'Nitawasikiliza wananchi'

Kampain hizi, jamaa anajipanga taratibu
 
John Pombe Magufuli anaweza kutuweka sawa... Hana makashafa kila leo kama huyo ambaye ni muasisi wa falsafa ya UFISADI KUPITIA UONGOZI.

Appetite ya kujilimbikizia mali ya muasisi wa UFISADI KUPITIA UONGOZI ni insatiable. Jamaa hata leo hii apewe migodi yote ya dhahabu iwe anaimilkika na familia yake. Ikitokea kuna kuibinafsisha Tanesco, atafanya hila aimiliki yeye, akijua kuna account ingine design ya EPA pale BoT, atachora mpaka waichote... Jamaa imefikia mahali ni kama ana ugonjwa wa akili when it comes to opportunity ya ufisadi inapomtokea.

Ukitazama estates zake Dar es Salaam na Arusha, Ranchi kubwa za taifa za NARCO alizokomba wakati yupo maji na mifugo, investment ya Vodacom, investment ya Safaricom Kenya, Ardhi ya General Tyre Arusha anayoizungukia kila kukicha(na hapo ana ardhi nyingi tu), no wonder kile kiwanda kinakufa sababu watu wanataka wagawane properties. Yani the list is endless...Na miaka yote hiyo tangu ujana wake ni mtumishi wa umma.

Mwenyewe kama kweli ni mcha mungu kama anavyopenda kujiportray, basi nafsi yake itakua inamsuta kama bado anataka uongozi wa nchi hii ya watu masikini wa hali na akili.

Yeye kuwa na mali ambazo kazinunua ni kosa lake binafsi? Je ni wapi imeandikwa katika Sheria za Tanzania na kanuni za maadili kuwa ni mwiko kwa kiongozi kuwa na mali?

Kwani mali alizonazo si zimeandikishwa kule tume ya maadili na Serikali inajua? kama sivyo basi ni jukumu la nani kumweka kitanzi imhoji jinsi alivyojipatia mali?
 
Kuwa na mali si dhambi bali dhambi ni kuwa na mali iliyopatikana ktk njia ambazo si halali, bahati mbaya ni kwamba kwa sasa uongozi na mali vinaenda kwa pamoja na huko ndio kuna viashiria vya rushwa...
 
Rev. Ningekushauri uyahusianishe mabaya na mazuri yake ndo ujaribu kupiga campaign! Inawezakana huyajui mabaya yake yote aliyoyafanya! Fanya comparative analysis iyo halafu urudi utueleze!
 
Rev. Ningekushauri uyahusianishe mabaya na mazuri yake ndo ujaribu kupiga campaign! Inawezakana huyajui mabaya yake yote aliyoyafanya! Fanya comparative analysis iyo halafu urudi utueleze!

Mairo,

Ulishawahi kusoma Deconstructing Lowassa?
 
Yes, I have said it. Ili tuendelee, tunamhitaji Edward Ngoyayi Lowassa!

Kama unaye wa kwako, tupe jina na umnadi, wangu miye ni Lowassa!

Kama una maana arudi kama PM naona unamrudisha mwenzio nyuma? Nielewavyo mimi, yeye ana aspire kuwa President, kashafa zote notwithstanding. Habari za kuaminika ni kuwa wapambe wake wanamsukuma kuongombea 2010, lakini target hasa ni 2015.

Jee Rev. unapima joto la 2010 au vipi. Kama ni hivyo, bado ni mapema mno. Unajua katika siasa si lazima yote yanayosemwa juu yako yawe ni ya kweli. Kinachogomba ni perception ya watu kuhusu wewe kwa wakati huo. Kwa hali ya sasa bado ki chama EL anaupinzani mkubwa katika chama na wapigakura bado mawazo yao yamo katika shutuma za ufisadi wake. Hapa sina maana kuwa shutuma hizo ni za kweli au hapana kwani mimi mwenyewe naamini kuwa Kamati ya Mwakyembe haikumtendea haki kwa kutompa nafasi ya kujitetea.

Ni vizuri angengoja 2015. Hapo CCM itakuwa imesahau shutma zilizopo juu yake. Njia hii ndiyo aliyotumia mwenzie Malecela wakati alipobomolewa na Mwalimu mwaka 1995 na haikuibuka tena mpaka 2005.
 
TK,

Kwa nini Lowassa asubiri mpaka 2015? kwa minajili gani? yani asubiri tuendelee kudorora kwa miaka mingine mitano? Iwe Lowassa, Mwandosya au Shibuda, kwa nini waendelee kusema tumpe Kikwete Mji upya?

Same thing kwenye majimbo ya Wabunge, kwa nini tuendelee kuongeza mkataba na watu ambao wameshindwa kutuletea maendeleo, kutuongoza na kututumikia?

Kwa nini tumpe Sitta au Mzindakaya nafasi ingine huku wao wamekuwa viongozi na wawakilishi wa majimbo takribani miaka 30+?
 
Rev.

Hiyo nimetoa kama stratergy ya ku achieve lengo hilo hilo ulilonalo. Madhara ya kutongoja ni kuwa, kama akijitosa sasa wakati public opinion juu yake si nzuri na akashindwa basi ajue kuwa atakuwa amepoteza nafasi hiyo for good. Kuepusha hilo, ni vema akajiwekea mkakati wa muda in order to cover enough ground kwa Chama na pia wapiga kura.

Unajua hizo kwa nini nyingi nyingi ulizoziltoa ni lazima tukubali ukweli kuwa wanaochagua viongozi sio mimi na wewe au watu ambao wana think staight. Kuna clique ambayo tukubali tusikubali ndio king makers na baadaye wapigakura ambao nao pia huwa influenced na clique hiyo hiyo.

Sasa kama kweli EL anafaa basi naye atafute njia ya aidha kuungana na clique hiyo,(kama alivyofanya rafiki yake JK) au atafute clique mbadala.
 
Nakuunga mkono Rev. Kuna tangible results za juhudi za Lowasa nyingi sana, sijaona matokeo ya juhudi binafsi za Kikwete hata moja.

Ni kweli hili tuendelee tunaitaji mtu kama Lowasa ili tuwe na upungungufu wa umeme kama ilivyo sasa, thanks to Richmond! Kusema "kweli" kama alivyosema Rev. Kishoka hakuna mwingine kama Lowassa. Nani anabisha?

Shakespear alisema mazuri aliyofanya mtu akifa huzikwa pamoja nae, mabaya aliyofanya hudumu kwa muda mrefu baada ya kifo chake!!
 
Rev.

Hiyo nimetoa kama stratergy ya ku achieve lengo hilo hilo ulilonalo. Madhara ya kutongoja ni kuwa, kama akijitosa sasa wakati public opinion juu yake si nzuri na akashindwa basi ajue kuwa atakuwa amepoteza nafasi hiyo for good. Kuepusha hilo, ni vema akajiwekea mkakati wa muda in order to cover enough ground kwa Chama na pia wapiga kura.

Unajua hizo kwa nini nyingi nyingi ulizoziltoa ni lazima tukubali ukweli kuwa wanaochagua viongozi sio mimi na wewe au watu ambao wana think staight. Kuna clique ambayo tukubali tusikubali ndio king makers na baadaye wapigakura ambao nao pia huwa influenced na clique hiyo hiyo.

Sasa kama kweli EL anafaa basi naye atafute njia ya aidha kuungana na clique hiyo,(kama alivyofanya rafiki yake JK) au atafute clique mbadala.

TK,

Tuondoe mazoea na mizenge iliyomo CC na NEC, je majina haya manne yakifikishwa kwenye mkutanoo mkuu wa CCM kumteua/kumchagua mgombea wa CCM ni nani atashinda?

Majina haya ni Kikwete, Lowassa, Mwakyembe na Dr. Bilali!
 
Back
Top Bottom