In Edward Lowassa, I trust...

In Edward Lowassa, I trust...

Kweli kabisa Mkuu. Tanzania tunakuwa maskini kwa sababu ya Rushwa. Lowasa mla rushwa hafai hata kuwa mtendaji wa kijiji

Hee! kwa hiyo rais kikwete 2010 alikwenda Monduli kumpigia kampeni mla rushwa awe mbunge? maskini nchi yangu
 
Ni halali na dhahiri kabisa km tutataja mwaka 2014 kama vipindi vigumu zaidi ktk historia ya nchi hii kuwahi kutokea. Kipindi kinachoshuhudia kuwepo kwa maamuzi mazito na yenye kuweza kubadili maisha ya wananchi wa taifa hili na hali nzima ya kisiasa na kiuchumi. Suala la kwanza ni Mchakato wa katiba mpya, chombo kinachoonesha muundo wa serikali na mwongozo mzima wa mfumo wa utawala wa nchi.

Suala la pili na lenye mashiko zaidi ni harakati za kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao 2015. Na hapa macho ya wengi ni katika kiti muhimu kabisa cha Urais. Uchaguzi huo ndio utakaodhihirisha 'commitment' yetu ya kutaka mabadiliko na maendeleo ya kweli ya taifa hili lenye miaka 50 tangu kupata uhuru wake lkn bado laitwa changa. Ndio uchaguzi utakaoonesha ukomavu wetu wa kutoka mabegani kwenda juu na sio chini. Utaonesha uimara wetu ktk kuamua kilicho sahihi kwa wakati huu kwa nchi yetu.

Tumesikia wengi kujinadi kwa kila mmoja kwa namna yake-wengine wazi na wengine kwa kificho-lakini hapa tujadili machache kuhusu aina/sifa za yule tumtakaye;

1. Uimara, hapa sizungumzii ukubwa wa misuli ktk kunyanyua vyuma au uwezo wa kutimua umbali wa maili nyingi, la hasha, hapa nazungumzia uimara wa kuchukua maamuzi, maamuzi magumu na yenye tija kwa nchi na yanayozingatia hali halisi ya nchi kwa sasa.

2. Mtendaji zaidi kuliko mnenaji, hapa ni uwezo wa yeye kuweza kutekeleza yale aliyoahidi na anayoamua. Hapa tuangazie zaidi ufanisi ktk nyadhifa walizowahi kuzishika.

3. Nguvu ya ushawishi, utawala na uongozi-hakika ni muhimu kiongozi kuwa na uwezo wa kiutawala ndipo uweze kuongoza kundi husika. Nguvu ya utawala itatokana na ushawishi wake ktk jamii na sio vinginevyo.

Kwa kuzingatia hayo yaliyoorodheshwa hapo juu naomba nioneshe inspiration yangu kwa Mbunge wa Monduli Mh. Edward Ngoyai Lowassa. Amekidhi vigezo vinavyotizamwa na kundi la walio wengi.

Itaendelea....
 
Ni ukweli usiopingika kuwa Waziri msataafu E.Lowassa anafaa kuwa Rais ajaye wa Tanzania. Kiongozi huyu ni jasiri katika kufuatilia utekelezaji wa masuala mbalimbali mfano ujenzi wa shule za kata, upatikanaji wa maji kutoka ziwa victoria, kuzuia uuzaji wa eneo la mnazi mmoja na kuwawajibisha viongozi wazembe. Ni aina ya kiongozi ambaye Tanzania inamhitaji kwa siku zijazo. Ili kutengeneza njia ya kuelekea huko ni vizuri ayaweke wazi masuala yafuatayo:-
1. Richmond/Dowans/Symbion ni ya nani hasa (ni yake, ya serikali au ya nani?)
2. Nini chanzo cha mali zake kwani kumekuwa na uvumi mwingi (Je kuna anayelalamika kuwa alimuibia?)
3. Akiwa Rais atakuwa na kulipiza kisasi kwa mahasimu wake au la (awatoe hofu wote).
4. Alkiwa Rais ataunda serikali ya mseto au la (Liwe wazi kama sehemu ya kampeni)
5. Nini vipaumbele vyake atakapokuwa Rais wa Tanzania.
Haya na mengine mengi ni muhimu sana kuwekwa wazi na kiongozi wetu wa nchi ajaye na atakayeivusha Tanzania kuwa taifa la kati kimaendeleo. Ni kiongozi aliyejitosheleza na hivyo kazi yake itakuwa kulijenga taifa lake. Uwanja ni wenu kwa wanotaka kuchangia mada hii. KARIBUNI.
 
Baada ya Edward Lowassa kusifiwa na rais Magufuli kuwa ni Superman, namdurufu kidogo Lowassa kwa kujikumbusha niliwahi kusema nini kuhusu mtu huyu.
P
 
Back
Top Bottom