In Edward Lowassa, I trust...

In Edward Lowassa, I trust...

Heshima mbele wanaJF wote, na big up kwa Rev. Kishoka, mimi nilishasema siku nyingi na wala sioni aibu, i just love the man, PERIOD!

Watanzania wenzangu, na hata ambao siyo watanzania wanaochangia humu ndani, tukitaka kweli kujadili viongozi wetu, tufanye kutoka rohoni kwa kina, tusifanye kwa emotions ambazo zimekuwa influenced na magazeti pekeyake yake au kikundi cha watu kupitia medium yoyote ile.

Nchi yetu ni nchi ya dunia ya tatu, bado wannchi wengi wetu wapo vijijini na uelewa wao ni mdogo sana, kiasi kwamba wanategemea vijana wao waliowapeleka shule, ambao ndiyo anaJF, waweze kuwafafanulia na kuwachambulia mambo, lets not dissappoint them.

Nchi yetu ni ya kijamaa in theory, lakini tunaishi kwenye dunia ya kidepari, na bahati mbaya kwasababu ni nchi changa hatuwezi kupingana sana na mifumo ya kidunia na wananchi wote Tanzania wanaishia kwa kujitafutia wenyewe siku hizi, maanayake kibepari zaidi. Tusifanye kama mtu nazo qualities za kutuongoza, at any level, kufanya aonee aibu mali aliyoitafuta kwa jasho, cha msingi ni asitufiche kuhusu hizo mali zake ili siku kunakuwa conflict of interest kwenye maamuzi,anasema, na asiposema, vyombo vyetu vya dola vikibaini, vinaschukua hatua za kisheria.

Budget za wabunge wetu kwenye kampeni peke yake ni zaidi ya millioni mia moja (100M) karibu kila jimbo, hivi tunataka hawa watu waende kuomba kwa wahindina wafanyabiashara kila siku? Halafu wakishakuwa wabunge wanakuwa vibaraka wao, tukubali kwamba wafanye kazi/biashara transaparently.

Sina ubaya na Mzee Mengi kwasababu angalau anacheza kadi ya uzawa, lakini unaweza kuona kabisa kwasababu ya nguvu yake ya pesa na vyombo vya habari, viongozi wetu wengi wapo chiniyake, wanamsikiliza na kumuogopa, hiyo siyo siri. Kwa mfanyabiashara tanzania kumtukana a former persident in Mkapa kama vile, lazima kuna utaratibu haupo sawa, ingekuwa serikali imekosa imani na viongozi wake waliopita ningeelewa, serikali inawakilisha wananchi wote, lakini mtu mmoja tu kuamua, inatia mashaka, asiponipenda mtu kama mimi si ndiyo atanimaliza kabisa, lakini kwanini? Ni sawa kweli?

Lowassa is a true servant of Tanzanians, he has delivered at very level, with a passion. His style is unique, he calls a spade, a spade, thats why he has those enemies. Unajua kubadilisha tabia na mfumo wa kufanya kazi wa civil servants, seriously we miss the guy, that thing was changing, nyie wenzetu mnaoishi huko nje hamuwezi kujua.

Tumuombe Mungu uzima, upendo na amani nchini kwetu, kwasababu saa nyingine siku izi inaanza kutia hofu.
 
KGBtz,
Mkuu hata sikuelewi kabisa.. yaani nemeshindwa kuunganisha Lowassa na hayo uloandika hapo juu..
Kwanza kabisa Lowassa ni kiongozi aliye fail ktk ngazi zote za Ubepari, hivyo kumpima kwake hakuwezi kuwa admired pasipo kipimo kinacholingana na Uongozi bora..Ukweli ni kwamba hata mimi namadmire sana Rostam na hao kina Chenge kuweza kutuibia mabillioni na wanajifua kama Kenya..mbinu walizotumia hazina ufundi wowote zaidi ya dhulma sawa na jambazi liloingia bank likaiba kwa kutumia kipande cha ndizi..sasa hapa sielewi sifa inakuja vipi haswa..

Kwa nini watu wanamtaka Lowassa awe rais mtarajiwa ni upuuzi ambao mimi untokana na hizi admiration, which is furthest thing from understanding the concept!. Lowassa ni sawa na mtu anayeongozwa na shetani, na nguvu kubwa anayoiweka ktk utendaji kazi wake ni kwa malengo ya kishetani, You can admire as mucha as U want kwani ndivyo shetani linavyo operate. Shetani huwafuata wale wasiokuwa na imani na kuwapa matunda yanayolingana na kufikiri kwao.

Kwa hiyo nguvu ya kutangaza Gospel ya shetani mara zote huja na vishawishi vingi sana, Hata Yesu kavipitia na hakika kama angekuwa na imani hafifu, hakuelewa ukweli ni upi basi bila shaka angejazwa Ujinga asifunge siku 40 huko mlimani.. Hii ndio imani inavyopimwa kumshinda shetani na sii kupokea matunda ya shetani na ukasikfia shibe ya siku moja...

Tatizo la mada hii ni pale napoona watu mnajazwa ujinga.. Lowassa hawezi yafanya haya maajabu ya Firauni kujenga Pyramids kwa kutumia mijeredi, jasho lenu pasipo malipo halali kisha mkayajengea heshima na hekalu hali roho zenu zinatokota kwa utumwa.
Mkuu wangu unachukia kuona mfanyabiashara akimtukana Kiongozi wako (Mkapa) wakati huo huo unnapenda kuona uwazi wakati ukielewa wazi hakuna kiongozi hata mmoja nchini aliyekuwa na UTAJIRI kwa kutumia jasho lake, hakuna.. Utajiri wa viongozi wetu ni sawa na zama zile za kifalme, kina Pharaoh, Kabaka, Solomon na kadhalika... Ni jasho lako linalojenga utajiri wao wakati wewe unabakia mtumwa wa bwana.

Jamani inachosha kusoma mada hii hasa kama huelewi maana. Rev. Kishoka kaja hapa kuzikoga roho zetu, kuangalia jinsi mnavyofikiria na hasa kupima imani zenu ktk kutazama struggle between two factions: Kikwete na Lowassa, as to say ni rahisi kwa kanisa lake kupambana na shetani mwenyewe (Lowassa) kuliko mtu aliyepandishwa pepo (Kikwete) kwa sababu huyu Kikwete ni binadamu na muungwana aliyekuwa possessed..Ni rahisi kusoma misahafu yake in full force pasipo imani kumtokomeza Devil Lowassa kuliko huyu binadamu aliyekuwa possessed by a demons..hivyo kunakuwepo na kazi ya ziada kuokoa maisha ya binadamu..Na pengine ndio inayomkwaza rev. Kishoka kwenda full force maanake anatweza hata kumtoa roho Kiketwe kazi yote inakuwa ni kupoteza muda..
 
Bhaghosha,

Hata kama ulichapa kazi na ukaja ukavurunda wewe your nothing to your people ni ume prove failure kabisa kwani ulikuwa watenda izo kazi zako kwa juhudi na ukawa na lako jambo ni ume perform zero hapo na umepoteza the whole trust kabisa and no one will appreciate you at this particular juncture.

Kwa jimbo lake alipewa dada mmoja kuwa mkuu wa wilaya na akajitahidi kumletea maendeleo wamasai wajanja wakamkataaa kwa sababu ya uozo wao pale mundoli kwani walibanwa na kutochezea kodi za wananchi, mudi si mchache EL akamwamisha huyo mkuu wa wilaya hebu chunguzeni mjue huko aliko hamishiwa maendeleo yakoje kama Mundoli ina gusa kwa ukusanyaji kodi? ni zero,

Leo ati waja na kumsifia EL ivi wewe wamjua au umepewa profile juu juu?? maana hizi ndizo nyakati za uchaguzi watu wengi ndi hupishana ka magari mabovu yaendayo kwa garage. nawe umeisha onjeshwa eeeeeeh??

Kumbuka Mwl. J.k. Nyerere aliwatabiria EL na JK Mrisho kuwa wao bado sana na matokeo yake hayoooo mwayaona sasa na bado sasa.

please come up with another personal profile and not EL
 
.

Lowassa is a true servant of Tanzanians, he has delivered at very level, with a passion. His style is unique, he calls a spade, a spade, thats why he has those enemies. Unajua kubadilisha tabia na mfumo wa kufanya kazi wa civil servants, seriously we miss the guy, that thing was changing, nyie wenzetu mnaoishi huko nje hamuwezi kujua.

Tumuombe Mungu uzima, upendo na amani nchini kwetu, kwasababu saa nyingine siku izi inaanza kutia hofu.
Hata Mafia hutoa michango ya kusaidia jamii kule Sicily. But that does not negate the fact that they are mafia and their business is illegal. Lowassa ni Mafia wa Tanzania na hata kama ni mchapa kazi, makini, etc.etc. the fact that he has made his illegal money on the backs of Tanzanians inamfanya awe mtu asiyefaa kabisa kusogelea kiti cha uongozi. Mwalimu was right na jinamizi la Mwalimu linamwandama Lowassa.
 
kama ukiwa mchapakazi makini lakini watu wana mashaka na integrity yako nayo ni kazi bure. Nafikiri mkubwa umetueleza vizuri sana hapa maana kama ni wema hata mafia ambao wanaua na kuuza mihadarati nao wanatoa michango na sadaka. Hiyo haitoi hoja ya msingi kwamba wanayoyafanya sio sahihi
 
Yes, I have said it. Ili tuendelee, tunamhitaji Edward Ngoyayi Lowassa!

Ni mchapakazi, mfuatiliaji na mkali asiye na masikhara na walioko chini yake si kuwa wanamheshimu tuu, wanaogopa kushukiwa na zali kutokana na ukali na ufuatiliaji wake.

Kila kazi aliyopewa, kaifanya kwa bidii na kwa ufanisi. Kuna tofauti kubwa sana za kiutendaji kati yake na wenzake walioshika nafasi za uongozi ambazo alizishikilia.

Naamini kwa dhati kuwa ili Tanzania iweze kuamka na kurudi katika mstari ulionyooka wa kujituma, kufanya kazi kwa bidii na maarifa bora na la zaidi kwa nidhamu ili tuendelee vyema na safari yetu ya kujijenga kiuchumi na kijamii ili kuleta maendeleo ya kweli, basi hakuna mwingine zaidi ya Lowassa!

Kama unaye wa kwako, tupe jina na umnadi, wangu miye ni Lowassa!

Hakika Rev.Kishoka umenena no one like EDWARD N. Lowassa,bado watanzania tunamuhutaji ni mfuatiliaji mzuri sana.hakika mie niliumia sana pale alipojiuzulu na kuzuliwa mambo kibao,ndio ni binadamu hakosi kasoro,lakini kufuatilia mambo ni makini sana angalia mfano shule za kata,na mambo mengi tu.Kweli wakweli huwa awadumu katika utawala.
lakini bado tunamitaji ENL.Hope bado anayo nafasi.
 
Hvi, mnaonituhumu kuwa nimemegewa au ni msaliti, je mmesona na kuelewa ni sifa zipi nilizompa Lowassa mpaka nikasema anafaa kutuongoza?

Je hamjaona niliposema kuwa nilichosema kwenye Deconstructing Lowassa kinabakia?

Hapa nimemzungumzia Lowassa mchapa kazi na mfuatiliaji ambazo ni baadhi ya wasifu chanya kuhusu yeye.

Kama ningetaka kuongelea sifa hasi, ningefanya hivyo lakini nimelenga kwenye sifa chanya.

Lakini upofu wetu hauoni mbali wala kufikiri, tunaishia kuwa na mihasira mingi tuu na kudai hatufai. Je hafai kama mchapa kazi na mfuatiliaji?
Mchungaji salam,
At this point and moment and for the future LOWASA hafai, ni Chumvi iliyoharibika unajua agizo la Bw. Yesu juu ya Chumvi iliyoharibika.
 
Yes, I have said it. Ili tuendelee, tunamhitaji Edward Ngoyayi Lowassa!

Ni mchapakazi, mfuatiliaji na mkali asiye na masikhara na walioko chini yake si kuwa wanamheshimu tuu, wanaogopa kushukiwa na zali kutokana na ukali na ufuatiliaji wake.

Kila kazi aliyopewa, kaifanya kwa bidii na kwa ufanisi. Kuna tofauti kubwa sana za kiutendaji kati yake na wenzake walioshika nafasi za uongozi ambazo alizishikilia.

Naamini kwa dhati kuwa ili Tanzania iweze kuamka na kurudi katika mstari ulionyooka wa kujituma, kufanya kazi kwa bidii na maarifa bora na la zaidi kwa nidhamu ili tuendelee vyema na safari yetu ya kujijenga kiuchumi na kijamii ili kuleta maendeleo ya kweli, basi hakuna mwingine zaidi ya Lowassa!

Kama unaye wa kwako, tupe jina na umnadi, wangu miye ni Lowassa!

Hivi kama kauli hii ingetoka kwa Rais wa Tanzania Kikwete au kwa nafasi yake nyingine kama Mwenyekiti wa Chama, sisi tungelichukuliaje kauli hii (what would have been our reaction)?

Je nikiwaambia kuwa hivi ndivyo Rais wetu anavyomuona Lowassa, mtatapika?
 
ukiwa maskini unakuwa na mawazo ya chuki daima ,na unaona kuwa umaskini wako unasababishwa na wale walio nacho..hahaaaa...you people you have a long way to go..LOWASSA is the only PM nchi hii imepata kuwa naye kwa staili yake ya uchapakzi na itachukua nyakati nyingi sana kuja kumpata mtu wa aina yake...
 
Hakika Rev.Kishoka umenena no one like EDWARD N. Lowassa,bado watanzania tunamuhutaji ni mfuatiliaji mzuri sana.hakika mie niliumia sana pale alipojiuzulu na kuzuliwa mambo kibao,ndio ni binadamu hakosi kasoro,lakini kufuatilia mambo ni makini sana angalia mfano shule za kata,na mambo mengi tu.Kweli wakweli huwa awadumu katika utawala.
lakini bado tunamitaji ENL.Hope bado anayo nafasi.
Sina uhakika na Watanzania wenzangu imani yenu kwenu binafsi ikoje? Hivi ikiwa tutasema maneno haya kuwa no one like somebody kweli tutafika hapo tulipotarajia kufika siku zote. Sasa hivi naanza kupata shaka kuwa tuna matatizo sana kwenye utendaji wetu hata kwenye maofisi yetu kama tuna haya maneno ya 'I trust in somebody' "No one like somebody". This is nonsense kabisa, kama mtu ameshaondoka na aondoke kwa sababu zama zake zimekwisha. Tuna nafasi ya kumshauri mtu abadilike tu na siyo kuona kuwa nchi kama nchi haiwezi kuendelea kama fulani hayupo. Hebu pata picha mtu kama Rev. Kishoka ni waziri kwenye wizara nyeti halafu mtu anayemuona kuwa kama everything kwenye maisha yake na nchi yake anaondoka mnategemea nini tena hapo zaidi ya kurudi nyuma na kuweka mikono nyuma
 
Mchungaji;

Amani iwe nawe. Lowassa ni mchapa kazi, na pia kama tuanavyo Lowassa sio Richmond... Richmond yupo na Lowassa aliwaomba akina Mwakyembe wamtaje Richmond.

Je nani anaweza kumtaja Richmond? Nani anaweza Kumtaja Kagoda?

Lowassa ni shujaa, sio kama Hosea, mlipotaka ajiuzulu alijiuzulu. Shujaa gani mwingine kama huyo? hao mnaowasema wanang'ang'ania madaraka tuuu.

Yes REV nipo nawe na amani itutangulie!
 
Bado siku chache ifike tarehe 6/2/2008 siku ambayo Mh Lowassa alitangaza kujiuzulu Uwaziri Mkuu kufuatia Ripoti ya kamati ya bunge juu ya sakata la Richmord.

Si vibaya tunapotimiza miaka 2 ya historia ya demokrasia katika Nchi yetu tujadiliane na kuelimishana issue hii, Je msukumo wa kujenga/kuanzisha shule za kata & zahanati za kata nchini umekosa mfuatiliaji/ msimamiaji?

Siyo siri kasi yake imepungua sana!!
 
Kwa wakazi wa dar es salaam wanakumbuka mh. Lowassa alivyopiga marufuku uchimbaji wa kokoto kule Kunduchi, jamaa walianza taratibu sasa hivi biashara ya kokoto Kunduchi imerudi kama kawaida.

Na lile la barabara tatu kupunguza msongamano ameondoka nalo.
 
Nchi yetu inahitaji mfuatiliaji/msimiaji wa kweli kweli km tunataka maendeleo
 
na suala la richmondi limeshindikana kumalizwa. tuombe arudi kwenye u-PM atumalizie kadhia hii!!!!!!!
 
Back
Top Bottom