In Edward Lowassa, I trust...

In Edward Lowassa, I trust...

Kulamba matapishi hiyo ni mpya ya mtu aliyeishiwa. Maendeleo yanatuhitaji wote tuwajibike kwa kuwa na kiongozi na sio mtawala ambaye hana dira
 
IO,

NImehoji mwenye ushahidi, imeishia mimi kutuhumiwa eti nimerukwa akili na ni punguani.

La Richmond, Msabaha alisema kweli kuhusu Ubangusilo.

Sasa kwa kuwa FMES anashupalia sana kuwa Mwakyembe alifanya kazi nzuri n kumlazimisha Lowassa ang'oke mimi nitawajibu hivi wote wanaodai kuwa eti Richmond ulikuwa mkono wa Lowassa.

1. Kwa nini Rais alikataa ushauri wa Waziri Mkuu kufuta mkataba wa Richmond?
2. Pale Rais alipobaini Richmond ni wababaishaji, kwa nini aliridhia na kuruhusu wakapewa mkopo pamoja na kuwa alimwambia Msabaha atajinyonga?
3. Ilikuwaje Rostam ambaye inasemekana ana Ushemeji na Rais aendelee na kuhujumu nchi kwa kuwaingiza mjini Richmond na kisha kuuchukua mkataba ule wa Richmond kupitia Dowans?
4. Kwa nini mpaka leo, bado principal mkubwa wa Dowans ambaye ni Rostam bado anashikilia Serikali mateka akishirikiana na Rashid ambaye walishirikiana kuanza ulaji wa BOT 1994?

Hivyo ukweli ni kuwa kina Mwakyembe na wapiganaji walimkimbilia Lowassa wakamuacha principal character!
Mkuu hapana sii kweli kina Mwakyembe walimkimbilia Lowassa wakamuacha Principal character..Lowassa ndiye Principal...
Hawa kina Mwakyembe ni wanasiasa, wabunge ambao hoja nzima inahusiana na uhalali wa mkataba kwanza kuliko nani mmiliki wa Dowans au Richmond..Hata kama ungekuwa wewe mmiliki swala hili lisingekuwa tofauti... na hakuna mtu ambaye ange question Richmond na huyo Rostam ikiwa taratibu za kisheria zingetumika. na wala sii hoja kabisa Rostam kuwa owner wa Richmond, Dowans au bwana shemeji tunachokemea hapa ni uongozi mbaya..
The main character hapa ni Lowassa ambaye ndiye aliyeliwezesha shirika la Richmond kuingia mkataba kinyume cha sheria..Hivyo Rostam anaingia tu baada ya kupata makosa ya Uongozi.
Mkuu wangu siwezi kusahau mapanki hata siku moja na siwezi kusema ilikuwa Mkapa sijui wahindi wakati ni Lowassa aliyewawezesha Warusi kuingiza nchini zana za kivita kwa kificho cha biashara ya sangara (wizara yake)..Biashara ambayo ilisababisha vifo Kongo zaidi ya watu milioni 3, na kibaya zaidi wananchi wa Mwanza kushindia mapanki kama chakula.. Njaa ile siwezi kuisahau hata kidogo as a fact bado picha na harufu ya Mapanki ipo kichwani hadi leo hii..Kisha basi kaondoka kwake mambo sii mabaya kwa wavuvi wa Sangara na mazingira yanaboreshwa kuliko wakati ule..Huwezi linganisha wizara hiyo kiutendaji kati ya Lowassa na Magufuli.
 
Lowassa kuibukia bungeni

· <img alt="">
\\Majemedari' wake wajipanga
· Kikwete huenda akahusishwa
[FONT='Trebuchet MS', sans-serif]
[/FONT]
Na Saed KUBENEA
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
EDWARD Lowassa, aliyekuwa waziri mkuu, anatarajiwa kuibukia katika mkutano ujao wa Bunge na kupasua kile kinachoitwa "ukweli kuhusu utata wa mkataba wa Richmond," imefahamika.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika ndani ya kambi yake na katika serikali zinasema Lowassa amekuwa akishinikizwa na marafiki zake kuweka "mambo hadharani" kwa lengo la kujinasua kwenye kitanzi cha Richmond.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Mkutano huo wa Bunge la Muungano, unaoanza Jumanne ijayo mjini Dodoma, unakuwa muhimu kwa kuwa ndimo serikali iliahidi kuwasilisha ripoti ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond Development Company (LLC).
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Suala la Lowassa kupasua ukweli linakuja karibu mwezi tangu atamke kuwa yeye na Rais Jakaya Kikwete ni marafiki wa kweli, ambao hawakukutana njiani na kwamba hakuna wa kuwatenganisha.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Alisema yeye na Kikwete wametoka mbali na urafiki wao, "hauwezi kuvurugwa na kikundi kidogo cha watu."
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Hata hivyo, kauli ya Lowassa ilitolewa siku mbili tangu Rais Kikwete aseme, mapema mwezi uliopita, kwamba, "sina ndugu wala rafiki" katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Rais alikuwa akijibu swali la mmoja wa wananchi, katika kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo kwenye televisheni, ambaye alimtuhumu kulinda marafiki zake wanaotuhumiwa kwa ufisadi.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Rais Kikwete alinukuliwa pia akisema serikali yake ina mpango wa kutafuta msaada wa kitaalamu kutoka vyombo vya kimataifa ili kujiridhisha kuhusu utata wa zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Richmond.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Kampuni ya Richmond ambayo ilipewa zabuni ya kuagiza mitambo ya kufua umeme wa dharura mwaka 2006, ndiyo chanzo cha kujiuzulu kwa Lowassa na mawaziri wengine wawili.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Mawaziri waliojiuzulu ni Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha kutokana na kuhusika kwao katika mchakato wa mkataba wa Richmond ambao Rais Kikwete amebainisha kuwa ulijaa uzembe na ubabaishaji.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema kauli ya Lowassa ilikuwa "inatoa salamu" kwa Kikwete, kwamba siku atakayopata nafasi ya kuzungumza, hatakuwa na simile &#8211; ataanika kila kitu hadharani.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Haikufahamika iwapo "kuanika kila kitu" kunamaanisha kumhusisha Rais Kikwete katika kashfa ambayo tayari bunge limeitolea maamuzi.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
MwanaHALISI linaweza kuthibitisha kwamba Lowassa na wapambe wake wako mbioni kukamilisha wanachoita, "mkakati wa kusafisha njia kuelekea kilele cha uongozi."
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Chanzo cha habari cha gazeti hili kimemnukuu mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba akisema, "Ni lazima Lowassa apasue jipu katika mkutano huu."
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Serukamba, mmoja wa wabunge wanaotajwa kuwa ni watetezi wakubwa wa Lowassa ndani na nje ya bunge, anasema katika mahojiano hayo, "Tunategemea hivyo na kila kitu kitakwenda kama tulivyopanga."
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Mbunge Serukamba alikuwa akijibu swali aliloulizwa juu ya hatua waliyofikia kuhusu mpango wa Lowassa kuzungumza "kutoboa kila kitu bungeni."
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Kambi ya Lowassa inasemekana kupata nguvu mpya baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumsulubu Spika wa Bunge la Jamhuri, Samwel Sitta kwa madai kuwa anasababisha "kuchafuka kwa hali ya hewa" bungeni na kudhoofisha serikali.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Uchunguzi wa awali wa mkataba wa Richmond ulibainisha kuwapo kwa uzembe, jambo ambalo lilibainishwa na Kamati Maalumu ya Bunge ya Nishati na Madini, iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Wakati Lowassa akipanga kujisafisha, mmoja wa wajumbe wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba huo amesema wanasubiri kauli yake "kwa hamu kubwa."
"Unasema amepanga kulipuka bungeni? Ha, ha! Tunamsubiri. Nakuhakikishia hapatatosha," alisema akitoa kicheko chembamba.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Alisema, "Kwa kweli mdogo wangu, nakwambia ataumbuka; maana hata zile taarifa za ndani, ambazo hazikuwa zimepata mwanya wa kutoka, zitawekwa kwenye paa la nyumba."
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Sakata la Richmond linatarajiwa kuchukua sura mpya katika mkutano huu wa bunge iwapo serikali itatoa taarifa ya utekelezaji, kama ilivyoahidi na baadaye kujadiliwa na wabunge.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Ni katika hatua hiyo, taarifa zinaeleza, wapambe wa Lowassa wanataka kujipanga ili kushawishi wabunge kuwa kigogo huyo "hakuhusika" katika kashfa ya Richmond.
Mkataba wa Richmond ndio ulisukuma Lowassa nje ya uwaziri mkuu hapo Februari mwaka 2008. Tangu hapo, Lowassa na wapambe wake wamekuwa wakijitahidi bila mafanikio kutaka kurejesha hadhi hiyo ya kisiasa.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Taarifa zinasema tayari kuna mkakati wa kupanga "idadi nzuri" ya wabunge ili wakati Lowassa anazungumza, waweze kumshangilia kwa kupiga makofi ili kuzima nguvu ya "wapinzani wake."
"Ndiyo, tumeshapata zaidi ya wabunge 100 wanaotuunga mkono. Tunataka pale Lowassa anapozungumza asitokee mtu wa kutujibu. Na kila anayetaka kujibu akutane na kishindo chetu," mbunge mmoja alimueleza mtoa taarifa.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Kuna taarifa kuwa kundi la Lowassa limepanga kutumia mbinu iliyotumika katika NEC kuzima sauti na ushawishi wa wabunge wanaopinga mkataba huo wa Richmond.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Hata hivyo, mjumbe mmoja wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini aliliambia MwanaHALISI kwamba ni lazima Lowassa aje na utetezi wa nguvu, vinginevyo anaweza kujikuta anazama badala ya kuibuka.
Kamati Teule iliyochunguza Richmond, ilitoa mapendekezo 23, yakiwamo ya kuwachukulia hatua waliohusika kuibeba kampuni hiyo kinyume cha taratibu na hata sheria za nchini.
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Iwapo Lowassa atapata fursa ya kutimiza azma yake, kuna uwezekano wa kuchafuka tena kwa hali ya hewa bungeni kutokana na kile ambacho baadhi ya wabunge wanadai "kutokubali kusafisha watuhumiwa."
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Kundi la Lowassa linataka kutumia kauli ya Rais Kikwete kwamba alizuia waziri wake mmoja kufanya malipo ya awali kwa Richmond akihofia "inaweza kuwa kampuni ya mfukoni."
[FONT=Georgia, serif]
[/FONT]
Kwa mujibu wa mtoa taarifa, kauli hiyo ya rais inatafsiriwa kusema kuwa Lowassa alishirikisha kiongozi huyo wa nchi katika "hatua zote za kufikia mkataba" ambao ulikuja kufahamika kuwa wa upendeleo na unaovunja kanuni na sheria.
"Sisi hatujali nani anaumia na nani ananufaika. Tulichopanga ni kupasua jipu," anasema mbunge huyo kutoka kambi ya Lowassa.
[FONT=Georgia, 'Trebuchet MS', 'Century Gothic', Verdana, Arial, sans-serif]
[/FONT]
[FONT=Georgia, 'Trebuchet MS', 'Century Gothic', Verdana, Arial, sans-serif]Chanzo: Gazeti la Mwanahalisi 21-10-2009[/FONT]
 
Wangu mimi ni mtu saaaaaafi, mchamungu not and never contaminated by ufisadism...BENJAMIN WILLIUM MKAPA...wenye wivu wajinyonge.
 
Jasusi,
Ebu waulize haop wanaosema haya, ni mara ngapi Lowassa kahudhuria vikao vya Bunge!.. nasikini jamaa hafiki kabisa ila siku anazopenda yeye na kuna baadhi ya watu wanasema Lowassa kisha kiuka taratibu nyingi za Bunge ktk kuhudhuria lakini hakuna wa kumgusa na fedha zake anavuta kama kawa!.
 
Jasusi,
Ebu waulize haop wanaosema haya, ni mara ngapi Lowassa kahudhuria vikao vya Bunge!.. nasikini jamaa hafiki kabisa ila siku anazopenda yeye na kuna baadhi ya watu wanasema Lowassa kisha kiuka taratibu nyingi za Bunge ktk kuhudhuria lakini hakuna wa kumgusa na fedha zake anavuta kama kawa!.
Mkandara,
Na mimi nasubiri hilo jipu lilipuke. Lisije tu kumlipukia usoni mlipuaji.
 
Mkuu hapana sii kweli kina Mwakyembe walimkimbilia Lowassa wakamuacha Principal character..Lowassa ndiye Principal... .

MKandara,

Kwa nini miezi miwili au mitatu iliyopita Ikulu na Serikali ilikimbilia kumsafisha Kikwete kuhusiana na Richmond?

Kwa nini wamekimbilia kusema ni Arthur Mwakapugi na watendaji wengine ndio wawajibike ambapo okay ya kuwalipa Richmond ilifanywa na Cabinet nzima?

Ukitaka ukweli kuhusu Richmond, no one will be safe including Muungwana! It was embarrasing and shameful act!
 
IO,

NImehoji mwenye ushahidi, imeishia mimi kutuhumiwa eti nimerukwa akili na ni punguani.

La Richmond, Msabaha alisema kweli kuhusu Ubangusilo.

Sasa kwa kuwa FMES anashupalia sana kuwa Mwakyembe alifanya kazi nzuri n kumlazimisha Lowassa ang'oke mimi nitawajibu hivi wote wanaodai kuwa eti Richmond ulikuwa mkono wa Lowassa.

1. Kwa nini Rais alikataa ushauri wa Waziri Mkuu kufuta mkataba wa Richmond?
2. Pale Rais alipobaini Richmond ni wababaishaji, kwa nini aliridhia na kuruhusu wakapewa mkopo pamoja na kuwa alimwambia Msabaha atajinyonga?
3. Ilikuwaje Rostam ambaye inasemekana ana Ushemeji na Rais aendelee na kuhujumu nchi kwa kuwaingiza mjini Richmond na kisha kuuchukua mkataba ule wa Richmond kupitia Dowans?
4. Kwa nini mpaka leo, bado principal mkubwa wa Dowans ambaye ni Rostam bado anashikilia Serikali mateka akishirikiana na Rashid ambaye walishirikiana kuanza ulaji wa BOT 1994?

Hivyo ukweli ni kuwa kina Mwakyembe na wapiganaji walimkimbilia Lowassa wakamuacha principal character!

- Swali kwako ni kwa nini Lowassa alikimbia cheo bila kufukuzwa iwapo alijua kwamba yeye sio mhusika wa Richimonduli? Na kwa nini mtoto wake alikuwa akienda kuchukua cheki ya Richimonduli kila mwezi akifuatana na mtu wa Rostam kule Hazina?

- Kumsafisha Lowassa mbele ya macho yetu sio rahisi mkuu, labda uende huko kijijini utafute wananchi waliolala usingizi maana hapa JF kuna waliomsaidia sana Mwakyembe na ripoti, yaani simply unajaribu kumsafisha Lowassa kwenye the wrong field yaani hapa JF!

- Tanzania tuna wananchi wengi sana wanaoweza kuongoza, ifiek mahali tuanze kuongelea watu wengine sio kina Lowassa kila siku, inachosha!

Respect.

FMEs!
 
Lole Gwakisa,

Ni wapi nimemsafisha Lowassa?

Kusema anafanya kazi kwa bidii ni kumsafisha?

Ukisema EL anafanya kazi kwa bidii, labda hatujakuelewa, pengine unamaanisha anafanya kazi kwa bidii ya UFISADI. Labda unamaanisha hivyo mkuu.
 
MKandara,

Kwa nini miezi miwili au mitatu iliyopita Ikulu na Serikali ilikimbilia kumsafisha Kikwete kuhusiana na Richmond?

Kwa nini wamekimbilia kusema ni Arthur Mwakapugi na watendaji wengine ndio wawajibike ambapo okay ya kuwalipa Richmond ilifanywa na Cabinet nzima?

Ukitaka ukweli kuhusu Richmond, no one will be safe including Muungwana! It was embarrasing and shameful act!
Mkuu wangu nimeshasema kwamba sisi Miafrika siku zote hatukubali makosa, always kuna mtu mwingne alosababisha..hata mtu akifumaniwa husingizia Beer, ya kuwa alilewa sana hajui kilichotokea. Hivyo huwezi kuipeleka chupa mahakamani..
Kuhusiana na JK kuhusika na Richmond hilo mkuu wangu nitahitaji ushahidi zaidi na sidhani kama muungwana alikuwa mjinga kiasi cha kuanzisha uchunguzi wa Richmond hali angeweza kabisa kulizima kama alivyozima uchunguzi wa Mkapa na Kiwira.
Labda nikuulize wewe kama JK angesema hakuna uchahidi wowote dhidi ya Lowassa isipokuwa mambo yote yalifanywa na viongozi wa tanesco na wale walioweka sahihi ya mkataba tungekuwa na hoja zaidi..maanake najua sisi wadanganyika angefukuza watu wachache tu ingetosha,, Mkapa alifanya hivyo NBC, watu wachache wakatiwa ndani, msukosuko wa kodi na kadhalika kumbe bomu la NBC lilikuwa kubwa kuliko tunavyoelewa, nani alitaka kujua zaidi.
 
- Swali kwako ni kwa nini Lowassa alikimbia cheo bila kufukuzwa iwapo alijua kwamba yeye sio mhusika wa Richimonduli? Na kwa nini mtoto wake alikuwa akienda kuchukua cheki ya Richimonduli kila mwezi akifuatana na mtu wa Rostam kule Hazina?

- Kumsafisha Lowassa mbele ya macho yetu sio rahisi mkuu, labda uende huko kijijini utafute wananchi waliolala usingizi maana hapa JF kuna waliomsaidia sana Mwakyembe na ripoti, yaani simply unajaribu kumsafisha Lowassa kwenye the wrong field yaani hapa JF!

- Tanzania tuna wananchi wengi sana wanaoweza kuongoza, ifiek mahali tuanze kuongelea watu wengine sio kina Lowassa kila siku, inachosha!

Respect.

FMEs!

Kama huu ni ushahidi wako, kama unadai Ki-Freddy kwenda chukua pesa Hazina, kwa nini basi wote Baba na Mwana hawafikishwi Mahakamani?
 
- Ni afadhali nife nikiwa CCM, kuliko kuwa Chadema ya Zitto na wazee wa chama.

- nilisema hawawezi kuwashinda kwa kikao kimoja tu cha butiama, it takes a lot of works na commitment na ndipo walipo sasa wapiganaji wako on the right track ndio maana sasa hata Makamba anawaunga mkono.

- Naona unasema nikupigie simu, hapana sina huo muda ili unisaidie kukubali ku-trust in Edward? Bwa! ha! ha!

Respect.

FMEs!

Zitto wamtupia madongo ya nini huku waliovurunda mikataba ya Tanzania ni CCM?

Kwa nini hao unaodai walileta varangati Bungeni wakati wa Richmond mpaka leo wanashindwa kufukuta ndani ya CCM?

Mbona hatuwasikii wakishinikiza ndani ya CC au NEC kuwa kina Lowassa na wenzao wafukuzwe uanachama kama ni kweli wao ni wapiganaji wanaopigania maslahi ya Tanzania?

Acha ubabaishaji wa kusema wao hawana nguvu au eti itachukua muda mrefu kusuka mabadiliko ndani ya CCM!

NImewambieni, kama mnadai Mafisadi wamekishikilia CCM yenu, basi ondokeni CCM nendeni kwingine au anzisheni chama kipya, lakini huishi kudai wewe ni CCM wa kudumu, CCM wa Maisha, je ni maslahi gani mnayoyasubiri kupitia CCM mpaka mnaogopa kuambiana ukweli ndani ya CCM na kukimbiliaa Magazeti na Bungeni ambako nako hamna nguvu wala kura za kutosha?
 
Zitto wamtupia madongo ya nini huku waliovurunda mikataba ya Tanzania ni CCM? Kwa nini hao unaodai walileta varangati Bungeni wakati wa Richmond mpaka leo wanashindwa kufukuta ndani ya CCM? Mbona hatuwasikii wakishinikiza ndani ya CC au NEC kuwa kina Lowassa na wenzao wafukuzwe uanachama kama ni kweli wao ni wapiganaji wanaopigania maslahi ya Tanzania?

- Mchungaji, inachosha sana kurudia yale yale kila wakati, wapiganaji wanafurukuta sana ndani ya bunge mpaka kwenye NEC, tumejionea wenyewe jinsi Rais akiwakana mafisadi, mpaka Makamba, Chiligati, Sofia Simba, nao wakijaribu kuwakana mafisadi, ni baada ya ile vurungati ya NEC na Sitta, no matter how you try to discourage them, effect yao ni kubwa sana kwa masilahi ya taifa kuliko anybody unayejaribu kum-promote na hizi empty rants.

- Ni wapiganaji 11 against mafisadi wapatao 5000, pamoja na supporters wao humu JF ambao utawajua kwa maneno yao, kwamba Lowassa anfaa kuwa kiongozi wetu after all the mess aliyokwisha create, huenda wapiganaji kwako ni wendawazimu lakini demokrasia inaruhusu hilo yaani wewe na that kind of thinking, ila kwangu mimi na wananchi wengine wengi wapiganaji ni very effective na we are with them mpaka mwisho wa safari na mtu kama mimi ninaenda out of my way, kuwatafutia misaada as mucha as I can na I believe in them na what they are doing kwa our nation.

Acha ubabaishaji wa kusema wao hawana nguvu au eti itachukua muda mrefu kusuka mabadiliko ndani ya CCM!

- Sikutegemea lugha low kama hii toka kwako katika kujaribu kujenga hoja useful kwa masilahi ya taifa, punguza jazba mkuu, haya ni majadiliano tu na kuelimishana na sio lazima utumie hizi lugha za vichochoroni ili kueleweka.

NImewambieni, kama mnadai Mafisadi wamekishikilia CCM yenu, basi ondokeni CCM nendeni kwingine au anzisheni chama kipya, lakini huishi kudai wewe ni CCM wa kudumu, CCM wa Maisha, je ni maslahi gani mnayoyasubiri kupitia CCM mpaka mnaogopa kuambiana ukweli ndani ya CCM na kukimbiliaa Magazeti na Bungeni ambako nako hamna nguvu wala kura za kutosha?

- Mimi naomba kurudia tena kwamba ni mwanachama damu wa CCM, so far sijaona chama ambacho ni alternative, mabadiliko ndani ya CCM yanawezekana, ila uozo uliojengwa for the last 47 years ndani ya CCM, hauwezi kuondolewa in one year na wapiganaji 11 tu, itachukua muda mrefu sana hasa ukizingatia mawazo ya baadhi ya wananchi kama yako, ya kujaribu kujifanya uko juu sana in thinking, wakati mafisadi wanatusumbua taifa zima na wewe included,

- Umeshikilia matatizo tu, lakini solution huna isipokuwa kushambulia tu wengine ni kweli kwa this kind of thinking, hawa mafisadi watatutawala mpaka mwisho wa dunia, it is about time sasa mkuu ukbadilika na kukubali kwamba huna ujanja wowote zaidi ya wananchi wengine iwapo unalia tu na matatizo bila ya kushauri workable solution kwa taifa letu, hii ni Tanzania sio majuu mkuu, shuka chini ndugu yangu unaonekana uko juu mno mpaka umesahau reality za bongo, kwamba huu ufisadi haukuanza leo wala jana, umeota mizizi for the last 47 years, wapiganaji 11 hawawezi kufanya miujiza in one or five years na kuondoa mziziz yote ya ufisadi, lakini atleats wameanza somwhere na wanahitaji our support, badala ya hizi empty rants taifa sio lao tu mkuu ni letu wote, sasa na wewe anza somewhere na solution, badala ya kulamu kila mtu mwingine as if taifa sio lako!

I support wapiganaji na wale wote wanaojaribu kushauri solutions, badala ya kushikilia negativity kila kukicha ni more negativity tu as if taifa ni la wapiganaji 11 tu, ni aibu!

Respect.

FMEs!
 
Kama huu ni ushahidi wako, kama unadai Ki-Freddy kwenda chukua pesa Hazina, kwa nini basi wote Baba na Mwana hawafikishwi Mahakamani?

- Hili swali ungewauliza vyama vya upinzani, hivi ni kwa nini tunawalipa ruzuku kwa kodi zetu, sio ili wafuatilie ishus kama hizi badala ya kusubiri CCM ijichunguze yenyewe, historia iko wazi kwamba CCM haina huo utamaduni!

Respect.

FMEs!
 
Lowasa ni kama pweza(Octopus)...ana mikono mingi na mirefu. Mingine inaweza kufanya kazi hata kama yeye mwenyewe amelala.

Mwanzoni walianza watu tuliowaita "vilaza" kina Serukamba, Komba na Guninita kumpigania kwa nguvu zao zote ili asafishwe.

Sasa hivi mpaka wachambuzi mahiri wa siasa jamii na siasa maendeleo nao wanataka kutuchanganya changanya hapa kwa maneno ya mbele nyuma, ilimradi conclusion iwe ileile ya akina Guninita. Ghafla JF wameanza kutakiwa walete ushahidi wa ufisadi wa Lowasa, akiwa Ardhi, akiwa PMO kitengo cha maafa(El nino), akiwa Maji na Mifugo na akiwa kama Waziri Mkuu....

Waulizeni machief editor kuhusu habari iliyokua iuwe watanzania kwa presha, baada ya kujulikana account ya Chenge ya Jersey. Watu walikuja na account yake mojawapo...ya chenge ilikua kweli ni "vijisenti" kwa hii yake. Lakini nguvu iliyotumika
huko kwenye media houses(TD ni moja wao) kuizima hii habari ya account, utafkiri his whole life depended on the secrecy of this account....ni mzigo mzito kwelikweli kajilimbikia na anajua hauelezeki ndio maana hataki ujulikane.

Pweza huyu kweli mkubwa!

- Maneno mazito sana mkuu Al, wenye macho waone na wenye masikio wasikie.

Respect.

FMEs!
 
i still can't believe kwamba baba mchungaji ndiye aliyedeclare kwamba ''...in edward,i trust..''! i really dn't knw.hapa ninakubaliana na nyani julius na signature yake
 
Mchapa kazi wakuchangamkia madili faster . Nchi yetu yetu haihitaji mtu kama luassa ili iendelee . Inahitaji watu kama Nyelele wenye uzalendo WATU KAMA lOWASSA wanajenga matabaka . wewe unayemfagilia ni baba yako na wala si vinginenvyo . una masilahi binafisi na wewe Richmond tu. Achana na Luassa kuna watu wengi wazuri , naomba uungane nami tumfanye historia . Tangu lini mwizi akawa kiongozi mzuri.
 
Kama huu ni ushahidi wako, kama unadai Ki-Freddy kwenda chukua pesa Hazina, kwa nini basi wote Baba na Mwana hawafikishwi Mahakamani?
Mchungaji,
Andiko linaseha kilajambo na wakati wake, hivyo wakati ukifika si Baba na Mwana tu tutaburuza na washiriki wengine pia.
 
- Hili swali ungewauliza vyama vya upinzani, hivi ni kwa nini tunawalipa ruzuku kwa kodi zetu, sio ili wafuatilie ishus kama hizi badala ya kusubiri CCM ijichunguze yenyewe, historia iko wazi kwamba CCM haina huo utamaduni!

Respect.

FMEs!
FMES,
Isingekuwa CHADEMA skandali la EPA lingekuwa chini ya zulia mpaka leo.
 
- Hili swali ungewauliza vyama vya upinzani, hivi ni kwa nini tunawalipa ruzuku kwa kodi zetu, sio ili wafuatilie ishus kama hizi badala ya kusubiri CCM ijichunguze yenyewe, historia iko wazi kwamba CCM haina huo utamaduni!

Respect.

FMEs!

Mbona hamjiulizi nyinyi wenyewe ndani ya CCM na wanachama wenu Milioni 5 kuwa mnang'ang'ania Katiba na hazina ya Tanzania kama ni mali yenu binafsi tena kwa mujibu wa ibara ya 15.1?

Mkandara kakuambia hili ni lenu ndani ya CCM, wewe ukadai ni la Taifa zima.

Tukichukulia mantiki ya tofauti ya CCM na Taifa, ki-Taifa basi ni shangwe kuwa Lowassa hayuko madarakani kwa sasa, lakini kwenu ki-CCM, bado mna kidonda dugu na ndio maana mnaogopa kumuondoa ndani ya Chama chenu, anajua siri zenu! kwi kwi kwi!
 
Back
Top Bottom