In Edward Lowassa, I trust...

In Edward Lowassa, I trust...

Mkuu FMES,
karibu sana mkuu wangu sijakusikia muda..
Mkuu mbona umekuja na wazimu mpya!

- Bob yaani nina wazimu mpya kuliko wa kwako wa kawaida na udini? Bwa! ha! ha!

Huyo Lowassa si wenu mkuu wangu iweje leo iwe mkosa ni yeye wakati makosa yote alofanya ni ktk mikakati na sera za chama..Hana makosa kwa sababu alofanya ni within sera za chama chenu na ndio maana hata rais na wabunge wengine wanamtetea kutokuwa na makosa.

- Kutetewa kuwa huna makosa haina maana kwamba hauna makosa, na haya ya chama chenu na other nonesense yanatokea wapi mkuu, kama ni chama CCM kinatawala Tanzania for the last 45 years, sasa unasema ni chama changu kuliko chako mkuu vipi hiyo? CCM ingekua na sera za kuiba Richimonduli basi Lowassa angekua bado ni Waziri Mkuu.

Ikiwa wewe unaona wazi kuwa Lowassa ni mkosa, basi hilo ni wewe, sii mawazo ya wanaCCM wote kwani siku zote mkosa hufikishwa mahakamani na kuhukumiwa. Haikufanyika hivyo yupo huru ni mtu asokuwa na makosa.

- Bob kuna mtu ameiba ID yako nini, I mean hii sio wewe eti kama Lowassa ana makosa ni mawazo yangu tu, that is too low of you mkuu, vipi huko mkuu una usalama kweli?

je nani wa kumlaumu ikiwa hata huyo kiongozi wa Takukuru anachaguliwa na kiongozi wa chama chako bila uchaguzi huo kupitishwa na Bunge... Hivi kweli unafikiria Lowassa alijiuzuru tu hivhivi yaani kjaamka asubuhi akafikiria kujiuzuru pasipo ushauri wa viongozi wenzake.. Na mbona alisema anafanya hivyo kukinusuru CHAMA! haya maneno yalikuwa na maana gani?

- Bob CCM ni chama changu kuliko wewe bro toka lini? CCM ni chama chetu wabongo wote ndio maana kimeweza kutawala miaka 45 na zaidi na bado kinaendelea, Lowassa alijiuzulu kwa sababu ya kukimbia kujibu mashitaka ya wizi wake, that has nothing to do na chama wala serikali, kulindana ni tabia za vyama vyote Tanzania hakuna bora kuliko kingine!

Mkuu wangu taifa stars wameshindwa kuingia world cup finals, tumetolewa round ya pili ni aibu kwa nchi yetu ni aibu kwetu sote na tukubali matokeo. Tanzania inakuwa ranked kutokana na hao watu 11 tu waliocheza sasa kama wewe unabisha kuhusiana na ranking hizo ati kwa sababu ni watu 11 tu walicheza.....kazi kwako!

- Off course wizi wa Lowassa ni aibu yetu wote waTanzania hapo uko right, lakini ya kumtumia Lowassa kama a tool ya ku-exploit what should be a strong opposition kwa CCM na uchaguzi uajo, ninasema ni mawazo mufilisi sana tena nonsense at best!

Respect.

FMEs!
 
Et tu Brute? Wajueni Ma-Yuda Iskariote wenu!
Rev. Kishoka
user_offline.gif
21st June 2008, 04:33 PM

Ewe Mtanzania,

Chukua muda utafakari unachokisoma hapa, chambua kwa undani ndani ya roho yako ujilize machungu unayoyapata kwa KUSALITIWA na hawa wafuatao ambao ni wawakilishi wako katika Serikali.

Uliwachagua kwa kuwapigia kura na kuwapa dhamana wawe Wabunge na Wawakilishi wako katika kujenga Serikali.

Jee utendaji kazi zao na kauli wanazotoa ni kweli zinakuwakilisha wewe kama Mwananchi na kukusaidia wewe Mwenye Nchi? Au kauli na matendo yao ni kujinufaisha na kulinda maslahi ya Chama chao CCM?

Jiulize, mwaka 2010, uko tayari kumuongezea huyu Msaliti wa maslahi yako na familia yako miaka mingine mitano ya kukulaghai kuwa yeye ni Mbunge wako?

1. Anna Abdallah
2. Abdalla Kigoda
3. Peter Msola
4. Peter Serukamba
5. Andrew Chenge
6. Mustafa Mkullo
7. Hawa Ghasia
8. Bernard Membe
9. Maua Daftari
10. Mohamed Seif Khatib
11. Nizar Karamagi
12. Ibrahimu Msabaha
13. Charles Keenja
14. Emmanuel Nchimbi
15. Edward Lowassa
16. Mary Nagu
17. Milton Mahanga
18. Rostam Aziz

........add to the list

- Bob hebu soma vizuri sana haya maneno kuhusu Lowassa, na aliyeyaandika ambaye sasa anadai Lowassa anafaa na sio mwizi maana hakuna ushaidi JF sometimes labda kuna spirits zinaiba Code zetu I mean no way tukawa tunageuka geuka rangi namna hii! phew!

- siku moja Lowassa ni Yuda, next day ni a hero na hakuna ushahidi tunachekesha sana sometimes!

Respect.

FMEs!
 
Mkandara,

Ni heri wewe umenisaida kumjibu FMES, maana inaelekea yeye U-Political strategist wake umeanza kuchokachoka na wala haoni na kuelewa ninachozungumza ambacho ni kwa faida yake yeye FMES na wale Wapiganaji wake!

Siasa ni mchezo mchafu, kila mtu anajua. Muulize Malecela, Salim, Msuya hata Lowassa mwenyewe na Kikwete, watakuambia siasa ni mchezo mchafu.

- Kama kushauri kwamba Lowassa ni kiongozi bora ndio kuwa the best political strategist katika Tanzania ya leo, basi mkuu keep it siuhitaji, uongozi wa Lowassa hauwezi kua kwa faida yangu labda yako wewe, simuhitaji kuniongoza mahali popote pale kwa sababu ni kiongozi mwizi na ushahidi upo tena wa wazi sana ndio maana akakimbia uongozi bila kufukuzwa, kuandika andika kila mahali JF haina maana kwamba ndio unakuwa the best strategist hasa na hizi context za ubora wa Lowassa, ni mufilisi tupu.

- Siasa ni mchezo mchafu haina maana kuongozwa na viongozi wezi, huku ukishangilia kwamba eti siasa ni mchezo mchafu, watu wenye akili nyingi wanapoongelea uchafu wa siasa, hawana maana kwamba fisadi kama Lowassa kurudishwa kwenye uongozi, hilo ni tatizo la utawala usioheshimu sheria kama wa kwetu, wanaposema siasa ni mchezo mchafu wana maana kama vile Mama Clinton alivyopambana na Obama kwenye uchaguzi na leo ni waziri wake, hawaongelei viongozi wezi kama Lowassa, ambaye hata Mwalimu alimsema wazi kwamba ni mwizi, leo wewe etu unashauri arudishwe tena kwenye uongozi, na kwamba eti ni kwa sababu siasa ni mchezo mchafu na kwamba wewe ni the best strategist hapa JF kwa kuwa na mawazo haya, it is absurd!

- Lowassa belongs to jail sio kwenye uongozi, inasikitisha sana kuwa hata na this kind of thinking kwa kisingizio cha siasa mchezo mchafu, kwa sababu it does not apply na hizi theory zako not even close.

Respect.

FMEs!
 
Ninachojua ni kwamba nikiletewa Lowassa na kikwete nichague na hakuna choice nyingine walai nampa Lowassa kuliko huyu ndugu yetu
 
Mbona me sikuhizi nashindwa kuelewa? Habari za kumpongeza EL zinashamiri kila kona na kila siku mambo haya yanazidi...JAMANI HUYU JAMAA..........SANA HATUFAI KWA KWELI...he should be charged to the crt of law
 
FMES,

Naomba usome tena nilichoandika. Tea soma vizuri sana na tumia zile hekima na busara zako za Ki-Sauti ya Umeme!

Kama bado hujanielewa, nipigie simu nikueleweshe!
 
Yes, I have said it. Ili tuendelee, tunamhitaji Edward Ngoyayi Lowassa!

Ni mchapakazi, mfuatiliaji na mkali asiye na masikhara na walioko chini yake si kuwa wanamheshimu tuu, wanaogopa kushukiwa na zali kutokana na ukali na ufuatiliaji wake.

Kila kazi aliyopewa, kaifanya kwa bidii na kwa ufanisi. Kuna tofauti kubwa sana za kiutendaji kati yake na wenzake walioshika nafasi za uongozi ambazo alizishikilia.

Naamini kwa dhati kuwa ili Tanzania iweze kuamka na kurudi katika mstari ulionyooka wa kujituma, kufanya kazi kwa bidii na maarifa bora na la zaidi kwa nidhamu ili tuendelee vyema na safari yetu ya kujijenga kiuchumi na kijamii ili kuleta maendeleo ya kweli, basi hakuna mwingine zaidi ya Lowassa!

Kama unaye wa kwako, tupe jina na umnadi, wangu miye ni Lowassa!

Reverand unasema ili tuendelee tunamuhitaji Lowassa,at the same time unakiri kwamba ufisadi ni kikwazo cha maendeleo,kwa maana kwamba umemsafisha Lowassa maana maneno "I trust in" ni mazito. Pengine una insight zaidi,kama unakubaliana kuwa ufisadi ni kikwazo cha maendeleo then kumchagua kiongozi fisadi mchapa kazi ni sawa na ile wanaita maktaimu....Narudia mkuu inawezekana una insight nzuri zaidi kuhusiana na kashfa za Richmond nk. Binafsi ikigundulika kuwa Lowassa hakuwa na makosa ya ufisadi kwenye kashfa hizo basi nitakuunga mkono.
 
Mushi,

Umeshawahi jiuliza kwa nini Lowassa hajafikishwa mahakamani kwa uzembe wa Richmond au kupewa karipio na Kamati Kuu au NEC ya CCM?
 
FMES,
Mkuu wangu la Udini wala sidhani utapenda kwenda huko kwa sababu wanijua vizuri sana na nakufahamu vizuri sana. Kati yetu mimi na wewe huwezi kamwe kuniita mimi mdini wakati unafahamu fika wewe ni Mlokole na mimi napiga mai kama jana. Dini ni ELIMU tu kwangu ambayo inaniongoza mimi ktk maisha yangu..Naitumia Dini kama navyotumia masomo mengine ktk kuendesha maisha yangu na sii kuabudu maandishi kama mnavyofanya kina nyie.. Najua jina unaloitumia unapokuwa huko kwenye mijadala ya dini... mkuu sidhani kama unataka kwenda huko ambako nilikwisha mwambia usinivae kabisa ktk maswala hayo ya dini..

Pili, unayoandika hapo juu kuhusu CCM haihusu kabisa.. CCM sio chama changu ati kwa sababu kinaniongoza kwa miaka 45.. Hizi fikra ni finyu mkuu wangu, na ndio maana huwezi kuelewa na haswa mimi.
Labda niweke lugha safi na nyepesi kwako.. Kutawaliwa na CCM ni sawa na kutawaliwa na mkoloni sasa nambie unapotawaliwa na mkoloni basi nawe unabadilika kuwa mkoloni kwa sababu tu ya hesabu ya miaka ulotawaliwa!.. Utaweza vipi kuwa mwana mapinduzi au Mpiganaji ikiwa wewe mwenyewe umeshakubali kutawaliwa..Hayo ni mawazo ya kina Raila na Morgan ambao wapo tayari kusalimu amri kuungana na shetani. Sii mimi na ndio maana siwezi kuitetea CCM hata siku moja wala kutenganisha matendoi ya viongozi wake na chama...Injini ya gario lenu CCM ni viongozi wake haiwezekani injini ya gari kuwa mbovu ukasema gari zima isipokuwa injini ndio mbaya.. Hiyo ni lugha muflisi..Binafsi CCM ni watu, CCM ni Uongozi wake kama ulivyokuwa Ukoloni..
 
FMES,

Watu tuliacha kuwa wanachama na wafuasi wa CCM vlipokuja vyama vingi miaka 18 iliyopita. Aliyebakia king'ang'anizi kuwa CCM ndio jibu ni wewe peke yako!

Sasa kwa hili la CCM si wewe uliyedai miezi miwili iliyopita kuwa wapiganaji 11 hawana ubavu kushindana na mafisadi 5000 ndani ya CCM au nawe ulikuwa umeingiwa pepo na mtu kukuibia password yako ulipotoa kauli hiyo?

Then acheni majority y CCM ishike hatamu na Lowassa si ndio kiongozi wao, la sivyo tunadanganyana kuwa CCM itafanikiwa kuondoa Ufisadi!

Labda nikuulize, ni nani vile alimtetea na kusababisha kurudishwa Lowassa kwenye uongozi baada ya lile kata funua la Nyerere 1995?

- Wapiganaji 11 hawawezi kuwaondoa mafisadi karibu 5,000 walioko CCM kwa kikao kimoja tu cha Butiama, ni kama vile Zitto alivyoshindwa na wazee wa chama, yaani mtu mmoja tu hawezi kushindana na wazee wengi huko kwenye chama waliomlazimisha kurudisha fomu anahitaji wananchi wengi wa kumuunga mkono kama wapiganaji wanahitaji sana msaaada wetu wananchi, badala ya kuwavunja nguvu kama unavyofanya.

FMEs!
 
FMES,
Mkuu wangu la Udini wala sidhani utapenda kwenda huko kwa sababu wanijua vizuri sana na nakufahamu vizuri sana. Kati yetu mimi na wewe huwezi kamwe kuniita mimi mdini wakati unafahamu fika wewe ni Mlokole na mimi napiga mai kama jana. Dini ni ELIMU tu kwangu ambayo inaniongoza mimi ktk maisha yangu..Naitumia Dini kama navyotumia masomo mengine ktk kuendesha maisha yangu na sii kuabudu maandishi kama mnavyofanya kina nyie.. Najua jina unaloitumia unapokuwa huko kwenye mijadala ya dini... mkuu sidhani kama unataka kwenda huko ambako nilikwisha mwambia usinivae kabisa ktk maswala hayo ya dini..

Pili, unayoandika hapo juu kuhusu CCM haihusu kabisa.. CCM sio chama changu ati kwa sababu kinaniongoza kwa miaka 45.. Hizi fikra ni finyu mkuu wangu, na ndio maana huwezi kuelewa na haswa mimi.
Labda niweke lugha safi na nyepesi kwako.. Kutawaliwa na CCM ni sawa na kutawaliwa na mkoloni sasa nambie unapotawaliwa na mkoloni basi nawe unabadilika kuwa mkoloni kwa sababu tu ya hesabu ya miaka ulotawaliwa!.. Utaweza vipi kuwa mwana mapinduzi au Mpiganaji ikiwa wewe mwenyewe umeshakubali kutawaliwa..Hayo ni mawazo ya kina Raila na Morgan ambao wapo tayari kusalimu amri kuungana na shetani. Sii mimi na ndio maana siwezi kuitetea CCM hata siku moja wala kutenganisha matendoi ya viongozi wake na chama...Injini ya gario lenu CCM ni viongozi wake haiwezekani injini ya gari kuwa mbovu ukasema gari zima isipokuwa injini ndio mbaya.. Hiyo ni lugha muflisi..Binafsi CCM ni watu, CCM ni Uongozi wake kama ulivyokuwa Ukoloni..

jaji
kulikoni tena??
tatizo la tz ni tatizo la kitanzania ,tatizo kubwa mime nilionalo ni kujaribu kutumia ccm kama steping stone ya ku escape utanzania wetu.

ccm has nothing to do na ujinga wetu,but ujinga wetu has something to do with ccm.

Kikwete hoyeeeeee, ccm hoyeeeeeee
 
Mkandara,

Ni heri wewe umenisaida kumjibu FMES, maana inaelekea yeye U-Political strategist wake umeanza kuchokachoka na wala haoni na kuelewa ninachozungumza ambacho ni kwa faida yake yeye FMES na wale Wapiganaji wake!

Siasa ni mchezo mchafu, kila mtu anajua. Muulize Malecela, Salim, Msuya hata Lowassa mwenyewe na Kikwete, watakuambia siasa ni mchezo mchafu.

Leo hii kila mtu kakata tamaa ya kuongozwa na Kikwete, lakini hakuna mwenye kuamka na kusema huyu bwana hafai tena! Lakini tunampigia debe na kusema apewe miaka mingine mitano, ili afanye nini?

Kama katika miaka hii mitano ya kwanza kashindwa kuonyesha kuwa ana uwezo wa kuwa Rais, je hiyo mitano iliyobakia atatuthibitishia nini kuwa yeye ana uwezo wa kuongoza nchi?

Hao wanaosema jamani mwacheni Kikwete aendelee kutawala na tatizo si Kikwete bali ni Mafisadi, ni sawa na punguani. Leo tunadiriki kusema eti Mafisadi wana nguvu kuliko dola? Kama ni hivyo basi dola ina maana gani kuendelea kuwepo?

Ikiwa JK na unyenyekevu wake na uadilifu wake anashindwa kuwa na sauti ya kiutawala, yenye nguvu za kirais, si heri basi tumpe huyu Lowassa ambaye anatuhujumu, lakini ana nguvu za kiutendaji na akinena anasikilizwa?

Hatuwezi kuendelea kulaumu Mafisadi kwa kila kitu kinachotokea Tanzania ikiwa Serikali iliyoko madarakani inafanya kazi kama imetekwa nyara! Basi wapeni hao mafisadi hatamu waongoze nchi maana kama wameshikilia nchi nzima kiasi cha Mkuu wa Polisi kudai Polisi haina nguvu kukabiliana na Mafisadi, then pave the way for Mafisadi to rule and govern tujue moja.

Mafisadi hawana tofauti na Mabeberu, lao moja, lakini leo tunakaribisha Ubeberu kwa kupitia mfumo wa kibepari ambao unatuacha tunanyanyasika kwa jina la Uwekezaji.

Then tuwaachie Mabeberu wa ndani watuongoze na wajenge majumba na miji ndani ya nchi yetu na si kupeleka pesa na hazina Toronto exchance kama Barrick wanavyofanya.

Ikiwa Serikali ya CCM inashindwa kutoa hamasa za kuzalisha mali na kuimarisha shughuli za maendeleo, kisa mikono ya mafisadi, ikiwa Serikali ya CCM inashindwa kuleta utiifu na unyoofu wa sheria na kuanuni kisa Mafisadi wana nguvu sana, ikiwa Serikaili ya CCM inakataa hata kuangalia upande wa pili na kubadili mfumo wa katiba ili kuwepo na nguvu mpya ya Uwakilishi na Upinzani ndani ya mfumo wa kisiasa kisa eti Mafisadi hawapendi hilo na si maslahi ya Chama, then kama Chama cha Mapinduzi kimeshikiliwa na Mafisadi, then kila inachokifanya si kwa ajili ya maslahi ya Watanzania au wanaCCM (Chama) bali ni kwa maslahi ya Mafisadi wanaokihodhi chama na kukidhibiti.

Hivyo ama kulikuwa na upeo finyu sana kunielewa au ni hasira za kitoto kukimbilia kudai Mchungaji karukwa akili au kamegewa.

Its all about politics and if they dare to play the dirty game, why should JF and Mchungaji also play dirty game?

But I still stand on my argument, give the job to Lowassa and you will see the turn around, regardless of his filthyness.

As far as I am concerned, there is no one within CCM who is not tainted or will never bow down to preasure from Ufisadi and Mafisadi! They are all the same and to save the party's image they will never dare to reform the party or get rid of Mafisadi led by Lowassa, Rostam, Chenge and others!
Mchungaji,hatimaye nimekuelewa sasa! Tatizo lugha uliotumia imekuwa ngumu kueleweka na wengi waliochangia tangu mwanz😵mbi langu,siku nyingine tumia lugha nyepesi kidogo,vinginevyo utafanya watu wazimie bure lol!
 
Mushi,

Umeshawahi jiuliza kwa nini Lowassa hajafikishwa mahakamani kwa uzembe wa Richmond au kupewa karipio na Kamati Kuu au NEC ya CCM?

Mkuu umesema three quaters ya CCM wanamsikiliza Lowassa ama wana imani naye,na kwamba ni mtu mwenye kufanya kazi kwa bidii,asiyetaka mchezo,hata hivyo alishindwa kusimamia ukweli,na bila kuwa mkweli sifa nyinginezo hazina uzito kwani trust haitakuwepo. Ikasemekana alijiuluzulu ili kukinusuru chama,kama ni kweli utendaji wake haukuwa na mashaka sidhani kama angejiuzulu given sifa zote hizi anazomwagiwa....Kwamba ni kiongozi jasiri,sasa kujiuzulu na kushindwa kusimamia ukweli ni sawa na usaliti kwa wananchi amabao ndio anaowatumikia.Anaposema anakinusuru chama in leu of National interests and security,then sifa nyingine zote zinakuwa hazina maana kwasababu impact ya ufisadi ni kubwa mno,umetembelea bongo umekumbushwa reality,na ndio maisha ya kawaida,kama EL atashindwa kuwa mfano basi hata awe mkali kiasi gani na ufuatiliaji wa aina gani kama wananchi hawatakuwa na imani naye maendeleo yatabakia kuwa hadithi.

Najuwa EL hajafikishwa mahakamani,lakini bado nina haki ya kujuwa what went down,yani ukweli wote kabla sijachukuwa uamuzi wa kusema i trust in him....Sitaki kuingia mtegoni na kucheza kwenye tope....Walichunguzana wenyewe na wote wanajuwa ukweli ila wanatoa habari nusu nusu kila mtu akitoa zile zitakazoonyesha kuwa yeye ndio mkweli na huku wakitumia sababu mbali mbali za wao kutozitoa habari zote,sitoingia mtegoni na kufanya maamuzi kutokana na kauli za kisiasa....Siyo kweli kwamba kwasababu hakufikishwa mahakamani basi hakuhusika,maybe kisiasa...Lakini kwakuwa hakujiuzulu bure,then tunataka tujue ukweli....Hawezi tu kujiuzulu aseme ni kwa kukinusuru chama then na sisi tu conclude kuwa ni mkweli na safi. Pia sikubali kuwa solution ni kuwapa mafisadi nchi....Ni sawa na kumpa shetani mamlaka yote kwasababu malaika wa bwana wameshindwa kazi yao na hivyo kutegemea kuwa shetani atazifanya kazi za malaika hao wa bwana,kwa niaba yao...Mkuu binafsi naamini kuwa maendeleo na ufisadi ni kama mwanga na giza,haviwezi ku coexist,lazima kimoja kitake over,pia kumbuka ufisadi kwa nchi zinazoendelea na zilizoendelea una impact za tofauti na hivyo kutegemea kuwa mafisadi wataleta maendeleo ni ndot ya mchana unless uni convince otherwise.
 
- CCM itaendelea kututawala mpaka siku moja tutakapoamuka usingizini na kuanza ku-think right, otherwise tutaendelea kurushiana maneno yasiyo na faida which is good for CCM anyways,

- Mchungaji siku moja unasema Lowassa ni yuda, halafu siku nyingine unasema In Lowassa you trust, na maneno mengi ambayo hayana faida yoyote kwa masilahi ya taifa zaidi tu ya kujenga chuki katika jamii, taifa letu lina matatizo ambayo wote tumeshindwa kuyatafutia majibu ni tatizo letu wote wananchi wa Tanzania, hakuna alie juu au bora kuliko au mwenye akili kuliko, wote tumekwama, ndio maana ninawaheshimu sana wapiganaji maana angalau wanafanya kwa vitendo.

- Bob, kama unataka kujadili hoja ya IN Edward I Trust, ninakukaribisha anytime, hayo mengine sina time maana hayana faida yoyote kwa taifa.

Kwa kumaliza ni either Lowassa ni Yuda Iskariote, au ni the best ever chagua moja mkuu!, na muwe mnafikiri kabla ya kuandika kwamba tutakaosoma ni wananchi wenye akili ya kutosha sana.

Respect na Later!, I mean nitarudi niktakapopata nafasi tena.

FMEs!
 
FMES,

Watu tuliacha kuwa wanachama na wafuasi wa CCM vlipokuja vyama vingi miaka 18 iliyopita. Aliyebakia king'ang'anizi kuwa CCM ndio jibu ni wewe peke yako!

- Ni afadhali nife nikiwa CCM, kuliko kuwa Chadema ya Zitto na wazee wa chama.

Sasa kwa hili la CCM si wewe uliyedai miezi miwili iliyopita kuwa wapiganaji 11 hawana ubavu kushindana na mafisadi 5000 ndani ya CCM au nawe ulikuwa umeingiwa pepo na mtu kukuibia password yako ulipotoa kauli hiyo?

- nilisema hawawezi kuwashinda kwa kikao kimoja tu cha butiama, it takes a lot of works na commitment na ndipo walipo sasa wapiganaji wako on the right track ndio maana sasa hata Makamba anawaunga mkono.

- Naona unasema nikupigie simu, hapana sina huo muda ili unisaidie kukubali ku-trust in Edward? Bwa! ha! ha!

Respect.

FMEs!
 
- CCM itaendelea kututawala mpaka siku moja tutakapoamuka usingizini na kuanza ku-think right, otherwise tutaendelea kurushiana maneno yasiyo na faida which is good for CCM anyways,

- Mchungaji siku moja unasema Lowassa ni yuda, halafu siku nyingine unasema In Lowassa you trust, na maneno mengi ambayo hayana faida yoyote kwa masilahi ya taifa zaidi tu ya kujenga chuki katika jamii, taifa letu lina matatizo ambayo wote tumeshindwa kuyatafutia majibu ni tatizo letu wote wananchi wa Tanzania, hakuna alie juu au bora kuliko au mwenye akili kuliko, wote tumekwama, ndio maana ninawaheshimu sana wapiganaji maana angalau wanafanya kwa vitendo.

- Bob, kama unataka kujadili hoja ya IN Edward I Trust, ninakukaribisha anytime, hayo mengine sina time maana hayana faida yoyote kwa taifa.

Kwa kumaliza ni either Lowassa ni Yuda Iskariote, au ni the best ever chagua moja mkuu!, na muwe mnafikiri kabla ya kuandika kwamba tutakaosoma ni wananchi wenye akili ya kutosha sana.

Respect na Later!, I mean nitarudi niktakapopata nafasi tena.

FMEs!
Haya ndio maneno mkuu wangu wanijua vizuri kuliko watu wote humu JF... Kesho likinitokea baya ni wewe utakaye peleka habari kwa ndugu na kjamaa zangu haya maswala ya dini sijui yametokea wapi..

Kifupi ni wewe ulotaka kunihukumu mimi kwa sababu sijala Nguruwe..Kwa mtazamo wako watu wote wasiokula nguruwe ni waislaam hivyo yeyote anayebisha usafi wa nguruwe ni lazima awe Muislaam..Na kwa bahati mbaya kweli I'm a muslim lakini haiondoi hoja ya usafi wa nguruwe hata kama ningekuwa Mkristu...
A man must be big enough to admit mistakes, smart enough to profit from them, and strong enough to coreect them..That's me!.

Ya Lowassa mkuu wangu nakubaliana nawe pale unapomkwaa Rev. kwa kumnadi Lowassa..hilo tupo pamoja lakini kumtenganisha Lowassa na CCM wakati ni kiongozi ndani ya chama ati kwa sababu tu kajiuzuru uongozi wa nchi..Hapo mkuu wangu sipo, U miss the point, kwani ktk mtazamo huo mwenye kustahiri sifa anatakiwa kuwa Lowassa. he was a leader strong enough kuachia ngazi, sifa ambayo hakuna waziri mkuu aliyewahi kuifanya.
 
- CCM itaendelea kututawala mpaka siku moja tutakapoamuka usingizini na kuanza ku-think right, otherwise tutaendelea kurushiana maneno yasiyo na faida which is good for CCM anyways,

- Mchungaji siku moja unasema Lowassa ni yuda, halafu siku nyingine unasema In Lowassa you trust, na maneno mengi ambayo hayana faida yoyote kwa masilahi ya taifa zaidi tu ya kujenga chuki katika jamii, taifa letu lina matatizo ambayo wote tumeshindwa kuyatafutia majibu ni tatizo letu wote wananchi wa Tanzania, hakuna alie juu au bora kuliko au mwenye akili kuliko, wote tumekwama, ndio maana ninawaheshimu sana wapiganaji maana angalau wanafanya kwa vitendo.

- Bob, kama unataka kujadili hoja ya IN Edward I Trust, ninakukaribisha anytime, hayo mengine sina time maana hayana faida yoyote kwa taifa.

Kwa kumaliza ni either Lowassa ni Yuda Iskariote, au ni the best ever chagua moja mkuu!, na muwe mnafikiri kabla ya kuandika kwamba tutakaosoma ni wananchi wenye akili ya kutosha sana.

Respect na Later!, I mean nitarudi niktakapopata nafasi tena.

FMEs!
Haya ndio maneno mkuu wangu wanijua vizuri kuliko watu wote humu JF... Kesho likinitokea baya ni wewe utakaye peleka habari kwa ndugu na kjamaa zangu haya maswala ya dini sijui yametokea wapi..

Kifupi ni wewe ulotaka kunihukumu mimi kwa sababu sijala Nguruwe..Kwa mtazamo wako watu wote wasiokula nguruwe ni waislaam hivyo yeyote anayebisha usafi wa nguruwe ni lazima awe Muislaam..Na kwa bahati mbaya kweli I'm a muslim lakini haiondoi hoja ya usafi wa nguruwe hata kama ningekuwa Mkristu...
A man must be big enough to admit mistakes, smart enough to profit from them, and strong enough to coreect them..That's me!.

Ya Lowassa mkuu wangu nakubaliana nawe pale unapomkwaa Rev. kwa kumnadi Lowassa..hilo tupo pamoja lakini kumtenganisha Lowassa na CCM wakati ni kiongozi ndani ya chama ati kwa sababu tu kajiuzuru uongozi wa nchi..Hapo mkuu wangu sipo, U miss the point, kwani ktk mtazamo huo mwenye kustahili sifa hapa anatakiwa kuwa Lowassa, he was a leader strong enough kuachia ngazi, sifa ambayo hakuna waziri mkuu aliyewahi kuifanya. Kuondoka kwa Lowaasa ktk madaraka kimsingi kunaharibu jina la chama kizima ikiwa chama hakitachukua hatua yoyote dhidi yake.
 
Back
Top Bottom