Mchungaji Kishoka,
Nimesoma hii mistari uliyotiririsha hapa na kuirudia tena na tena. Halafu nikatafakari mambo unayoyaandika hapa siku zote, na hat uliyopata kuyaandika kuhusu huyuhuyu mmasai/mmeru nikakusikitikia sana na zaidi nikaisikitikia nchi yangu Tanganyika.
Naamini sasa kwamba ulipojiita kishoka hukufanya hivyo kwa bahati mbaya, yaani nimewakumbuka vishoka wanaotuunganishia umeme huku mitaani, nikasema kwakuwa jina umejipa mwenyewe sasa umeamua kujidhihirisha sura yako halisi.
Pamoja na yote unayosema, mafisadi mtawatumikia nyie msiokuwa na uzalendo halisi na nchi yenu. Hata ukimpaka mafuta na vikorombwezo vyoote madukani, fisadi lowasa hasafishiki!!!!
Mwita wa Maranya,
Je uliponisoma ulinielewa vizuri? Kama umeshanisoma miaka mingi ya kutosha na kuelewa weledi au siha ya Mchungaji, kimekushinda nini kunielewa na kufikia timilisho kuwa nami ni sawa na vishoka wa Tanesco au Dawasco?
Unajua nakumbuka Kitila Mkumbo aliposema kuwa kina Mwakyembe hawakufuata haki na kanuni kumsulubu Lowassa, watu tulifumbia macho ukweli wa kufuata haki na kanuni na kusema Kitila kapewa chochote na hatukusimamia haki.
Wakati Mwakyembe alipotukanana na Rostam kuhumu umeme wa nguvu za upepo, watu wakadai ah, hakuna kosa kwa Mwakyembe kuwa na kampuni ya umeme alimradi kitendo chake ambaco dhahiri ilikuwa ni kukiukwa miiko na kanuni tukakifanya ni sahihi kwa kuwa yeye ni "mkombozi".
Sasa leo "mkombozi na mpiganaji" akivunja miiko na kukiuka kanuni tunadai Ruksa, lakini tusiyempenda akifanya hilo hilo tunalia apelekwe kwa Pilato asulubbiwe, je haki iko wapi? je lini tunaweza kujenga jamii na Taifa lenye kufuata kanuni, lenye utu na lenye kusimamia haki?
Nimesema tena kwa kujikosoa kuwa hata pamoja na hasira zangu na maudhiko yangu hata chuku dhidi ya Lowassa nilizozisema kwenye Deconstructing Lowassa, bado kuna vitu ambavyo Lowassa alivvyokuwa akifanya kiutendaji kama uchapa kazi, ufuatiliaji na ile uwezo wa kuwa na nguvu za kidola na kufanya watu wachacharike bado anao na ni haiba yake.
Ndio maana nikasema, kuna haja ya kuwa na sacrifice na compromise kutoka kwetu, maana kati kundi na chama alichoko Lowassa, hakuna mwenye nguvu au uwezo wa kuongoza kiutendaji na hata hili la vita vya Ufisadi ni gumu kwao.
Lakini tabia yetu hapa JF ni kutaka tubainishiwe kila kitu, ndio maana umesikia watu wakilialia "aah Mchungaji mbona unatuchanganya, tukueleweje, sasa tufuate lipi unlosema" nami nimewajibu kwa kusema kuwa wao ni watu wazima wenye uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi bila kumtegemea Mchungaji.
Nimewaambia watmie busara zao wanapopewa Kuku na Yai wapigie kura kimoja wapo, lakini wengi humu ndani, wanadai eti wanatakak kujua ni kipi kilitangulia, Kuku au Yai! Ndio maana mko njia panda hamuelewi ninachokisema!