- Mkuu again wapiganaji 11 tu, hawawezi kufanya yote haya uliyoyasema in one year au hata five years, cha muhimu mimi na wewe tujitahidi kuwasaidia na kuwapa support hawa wapiganaji badala ya kuwabeza wakati ukweli ni kwamba wao wako front na sisi tuko nao na majina ya bandia, tuwasaidie na tusaidane nao kulisaidia taifa letu, taifa ni letu sio lao hawa wapiganaji 11 tu, unayoyasema wewe na anayoyasema Mwanakijiji ni maneno tu, yanahitaji hawa wapiganaji 11 kuyafanyia kazi huko bungeni as they always do, ninarudia kwamba mafisadi hawawezi kupoteza millions of money kuhonga wajumbe wa NEC kuwaondoa wapiganaji wasio effective na ambao wala hawawasumbui, haya ni mawazo mufilisi na ni ya kuyaogopa kama ukoma!
Again, please tuwape support hawa wapiganaji wao wanatuhitaji na sisi tunawahitaji.
Respect.
FMEs!
Jemedari FMES,
Mara nyingine huwa unaniacha hoi. Sasa kama uwiano unaousema wa Wapiganaji 11 dhidi ya mafisadi 5000 na bado unadai CCM ni safi, unategemea ni lini hao Wapiganaji wataweza kushika hatamu?
Hiyo kauli yako niliyonukuu hapo juu, mshikaji wako Kitila Mkumbo akiiona, atakupa uanachama wa CHADEMA wa maisha bure... kwi kwi kwi!
Kama kupigana vita dhidi ya Uhujumu vilianza na Sokoine, tukashindwa kubadilisha mfumo wa Kisiasa, Sheria na Kiuchumi ili kupunguza kasi ya Wahujumu, utatuambiaje leo tuikumbatie CCM kwa ajili ya hao 11 ambao wanapigana vita butu?
Je huoni kama Wapiganaji wangewekeza nguvu zao kumpa Mtanzania nguvu za kujitegemea kwa kupeleka maendeleo ya kweli kwa wananchi na hivyo wananchi kuwa na uwezo wa kuwa huru na wenye kujitegemea bila kumtegemea mtu au kuhongeka kirahisi, huoni hii vita dhidi ya ufisadi ingekuwa rahisi?
Leo Mtanzania akijua kuwa ana chakula cha kutosha na cha akiba nzuri, ana ajira yenye kipato kinachokidhi maisha na mahitaji yake, Watoto wake wanakwenda shule na kuelimika na si kutaabika, akiugua anajua akienda hospitali au zahanati yoyote atapata matibabu na hahitaji kupelekwa India, akilima mazao, ana uhakika kuwa ujuzi aliofundishwa, utampa mazao ya kutosha na atapata soko kabambe na si kuhangaika kutafuta mnunuzi, huoni kuwa Mtanzania huyu ni rahisi kwake kupiga kura ya hapana kwa yule ambaye hafai?
Ni mara ngapi humu na hata kule BCS nimesema kuwa kwa Tanzania kupata maendeleo ya kweli na kushinda Ujinga, Umasikini, Maradhi na Ufisadi ni lazima Mtanzania awe huru na mwenye kujitegemea na kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi bila kulazimishwa au kulaghaiwa na kofia, fulana na ubwabwa?
Hitimisho langu ni hili, mtazamo wetu katika wajibu wa hao "wapiganaji" unatofautiana sana na si ajabu kuwa hatuoni wanachokifanya kwa mtazamo mmoja.
Kwangu mimi, mpiganaji wa kutetea haki za Mwananchi na kulinda nchi yake, hachagui vita au adui wa kupigana ili kushinda kinachomdhoofisha. Kwangu mimi vita ya kweli ni ya kupigana na mfumo mzima wa Utawala usio makini, fanisi, uliojaa uzembe, wivu, ufujaji, kutokujali, wenye kauli kibao kama za Ari, Kasi na Nguvu Mpya na hata sasa Kilimo Kwanza lakini hakuna msukumo wa kufanya kauli hizo ziwe vitendo.
Sasa naelewa kuwa mwenzangu mtazamo na matarajio yako kwa Wapiganaji ni kupigana vita moja, ya Ufisadi na zaidi dhidi ya kikundi fulani ambacho hukubaliani nacho kwa sababu fulani.
Hivyo basi, tofauti yetu ni kuwa mimi naangalia kwa upana mstakabali wa Taifa zima kupata maendeleo, kwa kutumia nguzo zile nne za Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora ili kuondokana na Umasikini, Ujinga, Maradhi, Unyonge na Uonevu kwa kutumia Juhudi na Maarifa yanayoambatana na Uwajibikaji, Ufanisi, Unyenyekevu, Busara na Hekima katika kujenga Taifa lenye Umoja wa Kweli, Mshikamano Thabiti na Utulivu wa Roho.
Je weye Rafiki yangu, mtazamo wako ni upi? Je ni ule ule wa kusema ni CCM na CCM pekee, kwa manufaa ya CCM kwanza na ndipo Tanzania tufuate?
Sasa kama tunaimba "Msalaba Mbele, Dunia Nyuma" kanisani na sisi tunaolilia Mabadiliko na vita ya Kweli tunaimba "Tanzania Mbele, Chama Nyuma" weye unaimba "CCM mbele, Tanzania Mwisho"?