Vyama vyote vya Siasa Tanzania utapeli mtupu. CHADEMA baada ya kutupa matumaini Watanzania kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuibua ufisadi mbali mbali na hivyo kujenga matumaini kwamba labda wataibuka na viti vingi vya Bunge 2010, sasa wameanza kusambaratika na kukiachia Chama cha Mafisadi njia nyeupe ya kuzoa viti vingi vya Bunge 2010. Kweli Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kwa mtaji huu chama cha mafisadi kitabaki madarakani milele na kuendelea kuifisadi nchi yetu mpaka ifilisike kabisa. 🙁
Kweli inahuzunisha sana, ukiangalia growith curve ya hivi vyama na rate yake inahuzunsiha sana.
Slaa anasema waliondoka akina Kaborou, hata yeye na Mbowe wakiondoka leo Chadema itakuwepo tu.
Sijajua kama ameevaluate ni kwa namna gani hii migogoro inaathiri upinzani wote na kuwajenga hawa mafisadi.Sijajua kama ni busara kamgogoro haka washindwe kutatua watu ambao tunaamini wanaweza kushika dola!
Kwa migogoro hii Slaa watu wanadharau Upinzani woote , sio chadema tu, wanachama wapya wanaogopa kuingia at its worse kwenye chaguzi watu hawapigi kura na tafiti zinaonyesha wasiopiga kura ni wengi na ndio wenye uwezo wa kubadilisha mambo.
Siamini kama Slaa amegeuka Makamba kiasi hiki, kingeathiri nini ukakaa kimya, mtafute huyo msaidizi wako (for God sake), mjadili muyamalize, pia angalia ni wapi umekosea wewe, you are mediator na kwa cheo chako ungefanyika msaada sana wa kuwaunganisha Mbowe na Zitto.Kinachoonekana hapa ni umechagua side na maamuzi mengi msaidizi wako aidha hayajui au unamruka!
Msiwafanya binadamu kama mbwa you can say and do anthing without reaction, hali kadhalika ama Zitto ana makosa naye asiwafanye nyie mbwa wa kuwafanya chcochote.we need you guys to resolve your issues which are stink right now,however, the authors of all these messy are known