Ili kuvunja circle ya umasikini tuliyo nayo watu weusi ni muda sasa tuzingatie "FAMILY BUSINESS"

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,031
12,356
Ili kuvunja poverty circle tuliyo nayo ni muda sasa kuanzisha na kuzingatia miradi au biashara za kifamilia.

Tujifunze kwa hawa ndugu zetu watu weupe.

Tusione ufahari mradi, kilimo au biashara kufahamiwa na mtu mmoja tu kwenye familia akifa yeye na yenyewe inakufa naye unabaki mgogoro wa mali kila mtu akitaka chake.

Dunia sasa inabadilika ni vyema nasi kubadilika wanafamilia na wazazi wasione sifa kuwa fichia white watoto wao na kuwafukuza ili wakabangaize hovyo kwenye umasikini kwa kuanza kwenye zero.

Ni muda sasa ujuzi kuanza kuamishiana tukiwa hai iwe ujuzi wa biashara, kilimo, kazi nyingine yoyote kutoka kwa baba/mama kwenda kwa mtoto naye anafanya hivyo kwa watoto wake nao wanafanya hivyo kwa watoto wao inakuwa muendelezo.

Kupambana sasa na umasikini inabidi tulinde hata kile kidogo tulicho nacho na kukikuza ili kiongezeke ukubwa.

Tusione mila na tamaduni za wahindi na waarabu kuhusu mali ni za hovyo bali tuzione ni bora kabisa kuigwa katika kuvunja umasikini unao tuzunguka.

Tuamke sasa.
 
Mzazi unapokwenda kujumua mzigo wa dukani kuwa karibu na mwanao/wanao mpe knowledge.

Mzazi unapofunga mahesabu kuwa karibu na familia funga siku za mwanzo wewe baada ya hapo anza kuwa simamia wanao wafunge mbele yako.

Kama kwenye kilimo kuwa karibu na familia yale unayo fanya hakikisha kila kitu mtoto anafahamu A-Z wakati mwingine mwachie usimamizi wewe ukiwa pembeni ukifuatilia.
 
Tatizo ni kwamba unakuta huko kwenye hiyo FAMILY kuna WACHAWI na WAGANGA WA KIENYEJI. Bila kusahau WENYE HUSDA na VIJICHO kama bundi.

Hata ukitaka kuwasaidia unashangaa WANAKUROGA na Kukutumia MASHETANI. Wanakutengenezea MITEGO.

Achana kabisa na hawa wanaitwa NDUGU ni NYOKA. Kama una biashara yako au kazi yako kaa nao mbali. FUNGA NA VIOO. TINTED.

Pakikucha wasalimie KATA KUSHOTO.
 
Ni kuomba Mungu sana akupe watoto wema na waadilifu.
Tuliowahi kufanya kazi kwenye kampuni za familia tulikutana na mengi, wakati mwingine unaionea uchungu mali ya boss kuliko mwanae.
Mzazi unajukumu no.1 la kufanya mtoto awe bora kwa kiwango kinachopaswa kuwa Mungu hausiki bali malezi ya mzazi ndio yanahusika.

Namna mtoto anavyolelewa kuna asilimia kubwa kukua hivyo hivyo.
 
Na watoto wenyewe ndio hawa wanaovaa MILEGEZO, hata ukimuuliza MASWALI YA UFAHAMU hajui chochote.

Anajua tu SIMBA na YANGA na MAYELE. Kichwa kimejaa ukurutu.

Ukimpa biashara yako anaimaliza ndani ya mwaka mmoja. Anatumbua hela na kwenda kula na MADEM. Ati MADEM!! Na amevaa mlegezo.

Ukizaa hakikisha unazaa watoto wenye akili timamu. Ni ngumu sana kupata mtoto timamu. WENGI NI MAZOMBI.

Yale MACHANJO YALE na MADAWA UCHWARA YA UZAZI. Taifa linazalisha MAZOMBI wanaotembea wima.

Hawawezi kuhoji, hawawezi kuuliza, hawawezi kufikiri, wanachojua ni SIMBA na YANGA.
 
Back
Top Bottom