Waafrika tunaupenda umasikini na kuona ni ufahari. Ubinafsi unatuangamiza

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,017
12,308
Waafrika sisi watu watu weusi neno umasikini kwetu ni neno la faraja na utajiri ni chukizo masikioni mwetu.

Je, ni wazazi wangapi au familia ngapi za watu weusi zinafanya hivi? ⏬ Au ndio tuna andaa tabaka la kimasikini katika jamii yetu kila siku?

[IMG alt="lukesam"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/275/275627.jpg?1500562796[/IMG]

lukesam

JF-Expert Member​

"Hatuwezi kuwa matajiri wote kama Bakhresa lakini ni vizuri sisi watu weusi tukajifunza kwao na jamii nyingine kama za wahindi.

Inawezekana wazee wetu walishakosea huko nyuma ila sasa ni muda wa kujisahihisha na kuwa bora kuliko wao.

Wazazi wa kiafrika wana tabia za kichoyo na kibinafsi, hata akiwa na duka lake hataki mtoto wake auze au ajue jinsi ya kuendesha biashara, anaogopa kuibiwa hata kijana wake hamuamini.

Watoto wetu wanahangaika sana kutafuta ajira kwasababu walienda shule kusomea taaluma za ndoto zao bila kujua baada ya kumaliza wataenda kufanyia kazi wapi. Tofauti na sisi, hawa wenye asili ya kihindi na matajiri wengine, watoto wao wanaenda shule kusomea taaluma ambazo wanajua wakitoka hapo wataenda kupata ajira kwenye miradi ya familia.

Tuweke nguvu katika kuanzisha miradi ya kifamilia, familia za kitanzania tuache ubinafsi. Ndio maana hata ukimshauri mtu aandike wosia au agawe mali zake akiwa hai anakushangaa, mzee kabisa anataka afe akiwa anamiliki mali zake zote.

Suluhisho la kusomea uhasibu au uchumi na kuishia kuwa muuza chipsi au bodaboda ni kuanzisha miradi ya kifamilia. Binafsi naona hii itapunguza sana tatizo la ajira na hali ya umaskini katika familia zetu.

Inaumiza sana kupoteza miaka mingi shuleni na kuishia kufanya kazi ambazo hata hazihitaji elimu".

Tazama hapa nchini watoto wanakwenda shule saa 12 mpaka 12 kufika nyumbani saa 1-2 mpaka 3 wengine. ni muda ngani huyu mtoto anapata hata muda wa kupata maarifa ya kujiendeleza tofauti na maarifa karirishi ya shuleni ?

Watoto wanasoma kuanzia Jumatatu mpaka Jumapili kwa ajili ya kufaulu tu mitihani ya kukariri hakuna kingine. Huu ni upuuzi.

Ni wazazi wangapi wapo tayari kuwafundisha watoto wao kilimo na usimamizi bora na kuwaacha kuongoza ?

Ni wazazi wangapi wapo tayari kutoa mgawanyo wa mali za familia wakiwa hai kama wahindi, waarabu na wao wakibaki kama wasimamizi na kuwaacha watoto wazalishe ?

Ni wazazi wangapi wapo tayari wawafundishe ujuzi watoto wao sehemu za kazi wanazo fanyia au ndio wapo tayari kulipa ada ya tuition watoto wakeshe huko kukaririshwa ?

Ni wazazi wangapi wapo tayari kuweka mali zao wazi familia nzima ijue na kujenga utaratibu wa kuchagua kiongozi wa biashara kila baada ya muda fulani au mali zake ni zake pekee hata mke au mme wala watoto hawajui mpaka kifo na nyingine kupotekea bank ?

Ni wazazi wangapi biashara zao na pesa zao zipo wazi kwa familia ?

Ni wazazi wangapi biashara zao zinaongozwa na watoto wao au baada ya kukua atoke kwako aende kusiko julikana akaanze zero na kudunduliza kama masikini kujitafutia na yeye chake hivi ndio tunaona maisha ?

Tumewahi jiuliza kwa nini utajiri wa taifa letu umeshikiliwa na wahindi na waarabu ? Of course ni Watanzania na wa wala siwachukii lakini kwa nini hatujiulizi matajiri wakubwa nchi hii ni kutoka races hizo na sio weusi ?
 
Sisi kwetu umasikini ni ufahari bila shaka maana utajiri tunaona sio wa kwetu.
 
Kwanza matajiri hamtauona ufalme wa Mungu, hela zenyewe za firimasoni umewatoa ndugu zako kafara.
 
"Tuliwakataa, tuliwatenga na kuwaengua kabisa WATU WEUSI katika mchakato wa maendeleo ya nchi na ujenzi wake kwa sababu HAWANA AKILI NZURI, endapo kama tungewajumuisha basi wangetuharibia mambo yetu mazuri yaliyopo Afrika ya Kusini leo hii."
Na Pieter W. Botha, Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini enzi za Utawala wa Ubaguzi wa rangi.
 
"Tuliwakataa, tuliwatenga na kuwaengua kabisa WATU WEUSI katika mchakato wa maendeleo ya nchi na ujenzi wake kwa sababu HAWANA AKILI NZURI, endapo kama tungewajumuisha basi wangetuharibia mambo yetu mazuri yaliyopo Afrika ya Kusini leo hii."
Na Pieter W. Botha, Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini enzi za Utawala wa Ubaguzi wa rangi.
Eeeeeh!
 
Back
Top Bottom