Je, Siasa ni Ajira? Ni Kazi ya Mshahara au ni Kazi ya Kujitolea? Kwa Umasikini Wetu Huu Uliotopea, Ni Haki Kulipa Ruzuku kwa Vyama vya Siasa?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
51,125
115,566
Wanabodi,

Wiki iliyopita, nimehudhuria Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa kujadili miswada mitatu ya Sheria ya Uchaguzi, Sheria ya Vyama vya Siasa, na Sheria ya Tume ya Uchaguzi, Ulifunguliwa na Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, na kufungwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dotto Biteko jijini Dar es Salaam.

View: https://youtu.be/PBpjDhH2XiA?si=Tw3ZKmjI-AFC4rPW

Naomba nianze na pongezi kwa watu au taasisi tatu zifuatazo, kwanza kwa Rais wa JMT, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuunda kikosi kazi kilichopelekea mabadiliko haya ya sheria hizi. Pili kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kwa kutualika watu kama akina sisi ambao sio viongozi wa vyama vya siasa, lakini ni wadau muhimu wa siasa za nchi yetu, na kusema ukweli nilichoshuhudia kwenye mikutano hii, kiukweli kabisa, kwenye masuala nyeti ya kisheria kama haya, vyama vyetu vya siasa ni kama hakuna kitu kabisa!, msaada mkubwa na michango mikubwa ya maboresho ya sheria hizo, umetoka kwa wadau ambao sio vyama vya siasa, ukiwemo mchango muhimu kutoka kwa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, Tanganyika Law Society, TLS, uliowakilishwa Wakili Msomi, Alex Mgongolwa.

Pongezi zangu za tatu, ziende kwa vyama vya siasa na haswa kwa chama kikuu cha upinzania huku Bara, kwa kuhudhuria mkutano huu baada ya maridhiano na kukubaliana kugawana nusu mkate! baada ya maridhiano na CCM, na kukubaliana kugawana kiti kinachoitwa “Nusu Mkate”, kwa sababu Baada ya kuususia ule Mkutano wa kwanza wa Dodoma, nikawaomba msisuse, Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.

Kususa kule kukawa na faida kwa Chadema, kukazaa matunda ya maridhiano, lakini kususia Mkutano wa pili wa JNICC Dar es Salaam, hakukuwa na manufaa yoyote, hivyo mkutano huu wa tatu, nikawatumia Chadema ombi mahsus “Nawaombeni sana, msiendelee kususa na kuzira, Please, hata kama mna hoja, njooni mezani, zileteni mezani, tukae pamoja, tuzijadili pamoja, tukiwa wamoja, ili twende pamoja!. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu, kuna vitu, ili ufanikiwe, vinahitaji a team spirit na team work, hivyo you have to be a team player and it's only if you are together, you can!” Chadema wakalipokea ombi hili, wakaja mezani.

Kwenye mikutano yote miwili, mimi nilibahatika kupata fursa ya kuchangia maoni na mawazo yangu, na siku zote nimekuwa nikichangia kuhusu lile ambalo kwangu naliona ndilo kubwa kuliko na muhimu kuliko hata sheria zenyewe, ni hitaji la mabadiliko madogo ya katiba kwanza, ili kuondoa ubatili fulani kwenye katiba, unaonyima haki ya kuchagua na kuchaguliwa, kisha ndipo tuje kwenye sheria.

Hili la ubatili wa katiba, kwa vile ni la kisheria, masikini vyama havilioni, tunakwenda kubadili sheria ya zamani yenye ubatili, na kwasababu, ubatili huo, uko kwenye katiba, na hakuna mabadiliko ya katiba, hivyo tunakwenda tena kutunga sheria nyingine mpya yenye ubatili!. Sijui kwanini hili la ubatili wa katiba wenzwtu hawalioni.

Mchangiaji mmoja akapendekeza tutenge asilimia 10 ya bajeti ya taifa, ilipwe kama ruzuku kwa vyama vyote vya siasa nchini!, mimi katika mchango wangu, hili nililipinga

“Ndugu zangu wa vyama vya siasa, wenzetu nchi za Ulaya, upngozi wa chama cha siasa, ni utumishi wa umma wa kujitolea, upmgozi wa chama sio ajira, vyama vya siasa tangu TANU havikuwa vinapewa ruzuku, vilikuwa 'funded' na wapenzi na wanachama, ifikie mahali tuingie huruma na imani Watanzania wengi ambao wanaishi kwenye lindi la umaskini uliotopea, wetu, kwanini tuendelee kuvipa vyama vya siasa ruzuku kwa kuwalipa watu wazima bukheri wa afya, wenye vioungo vyao timamu, tuwalipe kwa kupiga domo?”

Hili la kupinga ruzuku, sikuanza nalo leo, enzi za Magufuli, niliandika "asiyefanya kazi na asile". Jee siasa nayo ni kazi ya kustahili ujira wa mshahara kwa jina la ruzuku kwa vyama vya siasa? . Ruzuku hii iendelee kuwepo watu waendelee kuitafuna au ifutwe? .

Japo sijafanya utafiti wa ni nchi ngapi zinagawa ruzuku kwa vyama vya siasa lakini kwa nchi masikini kama Tanzania , serikali inayowajibika kwa watu wake na kuheshimu rasilimali kiduchu za taifa, haiwezi fedha zinazokamuliwa kama kodi kwa wananchi masikini wa kutupwa wanaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu fedha hizo zinakuja kugawiwa bure kama ruzuku kwa vyama vya siasa, watu wazima wenye nguvu zao, na vioungo vyao timamu, wanalipwa wazitafune kwa kazi ya kupiga domo! .

Katika kuunga mkono juhudi za rais Magufuli za kubana matumizi ikiwemo kupunguza safari za nje, kuwaengua watumishi hewa, kufanya tumbua tumbua majipu ya ufisadi, namshauri rais wetu aziangazie ruzuku kwa vyama vya siasa.

Enzi za Nyerere kulitolewa ruzuku ya mbolea, mbegu bora na pembejeo za kilimo ili kuimarisha uzalishaji mali, sasa ruzuku hizo zimefutwa na badala yake mijitu mizima isiyo na matatizo yoyote, au changamoto za kiafya, ndio inakaa bure kutafuna ruzuku ya bure bure huku masikini wakitaabika!.

Asiyefanya kazi na asile! . Siasa sio kazi ya mshahara bali ni kazi ya kujitolea, ruzuku kwa vyama vya siasa ni ufisadi, ifutwe?.

Paskali
 
Tena hao waliopendekeza 10% ni kama wamependekeza kidogo. Kama Kuna pesa Hadi za kulipa wenza wa viongozi wastaafu, hizo hela za mabwege unaziicha Ili iweje?
 
Kwa Africa Siasa ni ajira inayootwa na wengi. Wanasiasa wa Africa ni kama wakoloni, wanaposhika madaraka hukusanya na kujilimbikizia fedha baada ya muda fedha hizo upelekwa kwenye mabeki ya ughaibuni na kuacha ombwe kubwa la ukosefu wa fedha ambazo zingetumika kuendeshea idara mbalimbali. Hii inatokana nakwamba, wanasiasa wengi wametokea kwenye Koo zenye umasikini wa kutupwa.

Kwa Ulaya Siasa sio ishu, sababu wanasiasa wa Ulaya wanaongozwa na wataalam katika kufanya maamuzi mbalimbali.
Africa ukitaka mafanikio ya haraka ingia kwenye Siasa, sababu Siasa itakuwezesha Moja Kwa Moja kufanya biashara na serikari.
SIO NIMEENDA NJE YA MADA
 
Siasa siyo ajira Ila Kuna kikundi Cha watu wamegeuza ajira baada ya kuona jinsi watu walivyonufaika kwenye siasa.
Kama ulivyosema wenzetu ulaya ni kazi ya kujitolea Ila huku wamegeuza ajira.
Kuhusu mgombea binafsi tunahitaji watu wa kupush maana hukumu ilishatolewa lakini utetezi wa serikali ukawa limeingizwa kwenye rasimu ya katiba wakati serikali haina Nia ya kutengeneza katiba mpya.
 
Wanabodi,

Wiki iliyopita, nimehudhuria Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa kujadili miswada mitatu ya Sheria ya Uchaguzi, Sheria ya Vyama vya Siasa, na Sheria ya Tume ya Uchaguzi, Ulifunguliwa na Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, na kufungwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dotto Biteko jijini Dar es Salaam.

View: https://youtu.be/PBpjDhH2XiA?si=Tw3ZKmjI-AFC4rPW

Naomba nianze na pongezi kwa watu au taasisi tatu zifuatazo, kwanza kwa Rais wa JMT, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuunda kikosi kazi kilichopelekea mabadiliko haya ya sheria hizi. Pili kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kwa kutualika watu kama akina sisi ambao sio viongozi wa vyama vya siasa, lakini ni wadau muhimu wa siasa za nchi yetu, na kusema ukweli nilichoshuhudia kwenye mikutano hii, kiukweli kabisa, kwenye masuala nyeti ya kisheria kama haya, vyama vyetu vya siasa ni kama hakuna kitu kabisa!, msaada mkubwa na michango mikubwa ya maboresho ya sheria hizo, umetoka kwa wadau ambao sio vyama vya siasa, ukiwemo mchango muhimu kutoka kwa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, Tanganyika Law Society, TLS, uliowakilishwa Wakili Msomi, Alex Mgongolwa.

Pongezi zangu za tatu, ziende kwa vyama vya siasa na haswa kwa chama kikuu cha upinzania huku Bara, kwa kuhudhuria mkutano huu baada ya maridhiano na kukubaliana kugawana nusu mkate! baada ya maridhiano na CCM, na kukubaliana kugawana kiti kinachoitwa “Nusu Mkate”, kwa sababu Baada ya kuususia ule Mkutano wa kwanza wa Dodoma, nikawaomba msisuse, Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.

Kususa kule kukawa na faida kwa Chadema, kukazaa matunda ya maridhiano, lakini kususia Mkutano wa pili wa JNICC Dar es Salaam, hakukuwa na manufaa yoyote, hivyo mkutano huu wa tatu, nikawatumia Chadema ombi mahsus “Nawaombeni sana, msiendelee kususa na kuzira, Please, hata kama mna hoja, njooni mezani, zileteni mezani, tukae pamoja, tuzijadili pamoja, tukiwa wamoja, ili twende pamoja!. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu, kuna vitu, ili ufanikiwe, vinahitaji a team spirit na team work, hivyo you have to be a team player and it's only if you are together, you can!” Chadema wakalipokea ombi hili, wakaja mezani.

Kwenye mikutano yote miwili, mimi nilibahatika kupata fursa ya kuchangia maoni na mawazo yangu, na siku zote nimekuwa nikichangia kuhusu lile ambalo kwangu naliona ndilo kubwa kuliko na muhimu kuliko hata sheria zenyewe, ni hitaji la mabadiliko madogo ya katiba kwanza, ili kuondoa ubatili fulani kwenye katiba, unaonyima haki ya kuchagua na kuchaguliwa, kisha ndipo tuje kwenye sheria.

Hili la ubatili wa katiba, kwa vile ni la kisheria, masikini vyama havilioni, tunakwenda kubadili sheria ya zamani yenye ubatili, na kwasababu, ubatili huo, uko kwenye katiba, na hakuna mabadiliko ya katiba, hivyo tunakwenda tena kutunga sheria nyingine mpya yenye ubatili!. Sijui kwanini hili la ubatili wa katiba wenzwtu hawalioni.

Mchangiaji mmoja akapendekeza tutenge asilimia 10 ya bajeti ya taifa, ilipwe kama ruzuku kwa vyama vyote vya siasa nchini!, mimi katika mchango wangu, hili nililipinga

“Ndugu zangu wa vyama vya siasa, wenzetu nchi za Ulaya, upngozi wa chama cha siasa, ni utumishi wa umma wa kujitolea, upmgozi wa chama sio ajira, vyama vya siasa tangu TANU havikuwa vinapewa ruzuku, vilikuwa 'funded' na wapenzi na wanachama, ifikie mahali tuingie huruma na imani Watanzania wengi ambao wanaishi kwenye lindi la umaskini uliotopea, wetu, kwanini tuendelee kuvipa vyama vya siasa ruzuku kwa kuwalipa watu wazima bukheri wa afya, wenye vioungo vyao timamu, tuwalipe kwa kupiga domo?”

Hili la kupinga ruzuku, sikuanza nalo leo, enzi za Magufuli, niliandika "asiyefanya kazi na asile". Jee siasa nayo ni kazi ya kustahili ujira wa mshahara kwa jina la ruzuku kwa vyama vya siasa? . Ruzuku hii iendelee kuwepo watu waendelee kuitafuna au ifutwe? .

Japo sijafanya utafiti wa ni nchi ngapi zinagawa ruzuku kwa vyama vya siasa lakini kwa nchi masikini kama Tanzania , serikali inayowajibika kwa watu wake na kuheshimu rasilimali kiduchu za taifa, haiwezi fedha zinazokamuliwa kama kodi kwa wananchi masikini wa kutupwa wanaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu fedha hizo zinakuja kugawiwa bure kama ruzuku kwa vyama vya siasa, watu wazima wenye nguvu zao, na vioungo vyao timamu, wanalipwa wazitafune kwa kazi ya kupiga domo! .

Katika kuunga mkono juhudi za rais Magufuli za kubana matumizi ikiwemo kupunguza safari za nje, kuwaengua watumishi hewa, kufanya tumbua tumbua majipu ya ufisadi, namshauri rais wetu aziangazie ruzuku kwa vyama vya siasa.

Enzi za Nyerere kulitolewa ruzuku ya mbolea, mbegu bora na pembejeo za kilimo ili kuimarisha uzalishaji mali, sasa ruzuku hizo zimefutwa na badala yake mijitu mizima isiyo na matatizo yoyote, au changamoto za kiafya, ndio inakaa bure kutafuna ruzuku ya bure bure huku masikini wakitaabika!.

Asiyefanya kazi na asile! . Siasa sio kazi ya mshahara bali ni kazi ya kujitolea, ruzuku kwa vyama vya siasa ni ufisadi, ifutwe?.

Paskali

Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia. Tuendelee kuwapa ruzuku tu kinyume cha hapo tutatawaliwa na watu wasio na uwezo wa uongozi bali wana fedha.
 
Hiyo ruzuku ifutwe tu kwa vyama vyote!
Katiba ifute uwepo wa Wabunge wa viti maalum na wale wa kuteuliwa na Rais! Maana wanatuongezea tu walipa kodi gharama za kuwahudimia.

Katiba iondoe kioengele cha kuwaruhusu Wabunge kutoka Zanzibar, kushiriki kwenye vikao vya Bunge la Tanganyika, huku tayari wenyewe wana Bunge lao (Baraza la Wawakilishi)

Kiundwe chombo maalum (Bodi ya mishahara) kwa ajili ya kusimamia mishahara na posho za watumishi wote wa umma mfano Wabunge na wale wafanyakazi wote wa mashirika ya umma na taasisi zote za serikali.
 
Wanabodi,

Wiki iliyopita, nimehudhuria Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa kujadili miswada mitatu ya Sheria ya Uchaguzi, Sheria ya Vyama vya Siasa, na Sheria ya Tume ya Uchaguzi, Ulifunguliwa na Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, na kufungwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dotto Biteko jijini Dar es Salaam.

View: https://youtu.be/PBpjDhH2XiA?si=Tw3ZKmjI-AFC4rPW

Naomba nianze na pongezi kwa watu au taasisi tatu zifuatazo, kwanza kwa Rais wa JMT, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuunda kikosi kazi kilichopelekea mabadiliko haya ya sheria hizi. Pili kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kwa kutualika watu kama akina sisi ambao sio viongozi wa vyama vya siasa, lakini ni wadau muhimu wa siasa za nchi yetu, na kusema ukweli nilichoshuhudia kwenye mikutano hii, kiukweli kabisa, kwenye masuala nyeti ya kisheria kama haya, vyama vyetu vya siasa ni kama hakuna kitu kabisa!, msaada mkubwa na michango mikubwa ya maboresho ya sheria hizo, umetoka kwa wadau ambao sio vyama vya siasa, ukiwemo mchango muhimu kutoka kwa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, Tanganyika Law Society, TLS, uliowakilishwa Wakili Msomi, Alex Mgongolwa.

Pongezi zangu za tatu, ziende kwa vyama vya siasa na haswa kwa chama kikuu cha upinzania huku Bara, kwa kuhudhuria mkutano huu baada ya maridhiano na kukubaliana kugawana nusu mkate! baada ya maridhiano na CCM, na kukubaliana kugawana kiti kinachoitwa “Nusu Mkate”, kwa sababu Baada ya kuususia ule Mkutano wa kwanza wa Dodoma, nikawaomba msisuse, Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.

Kususa kule kukawa na faida kwa Chadema, kukazaa matunda ya maridhiano, lakini kususia Mkutano wa pili wa JNICC Dar es Salaam, hakukuwa na manufaa yoyote, hivyo mkutano huu wa tatu, nikawatumia Chadema ombi mahsus “Nawaombeni sana, msiendelee kususa na kuzira, Please, hata kama mna hoja, njooni mezani, zileteni mezani, tukae pamoja, tuzijadili pamoja, tukiwa wamoja, ili twende pamoja!. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu, kuna vitu, ili ufanikiwe, vinahitaji a team spirit na team work, hivyo you have to be a team player and it's only if you are together, you can!” Chadema wakalipokea ombi hili, wakaja mezani.

Kwenye mikutano yote miwili, mimi nilibahatika kupata fursa ya kuchangia maoni na mawazo yangu, na siku zote nimekuwa nikichangia kuhusu lile ambalo kwangu naliona ndilo kubwa kuliko na muhimu kuliko hata sheria zenyewe, ni hitaji la mabadiliko madogo ya katiba kwanza, ili kuondoa ubatili fulani kwenye katiba, unaonyima haki ya kuchagua na kuchaguliwa, kisha ndipo tuje kwenye sheria.

Hili la ubatili wa katiba, kwa vile ni la kisheria, masikini vyama havilioni, tunakwenda kubadili sheria ya zamani yenye ubatili, na kwasababu, ubatili huo, uko kwenye katiba, na hakuna mabadiliko ya katiba, hivyo tunakwenda tena kutunga sheria nyingine mpya yenye ubatili!. Sijui kwanini hili la ubatili wa katiba wenzwtu hawalioni.

Mchangiaji mmoja akapendekeza tutenge asilimia 10 ya bajeti ya taifa, ilipwe kama ruzuku kwa vyama vyote vya siasa nchini!, mimi katika mchango wangu, hili nililipinga

“Ndugu zangu wa vyama vya siasa, wenzetu nchi za Ulaya, upngozi wa chama cha siasa, ni utumishi wa umma wa kujitolea, upmgozi wa chama sio ajira, vyama vya siasa tangu TANU havikuwa vinapewa ruzuku, vilikuwa 'funded' na wapenzi na wanachama, ifikie mahali tuingie huruma na imani Watanzania wengi ambao wanaishi kwenye lindi la umaskini uliotopea, wetu, kwanini tuendelee kuvipa vyama vya siasa ruzuku kwa kuwalipa watu wazima bukheri wa afya, wenye vioungo vyao timamu, tuwalipe kwa kupiga domo?”

Hili la kupinga ruzuku, sikuanza nalo leo, enzi za Magufuli, niliandika "asiyefanya kazi na asile". Jee siasa nayo ni kazi ya kustahili ujira wa mshahara kwa jina la ruzuku kwa vyama vya siasa? . Ruzuku hii iendelee kuwepo watu waendelee kuitafuna au ifutwe? .

Japo sijafanya utafiti wa ni nchi ngapi zinagawa ruzuku kwa vyama vya siasa lakini kwa nchi masikini kama Tanzania , serikali inayowajibika kwa watu wake na kuheshimu rasilimali kiduchu za taifa, haiwezi fedha zinazokamuliwa kama kodi kwa wananchi masikini wa kutupwa wanaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu fedha hizo zinakuja kugawiwa bure kama ruzuku kwa vyama vya siasa, watu wazima wenye nguvu zao, na vioungo vyao timamu, wanalipwa wazitafune kwa kazi ya kupiga domo! .

Katika kuunga mkono juhudi za rais Magufuli za kubana matumizi ikiwemo kupunguza safari za nje, kuwaengua watumishi hewa, kufanya tumbua tumbua majipu ya ufisadi, namshauri rais wetu aziangazie ruzuku kwa vyama vya siasa.

Enzi za Nyerere kulitolewa ruzuku ya mbolea, mbegu bora na pembejeo za kilimo ili kuimarisha uzalishaji mali, sasa ruzuku hizo zimefutwa na badala yake mijitu mizima isiyo na matatizo yoyote, au changamoto za kiafya, ndio inakaa bure kutafuna ruzuku ya bure bure huku masikini wakitaabika!.

Asiyefanya kazi na asile! . Siasa sio kazi ya mshahara bali ni kazi ya kujitolea, ruzuku kwa vyama vya siasa ni ufisadi, ifutwe?.

Paskali

Naona "point" yako... na tungeenda mbele zaidi hata mpaka kwa wabunge... Kwani ubunge unasomewa wapi? Kabla wakati, na baada ya ubunge si wakuwa na kazi/biashara zao> Kwanini mbunge asiwe tu anajitolea? Maana ni kazi ya kisiasa pia!!!
 
Back
Top Bottom