IKULU: Kikwete si mmiliki DOWANS!

IKULU: Kikwete si mmiliki DOWANS!

muongo lazima umsute kwa lugha kali, slaa kuitwa kidhabidhabina si tusi. Kidhabi maana yake ni muongo na dhabina wa waongo. Kwa hiyo, kidhabidhabina ina maana muongo wa waongo. Au huoni uongo wake wa kuwazido waongo?

Leo kafikia mpaka kudanganya kuwa rais ndie mmiliki wa dowans? Haaa, anashangaza kidhabu mkubwa huyu.

unajuaje kama kadanganya mkuu? Na kama unajua kadanganya, waweza kutupatia data za ukweli ili tuzione hapa jf na kujiridhisha nasi tuweze kumpuuza kwa maneno yake? Unaingia kwenye mtego uleule. Ili uje na kukanusha kitu au uongo ni lazima uje na kitu cha kuthibitisha kuwa ule ulikuwa uongo na ukweli ndo huu. That simple.
 
Salva Rweyememu:

1. Alikuwa moja wa right wings wa kumwingiza JK Ikulu 2005 bila kumsahau Kinara wao Rostam Aziz wakitumia hela za EPA.
2. Baada uchaguzi kuisha hakupata cheo. Akamwandikia Rostam Aziz akilalama kusahauliwa. Ref. Thread iliyowahi kutolewa hapa. Matokeo yake akapewa Ukurugenzi wa mawasiliano Ikulu. Before that aliwahi kufanya kazi Ricmund as public relations Officer.
3. Rostam Azizi, JK na Lowasa ni best friends in Business. The trio are the owners of Richmund a.ka Dowans.
4.Salva Rweyememu aka Boot leaker, amepanick baada ya kugundua siri imefichuka. Remember, Kabla ya hapa JK hakuwahi kutajwa explicilty kuwa ndio mmilki wa Dowans so everything was cool for him(JK) though alimtosa EL katika harakati za kuficha ukweli.
5. Hatushangai the Boot leaker kukurupuka na lugha za uswazi katika hili sasa hivi. Hapo brain haifanyi tena kazi ni mdomo tu. When you are angry or panicked , mouth works faster than the brain. And that is a typical foolish behavior of any thief when he is caught pants down.

Ukiwa kachero this could be the best time to squeeze the beans out of him, although you do not need any other proof because the reaction itself has spoken out the truth. JK is the owner of Dowans. Period
 
Kwanini Salva anajibu kwa Jazba? kama kamsingizia ni kwanini Dk slaa asishtakiwe kwa kusema uongo ili ukweli ubainike?

ezan mimi ninaipenda sana michango yako humu..... lakini ninakuwa na waswasi sana wakati nikiwa nyumbani kwani watoto wangu wakisogelea laptop yangu..... hiyo avature yako itaniponza.... watakujakuificha na kuichoma moto hii laptop
 
Hii inaonyesha jinsi gani ikulu imegeuzwa kama kijiwe hata wahuni nao wamo ndani vile vile wankula mema ya nchi kwa kodi zetu, Its time to wake up and be more serious with this issue kama kweli sio wasanii watupu wamejaa huko.
 
Hii inaonyesha jinsi gani ikulu imegeuzwa kama kijiwe hata wahuni nao wamo ndani vile vile wankula mema ya nchi kwa kodi zetu, Its time to wake up and be more serious with this issue kama kweli sio wasanii watupu wamejaa huko.

Badala ya kutukana, tungejiuliza Je, Tanzania tuna Ikulu yenye qualities/attributes za kuitwa Ikulu?
 
Kitendo cha kutudanganya kwamba gazeti la tanzania daima linamilikiwa na Chadema ni dalili za kwanza kwamba Salva yeye ndie muongo. Ina maana gazeti la uhuru kwa kuwa ni la CCM basi ni la Kikwete? Mbona hatujawahi sema magazeti ya Rostam ni ya CCM? hiyo ni moja.

Pili, Mbona hajatuambia mmiliki wa Dowans ni nani sasa kama siyo Kikwete? Kama hana majibu amuulize Mwakyembe na Samwel Sitta wanajua kuwa mmiliki ni JK.

Anaposema Slaa anataka kuleta machafuko ana maana gani? Kwanini kila mara CCM wanakilmbilia kwenye machafuko? Wanamtishia nani? Hakika kama hawamtaji mmiliki wa Dowans machafuko yatatokea kwa sababu watu hawapo tayari kulipa kiwango hicho cha pesa kwa mtu asiyejulikana wakti serikali haina pesa ya kuajiri walimu 16,000.

Poor Tanzanians na sisi tumelala tu huku watu kama Salva, Kombani na Werema wakitaka kutupeleka Somalia. Taarifa ya Salva ni ya Kichochezi na anastahili kuwa namba moja kwenda ICC kama yule mwandishi wa Kenya.
 
Salva ni mmoja wa wanahabari I used to admire wakati yupo Habari Corp ya kina Mbwambo na Ulimwengu.

Sina muda mrefu toka nimeingia jamvini hapa na huwa nasoma kuna "BAN". Isingekuwepo BAN ningemporomoshea shhxxxnzy type kibao maana taarifa yake imeniamsha upako wa matusi ndani yangu.

Kuna hadithi zamani usukumani alikuwepo jamaa anaitwa Mwanamalundi, alikuwa anaweza kunyooshea mti kidole na unakauka. Angekuwepo leo ningemwomba Mwanamalundi afungulie Tsunami hapo magogoni lakini Ikulu peke yake ndo iteketee.
 
Kama si yeye ampeleke Dr.mahakamani,Huyo ndiye mhusika mkubwa.
 
Salva huyuhuyu au fotokopi?....maana naona sasa kaacha kulamba viatu analamba miguu kabisa!..eish,ikifika 2013 tutaona 'press release' za aina gani?...too low!
 
Jibu hoja, wacha firimbi. Slaa ni muongo tena kizabizabina, hayo ndio inatakiwe uyatetee au uyakubali, achana na ngonjera.
Hata Salva hajajibu hoja zaidi ya kuleta matusi. Majibu sahihi atuambie nani hasa anamiliki Dowans? Hata wewe Dar es salaam, Jeykey, malaria Sugu saidianeni na Salva kuhusu umiliki wa Dowans la sivyo mpelekeni Dr Slaa mahakamani akafungwe kama muongo. Mtindo wakuleta ngonjera humu hautatusaidia kabisa. Kumuita Slaa mzee wakti Kikwete pia mzee na salva pia atazeeka ni jazba za kipuuzi ambazo hazina tija kwa maendeleo ya watz
 
Dah Mkuu Realman umenifanya nicheke hata kama nilikuwa nimekunja uso nusura nibamize laptop yangu kwa taarifa hiyo ya salva lakini habari ya Mwanamalundi imenichekesha sana kwani tulisoma zamani kwenye vitabu.

Hakika Ingekuwa inawezekana Ikulu isafishwe kabisa kwa njia halali na haramu si wanasema "The end justifies the means?"
 
Nadhani angetoa maelezo ya kina ni bilion ngapi inatakiwa ilipwe, Kwanini wengine wanasema bilioni 97 wengine wanasema 185.5?

Msimamo wa ikulu kuhusu kukata rufaa, lini bei ya umeme itashuka katika mipango kadhaa, kutaja wamiliki wa dowans, na kwa nini hawato mshtaki Dr SLAA kwa kuwasingizia hizo ndo facts wa tz tunataka siyo unaleta pumba, lini hapo ikulu mtakuwa mnatoa details za maana?

Tunataka maelezo ya kwa nini tuko hapa na tunafanya nini kutoka hapa tulipo ili tusonge mbele kimaendeleo, siyo unatuletea maelezo kama mashairi ya taarabu, wote mliopo ikulu kuanzia mkwere get real!
 
Wadau,

Ifuatayo ni taarifa nzima ya Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu, ambaye aliwahi kuajiriwa na Richmond/Dowans kufanya kazi za public relations kwa kampuni hizo kwa kuunganishwa na Rostam Aziz. Nime-forwardiwa email hii na mwandishi mmoja aliyepata nikaona ni vyema niiweke humu JF. Naomba tuitafakari kama ilivyo:

Kaka Salva hii umeandika ki-CCM zaid na si kiserikali, you need another Ngurdoto seminar kujua unatakiwa ufanye vipi kazi

MIAKA MITANO IJAYO HAIKO MBALI TUNAKUSUBIRI MTAANI UJE KUJIBU VYEMA HIZI SHUTUMA
 
[FONT=Book Antiqua, serif]TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU.


[FONT=Book Antiqua, serif]KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Wilboard Slaa, leo, Jumapili, Januari 2, 2011, amekaririwa na Gazeti la Tanzania Daima, linalomikiwa na chama chake hicho, akidai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ni mmoja wa wamiliki wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Dowans.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Huu ni uongo wa mchana, ni uzushi wa karne na propaganda ya hatari. Kwa hakika na kwa namna isiyoweza kuelezeka kwa ufasaha, tumeshtushwa sana na kauli hii ya Dkt. Slaa na hatutaki kuamini kabisa wala kukubali kuwa ni kweli kauli hii imetolewa na mtu ambaye majuzi tu alikuwa akiwania kuwa kiongozi wa juu wa taifa letu, yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Na kama kweli Dkt. Slaa ametoa kauli hii na kusema maneno ya namna hii basi sasa Watanzania wanayo kila sababu na haki ya kuamini kuliko wakati mwingine wowote kuwa mzee huyu sasa amechanganyikiwa na ni mtu wa hatari sana kwa utulivu wa nchi hii. Kwa nini?[/FONT]

[FONT=Book 
Antiqua, serif]Sababu ni rahisi sana. Mheshimiwa Rais Kikwete siyo mmiliki wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Dowans. Hakupata kuwa mmiliki, siyo mmiliki na wala hatakuwa, hata siku moja, mmiliki wa Kampuni hii. [/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Kama Dkt. Slaa anataka kweli kujua wamiliki wa Kampuni ya Dowans, basi atafute ukweli huo na aachae tabia ya kutapatapa na udhabinadhabina yenye lengo la kuwapaka watu watope. Tabia ya kuwasingizia na kusema uongo kuhusu viongozi wa taifa letu ni tabia ya hatari.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Mheshimiwa Rais Kikwete hahusiki na Kampuni ya Dowans wala na kampuni nyingine yoyote ya kibiashara. Yeye ni kiongozi wa juu kabisa wa siasa wa nchi yetu na siyo heshima wala haki kumhusisha na jambo la kutunga na kuzua na lisilokuwa la ukweli wowote.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Kiongozi huyo wa upinzani ametoa shutuma zake dhidi ya Rais Kikwete kufuatia Kampuni ya Dowans kulishitaki Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na Mahakama hiyo ikaamua kuwa Dowans ilipwe kiasi cha sh bilioni 185.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Dkt. Slaa amezomoko na kumshutumu Rais Kikwete eti kwa sababu Mheshimiwa Rais hakuzungumzia suala hilo katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Ijumaa iliyopita.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Mwaka huu, Dkt Slaa aliwania urais wa Tanzania kupitia CHADEMA na akashindwa vibaya sana. Tokea wakati huo amekuwa mtu wa kutunga na kuzua stori za kila aina ya uongo na umbea kuwachanganya Watanzania kwa sababu ya kinyongo chake cha kushindwa. [/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Tunapenda kuwataka na kuwaomba Watanzania, kama ambavyo wamekuwa wanapuuza uongo na uzushi mwingine wa mara kwa mara wa Dkt. Slaa, waupuuze uzushi na uongo wa sasa kuhusu miliki ya Dowans. Ni sehemu ya tabia iliyoanza kuzoeleka sasa ya Mzee huyo kutapatapa kisiasa.[/FONT]

[FONT=Book 
Antiqua, serif]Imetolewa na Salva Rweyemamu – Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais - Ikulu[/FONT][/FONT]

Sikuwahi kutegemea kwamba Salva rweyemamu ni mtu mwenye fitina na hasira namna hii nadhani hasira zake zinajibu hali halisi aliyonayo jakaya kwa wakati huu,kikwete na Slaa wanapishana miaka miwili kwa umri namna nyingine wako umri mmoja kumuita Mzee ni kweli ni mzee lakini salva anataka kutuaminisha kwamba amezeeka hana akili ya kufikiri na kama ni hivyo hofu yetu kwa kikwete kwamba hana akili Salva anaithibitisha
aanaposema kiongozi wa juu sana wa nchi hapaswi kusemwa anataka kutuambia kuwa Kikwete yuko juu ya sheria na ndio maana anafanya kila anachokifanya kufuja rasilimali zanchi kwa sababu anajiona yuko juu ya sheria
jamani salva anasema amezomoka hivi hili ni neno la kiswahili
pia anasema dr Slaa atafute wamiliki wa Dowans kwa nini kurugenzi ya mawasiliano wasituambie wamiliki halisi wa Dowans hivi anadhani sisi wananchi ni mazumbukuku hatujui kuchambua mbichi na mbivu unakataa kusema Raisi Kikwete sio mmliki wa Dowans halafu husemi mmiliki halisi ni nani jibu sisi tunaosoma waraka wake ni kwamba mmiliki ni raisi kikwete bila kificho ila yeye Salva anaendekeza propaganda
 
Back
Top Bottom