Sometimes nashindwa kuelewa Ikulu yetu ina-operate vipi. Hivi nani anaweza kuwaweka sawa hawa jamaa?
Angalia anachoandika Salva:
....[FONT=Book Antiqua, serif]hatutaki kuamini kabisa wala kukubali kuwa ni kweli kauli hii imetolewa na mtu ambaye majuzi tu alikuwa akiwania kuwa kiongozi wa juu wa taifa letu, yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.[/FONT]
Salva, angetoa kauli hiyo nani na ninyi mkubali kumjibu au kuja out clean?
You mean ukishagombea urais basi unatakiwa kukaa kimya kwenye mambo ya msingi ati unalinda Status Quo? Unataka kutwambia kuwa huelewi kwanini Slaa katumia njia hii mbadala kusababisha walau mtoe kauli yenu juu ya DOWANS?
[FONT=Book Antiqua, serif]Na kama kweli Dkt. Slaa ametoa kauli hii na kusema maneno ya namna hii basi sasa Watanzania wanayo kila sababu na haki ya kuamini kuliko wakati mwingine wowote kuwa mzee huyu sasa amechanganyikiwa na ni mtu wa hatari sana kwa utulivu wa nchi hii. Kwa nini?[/FONT]
Kauli hizi tulizisikia toka KWAKO wakati wa EPA, baadae mkaanza mazingaombwe! Mtu gani si wa hatari kwa taifa hili kwa upande wenu? Unataka 'kutunywesha' kuwa ili kuwa muungwana kwa taifa lako hutakiwi kumnyooshea kidole rais aliye madarakani?
[FONT=Book Antiqua, serif]Mheshimiwa Rais Kikwete hahusiki na Kampuni ya Dowans wala na kampuni nyingine yoyote ya kibiashara. Yeye ni kiongozi wa juu kabisa wa siasa wa nchi yetu na siyo heshima wala haki kumhusisha na jambo la kutunga na kuzua na lisilokuwa la ukweli wowote.[/FONT]
Salva bro, WE will prove you wrong soon... Amini usiamini! Watch this space
[FONT=Book Antiqua, serif]Mwaka huu, Dkt Slaa aliwania urais wa Tanzania kupitia CHADEMA na akashindwa vibaya sana. Tokea wakati huo amekuwa mtu wa kutunga na kuzua stori za kila aina ya uongo na umbea kuwachanganya Watanzania kwa sababu ya kinyongo chake cha kushindwa. [/FONT]
Hizi kauli hizi...!
Sasa, ni upi msimamo wa rais (si wewe Salva) juu ya DOWANS?
Baada ya Dr. Slaa kumsingizia Mhe. Rais (kitu ambacho hata mimi kimenikera SANA), mheshimiwa Rais anatwambia nini juu ya dudu hili (DOWANS), ni la nani haswa? Ni nini hatma ya taifa katika mgawo ambao unaendelea nchi nzima?
Well, huu uzushi wa Slaa tuuweke kando, vipi mnatudanganya kama vile sisi hatujaiona hiyo hukumu ya ICC na mnataka kutuaminisha kuwa kinachotakiwa kulipwa ni Bil 185.85 Tshs (hatujui nani mpokeaji); salio ni la nini lililoongezwa?
Acheni siasa kwenye mambo ya msingi, come out clean mkuu. Taifa hili ni letu sote, mnapochemka mkakosolewa kama hamna majibu sawia kaeni kimya, tutadhania mnayafanyia kazi maoni/malalamiko ya wananchi lakini kujibu kisiasa na kwa kebehi haitatusaidia kama taifa!