IKULU: Kikwete si mmiliki DOWANS!

IKULU: Kikwete si mmiliki DOWANS!

Salva Rweyemamu...... Mohhamed SaeEd Al Sahaf
 
Rweye lazima mseme hivyo ili msimkere,
Hivi ikulu sasa imetuona sisi wanasesere,
Au kuona wananchi kama ngoma ya segere,
Kucheza utacheza bila hata kwenda Makerere,
Na kutapatapa kwa kauli kumtetea mkwere!!!

Mmiliki wa DOWANS ndio kauli tunayoitaka.

 
Ukiona hivyo pata picha kuwa ikulu hakukaliki na vikao kila kukicha...

Mwakilishi wa dowans kwenye kesi ufaransa ni kutoka caspian contraction ambayo inamilikiwa na rostam aziz..

Sasa rostam katoa hela ya uchaguzi ni lazima zirudishwe.. But how??

Kwa kauli za rweyemamu unapata picha kuwa dowans ni mali ya ikulu sasa itakuwa vipi nadhani ndiyo wanajaribu kuchakachua...

Wewe subiri tu jk anakataa dowans mbaona hatoi tamko la kusema ni ya nani??

Je bilila kempinsky ni ya nani?? Ambayo anaipigia debe kuweka barabara ya lami????
 
Ukitupa jiwe likampana mbwa, ni kawaida lazima mbwa atalia. jiwe hili limetua kwenye migongo sahihi
 
[FONT=Book Antiqua, serif]TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU.


[FONT=Book Antiqua, serif]KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Wilboard Slaa, leo, Jumapili, Januari 2, 2011, amekaririwa na Gazeti la Tanzania Daima, linalomikiwa na chama chake hicho, akidai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ni mmoja wa wamiliki wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Dowans.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Huu ni uongo wa mchana, ni uzushi wa karne na propaganda ya hatari. Kwa hakika na kwa namna isiyoweza kuelezeka kwa ufasaha, tumeshtushwa sana na kauli hii ya Dkt. Slaa na hatutaki kuamini kabisa wala kukubali kuwa ni kweli kauli hii imetolewa na mtu ambaye majuzi tu alikuwa akiwania kuwa kiongozi wa juu wa taifa letu, yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Na kama kweli Dkt. Slaa ametoa kauli hii na kusema maneno ya namna hii basi sasa Watanzania wanayo kila sababu na haki ya kuamini kuliko wakati mwingine wowote kuwa mzee huyu sasa amechanganyikiwa na ni mtu wa hatari sana kwa utulivu wa nchi hii. Kwa nini?[/FONT]

[FONT=Book
Antiqua, serif]Sababu ni rahisi sana. Mheshimiwa Rais Kikwete siyo mmiliki wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Dowans. Hakupata kuwa mmiliki, siyo mmiliki na wala hatakuwa, hata siku moja, mmiliki wa Kampuni hii. [/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Kama Dkt. Slaa anataka kweli kujua wamiliki wa Kampuni ya Dowans, basi atafute ukweli huo na aachae tabia ya kutapatapa na udhabinadhabina yenye lengo la kuwapaka watu watope. Tabia ya kuwasingizia na kusema uongo kuhusu viongozi wa taifa letu ni tabia ya hatari.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Mheshimiwa Rais Kikwete hahusiki na Kampuni ya Dowans wala na kampuni nyingine yoyote ya kibiashara. Yeye ni kiongozi wa juu kabisa wa siasa wa nchi yetu na siyo heshima wala haki kumhusisha na jambo la kutunga na kuzua na lisilokuwa la ukweli wowote.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Kiongozi huyo wa upinzani ametoa shutuma zake dhidi ya Rais Kikwete kufuatia Kampuni ya Dowans kulishitaki Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na Mahakama hiyo ikaamua kuwa Dowans ilipwe kiasi cha sh bilioni 185.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Dkt. Slaa amezomoko na kumshutumu Rais Kikwete eti kwa sababu Mheshimiwa Rais hakuzungumzia suala hilo katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Ijumaa iliyopita.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Mwaka huu, Dkt Slaa aliwania urais wa Tanzania kupitia CHADEMA na akashindwa vibaya sana. Tokea wakati huo amekuwa mtu wa kutunga na kuzua stori za kila aina ya uongo na umbea kuwachanganya Watanzania kwa sababu ya kinyongo chake cha kushindwa. [/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Tunapenda kuwataka na kuwaomba Watanzania, kama ambavyo wamekuwa wanapuuza uongo na uzushi mwingine wa mara kwa mara wa Dkt. Slaa, waupuuze uzushi na uongo wa sasa kuhusu miliki ya Dowans. Ni sehemu ya tabia iliyoanza kuzoeleka sasa ya Mzee huyo kutapatapa kisiasa.[/FONT]

[FONT=Book
Antiqua, serif]Imetolewa na Salva Rweyemamu – Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais - Ikulu[/FONT][/FONT]

Sikuwahi kutegemea kwamba Salva rweyemamu ni mtu mwenye fitina na hasira namna hii nadhani hasira zake zinajibu hali halisi aliyonayo jakaya kwa wakati huu,kikwete na Slaa wanapishana miaka miwili kwa umri namna nyingine wako umri mmoja kumuita Mzee ni kweli ni mzee lakini salva anataka kutuaminisha kwamba amezeeka hana akili ya kufikiri na kama ni hivyo hofu yetu kwa kikwete kwamba hana akili Salva anaithibitisha
aanaposema kiongozi wa juu sana wa nchi hapaswi kusemwa anataka kutuambia kuwa Kikwete yuko juu ya sheria na ndio maana anafanya kila anachokifanya kufuja rasilimali zanchi kwa sababu anajiona yuko juu ya sheria
jamani salva anasema amezomoka hivi hili ni neno la kiswahili
pia anasema dr Slaa atafute wamiliki wa Dowans kwa nini kurugenzi ya mawasiliano wasituambie wamiliki halisi wa Dowans hivi anadhani sisi wananchi ni mazumbukuku hatujui kuchambua mbichi na mbivu unakataa kusema Raisi Kikwete sio mmliki wa Dowans halafu husemi mmiliki halisi ni nani jibu sisi tunaosoma waraka wake ni kwamba mmiliki ni raisi kikwete bila kificho ila yeye Salva anaendekeza propaganda

Haya maneno hayapaswi kuwa msemaji wa Ikulu na ni uzushi anaposema "Dkt Slaa aliwania urais wa Tanzania kupitia CHADEMA na akashindwa vibaya sana," hii kauli ni uzushi.
 
Hii imekaa kimipasho mipasho hivi. Njia pekee ya kuweka rekodi sawa ni kuonesha nyaraka halali za umiliki wa Dowans, hapo ndio tutajua kama Slaa kadanganya au la. Lakini hii ya kupashana kwa kutumia letterhead za ikulu ni aibu.
 
.....too low to be coming from Ikulu!

Huu ni uongo wa mchana, ni uzushi wa karne na propaganda ya hatari.

mzee huyu sasa amechanganyikiwa na ni mtu wa hatari sana kwa utulivu wa nchi hii
Hakupata kuwa mmiliki, siyo mmiliki na wala hatakuwa, hata siku moja, mmiliki wa Kampuni hii.
....tabia ya kutapatapa na udhabinadhabina yenye lengo la kuwapaka watu watope....
....Mheshimiwa Rais Kikwete hahusiki na Kampuni ya Dowans wala na kampuni nyingine yoyote ya kibiashara.....
Mwaka huu, Dkt Slaa aliwania urais wa Tanzania kupitia CHADEMA na akashindwa vibaya sana. Tokea wakati huo amekuwa mtu wa kutunga na kuzua stori za kila aina ya uongo na umbea kuwachanganya Watanzania kwa sababu ya kinyongo chake cha kushindwa.

Tunapenda kuwataka na kuwaomba Watanzania, kama ambavyo wamekuwa wanapuuza uongo na uzushi mwingine wa mara kwa mara wa Dkt. Slaa, waupuuze uzushi na uongo wa sasa kuhusu miliki ya Dowans. Ni sehemu ya tabia iliyoanza kuzoeleka sasa ya Mzee huyo kutapatapa kisiasa.

....hivi jamani mbona huyu kilaza povu linamtoka hivi mdomoni? siamini kama hayo maneno hapo juu yametolewa na msemaji wa Ikulu ya Tanzania!


 
Salva Rweyemamu ni mtu mzima hovyo, kabisa hana soni,anaweza kutetea hata wale wanaopaka mavi mwilini kugombea haki zao akadhani ni poda hadanganyiki mtu Raisi KIKWETE kwa mujibu wa taarifa ya kurugenzi ya Mawasiliano ikulu ndio mmiliki wa Dowans
 
Nilijua Dr. Slaa kawagusa pabaya......sasa angalia wanavyohaha!!

Wanatoa maelezo mengi ya kujikanyaga kanyaga badala na kuja na press release ya paragraph 2 tu, paragraph ya 1, ikikanusha Kikwete kuwa mmiliki wa Dowans na paragraph ya pili ikitaja wamiliki wa Dowans. Period

Naona bado Salva ana hang over za nyimbo za kiduku walizokuwa wanacheza kipindi cha kampeni....piiipiiii za kina Marlaw!!
 
Utazungumzaje bila kuusema ukweli wa jambo. Salva anafanya kampeni ya udiwani kwa tiketi ya CCM!
 
Mnashikwa pabaya nyie Kina REYEMAMU!!!! Kama mnathubutu Nendeni mahakamani basi ili tugundue mengi zaidi....Hakuna siku Dr Slaa amewahi kuzusha! Kipindi anatangaza List of shame Mlimchamba sana mkatishia kumshtaki lakini tumeyaona wenyewe na yametufumbua wananchi na tuna imani mengine yanakuja WEAK LEAKS etc vitatusaidia. Haponi mtu hapo mpo pabaya mwana wane MWANGALUKA MWAYO ULE MHOLA?
 
sky0.jpg

Salva Rweyemamu Vs Mohhamed Saeed Al Sahaf

former iraqi informtion Minister maarufu kama Al Sahaf....... yupi bora
 
Yaani baada ya kushindwa URAIS, kwenye uchaguzi ulio huru na wa haki, Slaa na wapenzi/wanachama wake wamechanganyikiwa kabisa, hawajui wafanyalo wala wafikirialo. Kila siku ni majungu, fitina, uzushi, uzabizabina, unafiki. Kweli CDM si chama cha kuliongoza taifa hili kamwe, Mungu tuepushe nacho, amen !
Naogopa BAN vinginevyo. Kiufupi wewe ni Mwehu mkubwa. Umeme hauwaki, bei inapanda , maisha yanazidi kuwa magumu, Jk analeta usanii kwenye katiba wewe unaleta upupu hapa? Fujo zinaletwa na CCM na serikali yake wewe huoni vituko vya salva, Kombani na Werema. Kama CDM ni ya kuogopwa kwanini Jk anatekeleza ilani yake kuhusu katiba ndani ya siku 100? Naweza nikawa nabishana na mtu wa viwango vya chini ngoja niishie hapa
 
Ikulu imejaza wendawazimu?

Mtoto wangu wa miaka mitano anayesoma St. Joseph hapa Marekani hawezi kuandika upumbavu usio na mashiko kama huu wa Salva. Salva angesema Mumuiliki ni nani na akatoa sababu sahihi zenye kuchanganua masuala vizuri zinazoweza kutushawishi kuona kuwa Dr. Slaa kweli kapotosha Umma.

Salva ameonesha ujinga ulioko kichwani mwake na ameshindwa kushawishi watanzania kuhusu Dowans. ....
Salva amesahau kabisa kuwa Kikwete alihusika bila hofu kwenye maamuzi ya kuiweka Dowans. Watanzania hatusahau haraka hivyo ila naomba sana Rweyemamu arejee kwenye hotuba za Kikwete na rekodi za Bunge ndo ataona ushiriki wa Kikwete kwenye maamuzi ya Richmond na Dowans.

Ni uzembe kweli............

Iko siku rungu la kilo hamsini litakuwa kama kilo 3 kukong'oli wajinga
 
Mwenye haki hataondolewa milele; Bali wasio haki hawatakaa katika nchi. Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima; Bali ulimi wa ukaidi utakatiliwa mbali. (Methali 10:31-31)
 
MM. Hiyo ndiyo dua niliomuombea Slaa wakati wa uchaguzi. Mchana na usiku na Mungu akajibu. Wee!!!:
Zaburi 35:
4[FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][FONT=Arial Narrow,Arial Narrow]Wafedheheshwe na waaibishwe
wale wanaotafuta uhai wangu,
wanaofanya shauri kuniangamiza
warudishwe nyuma kwa hofu.
[/FONT]
[/FONT]5[FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][FONT=Arial Narrow,Arial Narrow]Wawe kama makapi yapeperushwayo na
upepo,
malaika wa BWANA akiwafukuza,
[/FONT]
[/FONT]6[FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][FONT=Arial Narrow,Arial Narrow]njia yao na iwe giza na ya utelezi,
malaika wa BWANA akiwafuatilia.
[/FONT]
[/FONT]7[FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][FONT=Arial Narrow,Arial Narrow]Kwa vile walinifichia wavu wao bila sababu
na bila sababu wamenichimbia shimo,
[/FONT]
[/FONT]8[FONT=Arial Narrow,Arial Narrow][FONT=Arial Narrow,Arial Narrow]maafa na yawapate ghafula,
wavu walionifichia na uwatege wenyewe,
na waanguke katika shimo hilo,
kwa maangamizo yao.
[/FONT]
[/FONT]
 
Hivi Rweyemamu alikuwa mhariri wa gazeti la UDAKU nini? tunaomba CV yake ianikwe hapa jamvini tumuchambue. Hapa ametuonyesha kwamba UDAKU ndo anaoweza. Hatuwezi kushangaa kuteuliwa na mkwere kuwa msemaji wake maana ndo ufahamu wao unapoishia.

Tulitegemea Ikulu ijibu hoja kwa makini na kwa statement zilizo simama na katika hali ambayo hakuna atakayetilia shaka habari hiyo. Hapa Ikulu imetoa habari za UDAKU tu.

Tena inashangaza Wizara nzima inatoa habari za kidaku na Waziri wake TYSON yuko kimya!

TYSON tunaomba ukanushe huu UDAKU wa Kijana wako!

Tunayo kazi! mpaka 2015 jamani? mimi nitakuwa nimechoka kabisa!
 
Jamani mbona kila baya awe anasukuwa tu JK, tatizo ni nini hasa ndugu zetu?

Hii sasa inafika mahali mpaka inaudhi kweli. Ndiyo maana tangu sasa bora ikulu iwekiwaporomosheeni matusi ya nguoni hivyo ndiyo mkome na umbeambea wenu huo.

Amejitakia mwenyewe, kujipambanua miongoni na mafisadi, halafu alishaambiwa kuwa uwezo wa kuongoza hana, yeye akalazimisha tu. Sasa ngoja aipate na bado kuna mengi yanakuja, kama asipojiuzulu kabla ya miaka 5 sijui!!!!!
 
Salva Rweyememu:

1. Alikuwa moja wa right wings wa kumwingiza JK Ikulu 2005 bila kumsahau Kinara wao Rostam Aziz wakitumia hela za EPA.
2. Baada uchaguzi kuisha hakupata cheo. Akamwandikia Rostam Aziz akilalama kusahauliwa. Ref. Thread iliyowahi kutolewa hapa. Matokeo yake akapewa Ukurugenzi wa mawasiliano Ikulu. Before that aliwahi kufanya kazi Ricmund as public relations Officer.
3. Rostam Azizi, JK na Lowasa ni best friends in Business. The trio are the owners of Richmund a.ka Dowans.
4.Salva Rweyememu aka Boot leaker, amepanick baada ya kugundua siri imefichuka. Remember, Kabla ya hapa JK hakuwahi kutajwa explicilty kuwa ndio mmilki wa Dowans so everything was cool for him(JK) though alimtosa EL katika harakati za kuficha ukweli.
5. Hatushangai the Boot leaker kukurupuka na lugha za uswazi katika hili sasa hivi. Hapo brain haifanyi tena kazi ni mdomo tu. When you are angry or panicked , mouth works faster than the brain. And that is a typical foolish behavior of any thief when he is caught pants down.

Ukiwa kachero this could be the best time to squeeze the beans out of him, although you do not need any other proof because the reaction itself has spoken out the truth. JK is the owner of Dowans. Period

Interesting analysis!
 
Back
Top Bottom