IKULU: Kikwete si mmiliki DOWANS!

IKULU: Kikwete si mmiliki DOWANS!

Ni ukuta gani huo uliouona ukibomoka?
Kaka/ Dada, dont take things as the way you see it. think out of the box. Naona mwenzetu hujui tunaongelea nini hapa. Labda kwa kuwa mwenzetu unalipiwa bill ya umeme na wala kwako hakuna mgao wa umeme n.k. basi unakuja kuongea upupu wako hapa.
Kosoa hoja kwa kuleta hoja
 
weired......Rutashubanyuma kinachoniuma ni kwamba hakuna anaehoji mambo haya zaidi ya DR,sisi ndege waoda tunaficha mbawa zetu natamani ingefika mahali tuimbe wimbo mpya wa saa ya ukombozi nisasa!mi nimechoka na unyanyasaji huu!!
 
lets us provoke them...watatuambia tuuu..
 
Jamani mbona kila baya awe anasukuwa tu JK, tatizo ni nini hasa ndugu zetu?

Hii sasa inafika mahali mpaka inaudhi kweli. Ndiyo maana tangu sasa bora ikulu iwekiwaporomosheeni matusi ya nguoni hivyo ndiyo mkome na umbeambea wenu huo.
Mtakoma nyie manyang'au wezi wakubwa na ufisadi wenu na baba zenu, watu wazima hovyooooooo
 
JK amekanusha kwamba yeye siyo mmiliki wa dowans, tena katumia maneno makali mweli, ila ukweli unabaki pale kwamba, Kama Rais ana jukumu la kulitaarifu humu kwamba uozo wa Dowans unafanya na nani. Ikiwa ataki kutuambia mmilikiwa Dowans, basi yeye ndo mwenyewe

Kutumia ukali kwamba siyo mmiliki hakumaanishi kwamba yeye siyo mmiliki.
 
Kuna siku watu watachukua sheria mkononi hakya mungu inauma sana. Unapoona mambo yanafanyika kienyeji hongera dr kwa ujasiri wako tupate watu kumi kama wewe nchi inabadilika
 
JK hawezi kuukwepa ukweli kuwa ana masilahi mazito ndani ya DOWANS.......na huu hapa ni ushahidi:-

a) Uteuzi wa Dr. Idrissa Rashid kuiongoza Tanesco ulijaa mizengwe kibao..............Dr. Rashid mwenyewe alikiri kuwa pamoja na kuwa nafasi hiyo ilitangazwa magazeti yeye hakuiomba ila JK alimwomba amsaidie kwenye nafasi hiyo...........Hivyo pamoja na sheria ya Tanesco kuweka wazi kuwa Mtendaji Mkuu wa Tanesco atateuliwa na Bodi, JK aliingilia Bodi kinyume na sheria pale alipombandika swahiba wake pale Tanesco..........................Swali la kujiuliza JK alikuwa anatetea masilahi ya nani kwa kuiingilia Bodi ya Tanesco?

b) Kwa vile Dr. Rashid hakuwa ameteuliwa na Bodi ya Tanesco hivyo na yeye hakuona sababu ya kuishirikisha Bodi tajwa katika utoaji wa zabuni ya uzalishaji wa umeme kwa Richmond na hata zabuni hiyo haikupitishwa kwa Bodi ya zabuni na matokeo yake kampuni kivuli ikapewa kazi hiyo..........Kulingana na rekodi zilizopo Brella, Richmond haijawahi kusajiliwa hapa nchini na hivyoufanyaji wake wa kazi ulikuwa ni batili na haikupaswa kupewa zabuni tajwa............Haya ni makosa ya kijinai yaani "criminal negligence" na JK anashindwa nini kumkabidhi swahiba wake Takukuru? Hapa inaonyesha kabisa hoja za Dr. Hosea kwa Wikileaks ni za kweli ya kuwa JK ndicho kikwazo kikuu cha utawala bora hapa nchini...............

c) Baada ya Richmond kushindwa kuzalisha umeme ikaikabidhi kazi hiyo kwa DOWANS ambao walitumia dola za kimarekani 7.5 milioni kununua mitambo hiyo ya kuzalisha umeme kazi ambayo ilikuwa ndani ya uwezo wa Tanesco.........................na hivyo hawakuhitaji mzabuni yeyote..........................

d) Tanesco kwa matendo yao walimhalalisha Dowans kuwa mzabuni wa kumrithi Richmond bila ya kupata kibali cha Bodi ya zabuni....

e) Baada ya mkataba kuisha Tanesco wakaishinikiza serikali kununua mitambo ya DOWANS kwa bei ambayo ilikuwa ni zaidi ya mara 20 ya bei ambayo Dowans walinunulia mitambo tajwa.......na ili kuishinikiza serikali kuinunua mitambo ya DOWANS, Tanesco wakaamua kuitumia Mahakama Kuu kwa kuwazuia Dowans wasiondoke na mitambo yao kwa amri ya Mahakama.....................bila sababu za kimsingi.........

f) Kutokana na uvunjaji huo wa mkataba kwa kutumia visingizio vya kuwa Dowans hawajalipa kodi, Msuluhishi akaibandika Tanesco jumla ya Tshs 185 Bilioni ikiwa ni zaidi ya mara 18 ya gharama ambazo Dowans walinunulia ile mitambo...............

g) Mwanasheria Mkuu ametoa ushauri Dowans walipwe huku uamuzi huo haujatoa sababu ni maeneo yapi Tanesco ilikuwa imekiuka huo mkataba kitendo ambacho kwa AG makini angeligangamala kuhakikisha analifungua shauri upya hapa Dar kupinga tuzo ambayo hata sababu za Tuzo hiyo hazifahamiki.........................Katika hukumu hiyo Msuluhishi aliahidi kutoa sababu lakini sababu hizo hakuzitoa sasa mdaiwa ataonaje kuwa katendewa haki? Hivi tuna AG au tunambabaishaji ambaye anadai ameipitia hiyo hukumu na ameona ipo beneti na tuilipe tu...............Hawa ndiyo wateule wa JK ambao kazi yao kuu ni kujenga mazingira ya kulipora taifa hili changa..........

h) JK hayuko tayari kumfikisha mahakamani Dr. Idrissa Rashid kwa sababu alimpeleka pale Tanesco kwenda kulipora hilo shirika la umma na hasa ukizingatia ya kuwa JK alivunja sheria za tanesco kuhakikisha Dr. Rashid anakwenda pale tanesco kulifilisi shirika hilo na mzigo wa hasara hizo kutupiwa raia wanyonge ambao kosa letu ni kumvumilia JK ambaye hana sifa ya kuliongoza taifa hili masikini duniani........

i) Haya ni mazingira yanaonyesha ya kuwa JK ni mshiriki kwenye mradi wa Dowans na hata kama jina lake halipo ila linawakilishwa na swahiba wake wa karibu Rostam Aziz kama ushahidi huu kwenye hukumu ya Dowans unavyothibitisha ambao tanesco wenyewe waliutumia ................................

RostamAziz.jpg
 
Ngoja Wikileaks ije imtaje jina kabisa ndipo atajua watu wana data za uhakika.
 
RUTASHUBANYUMA, I would like to respond to your first post by giving facts ili tuwekane sawa tafadhali

A. Sheria inayounda mashirika ya umma inampa rais uwezo wa kuteua mtendaji mkuu wa shirika, hivyo uteuzi wa Dr Rashidi haukukiuka sheria yoyote, hoja kama ana uwezo ama hana ni nyingine

B. Dr Rashidi hakuidhinisha Richmond, aliingia jan 2007 na Richmond iliingia 2006 na walioiingiza si TANESCO ni Govenrment Negotiating Team, tume ya Mwakyembe imeainisha hilo.

C. Walichofanya Richmond baada ya kukosa uwezo ni kuwapa ile tender Dowans , na baraka zote from GNT

D. Dowans haikupitia kwenye Tanesco tender board bali GNT

E. TANESCO opted for Dowans because its already connected to the grid and cheaper than IPTL, all they did was to ask for permission to buy it and not 'kushinikiza' kwa mwenye kujua biashara ya umeme, kutembeza. IPTL ni billion 11 hali Dowans ni billion 2, kama mtu ni mfanyabiashara unaopt kilicho more reasonable cost ways..bei tajwa haikuwa mara 20 kwani haikuwa discussed sijui mwenzangu umepata wapi hii data ?? I commissioned Dowans and am involved in consulting change of IPTL from heavy fuel so I know what am talking about, DOWANS is better off (then )

F.ukiisoma judgement ya ICC utaona si TANESCO waliovunja mkataba ni dowans !! Walivunja na kushtaki TANESCO, thts why mitambo ilishikiliwa kwa kadhia ya kodi..

G, H and I siwezi kuyaongelea, Dr Rashidi amefanyia mengi TANESCO, ashtakiwe kwa mambo aliyofanya prior to TANESCO and not whilst there

Nimeona tu nirekebishee hii ili tujue ukweli uko vipi, kama una ya kuongezea karibu sana ila tunyooshane kwa amani
Mhandisi mifumo na njia kuu za umeme Nsiande.
 
Akili ya Rweyemamu na mawazo yake hayewezi kufanana wala kukaribiana na ya Dr. Slaa.
Slaa na mwamini, watasema tu mmiliki ni nani kwa makusudi au kwa kutojitambua kuwa wanamtaja
Kazi imeanza na safari hii mapema
 
hawana jeuri hiyo, wataishia kutukana tu na kujifanya watakatifu,ila tumeshawasoma hata waseme Dr slaa ni kichaa wa kwanza duniani hatuwaamini,kwani huyo rweyemam na mkwere pamoja na mafisadi woote ndio vichaa,wezi, majangiri na wachakachuaji.

Shuleni kwetu, mtu mmoja hakwenda mchakamchaka asubuhi kwa sababu aliuhusudu usingizi. Alipotafutwa na mwalimu wa zamu, akajifanya kichaa. Watu wakambeba kumpeleka hospitali ya vichaa. Akagoma akisema mimi siyo kichaa! Wakazidi kumbeba, naye akazidi kusema, mimi siyo kichaaxn. Je, wangemwaminije kama siyo kichaa? TAFAKARI....!
 
The state house is supposed to go further than that and tell us who are DOWANS na sio kuja na maneno ya kashfa kwa Dr Slaa
 
RUTASHUBANYUMA, I would like to respond to your first post by giving facts ili tuwekane sawa tafadhali

A. Sheria inayounda mashirika ya umma inampa rais uwezo wa kuteua mtendaji mkuu wa shirika, hivyo uteuzi wa Dr Rashidi haukukiuka sheria yoyote, hoja kama ana uwezo ama hana ni nyingine

B. Dr Rashidi hakuidhinisha Richmond, aliingia jan 2007 na Richmond iliingia 2006 na walioiingiza si TANESCO ni Govenrment Negotiating Team, tume ya Mwakyembe imeainisha hilo.

C. Walichofanya Richmond baada ya kukosa uwezo ni kuwapa ile tender Dowans , na baraka zote from GNT

D. Dowans haikupitia kwenye Tanesco tender board bali GNT

E. TANESCO opted for Dowans because its already connected to the grid and cheaper than IPTL, all they did was to ask for permission to buy it and not 'kushinikiza' kwa mwenye kujua biashara ya umeme, kutembeza. IPTL ni billion 11 hali Dowans ni billion 2, kama mtu ni mfanyabiashara unaopt kilicho more reasonable cost ways..bei tajwa haikuwa mara 20 kwani haikuwa discussed sijui mwenzangu umepata wapi hii data ?? I commissioned Dowans and am involved in consulting change of IPTL from heavy fuel so I know what am talking about, DOWANS is better off (then )

F.ukiisoma judgement ya ICC utaona si TANESCO waliovunja mkataba ni dowans !! Walivunja na kushtaki TANESCO, thts why mitambo ilishikiliwa kwa kadhia ya kodi..

G, H and I siwezi kuyaongelea, Dr Rashidi amefanyia mengi TANESCO, ashtakiwe kwa mambo aliyofanya prior to TANESCO and not whilst there

Nimeona tu nirekebishee hii ili tujue ukweli uko vipi, kama una ya kuongezea karibu sana ila tunyooshane kwa amani
Mhandisi mifumo na njia kuu za umeme Nsiande.

Nsiande,

Kimsingi uko sawa kujibu hoja. Mimi nakushauri USOME TENA neno kwa neno, hoja za Bwana RUTASHUBANYUMA, kisha uone kama unajibu tena au unatoa hoja!
 
Serikali imebanwa pabaya. Hata hivyo simshangai sana Salva na maneno yake ya kejeli maana anamuiga bosi wake JK nadhani wote mlikuwa mashahidi wakati JK anajibu hoja za wafanyakazi na mgomo wetu wa Mei 2010. Alitoa maneno ya aibu sana. Pia inkumbukwe kwamba Dr. Slaa yeye ndiye aliyepelekea vigogo wote hawa wa Richmond kufikishwa mahakamani na alipotoa orodha yake ya mafisadi alipingwa sana na kusakamwa kila kona na mwisho wa siku aliibuka kidedea. Pia suala la katiba mpya Dr. Slaa alipoliibua likapingwa sana na serikali na sasa ndo wameamua wenyewe kuanzisha mchakato huo.
 
Kama kweli Slaa ni mwongo na anahatarisha Amani ya nchi kwanini wasimshike wampeleke mahakamani na wamfukulie kesi za kumkashifu Raisi kama wanavyofanya kwa mchungaji Mtikila?
 
Mimi nashangaa wana jazba za nini kama wao sio wahusika na Serikali imesema iko tayari kuilipa Dowans basi wawataje wahusika kuliko kuanza kuhangahika na Slaa bure maana serikali haiwezi kulipa fidia mtu ambaye hawamjui kwahiyo hapa ngoma bado iko upande wao vyovyote vile watakavyofanya wasifikiri watanzania ni wajinga kiasi hicho kuwa eti serikali haiwajui wamiliki wa Dowans halafu still bado mnataka kuwalipa ndio pale nilipomshusha hadhi Pinda aliposema Dowans ni genge la watu wachache halafu hapo hapo anarudi na matashi anasema fidia kwa Dowans haikwepeki kama unajua ni genge la watu wachache kwanini usiwataje.

YOU CAN FOOL PEOPLE SOMETIME, BUT YOU CAN NOT FOOL PEOPLE ALL THE TIME
 
Wadau,

Ifuatayo ni taarifa nzima ya Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu, ambaye aliwahi kuajiriwa na Richmond/Dowans kufanya kazi za public relations kwa kampuni hizo kwa kuunganishwa na Rostam Aziz. Nime-forwardiwa email hii na mwandishi mmoja aliyepata nikaona ni vyema niiweke humu JF. Naomba tuitafakari kama ilivyo:

From: "Salvator Rweyemamu" rweyemamu.salvator@gmail.com
Date: Sun, January 2, 2011 11:29 pm
Subject: On Dkt Slaa na Madai yake dhidi ya Mheshimiwa Rais Kikwete kuhusu Dowans

Hi wakubwa

This is important in terms of kuweka ukweli sawa. Tunaomba msaada wenu kwa mujibu wa shughuli zetu za habari. Best regards na usiku mwema.

Salva

[FONT=Book Antiqua, serif]TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU.

[FONT=Book Antiqua, serif]KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Wilboard Slaa, leo, Jumapili, Januari 2, 2011, amekaririwa na Gazeti la Tanzania Daima, linalomikiwa na chama chake hicho, akidai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ni mmoja wa wamiliki wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Dowans.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Huu ni uongo wa mchana, ni uzushi wa karne na propaganda ya hatari. Kwa hakika na kwa namna isiyoweza kuelezeka kwa ufasaha, tumeshtushwa sana na kauli hii ya Dkt. Slaa na hatutaki kuamini kabisa wala kukubali kuwa ni kweli kauli hii imetolewa na mtu ambaye majuzi tu alikuwa akiwania kuwa kiongozi wa juu wa taifa letu, yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Na kama kweli Dkt. Slaa ametoa kauli hii na kusema maneno ya namna hii basi sasa Watanzania wanayo kila sababu na haki ya kuamini kuliko wakati mwingine wowote kuwa mzee huyu sasa amechanganyikiwa na ni mtu wa hatari sana kwa utulivu wa nchi hii. Kwa nini?[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Sababu ni rahisi sana. Mheshimiwa Rais Kikwete siyo mmiliki wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Dowans. Hakupata kuwa mmiliki, siyo mmiliki na wala hatakuwa, hata siku moja, mmiliki wa Kampuni hii. [/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Kama Dkt. Slaa anataka kweli kujua wamiliki wa Kampuni ya Dowans, basi atafute ukweli huo na aachae tabia ya kutapatapa na udhabinadhabina yenye lengo la kuwapaka watu watope. Tabia ya kuwasingizia na kusema uongo kuhusu viongozi wa taifa letu ni tabia ya hatari.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Mheshimiwa Rais Kikwete hahusiki na Kampuni ya Dowans wala na kampuni nyingine yoyote ya kibiashara. Yeye ni kiongozi wa juu kabisa wa siasa wa nchi yetu na siyo heshima wala haki kumhusisha na jambo la kutunga na kuzua na lisilokuwa la ukweli wowote.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Kiongozi huyo wa upinzani ametoa shutuma zake dhidi ya Rais Kikwete kufuatia Kampuni ya Dowans kulishitaki Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na Mahakama hiyo ikaamua kuwa Dowans ilipwe kiasi cha sh bilioni 185.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Dkt. Slaa amezomoko na kumshutumu Rais Kikwete eti kwa sababu Mheshimiwa Rais hakuzungumzia suala hilo katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Ijumaa iliyopita.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Mwaka huu, Dkt Slaa aliwania urais wa Tanzania kupitia CHADEMA na akashindwa vibaya sana. Tokea wakati huo amekuwa mtu wa kutunga na kuzua stori za kila aina ya uongo na umbea kuwachanganya Watanzania kwa sababu ya kinyongo chake cha kushindwa. [/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Tunapenda kuwataka na kuwaomba Watanzania, kama ambavyo wamekuwa wanapuuza uongo na uzushi mwingine wa mara kwa mara wa Dkt. Slaa, waupuuze uzushi na uongo wa sasa kuhusu miliki ya Dowans. Ni sehemu ya tabia iliyoanza kuzoeleka sasa ya Mzee huyo kutapatapa kisiasa.[/FONT]

[FONT=Book Antiqua, serif]Imetolewa na Salva Rweyemamu – Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais - Ikulu[/FONT]
[/FONT]
 
If they are aware that someone is NOT the owner then they must be in a position to know the owner of this Dowans. I wonder why they don't tell us. Is this really a genuine payment? Where is the controller and auditor general
 
Back
Top Bottom