IKULU: Kikwete si mmiliki DOWANS!

IKULU: Kikwete si mmiliki DOWANS!

Hivi inakuwaje nchi inakuwa na watu 'wazushi' na 'vizabizabina' na ambao ni hatari kwa 'usalama wa taifa' lakini wakati huo huo hawakamatwi na vyombo vya usalama? Kama Dr. Slaa ni mtu wa namna hiyo kwa nini hawamkamati? Mimi nashindwa kuelewa hapo! Lakini mkuu wa nchi alipata kusema kuwa 'ukiambiwa kitu jaribu kuchanganya na za kwako'!!

Yaani baada ya kushindwa URAIS, kwenye uchaguzi ulio huru na wa haki, Slaa na wapenzi/wanachama wake wamechanganyikiwa kabisa, hawajui wafanyalo wala wafikirialo. Kila siku ni majungu, fitina, uzushi, uzabizabina, unafiki. Kweli CDM si chama cha kuliongoza taifa hili kamwe, Mungu tuepushe nacho, amen !
 
Kwanza kamsemea mambo yake personal ya baadaye, kwa kusema Kikwete hajawahi, na wa wala hatakuja kuwa mmiliki wa Dowans. Amejuaje mipango binafsi ya Kikwete.

Salva sasa ajiangilie na matamshi yake itafika mahala kila mtu ataufahamu uwezo wake kwamba hatakiwi kufanya kazi ikulu na maamlaka husika zikishindwa kumuondoa kutoka katika ikulu ambayo kimsingi ni mali ya wananchi. Hii inaweza kupelekea watu wachukue sheria mikononi kwa kumuadhibu Salva anachefua sana kwanini hataki kukaa kimya ili heshima yake isichakachuliwe?.
Asipofanya hivyo anavyofanya atafukuzwa kazi....Jamani huyu Salva kwa sasa anatumwa tu hana jinsi...
 
"KURUGENZI ya Mawasiliano Ikulu imeelezea kukerwa kwake na hatua ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kumtaja rais Jakaya Kikwete kuwa alihusika katika uzembe uliosababisha taifa kutakiwa kuilipa kampuni ya Dowans sh bilioni 185 kama fidia.
Taarifa kali ya Ikulu iliyobeba ujumbe wenye maneno ya kebehi na ya mitaani ya kumwita Dk. Slaa mtu ‘aliyechanganyikiwa’ na ‘mzabinazabina’ ilisainiwa na Salvatory Rweyemamu ambaye kabla ya kwenda Ikulu alikuwa mmoja wa wahariri watendaji aliyekuwa akiheshimika kwa kutumia lugha fasaha na ya staha."

End of quote.

Inaonekana hivi sasa moja ya qualifications za mouthpiece ya ikulu yaani kurugenzi ya mawasiliano (Read😛ropaganda) pale ikulu yetu ni ujuzi wa mipasho na lugha za mtaani!Bila shaka na ujuzi wa kutunga mashairi ya taarab ni "added advantage"!Hivi huyu Rweyemamu anapata wapi jeuri ya kumtukana katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani hapa nchini kwa kumwita "KIZABIZABINA"??.Kwa maoni yangu si yeye wala bosi wake mwenye moral authority ya kufanya hivyo haswa kuhusiana na swala lililozungumziwa.Sote tunajua nini kinaendelea kati ya JK,EL,RA et al,Ningemshauri Rweyemamu na waliomtuma watumie lugha yenye hadhi ya ikulu(Diplomatic language)katika kufanya propaganda zake zenye lengo la ku wabrainwash wadanganyika huko vijijini na wasioelewa uozo wanaotaka kuusafisha.Vinginevyo hata hiyo hadhi kiduchu iliyobaki ya ikulu na taasisi yenyewe ya executive powers itakwisha manake wengi wetu tumeshachoshwa na madudu yanayofanyika!Yaani tumechoka kuliko TISS wanavyoweza kuanalyse public mood!!Ikulu yetu sasa haina hadhi!Huwezi kuilinganisha na ile ya mwl.Julius Nyerere wala ya Ben Mkapa.hii haina weledi katika kushughulikia masuala ya mawasiliano,Personal intergrity wala rules of engagement.No wonder wageni kama Lisa Rockefeller wanatushangaa!Lakini kama Rweyemamu ana echo anachoambiwa na bosi wake,hatutakiwi kushangaa.Nilipoangalia hotuba ya rais wa N*C kwenye luninga juzi nilijikuta najiuliza....Is this for real?....na kama Lisa nikasema kimoyomoyo....what a j**&!



"Kikwete plays too much, how can a president tell you something in the audience and when you see him he smiles at you like a little baby? Head of State? Please !!!!" L.M.R
 
Salva kaandika hii kitu saa 5 usiku! maana yake nini? mmmmh! alipewa mistari na wifey!
 
Bwana Salva,

Watanzania hata siku moja hawatakaa wampuuze Dr. Slaa, kwa sababu kasheshe ya ufisadi nchi hii ni yeye ndo aliianzisha..na mabomu yote ya wakubwa yenye kweli tupu ndani yake yeye ndo huwa anayaanzisha, sasa leo una sababu zipi za maana kututaka tupuuze taarifa za jamaa ambaye always ana sources za uhakika?? Au tumpuuze tu kwa hii taarifa yako ilojaa maneno ya street ova mtendaji wa kata ya kigogo ndo kaandika taarifa hii maake humo ndani maneno ya ki prezzo mwanzo mwisho.

Mimi naona kwa jamaa kumzushia prezidaa ni issue nzito, songeni mahakamani jamaa aitwe aambiwe atoe uthibitisho then akishindwa aswekwe mung'anda kwa uchochezi..inajua taarifa kama hizi ni hnyeti kiasi ambacho kina weza hata vunja amani ya nchi..so kuweni serious, kama mnataka watanzania wampuuze slaa chukueni stern measures otherwise mazee hii itakula kwenu.

Wabongo kwa sasa wanamuamini Slaa kuliko mtu mwingine yeyote hasa linapokuja suala nyeti kama hili..mimi ninavyoona mnataka kuipotezea kwa sababu mnajua mkienda court tuu jamaa anakuja na evidence za kutosha, then mshua anaweza hata mwaga unga si unajua...kazi ipo..

Slaa tupe tupe bwana tushachoka maisha yenyewe hayana tofauti na kuwa mfu hata kama sijawahi kufa..
 
Salva ana haja ya kutoa single yake katika mambo ya taarabu, am sure ita-hit sana
 
RUTASHUBANYUMA, I would like to respond to your first post by giving facts ili tuwekane sawa tafadhali

A. Sheria inayounda mashirika ya umma inampa rais uwezo wa kuteua mtendaji mkuu wa shirika, hivyo uteuzi wa Dr Rashidi haukukiuka sheria yoyote, hoja kama ana uwezo ama hana ni nyingine

B. Dr Rashidi hakuidhinisha Richmond, aliingia jan 2007 na Richmond iliingia 2006 na walioiingiza si TANESCO ni Govenrment Negotiating Team, tume ya Mwakyembe imeainisha hilo.

C. Walichofanya Richmond baada ya kukosa uwezo ni kuwapa ile tender Dowans , na baraka zote from GNT

D. Dowans haikupitia kwenye Tanesco tender board bali GNT

E. TANESCO opted for Dowans because its already connected to the grid and cheaper than IPTL, all they did was to ask for permission to buy it and not 'kushinikiza' kwa mwenye kujua biashara ya umeme, kutembeza. IPTL ni billion 11 hali Dowans ni billion 2, kama mtu ni mfanyabiashara unaopt kilicho more reasonable cost ways..bei tajwa haikuwa mara 20 kwani haikuwa discussed sijui mwenzangu umepata wapi hii data ?? I commissioned Dowans and am involved in consulting change of IPTL from heavy fuel so I know what am talking about, DOWANS is better off (then )

F.ukiisoma judgement ya ICC utaona si TANESCO waliovunja mkataba ni dowans !! Walivunja na kushtaki TANESCO, thts why mitambo ilishikiliwa kwa kadhia ya kodi..

G, H and I siwezi kuyaongelea, Dr Rashidi amefanyia mengi TANESCO, ashtakiwe kwa mambo aliyofanya prior to TANESCO and not whilst there

Nimeona tu nirekebishee hii ili tujue ukweli uko vipi, kama una ya kuongezea karibu sana ila tunyooshane kwa amani
Mhandisi mifumo na njia kuu za umeme Nsiande.

Mimi nilvyosoma judgement, baada ya Tanesco kusitisha mkataba walizuia mitambo kwa maelekezo ya Richmond juu ya utata wa umiliki wa mtambo, na mkataba kati ya Richmond na Dowans ulikuwa wazi kabisa juu ya ownership za ule mtambo. Kwa akili ya kawaida, kuna kiongozi au viongozi ambao watakuwa wametoa agizo kuwa Tanesco wazuie mtambo, na kwa busara ya kawaida ailyekuwa waziri kipindi cha kusitisha mkataba angewajibika tuu kwa kuliingizia Taifa hasa ya USD 64 million.

Ni maamuzi ya kitoto sana mfano una mafundi wanakujengea nyumba yako, wamemaliza kazi wewe unazuia wasiondoke na vifaa vyao vya kazi!!!
 
Hii bwabwaja bwabwaja ya Rweyemamu ni ya kipuuzi tu. Kama hii ni defamation kwa bosi wake toka kwa Dr. (wa kweli) Slaa si aende mahakamani?
Rweyemamu anawatumikia mabwana zake. Ukiitafakari lugha aliyotumia katika hiyo statement yake inafanana kabisa na ile tahariri ya kipumbavu iliyotolewa na daily news wakati wa kampeni, author ni mmoja, rweyemamu. Anyway your days are numbered.
 
wakuu mi nilijua nasoma lyrics za taarabu kumbe msemaji wa ikulu..tuhuma nzito kama hiyo haihitaji majibu ya mipasho,wamuweke hadharani mmiliki halisi watutoe kwenye hili giza,sio kumponda docta slaa bila kutupa majibu sahihi kwenye maswali magumu..kumbuka Epa,Eptl,kagoda..list ya top 10 ya mafisadi ..wanatoa majibu rahisi afu ukweli unawaumbua...

Topic hapa ni uongo wa Slaa!
 
Salva ana haja ya kutoa single yake katika mambo ya taarabu am sure itahit sana

Jibu hoja, wacha firimbi. Slaa ni muongo tena kizabizabina, hayo ndio inatakiwe uyatetee au uyakubali, achana na ngonjera.
 
Mwaka huu, Dkt Slaa aliwania urais wa Tanzania kupitia CHADEMA na akashindwa vibaya sana. Tokea wakati huo amekuwa mtu wa kutunga na kuzua stori za kila aina ya uongo na umbea kuwachanganya Watanzania kwa sababu ya kinyongo chake cha kushindwa.

Hii aya nadhani aliiandika 'mkwere' mwenyewe na sio Salva! Hivi hawa kina Salva mbona wanaidhalilisha sana Ikulu?
 
My take,

Hii siyo official communication ya Ikulu kwani kwenye covering email ameomba msaada washikaji kurekebisha mambo. Press release hazihitaji msaada wa mwandishi au mtu mwingine yeyote kudeliver message. Pia katumia email binafsi. Siamini ofisa wa ngazi yake katika nchi hata kama ni maskini hana email ya ki-ofisi. Kwa hiyo wakuu tusubiri kauli ya Ikulu. Hii ilikuwa ni teaser tu!

Hi wakubwa

This is important in terms of kuweka ukweli sawa. Tunaomba msaada wenu kwa mujibu wa shughuli zetu za habari. Best regards na usiku mwema.


Salva

Hata hivyo lengo la Dk Slaa limefanikiwa kwa asilimia zaidi ya 150! Na bado tutasikia mengi zaidi.

Babu DC!
 
Sikio la kufa halisikii dawa. Wakati wa ikulu ya tanzania kusima katika kusudi la Mungu aliye hai umefika. Wote waliotumbukia katika Ikulu kama Yona alivyotumbukia katika tumbo la Nyangumi, umefika wakati wao wa kutemwa. Tutaanza kushuhudia wakifa kwa presha na magonjwa ya aibu. Subirini misiba inakuja hivi karibuni.
 
Hivi jamani France hawana freedom of information act, hili tuweze kupata ruling ya ICC? Mimi najitolea kuilipia kwa pesa yoyote kama kutakuwa na gharama yoyote
 
Nenda BRELA au Chamber of Commerce, hiyo si kazi ya Salva.

Anayekanusha, na hasa kwa taasisi kama ikulu/serikali ni lazima ilistahili kuja na vielelezo sawia juu ya nani mmiliki wa Dowans, na hapo wangekuwa wamefanikiwa kumwondoa Rais katika kadhia hii lakini wameleta porojo na kejeli ambazo hata mtu yeyote anayetuhumiwa anaweza kutamka. Without coming out with evidences of disengaging the precident in this dirty game, in fact they have proved the president is part of it.
 
Show me your friends and I will tell who you are! majibu ya Salva yana reflect mojaa kwa moja maoni ya Boss wake! Wtz wote hivi saa si wageni tena wa tabia za JK, tunamjua ni mpenda sifa, mpenda visasi, mlimbikiza mali kwa kutumia majina ya watoto wake, puppet wa EL and RA so no suprising hata watendaji wa Ikulu wana act the same! Wote wanaishi kwa falsafa moja tu " Ukifanikiwa kuondoa ukweli wote, kinachobaki ndio ukweli wenyewe" yaani maana yake uongo ndio utakuwa ukweli!
 
Hivi huyo Salva ana elimu gani, labda tuanzie hapo.
Na hio Taarifa imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kwa maana Rais ndo kamwagiza aandike hivyo au ni yake Salva binafsi. kwa sababu i thought at last angesema Rais ana nia ya kumshtaki Slaa kwa maneno hayo yaliyotolewa,lkn hakuna kitu kama hicho, nnachokiona ni matusi tu. Halafu anataka Watanzania wapuuze maneno ya Slaa, kivipi, bila kuleta hoja za msingi
 
Hivi ndivyo taafia ya Ikulu ilivyoripotiwa na Tanzania Daima la leo (4 Jan 2011)

Dk. Slaa aishika pabaya Ikulu

• YATUMIA MANENO YA KEJELI, MTAANI KUJIBU HOJA ZAKE

na Edward Kinabo




KURUGENZI ya Mawasiliano Ikulu imeelezea kukerwa kwake na hatua ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kumtaja rais Jakaya Kikwete kuwa alihusika katika uzembe uliosababisha taifa kutakiwa kuilipa kampuni ya Dowans sh bilioni 185 kama fidia.

Taarifa kali ya Ikulu iliyobeba ujumbe wenye maneno ya kebehi na ya mitaani ya kumwita Dk. Slaa mtu ‘aliyechanganyikiwa' na ‘mzabinazabina' ilisainiwa na Salvatory Rweyemamu ambaye kabla ya kwenda Ikulu alikuwa mmoja wa wahariri watendaji aliyekuwa akiheshimika kwa kutumia lugha fasaha na ya staha.

Rweyemamu katika taarifa yake hiyo iliyoonyesha waziwazi kuandikwa na mtu mwenye hasira, chuki na dharau ama kwa Dk. Slaa, CHADEMA na Tanzania Daima alikwenda mbele na kumwita kiongozi huyo wa kisiasa kuwa ni mtu hatari.

Sehemu ya maneno makali ya Rweyemamu kwa Dk. Slaa ni kama yale aliyosema, "Na kama kweli Dk. Slaa ametoa kauli hii na kusema maneno ya namna hii basi sasa Watanzania wanayo kila sababu na haki ya kuamini kuliko wakati mwingine wowote kuwa mzee huyu (Slaa) sasa amechanganyikiwa na ni mtu wa hatari sana kwa utulivu wa nchi hii."

Rweyemamu aliendelea kueleza, "Kama Dk. Slaa anataka kweli kujua wamiliki wa Kampuni ya Dowans, basi atafute ukweli huo na aachane na tabia ya kutapatapa na uzabinazabina yenye lengo la kuwapaka watu watope."

Ikulu ambayo katika mazingira ambayo si rahisi kuyaeleza imekuwa na desturi ya kukanusha kwa nguvu kubwa kila wakati jina la Rais Kikwete linapohusishwa na sakata la kashfa ya Richmond/Dowans.

Hii ni mara ya pili kwa Ikulu kufanya hivyo baada ya mara ya kwanza kuchukua hatua kama hiyo wakati Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, alipokanusha hoja zilizokuwa zikijaribu kumhusisha Rais Kikwete na uhusiano wake na mkataba wa Richmond.

Wakati Ikulu ikikanusha mara kwa mara kuhusishwa kwa Kikwete katika sakata la Richmond/Dowans kwa namna yoyote ile, upo ushahidi wa kibunge (rejea ripoti ya Kamati Teule ya Mwakyembe) unaoonyesha kwamba, maamuzi kuhusu mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura ulioipa ushindi Richmond ulijadiliwa na Baraza la Mawaziri lililokuwa chini ya uenyekiti wa rais mwenyewe.

Kama hiyo haitoshi, gazeti moja la kila wiki linalomilikiwa na kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambalo Rweyemamu amepata kuwa mmiliki wake, limepata kuchapisha katika ukurasa wake wa mbele barua ikionyesha barua aliyoandika aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kwenda kwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini kuhusu suala la Richmond ambayo nakala yake ilikwenda pia kwa Rais Kikwete.

Uamuzi wa jana wa Rweyemamu kuandika taarifa kali dhidi ya Dk. Slaa unakuja siku chache baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa migogoro ya kibiashara hivi karibuni kuamuru Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) kuilipa Dowans fidia kubwa baada ya kuvunja mkataba nayo kinyume cha taratibu.

Katika mahojiano maalum na gazeti Tanzania Daima Jumapili, la juzi Dk. Slaa alikaririwa akisema chanzo cha suala zima lililopelekea Dowans kutakiwa kulipwa fidia hiyo ni uzembe wa serikali na Rais Kikwete mwenyewe kwani ndio waliohusika katika kuileta kampuni ya Richmond ambayo baada ya kuonekana ya kitapeli iliamua kurithisha kazi zake kwa Dowans.

Ikulu katika taarifa yake hiyo kwa sababu zisizojulikana ilijikuta ikipotoka ama kwa makusudi au kwa kutojua ilipoeleza kuwa gazeti la Tanzania Daima lililonukuu maelezo ya Dk. Slaa, linamilikiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakati taarifa zilizopo kwa msajili wa magazeti zinaeleza bayana kwamba, gazeti hilo ni la watu binafsi.

Ikipinga maelezo ya Dk. Slaa kuhusu uhusiano wa rais Kikwete na Dowans, taarifa hiyo ya Ikulu ilisema, "Huu ni uongo wa mchana, ni uzushi wa karne na propaganda ya hatari. Kwa hakika na kwa namna isiyoweza kuelezeka kwa ufasaha, tumeshtushwa sana na kauli hii ya Dk. Slaa
"Mheshimiwa Rais Kikwete siyo mmiliki wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Dowans. Hakupata kuwa mmiliki, siyo mmiliki na wala hatakuwa, hata siku moja, mmiliki wa kampuni hii."

Ikitumia lugha kali dhidi yake Ikulu iliwataka wananchi wampuuze Dk. Slaa ikidai kuwa ni mzushi na amechanginyikiwa.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa Dk.Slaa kuitwa mzushi na vigogo wa serikali kwani mara kwa mara anapoibua maovu amekuwa akipingwa kwa kuitwa jina hilo ingawa anayoibua huthibitika kuwa na ukweli ndani yake.

Source: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=22520
 
Back
Top Bottom