IKULU: Dkt. Bashiru Ally Kakurwa aapishwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na Balozi

kwakupewa hadhi ya diplomatic inaendana.na kazi yake hio mpya.lazima awe na gamba jekundu na akifika nchi yoyte anakuwa na sawa ya hadhi ya diplomat.uwage unauliza ikiwa kitu una ujinga nacho
Asante kwa jibu hili. Nilikuwa najiuliza uhusiano wa ubalozi na ukatibu mkuu.
 
Hahahaaaa...... hahahaaaa..... hahahaaaa......!

Nimekucheka sana na kukupuuza bwashee!
Siyo vizuri kuwacheka watu, hasa zama hizi ambazo watu kulazwa kwenye mitungi ya oxygen ni kawaida kama mzaramo kulala ngomani.
Ukute ndiyo amezinduka kutoka kwenye mtungi wa oxygen.
 
Hivi bado inaruhusiwa kuwa na vyeo viwili.

Ama ilikuwa ni kauli iliyowalenga baadhi ya watu tu baada ya wao kuguswa na wameisha sasa haihusu tena.
kaupata pamoja na ukatibu mkuu kwa mpigo ameteuliwa vyeo viwili wewe ndie huna habari.Sasa hivi ni balozi pia
 
Serikalini mijizi mjiandae kukiona cha mtema kuni akiwa katibu mkuu CCM kapambana na mijizi kweli kweñi na kurudisha mali za chama

Sasa kaja serikalini mtamkoma Dk Bashiru
Kwani yeye anakagua wapi? Acha kutisha watu. Labda kama atafanya siasa kuweka watu wake anaowataka.

Ubadhirifu kama hadi sasa wanashindwa kuumaliza na bashiru akiwa ndiyo mwenye chama kinachotwala na kuisimamia serikali sasa na yeye anaenda kusimamiwa na chama.

Kama ripot za CAG hazifanyiwi kazi.

Takukuru wanafanya siasa.

Huku kwa DCI ndo uozo mtupu.

Hatuwezi kutoboa bila ya kuwa na mifumo imara inayombana kila mtu ili awe muadilifu hata kwa lazima.
 
kaupata pamoja na ukatibu mkuu kwa mpigo ameteuliwa vyeo viwili wewe ndie huna habari.Sasa hivi ni balozi pia
Hatukusikia juu ya kuteuliwa kwake kuwa balozi, au ukiteuliwa tu kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, automatically unakuwa balozi?

Na ndivyo imekuwa hivyo wakati wote toka uongozi wa Mwalimu? Makatibu Wakuu Viongozi wote waliteuliwa pia kuwa mabalozi?

Marehemu Kijazi, najua alikuwa Balozi kwa sababu kabla ya uteuzi, alikuwa balozi nchini India.

Ufafanuzi - kutoka kwa mtu mwenye uelewa wa kutosha kuhusiana na hii nafasi.
 
Serikalini mijizi mjiandae kukiona cha mtema kuni akiwa katibu mkuu CCM kapambana na mijizi kweli kweñi na kurudisha mali za chama

Sasa kaja serikalini mtamkoma Dk Bashiru
Yehodaya, kama ukiacha ushabiki, kiuhalisia, rushwa na ubadhirifu, bado sana ndani ya CCM na Serikali.

Uchaguzi wa kura za maoni, kilikuwa kipimo kizuri sana. Tuna ndugu, marafiki ambao ni viongozi wa CCM, wanaCCM, viongozi wa Serikali, viongozi kwenye vyombo vya ulinzi na usalama, japo hakuna takwimu, lakini kama wapo wagombea ambao hawakutoa hongo kwa wajumbe, basi ni wachache sana.

Sisi wengine, tumewahi kuombwa rushwa, tena na watu wenye mamlaka makubwa, tunaowaheshimu, wateule wa Rais, tena anaowasifu sana kwa uchapakazi. Hata unapoambiwa, huamini kama ndiye aliyekuomba.

Unaweza kupinga, lakini nakuhakikishia, miongoni mwa Mawaziri hawa tulio nao, wenye uwezo wa kukataa rushwa, ni wachache sana. Wote wenye kujipendekeza sana kwa Rais, ni waoga maisha. Kwao uongozi wanaona ndiyo umewapa maisha. Hawa shida yao ni kuwa na hela, wakipewa hela, hawakatai. Wanamsifia Rais kupita kiasi kwa sababu wanaona ndiye anayewahakikishia wao kupata fedha.
 
Hatukusikia juu ya kuteuliwa kwake kuwa balozi, au ukiteuliwa tu kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, automatically unakuwa balozi?

Na ndivyo imekuwa hivyo wakati wote toka uongozi wa Mwalimu? Makatibu Wakuu Viongozi wote waliteuliwa pia kuwa mabalozi?

Marehemu Kijazi, najua alikuwa Balozi kwa sababu kabla ya uteuzi, alikuwa balozi nchini India.

Ufafanuzi - kutoka kwa mtu mwenye uelewa wa kutosha kuhusiana na hii nafasi.
Wewe peke yako ndio hujasikia na kusoma!
 
Hapa sijaelewa, Ni kwamba balozi Bashiru ataendelea pia kuwa Katibu mkuu wa CCM?

Au ile mipango yote ya CCM kwa kuwa anaijua basi sasa ana nafasi ya kuitekeleza yeye mwenyewe moja kwa moja katika nafasi yake mpya ya Katibu mkuu kiongozi?

Yote kwa yote naamini ilani ya CCM itatekelezwa kwa 100%

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom