IKULU: Dkt. Bashiru Ally Kakurwa aapishwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na Balozi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
45,145
2,000
Rais Magufuli leo saa 3.00 asubuhi ananamuapisha Katibu mkuu kiongozi mteule Dr Bashiru Ally.

Tukio hili muhimu litakuwa mubashara katika luninga zote za ndani zikiwemo Upendo tv, ITV, TBC, Channel ten, Star tv nk

Karibu.

Updates:

Rais Magufuli ameshaingia ukumbini na Dr Bashiru anakula kiapo chake cha ubalozi na kitafuatia cha ukatibu mkuu kiongozi.

Na sasa Katibu mkuu kiongozi balozi Bashiru anakula kiapo cha uadilifu mbele ya Jaji Mwangesi ambaye ni Kamishna wa Tume ya Maadili!

===
1614425002779.png

Dkt. Bashiru Ally leo ameapishwa kuwa Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo amesema alipata taarifa za uteuzi kupitia Mitandao ya Kijamii.

Akizungumza baada ya kula kiapo, ameeleza kuwa kwa maadili na utamaduni, kazi za Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi sio kazi za maneno bali ni za kusikiliza, kujifunza na kuchambua, kuamua na kutenda.

Amesema, "Wale waliotegemea kwamba nitazungumza tena kwa kweli nitazungumza kwa tahadhari na umakini kwasababu kiapo mmekisikia. Ni Katiba, Sheria, taratibu, mila, desturi".

Aidha, amezungumzia suala la umuhimu wa mawasiliano ndani ya Serikali na kati ya Serikali na Umma akisema watasimamia hilo

6A81EC38-CA68-43AB-850F-03D9EF8B6847.jpeg
 

Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
12,153
2,000
kaupata pamoja na ukatibu mkuu kwa mpigo ameteuliwa vyeo viwili wewe ndie huna habari. Sasa hivi ni balozi pia.
Nyie Ma Nyumbu mapiga Zumari mnabakia Kubweka bweka tu wakati wenzenu wanagawana keki ha Taifa.
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
1,441
2,000
Inaonekana hupo organized. Ndiyo maana mara nyingi tunakupuuza.

Bashiru, tangu lini ni balozi? Mtu asiye makini kwenye vitu vidogo, kamwe hawezi kuwa makini katika makubwa.
 

julaibibi

JF-Expert Member
Jun 16, 2020
1,064
2,000
Inaonekana hupo organized. Ndiyo maana mara nyingi tunakupuuza.

Bashiru, tangu lini ni balozi? Mtu asiye makini kwenye vitu vidogo, kamwe hawezi kuwa makini katika makubwa.
Kwakupewa hadhi ya diplomatic inaendana na kazi yake hio mpya. azima awe na gamba jekundu na akifika nchi yoyte anakuwa na sawa ya hadhi ya diplomat. Uwage unauliza ikiwa kitu una ujinga nacho
 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,610
2,000
Tangu jana kateuliwa balozi
Hebu nipe shule kidogo hapa.

Nilidhani balozi ni lazima kawakilishe maslahi ya nchi kwenye nyingine

Atawezaje kufanya hizi kazi mbili kama sio tatu(na ukatibu mkuu wa lumumba)?

Kuna ubalozi wa heshima? Una faida gani?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom