Ikulu, Dar: Mrejesho Ziara ya Rais Samia Nchini China na Misri

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu (DPC), Zuhura Yunus akizungumza na Vyombo vya Habari Ikulu jijini Dares Salaam leo Tarehe 12 Novemba, 2022



ZIARA YA RAIS SAMIA NCHINI CHINA

POLE ZA AJALI YA PRECISION AIR
Ningependa tu kwa niaba ya Rais kutoa pole kwa wafiwa wote wa ajali ambayo ilitokea ya kampuni ya Precision Air iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Bukoba. Kwa taarifa tu kutakuwa na mkutano wa dharura tarehe 14, siku ya Jumatatu, jijini Dodoma, utakaojadili zaidi janga hilo.

ZIARA YA KIHISTORIA
Na sasa baada ya taarifa hiyo tuelekee katika ziara yenyewe. Kama mnavyojua Mh. Rais kuanzia tarehe 2 - 4 mwezi huu Novemba, alikwenda nchini China kwa mwaliko maalum wa Rais wa nchi hiyo Xi Jinping. Ziara hiyo ilikuwa ni ya kihistoria. Hakika, ni kwasababu ni ziara iliyofanywa na kiongozi wa juu kutoka barani Afrika tangu kumalizika kwa mkutano wao wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CCCP).

ZIARA YA KWANZA YA KIONGOZI WA AFRIKA TANGU COVID-19
Vilevile, ziara hizo ni miongoni mwa za kwanza kabisa tangu lile janga la COVID-19. Yeye ndiyo kiongozi wa kwanza kabisa wa Afrika kutembelea nchi hiyo; kama nilivosema kwa mwaliko wa Rais mwenyewe - Xi Jinping.
Kwa ujumla wake, ziara ilienda salama; ilikuwa nzuri sana. Na mbali na kukutana na mwenyeji wake Xi Jinping, vilevile alikutana na Waziri Mkuu wa China na pia Spika wa Bunge la China. Kwahiyo, alikutana na viongozi wa nafasi zote - karibia - za juu.

USHIRIKIANO WA CHINA-TANZANIA
Kwa kifupi tu nitaelezea mafanikio. Kwanza, ni suala la kidiplomasia. Kulikuwa na mazungumzo ya kina sana hapa, hasa China na Tanzania kuendeleza ushirikiano, hasa kwakuwa nchi hizo tayari zianashirikiana katika masuala ya kimataifa na kikanda.

USHIRIKIANO WA KIMKAKATI
Na vilevile, walikubaliana kupandisha hadhi mahusiano yao - yaani baina ya China na Tanzania ili kuwa na ushirikiano wa kina na kimkakati katika nyanja zote. Kwa Kiingereza wanaita Comprehensive Strategic Cooperative Parternership. Hilo ni muhimu sana kwasababu maana yake ni nini; ni kwamaba nchi hizo zitakuwa na mawasiliano ya mara kwa mara muda wowotw kwa maslahi mapana ya nchi zote mbili.

Na vilevile, ushirikiano wa nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali yanakuwa yakipewa kipaumbele... na ndiyo maana kupandisha hadhi ushirikiano huo lilikuwa ni jambo kubwa sana na la muhimu.

UAGIZAJI WA BIDHAA KUTOKA TANZANIA
Kiuchumi ni kwamba wameongeza zaidi uagizaji wa bidhaa kutoka Tanzania. Kwahivyo, wafanyabiashara wetu wa Kitanzania watanufaika na hilo hasa katika bidhaa zetu za kilimo, mifugo uvuvi na madini.

KUTOTOZA USHURU KWA 98% BIDHAA ZINAZOTOKA TANZANIA
N vilevile China imeahidi kutotoza ushuru kwa 98% ya bidhaa zinazosafirishwa kutoka Tanzania kwenda China. Kwahiyo, bila shaka hilo ni jambo la msingi sana na lenye faida kwa wafanyabiashara wa Tanzania.

KUONGEZA UWEKEZAJI
China, vilevile, imeahidi kuongeza uwekezaji wa hapa Tanzania kwa kupitia makampuni yao ya China ili kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi yetu.

UJENZI WA VIWANDA
Zimekubaliana pia ushirikiano katika ujenzi wa viwanda ili kuiongezea nchi yetu uwezo katika uzalishaji, usindikaji na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.

UCHUMI WA KIDIGITALI
Na wakubaliana kukuza ushirikiano kwenye Uchumi wa Kidigitali - yaani Digital Economy; Uchumi wa Bluu (Blue Economy) na Maendeleo ya Kijani (Green Development) - ambayo kwa kifupi ni dhana ya kuhakikisha kwamba utekelezaji wa miradi mbalimbali unazingatia suala la mazingira.

KUFUFUA RELI YA TAZARA
Na pia miongoni mwa miradi ambayo wamejadili na bado mazungumzo yanaendelea, lakini wako tayari kuiunga mkono Tanzania, ni kutekeleza mradi wa kufufua Reli ya TAZARA.

ULINZI NA USALAMA
Nchi zote zimekubaliana kuimarisha ushirikiano ili kudumisha amani na usalama.

MASUALA YA KIJAMII
Mwaka 2024 nchi zote mbili zitaadhimisha miaka 60 ya mahusiano ya kidiplomasia; kwahiyo wamekubaliana kuwa uwe mwaka wa utalii wa utamaduni wa China na Tanzania. Namna ambavyo itakuwa tutajua baadaye lakini mwaka 2024 nchi zote mbili zitashirikiana katika hilo.

UFADHILI WA MASOMO na TIMU ZA MATIBABU
China wameahidi kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Kitanzania zaidi kwasababu tayari wanatoa, lakini ziada.

Na vilevile wameahidi kupeleka timu za matibabu Tanzania Bara na vilevile Zanzibar.

USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Mambo mengine ambayo wamezungumzia ni Ushirikiano wa Kimataifa ambao wamekuwa nao lakini wataongeza.

UTIAJI SAINI HATI ZA MAKUBALIANO 15
Jambo lingine kubwa ni utiaji saini Hati za Makubaliano mbalimbali, mikataba. itifaki pia. Jumla zilitiwa saini Hati za Makubaliano 15:

1. Fursa Zinazopatikana
i. Wakulima wa Tanzania - hasa wanaolima zao la parachichi, sasa wamefunguliwa fura kabisa ya kuuza maparachichi katika soko kubwa la China.

ii. Wavuvi wa Tanzania - hasa wanaofanya biashara ya kuuza mabondo ya samaki. Nao wamefunguliwa fursa ya kuuza bidhaa zao katika soko kubwa la China. Awali, kama mnavyojua, wauzaji wa mabondo walikuwa wanauza bidhaa zao katika la China lakini ilikuwa lazima wapitie nchi ya Vietnam. Lakini sasa, kuna makubaliano haya - itakuwa moja kwa moja.

2. Sekta ya Utalii
Sekta ya Utalii natyo imepata manufaa. Wamepata msaada wa kujenga Makumbusho ya kisasa ya kutunza nyayo za binadamu wa kwanza wenye umri wa miaka milioni 3 zilizopo katika Hifadhi ya Ngorongoro.


ZIARA YA RAIS SAMIA NCHINI MISRI - COP 27
Kulikuwa na mkutano mkubwa sana, ambao bado unaendelea, wa kiataifa, wa masuala ya tabianchi unaojulikana kama COP27.

Kwahiyo, Tanzania ni mojawapo ya nchi nyingi duniani ambazo zimehudhuria kule Sharm el-Sheikh, nchini Misri. Na mbali na kupambana na mabadiliko ya tabianchi pia lilikuwepo suala la kuchapusha miradi kupunguza Kaboni.

Jambo kubwa mojawapo lilikuwa uzinduzi wa kujenga uwezo wa kimtandao wa kuunganisha gridi za umeme za nchi za kusini mwa Afrika pamoja na nishati Jadidifu - maarufu kama Southern African Power Pool (SAPP). Na hii mahsusi ili kuvutia wawekezaji kuweza kuzalisha nishati jadidifu nafuu, kwa wingi, yenye kutosheleza na yenye kuzingatia utunzaji wa mazingira.

Katika mkutano huo ambao wenyeji walikuwa ni Tanzania, yaani Rais Samia Suluhu Hassani, ndiye alikuwa mwenyeji wa mkutano huo, mkutano wa namna hii unakuwa unafanyika pembeni ya mkutano mkuu. Ni jambo kubwa kwani mara nyingi kupata fursa ya kuandaa mkutano wa namna hiyo ni lazima upate Rais zaidi ya mmoja. Kwahiyo, katika mkutano huo, Rais Samia alifanikiwa kupata zaidi ya Marais walili, watatu.

Waliohudhuria ni:

1. Rais wa Zimbabwe - Emmerson Mnangagwa; Rais wa Malawi - Lazarus Chakwera; Rais wa Botswana - Mokgweetsi Masisi; Makamu wa Rais wa Angola. Na vilevile kulikuwa na taasisi mbalimbali kubwa za dunia. Ulihudhuriwa na Rais wa Benki ya Dunia, David Malpass; Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Akinwumi Adesina; Mwakilishi wa Africa 50; Mwakilishi wa Total Energies; Kamishna wa Umoja wa Afrika; Rais wa MEA; na wageni wengine mbalimbali.

Na kutokana na mkutano huo uliofanyika, Tanzania imeahidiwa dola za Kimarekani Bilioni 18 kutoka Benki ya Dunia (WB) kwa ajili ya uwekezaji kwenye miradi ya nishati jadidifu ikiwemo pia miyndombinu yake na usafirishaji wa umeme.

MIRADI YA NISHATI JADIDIFU
Marais wanachama wa SAPP nao bado mazungumzo yanaendelea kuongeza kasi kwenye miradi ambayo itaiunganisha nishati kutoka nchi moja hadi nyingine na kutoa ushirikiano unaohitajika katika ngazi ya kitaifa.
Africa 50 nayo imeahidi kufanya kazi na Tanzania kwenye miradi ya nishati jadidifu vilevile. Kuna taasisi nyinyine, Africa Energy, nao kwa kushirikiana na Jumuiya ya Viwanda vya Nishati Jadidifu ya China imesema nayo itasaidia maendeleo ya awali na miradi miwili ya nishati hiyo kwa njia ya msaada na kufanya kazi na serikali ya Tanzania kutambua na kuwashirikisha watekelezaji wa mradi huo.

BANDA LA TANZANIA COP27
Nchi yetu kwa mara ya kwanza imeweza kuwa na banda lake maalum kwenye shughuli hiyo ya COP27, ambalo sasa limetumika kuendesha mikutano mbalimbali pamoja na kutoa elimu ya mazingira. Washiriki tofauti waliokuwepo walipata fursa kuifahamu Tanzania kisera na kimkakati na jinsi ya kupambana na tabianchi.

FURSA HEWA YA UKAA (CARON CREDIT)
Na jambo kubwa lilikuwa pia jinsi Tanzania ilivyojipanga kuendesha na pia kunufaika na fursa ya rasilimali zitokanazo na hewa ya ukaa (carbon credit). Tanzania inaonekana ina uwezo mkubwa sana wa carbon credit. Taasisi mbalimbali katika mkutano huo zilionesha kuwa na nia katika biashara hiyo.

Katika banda la Tanzania pia Shirikisho la Vijana wa Afrika lilizinduliwa ili kukuza wajibu wa vijana hao kwenye Nishati Jadidifu na Nishati Kijani kupitia teknolojia ya sayansi na digital. Kulikuwa na nchi mbalimbali za Afrika kutoka Nigeria, Gambia, Kenya, Afrika Kusini, Uganda, na Tanzania yenyewe.

Jambo jingine ni Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, waziri Makamba, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (Mhandisi Mramba) na Mhandisi James Mataragio, walikutana na Rais na Afisa Mtendaji wa kampuni ya kimataifa ya nishati, Equinor, kujadili mradi wa kuchakata gesi asilia (LNG).

Kwa kifupi, katika mkutano huo, hayo ndiyo yaliyojiri.
 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu (DPC), Zuhura Yunus akizungumza na Vyombo vya Habari Ikulu jijini Dares Salaam leo Tarehe 12 Novemba, 2022


This is good!, huyu sasa ndio Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu.
Ukitokea mtu ukashauri jambo, halafu ukashuhudia hilo jambo linatelelezwa kama ulivyo shauri, hata kama utekelezaji huo sio kufuatia ushauri wako, hata usinge shauri wewe jambo hilo lilikuwa tayari kwenye mpango mkakati wao, bado huna budi ku appreciate. Alichokifanya Gerson Msigwa, New York alipaswa akifanye Siku Zote Ikulu. Zuhura Yunus Asiwe Bubu!
Humo nilisema
Wanabodi,
leo nilikuwa naangalia TBC Ardhio..
[*]Hongera Sana Gerson Msigwa kurudia kazi yako ya utangazaji!. Hiki ulichokifanya leo jijini New York, nchini Marekani, ndicho ulipaswa ukifanye Ikulu yetu, siku zote ilipokuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu.
[*]Kazi ya Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, sio tuu ni kuandika Press Release, bali pia kuiripoti direct from Ikulu kwa piece to camera kama ulivyo fanya leo.
[*]Ulipaswa kuturipotia shughuli muhimu za rais ikitokea Ikulu, na kuiripoti moja kwa moja into the news.
[*]Pia ulipaswa kuitisha Press Conference na kufanya Press Briefing kwetu sisi waandishi kama walivyofanya Balozi Choks, Balozi Nkurlu na Balozi Kalaghe, na kama wafanyavyo ma Press Sec wa wenzetu Duniani.
[*]Naamini Zuhura Yunus hata kuwa Bubu, ikitokea rais ana shughuli muhimu, asiishie kutusambazia just a press release bali sasa sambazeni multi media release yenye press release, photo gallery, audio footage, TV footage, social media footage na Peace to Camera.
[/LIST]
All and all, hongereni sana for all that you are doing, Leo sisi huku Bongo ni hakuna kulala mpaka hiyo saa 8:30 usiku wa manane.
Tunawasubiria tushuhudie.
Paskali.
P
 
Huyuhuyu!!!!
20220202_104305.jpg
 
Siamini kama kuna jambo la maana atakalo zungumzia! Zaidi tu ya bla bla za hapa na pale.
Hana jipya lolote, maana Boss wake kila siku anahutubia. Ama yeye atakuwa na mambo tofauti na anayohubiri boss wake?
Wakuu Tate Mkuu, na Tindo, please lets change atitude, ondoa negative pre conceived ideas ya kuamini kama atazungumza lolote la maana, be positive!, listern with forward looking aproach kwa kumsikiliza kwa makini, halafu akiisha maliza ndipo ufanye analysis na kusema kama kuna la maana ama hakuna!. Ukisha anza kuwa na a biased negative perspective, ubongo wako utapoteza objectivity, hiyo bias itakufanya hata azungumze mazuri vipi wewe hutayaona, hutayasikia na kuishia kuona hakuna la maana alilozungumza.
P
 
Mkuu Tate Mkuu, please lets change atitude, ondoa negative pre conceived ideas ya kuamini kama atazungumza lolote la maana, be positive!, listern with forward looking aproach kwa kumsikiliza kwa makini, halafu akiisha maliza ndipo ufanye analysis na kusema kama kuna la maana ama hakuna!. Ukisha anza kuwa na a biased negative perspective, ubongo wako utapoteza objectivity, hiyo bias itakufanya hata azungumze mazuri vipi wewe hutayaona, hutayasikia na kuishia kuona hakuna la maana alilozungumza.
P
Pascal with due respect hivi kweli Zuhura ataongea nini?....nchi ina hali mbaya sana...ni kweli mengine hayajasababishwa na Serikali lakini ukweli ni kwamba hawa tunaowaita viongozi HAWANA UWEZO wa kutatua hizi changamoto PERIOD.
 
Back
Top Bottom