CHIEF MASALAKULANGWA
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 794
- 646
Hapana mimi nashauri Bunge lianze kwa kupokea na kujadili Mswada wa Bima ya Afya Kwa Wote (Universal Health Coverage Bill).Hili kwangu na kwa Watanzania wengi ni la muhimu na la haraka sana kuliko la Katiba Mpya, ambalo, kwa kweli ni la viongozi wa CHADEMA tu kwani hata wanachama wao huko Mwanza na Iringa au Mbeya wamewakana na kuwataka viongozi wao waanzie na Katiba yao, ya CHADEMA, kwanza kabla ya hii wanayotaka.Suala la katiba lipewe kipaumbele sana.
Katiba ni uhai.
Yapo mengi ya hatari sana kwenye katiba hii.
Lakini hili la Mrithi wa rais anayefariki dunia, kuwa ni makamu wa rais (automated) ni hatari sana kwa marais endapo tukipata Makamu asiyemwaminifu.
Pia linachangia sana kumuweka mbali makamu wa rais kuwa karibu na rais kwa hofu ya kutoaminia! (Naturally internal conflict)
Kwa gharama yoyote naomba tuanze na katiba inafaida kwetu sote matajiri na masikini, viongozi na watawaliwa.