Ikiwezekana, Bunge lianze na mswada wa dharura kujadili Katiba Mpya; hii Katiba ya sasa kitendo cha Makamu kutambuliwa kuwa mrithi ni hatari

Katiba ni mbovu ndo maana tunataka waanze nayo
Mtu asiyejua kuendesha gari hata akilalamika Volkswagen Beetle haina speed anataka Ferrari atakuwa mzushi tu.

Kwa sababu hata akipewa Ferrari, tatizo lake la kutojua kuendesha gari halitatoweka.
 
Inashangaza sana tunavyotaka Katiba Mpya, kwani ipo kwenye Ilani ya Uchaguzi?
Hebu tumpe nafasi Rais ambaye ni chaguo la Mungu afanye kazi yake

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Mtu asiyejua kuendesha gari hata akilalamika Volkswagen Beetle haina speed anataka Ferrari atakuwa mzushi tu.

Kwa sababu hata akipewa Ferrari, tatizo lake la kutojua kuendesha gari halitatoweka.
Lakini kwenye mashindano ya magari hata ukiwa dereva mzuri kama utatumia trekta basi utakuwa huna mpango wa kushinda
 
Unaacha kujadili nikichokueleza.

Kama hujui kuendesha gari, it doesn't matter upewe trekta au Ferrari.

Katiba ya sasa imevunjwa wazi. Watanzania hawakuhitaji katiba mpya kupinga uvunjwaji wa katiba.

Ukipewa hiyo mpya halafu ikavunjwa tena kama ilivyovunjwa hii ya sasa utafanya nini?

Maana usije kuwa unasingizia katiba mpya kwenye mambo ambayo hata kwa katiba ya sasa yanawezekana kufanyika.
 
Nikuulize katiba hii ya sasa ikituhumu kiongozi fisadi inamfanya nini baada ya hapo?
 
Define "fisadi".

Swali lako halina mantiki.

Sijaitetea katiba ya sasa kwamba ni nzuri.

Swali lako lingeweza kuwa na maana kama ningeitetea katiba ya sasa kuwa ni nzuri.

Tukirudi kwenye mifano yetu, unaliponda trekta. Halina kasi.

Mimi sijasema kwambq trekta linakwenda kasi. Hivyo swali la kuhoji kasi ya trekta si swali langu, sijawahi kusema trekta linakwenda kasi.

Sijawahi kusema katiba ya sasa ni nzuri. Hivyo swali la kuhoji uzuri wa katiba ya sasa si langu, waukize wanaosema katiba ya sasa ni nzuri.

Ila, nakuambia hivi, mtu asiyejua kuendesha gari/ trekta, tatizo lake ni kubwa kuliko ukweli kwamba ana trekta lisiloenda kasi tu.

Kwa sababu hata akipewa Ferrari inayoenda kasi, kupewa Ferrari kama hajui kuendesha gari hakumsaidii kuendesha.

Nimekuuliza swali hujanijibu.

Katiba ya sasa imevunjwa, watu hawajafanya lolote.

Ukipewa hiyo mpya unayodai, ikavunjwa tena, utafanya kipi tofauti ambacho hukufanya?

Utaweza vipi kukifanya wakati awali hukuweza?
 
Suala la katiba lipewe kipaumbele sana.

Katiba ni uhai.

Yapo mengi ya hatari sana kwenye katiba hii.

Lakini hili la Mrithi wa rais anayefariki dunia, kuwa ni makamu wa rais (automated) ni hatari sana kwa marais endapo tukipata Makamu asiyemwaminifu.

Pia linachangia sana kumuweka mbali makamu wa rais kuwa karibu na rais kwa hofu ya kutoaminia! (Naturally internal conflict)

Kwa gharama yoyote naomba tuanze na katiba inafaida kwetu sote matajiri na masikini, viongozi na watawaliwa.
Mwenzetu si unatoka jimboni?

Kaa na mbunge wako mjenge akaweke hii hoja Bungeni
 
Even the best law on earth does not defend (or enforce) itself. Watu wajifunze kwanza haki zao na wajibu wao wa kiraia badala ya kulialia kila siku, “tunataka katiba mpya, tunataka katiba mpya”!
 
Suala la katiba lipewe kipaumbele sana.

Katiba ni uhai.

Yapo mengi ya hatari sana kwenye katiba hii.

Lakini hili la Mrithi wa rais anayefariki dunia, kuwa ni makamu wa rais (automated) ni hatari sana kwa marais endapo tukipata Makamu asiyemwaminifu.

Pia linachangia sana kumuweka mbali makamu wa rais kuwa karibu na rais kwa hofu ya kutoaminia! (Naturally internal conflict)

Kwa gharama yoyote naomba tuanze na katiba inafaida kwetu sote matajiri na masikini, viongozi na watawaliwa.
We vipi kwani hujapenda mama kuwa raisi? Katiba hapa ilicheza kama pele la sivyo saa hizi tungekuwa chini ya akina mataga!!! Mbona mabo safi tu!!! Tunademka tu na mama yetu!
 
Kusema nchi iingie kwenye uchaguzi ASAP baada ya kifo cha raisi ndo hatari zaidi.
Wewe hujamwelewa. Yaani yeye ndicho anachokitaka. Anajua kuwa ni hatari possbily kuzidi hata wewe unavyojua, ila amekuja hapa akajaribu kuandika kwa kuonyesha picha kama vile hajui!
Watu hawawezi kuishi maisha ya kuhujumu nchi yao halafu wakati huo huo wakapata maendeleo, haiwezekani. Hao ambao nchi zao tayari zimeshaendelea, huko nyuma walibahatika kuwa na watu wazalendo ambao walikuwa hawawezi kuzihujumu nchi zao, na ndiyo maana wameendelea. Sisi kwa hujuma tunazoendelea kufanya, inabidi tusahau kabisa kukutana na kitu kinachoitwa maendeleo mbele ya safari yetu.
 
Even the best law on earth does not defend (or enforce) itself. Watu wajifunze kwanza haki zao na wajibu wao wa kiraia badala ya kulialia kila siku, “tunataka katiba mpya, tunataka katiba mpya”!
Exactly my point.

Sheria zitakosa maana kama zinawekwa halafu watu hawajui kudai haki zao.

Tumeona katiba imevunjwa, watu wamekatazwa kufanya mikutano ya kisiasa na Magufuli.Hapi katiba ilivunjwa. Watu wakashindwa kudai haki yao.

Wakipewa katiba mpya inayowapa haki mpya na hiyo katiba mpya ikavunjwa watafanya nini?

Katiba nzuri bila ya watu wenye muamko wa kisiasa na ufuatiliaji ni bute tu.
 
Mtu asiyejua kuendesha gari unampa trekta?
Huyo jamaa anashindwa kujadili mambo kimantiki.

Hata baada ya kumuwekea mfano mzuri anauliza maswali pointless.

Swali lako ni zuri sana.

Kama tatizo ni mtu kutojua kuendesha gari/ trekta, akipewa Ferrari au trekta hatajua kuendesha tu.

Tatizo hapo si gari ni dereva.

Mfundishe mtu kuendesha huko mbele ukimpa Ferrari ajue kuendesha, sio unadai Ferrari wakati mtu hajui kuendesha gari.
 
True.
 
Ni bahati nzuri kwamba safari hii aliyeupitia uchochoro huo kapita bila kukusudia, hakupanga iwe hivyo. Lakini natabiri kuwa baada ya watu kuuona uwezekano huo kuna watu wataanza kuufanya uwe mojawapo ya mikakati yao. Hii ni hatari kwa rais aliyeko madarakani. Nashauri utaratibu huu ufutwe haraka kwa maslahi ya taifa.
Makamu wa Rais abaki na nafasi yake hiyohiyo, akitaka urais asubiri muda ufike agombee.
Ikitokea bahati mbaya kama iliyotokea kwa hayati JPM, basi makamu awe kaimu rais kwa muda maalum (kama mwezi tu), chama chake kiteue mtu mwingine kwa utaratibu rasmi, jina lipelekwe bungeni kuthibitishwa awe rais hadi muda wa uchaguzi mkuu kwa mujibu wa kalenda utakapowadia.
 
Back
Top Bottom