Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,273
- 6,637
Ni kweli kabisa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayo mamlaka ya kuvunja bunge na kisha kuitisha uchaguzi. Sababu za kuvunja Bunge na kuitisha uchaguzi zipo ibara ya 90 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni kweli kama Bunge litakataa kupitisha hoja ambazo zina maslahi kwa Taifa, Rais anaweza kuvunja Bunge.
Hivi sasa kuna hii sekeseke la wabunge kubishana juu ya mambo ambayo wengi wanaona kama hayana manufaa kwa umma. Wengi wa wafuasi na wakereketwa wa upinzani wanatoa wazo bunge livunjwe sababu limejaza wanaCcm kwa 99%.
Je, likivunjwa na kuitishwa upya kuna mpinzani anayeweza kuchaguliwa na kushinda uchaguzi? Yaani wananchi wa Nyamagana wamchague mtu kama Pambalu kweli? Au watu wa Hai wamchague Mbowe na kumuacha huyu mbunge wa sasa? Kawe wamtose Gwajima. Mbeya je? Hii ni mifano tu ya kujiuliza.
Kwa sasa upinzani bado, unatakiwa ujipange.