Maswali magumu ya Luhaga Mpina bungeni kuhusu Symbion kulipwa Bilioni 350 huku wananchi wakibaki na umasikini

Rege

Senior Member
Jul 9, 2022
112
140
MASWALI MAGUMU YA LUHAGA MPINA AKICHANGIA BUNGENI DODOMA TAREHE 2 NOVEMBA 2022 KUHUSU TAARIFA ZA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE ZA PAC NA LAAC KUHUSU RIPOTI YA CAG JUU YA MALIPO YA SHILINGI BILIONI 350 YALIYOFANYWA KWA KAMPUNI YA SYMBION POWER LLC

Taarifa ya Kamati inaeleza kuwa mkataba baina ya TANESCO na Symbion Power LCC wa kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo eneo la Ubungo Dar es Salaam uliingiwa mnamo Tarehe 7
Julai 2001 na kumalizika Tarehe 19 Septemba 2013 ambapo Mkataba huo uliongezwa miaka 2 hadi Tarehe 18 Septemba 2015.

Taarifa ya Kamati inaonyesha kuwa TANESCO na Kampuni ya Symbion walianza majadiliano ya kuwa na mkataba wa muda mrefu wa mauziano ya umeme, ‘Power Purchase Agreement’(PPA) ambapo makubaliano ya awali yalisainiwa Tarehe 15 Septemba 2015. Kampuni ya Symbion kuiuzia TANESCO megawati 112 kwa gharama za Dola za Marekani 0.01775 kwa KWh (50% x 0.285 plus
0.0035) lakini ilipofikia Tarehe 24 Mei 2016 Kampuni ya Symbion Power LLC ilitakiwa kuondoa mitambo yake kwenye Gridi ya Taifa baada ya kutokuelewana kwa pande zote mbili.

Baada ya uamuzi huo kujitokeza, mashauri 2 ya madai dhidi ya TANESCO yalifunguliwa na Kampuni ya Symbion katika Chemba ya
Kimataifa ya Biashara (ICC) na Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) kwa kuidai TANESCO Dola za Marekani 1,566,254,652.41 Ilipofikia mnamo Tarehe 21 Mei 2021 pande hizo mbili TANESCO na Kampuni ya Symbion Power LCC zilifikia makubaliano (Deed of Setlement) ambapo makubaliano yalikuwa malipo ya dola za
Marekani Milioni 153.43 sawa na kiasi cha Tsh Bilioni 350 bila kujumuisha kodi na gharama zinginezo.

Taarifa ya Kamati ya Bunge ya PAC haikufanya uchambuzi wa kina kuliwezesha Bunge kuelewa msingi wa malipo yaliyofanywa na Serikali kwa Kampuni ya Symbion yapo mambo mengi yaliyopaswa kuzingatiwa na kutolewa ufafanuzi kama ifuatavyo:-

(i) Je msingi wa makubaliano wa TANESCO kuilipa Symbion Power
LLC kiasi cha Tsh Bilioni 350 ulikuwa ni nini, kwanini taarifa haijaeleza kifungu cha mkataba kilichokiukwa na kupelekea nchi kulipishwa mabilioni ya fedha ambapo PPA ilikuwa na miezi 10 tu tangu iingiwe Tarehe 15 Septemba 2015.

(ii) Taarifa ya Kamati ya PAC haijaeleza kama kulifanyika tathmini ya kina kujua malimbikizo ya kodi na madai mbalimbali ya Serikali kwa Kampuni ya Symbion Power LCC tangu kuingia mkataba mnamo Tarehe 7 Julai 2001 (miaka 21 iliyopita) kabla ya kufikia uamuzi wa kuwalipa fidia ya Tsh Bilioni 350.

(iii) Taarifa ya Kamati ya PAC haijaeleza msingi wa kuongezwa muda wa mkataba baina ya TANESCO na Kampuni ya Symbion Power LLC Tarehe 15 Septemba 2015 wakati mkataba huo ulikuwa umebakiza siku tatu tu kufika mwisho wake tarehe 18 Septemba 2015.

Mkataba huo uliokuwa ukilitia hasara taifa na kuifanya TANESCO
ishindwe kujiendesha na kutoa huduma bora kwa wananchi umehuishwa na kuongezwa muda mrefu wakati miradi mikubwa ya kitaifa ya kuzalisha umeme wa Megawati 583 ilikuwa katika hatua za mwisho kukamilika. Mradi wa kufua umeme wa Kinyerezi I (Megawati 150) ulikamilika mwaka 2016, Kinyerezi II (Megawati 248) ulikamilika mwaka 2018 na Kinyerezi I extension (Megawati 185) ambao uko hatua za mwisho kukamilika na huku utekelezaji wa miradi mingine ya kimkakati ya uzalishaji umeme maeneo mbalimbali nchini ilikuwa ikiendelea.

Kukamilika kwa Miradi hii kulikuwa kunalifanya taifa letu kuwa na umeme wa ziada katika Gridi ya Taifa na kuliwezesha taifa kuziuzia umeme nchi jirani, sababu za kuhuisha mkataba baina ya TANESCO na Kampuni ya Symbion Power LLC, Tarehe 15 Septemba 2015 wenye uzalishaji wa Megawati 112 zilikuwa zimelenga kufanikisha kitu gani wakati Taifa lilikuwa linaenda kuongeza Megawati 583 katika Gridi ya Taifa kwa kipindi kifupi.

(iv) Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilishaagiza mkataba huu kusikitishwa kutokana na gharama kubwa za kuiuzia umeme TANESCO hali iliyokuwa inapelekea Serikali kulipa madeni ya TANESCO mara kwa mara, ni nani alitoa kibali cha TANESCO kuingia mkataba upya wakati nchi ilikuwa kwenye uchaguzi?

(v) Mara tu baada ya makubaliano baina ya TANESCO na Kampuni
ya Symbion Power LLC, Serikali ililipa fedha hizo Mei 2021 kiasi cha Tsh Bilioni 350. Je kiasi hicho cha fedha kiliruhusiwa na nani wakati Bunge lilikuwa limeshapitisha Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/2021 na kwanini ilipe Serikali na sio TANESCO. Je kulikuwa na udharura gani wa kufanya malipo hayo kwa haraka?

(vi) Taarifa ya Kamati inaeleza dosari za usimamizi wa mkataba na
kutofanyika kwa upembuzi yakinifu kabla ya kuvunja mkataba kati ya TANESCO na Symbion Power LLC lakini haiwataji wahusika ni akina nani na haielezi ni hatua gani zimechukuliwa kwa wahusika waliolisababishia taifa hasara kubwa.

KWA KUWA hakuna maelezo ya kutosha kwenye jambo hili lililoingizia hasara kubwa nchi yetu ya kiasi cha Tsh Bilioni 350 huku kukiwepo na mahitaji makubwa ya fedha kugharamia huduma
muhimu na maendeleo ya nchi tena kipindi kibaya ambacho nchi ilikuwa kwenye mtikisiko mkubwa wa uchumi kutokana na janga la Korona (Uviko-19),

NA KWA KUWA ufafanuzi wa kina haujaonekana kwenye Taarifa ya Kamati ya PAC wala Ripoti ya CAG,

HIVYO BASI Bunge liazimie kwamba iundwe Kamati teule ya Bunge kuchunguza suala hili ili kupata uhalali na haki za watanzania katika
mkataba huo.
 
Nchi hii wanafaidi wachache Kweli kabisa kama nchi ndio tumeibiwa Bilioni 350 huku vijijini hata zanahati hatuna watu wanakufa kwa kukosa huduma, maji hakuna, mafuta bei juu alafu tunaambiwa mtu mmoja tu ametengenezewa dili ya Bilioni 350 inauma sana Mama Tanzania
 
Mambo Haya Yanatia Kinyaa Sana
BBillions Zinaliwa Na Wachache, Halafu Mlala Hoi Mnambana Na Tozo Kila Eneo
Tanzania Viongozi Ndiyo Majizi Jamani

Mbaya Zaidi Hakuna Chombo Chochote Kitasema Lolote, Huku Walaji Wakionekana Hadharani, Ccm Kimya Kama Iko Kwenye Mtungi Inapoa


Wao Wakati Wote Husema Ndiyo Wenye Nchi Na Ilani Oneni Sasa
Yaani Rais Anaingia Mikataba Kuleta Pesa Nchini
Wachache Wanazichota Kwa Ujanja
 
Walikuwa wanamwita Lissu "MIGA" na kumkebehi kwamba ni mwehu. tulipe tu hakuna namna!!
Kama Taifa bado tunasafari ndefu sana tunapenda kubadilisha ajenda hili kufanikisha ulaji wa watu sasa Lissu anahusikaje huku unaambiwa malipo yamefanyika bila kuzingatia mambo hayo au hujasoma Hoja ya Mpina?
 
Kama Taifa bado tunasafari ndefu sana tunapenda kubadilisha ajenda hili kufanikisha ulaji wa watu sasa Lissu anahusikaje huku unaambiwa malipo yamefanyika bila kuzingatia mambo hayo au hujasoma Hoja ya Mpina?
Inahusiana. Lissu alisema tatizo letu liko kwenye mikataba yetu tunayoingia na hao wanaotudai. Na alishauri mambo ya mikataba yaangaliwe upya. Na Rais Samia Suluhu ndiyo maana kasema kuwa ni lazima SASA mikataba yote ipitie kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Tunalipa kwa kuwa tulikiuka mkataba na mahakama za kimataifa ndizo zimeamua hivyo.
 
Inahusiana. Lissu alisema tatizo letu liko kwenye mikataba yetu tunayoingia na hao wanaotudai. Na alishauri mambo ya mikataba yaangaliwe upya. Na Rais Samia Suluhu ndiyo maana kasema kuwa ni lazima SASA mikataba yote ipitie kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Tunalipa kwa kuwa tulikiuka mkataba na mahakama za kimataifa ndizo zimeamua hivyo.
Hakuna mkataba wa Serikali unaosainiwa bila kupitia kwa Mwasheria Mkuu wa Serikali.
 
Kama ilikuwa ni hivyo ni kwa nini basi Rais Samia Suluhu alisema "kuanzia SASA...mikaba yote ni lazima ipitie kwa Mwanasheria Mkuu" ina maana Rais hana taarifa sahihi kuliko wewe!!??
Hayo maombi yalikuwa ya Mwanasheria Mkuu hivyo Rais alijibu maombi ya AG ila sio kwamba Rais ndio alianzisha hiyo mada
 
Huyo Mpina akiwa wizara ya Mifugo na uvuvi kaumiza sana wananchi kwa kuwaharibia Vifaa vyao kuwapora leseni kwa sababu ya maslahi yake na mabwana zake leo anakuja na porojo za kijinga,Mnatuona waTz Mafala sana
Ungeyaweka hayo mambo aliyoyafanya Mpina ili wote tuelewe tusiojua
 
Hawa WEZI wote tumeshawashtaki kwa Mungu si muda mrefu mtaona kitakachowakuta
 
Back
Top Bottom