Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,583
Wanabodi,
Kwa maslahi ya Taifa, inakuletea mfufulilizo wa makala elimishi kuwaelimisha Watanzania, kuijua Jumuiya ya Afrika Mashari na Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na fursa zake. Ambapo mtangamano ukikamilika, unakwenda kuunda Taifa kubwa kabisa Afrika Mashariki, ambalo litakuwa na Serikali moja ya Afrika Mashariki.
Ambalo Taifa hilo litakuwa ndilo Taifa kubwa la 4 duniani, baada ya China, Marekani na Urusi. Ila pia kati ya nchi zote 7 za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania ndiyo nchi inayoongoza kwa fursa nyingi kwenye jumuiya hii kutokana na strategic location yake kupakana na bahari ya Hindi.
Ambalo ndilo lango na kuingiza bidhaa, Zambia, DRC, Rwanda na Burundi, ila kwa bahati mbaya sana, Watanzania bado hawazijui fursa lukuki zilizopo na hivyo kushindwa kuzichangamkia fursa hizi kilamilifu. Hivyo hizi ni makala elimishi kutufungua macho, tuchangamkie fursa!
Jumuiya ya Afrika Mashariki kuelekea kwenye Mtangamano wa Afrika Mashariki (kwa Kiingereza East African Community, kifupi EAC) unazihusisha nchi saba za kanda ya Maziwa Makuu ya Afrika Mashariki zenye utajiri mkubwa wa madini, maliasili, vyanzo vya maji na udongo wenye rutuba. Ambapo mtangamano ukikamilika na kuwa nchi moja, hakuna nchi nyingine yoyote barani Afrika, inaweza kushindana na utajiri huu.
Nchi hizo ni sisi Tanzania, Kenya Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani ya Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambayo itakuwa na eneo la kilomita za mraba milioni 4,810,363, na wakazi zaidi ya milioni 281,050,447 kwa kadirio la mwaka 2022), hivi kwamba ingekuwa nchi moja tu ingekuwa ya 7 duniani.
Hivyo nitawapeleka mdogo mdongo kwa kuanzia na kuwaelimisha kwanza kuujua Mkataba wa kuanzishwa upya kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliotiwa saini tarehe 30 Novemba, 1999 na kuanza kutumika rasmi tarehe 7 Julai, 2000 baada ya nchi washirika watatu wa mwanzo, Tanzania, Kenya na Uganda kuridhia mkataba huo.
Mkataba huo uliazimia kuziunganisha nchi washirika za mwanzo, Tanzania Kenya na Uganda kuwa nchi moja kupitia process inayoitwa Mtangamano ambayo inakwenda hatua kwa hatua hadi kufikia kuwa na shirikisho la nchi moja.
Mtangamano umeainisha kabla ya kuunda shirikisho, kwanza tuunganisha baadhi ya mambo tuwe na kitu kimoja ndipo tuje kuwa nchi moja.
Hatua ya kwanza ni kuunda vyombo, Sekretariat ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki, tutakuja kuwa na pasipoti moja, viza moja ya watalii, muungano wa sarafu, na mwisho ni shirikisho la kisiasa.
Maeneo hayo kujenga mfumo kamili wa ushirikiano katika Biashara, Uwekezaji na Maendeleo ya Viwanda; Sarafu na Sera za Fedha, Miundombinu na Huduma, Kilimo na Uhakika wa Chakula, Mazingira na Usimamizi wa Mali Asili; Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori.
Nyanja nyingine za ushirikiano zilizoainishwa katika Mkataba ni shughuli za Afya, Kijamii na Kitamaduni; Nafasi ya Wanawake katika Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi, Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi na Jumuiya ya Kiraia; pamoja na ushirikiano katika masuala ya Sheria na Utoaji Haki. Masuala ya kisiasa ikiwa ni pamoja na Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje.
Mkataba pia unaeleza hatua mbalimbali katika maendeleo ya mtangamano ukiwemo uanzishaji wa Muungano wa Forodha, ambao ni mlango muhimu katika shughuli za jumuiya, kisha baadaye Soko la Pamoja, likifuatiwa na Muungano wa Sarafu na hatimaye Shirikisho Ia Kisiasa la Dola za Afrika Mashariki.
Vyombo vya mamlaka za Jumuiya ambavyo ni pamoja ni Mkutano wa Wakuu wa Nchi, Baraza la Mawaziri, Kamati ya Uratibu, Kamati za Kisekta, Mahakama ya Afrika Mashariki, Bunge la Afrika Mashariki, na Sekretariati, Mkataba pia unasisitiza ushiriki wa Sekta Binafsi na jumuiya ya Kiraia katika mwenendo mzima wa Mtangamano.
Mkataba umetilia maanani maslahi ya eneo hili la Afrika Mashariki. Inaeleweka kwamba mataifa madogo, na dhaifu hayana mustakbali murua katika ulimwengu huu wa ushindani mkubwa. Kwa kuwezesha kuwapo kwa soko pana zaidi, Jumuiya itasaidia kukuza biashara na uwekezaji katika eneo hili.
Ushirikiano katika kukuza sayansi na teknolojia utatusaidia kwenda na wakati na kuongeza kasi ya ukuaji viwanda na hivyo kuongeza ajira na kubaresha hali za maisha ya watu Kwa ujumla, Jumuiya itatuongezea fahari, hadhi na kujiamini, tena itaboresha nafasi yetu katika mahusiano na jamii nyingine duniani.
Uelewa mzuri wa Jumuiya hii ndiyo mwanzo wa Watanzania kushiriki kikamilifu na kuchangamkia fursa za Mtangamano katika enea letu hili.
Lengo la mfululizo wa makala hizi ni kuwahabarisha, kuwaelimisha na kuwahamasisha Watanzania kuifahamu Jumuiya ya Afrika Mashariki na fursa zake ili Watanzania na sisi tuzichangamkie na kuzifaidi. Makala hizi zitafuatiwa na vipindi vya televisheni vya eulimishaji Umma kuhusu Jumuiya hii, ambavyo vitaendeshwa kwa lugha ya Kiswahili na kutangazwa katika Televisheni za Taifa za nchi zote 7 ambavyo pia vitasaidia kukikuza Kiswahili ambacho ni moja ya lugha rasmi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Historia, Jumuiya hii iliyopo sasa ni yenye nchi 7, Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani ya Kusini na DRC, ni Jumuiya ya pili, Jumuiya ya kwanza ilinzishwa ilianzishwa mwaka 1967 ikizihusisha nchi tatu tuu za Tanzania, Kenya na Uganga, Makao Makuu ya jumuiya hiyo ni Arusha, Tanzania. Kwa bahati mbaya sana, Jumuiya hiyo ilivunjika mwaka 1977.
Tukutane wiki iijayo, ili kujua kwa nini Jumuiya kwa kwanza ilivunjika, ili kuzitumia sababu hizo kuzuia hii Jumuiya ya pili nayo isije kuvunjika kama ile ya mwanzo.
Wasalaam,
Paskali

1. | 17,098,242 | |
2. | 9,984,670 | |
3. | 9,826,675 | |
4. | 9,596,961 | |
5. | 8,514,877 | |
6. | 7,741,220 |