Condester Sichalwe: Muunganiko Mabunge ya Afrika Mashariki ni Kichochea Ukuaji Uchumi na Kiswahili

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941
Mbunge wa Jimbo la Momba lililopo mkoani Songwe, Condester Michael Sichalwe amesema muunganiko wa mabunge ya Afrika Mashariki ni jambo linalolochochea shughuli za kiuchumi, kijamii, kisiasa pamoja na kusukuma ukuaji wa lugha adhimu ya Kiswahili.

Sichalwe amesema hayo wakati wa michezo ya mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoendelea jijini Kigali nchini Rwanda ikikutanisha mabunge yote ya Ukanda wa Afrika Mashariki kwa maana ya Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini.

"Muunganiko wa mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kitu kizuri sana. inafanya wana jumuiya kuwa pamoja na kusukuma shughuli za kiuchumi, kisiasa, kijamii na maendeleo kwa ujumla na kufanya kutangaza lugha ya Kiswahili. Muunganiko huu unafanya Warwanda, Waganda Sudan Kusini.

"Timu ya Bunge Sports Club kwenye michezo yote imejipanga vyema sana kuchukua ushindi wa kishindo na kumrudishia medali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na Watanzania wote." - Mbunge Sichalwe

Mbunge Sichalwe amesema muunganiko huo wa mabunge unasaidia sana na kuwaomba wakuu wa nchi zote pamoja na maspika wa mabunge yote kuendelea kuuimarisha umoja huo.

Mashindano hayo ya mabunge yamefunguliwa tarehe 8 Desemba, 2023 na Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Donatile Mukabalisa na yanatarajiwa kufungwa Desemba 18, 2023 huku wabunge 720 wakishiriki kwenye michezo ya mpira wa miguu, kikapu, gofu, pete, vishale na michezo mingine mbalimbali.

GBUZFDaXsAALr-H.jpg
 
Nilipita jimboni kwake kuna vivutio vizuri vya utalii! Hili analiongeaje kuhusu kufanikisha utalii momba ambako nikaribu na kalambo falls!
 
Back
Top Bottom