Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Kiapo hicho kilichoshuhudiwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Joseph Ntakirutimana kimefanyika kukidhi matakwa ya kanuni namba 5(4) na 9(2) ya kiambatisho cha 10, za uendeshaji wa shughuli za kila siku za EALA. Ambapo, kanuni ya 5 (4) inaeleza kuwa mjumbe rasmi wa maamuzi anaweza tu kuketi katika Bunge hilo baada ya kula kiapo cha Utii kwa Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
EALA inajumuisha wajumbe (Wabunge) tisa (9) wa kuchaguliwa kutoka kila nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri na/au Naibu Waziri mmoja kutoka nchi Wanachama wanaosimamia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki limeanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 9 ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo jukumu la msingi la chombo hicho cha uwakilishi ni kutunga sheria za Jumuiya na kusimamia majukumu ya Sekretariati katika kutimiza malengo ya Jumuiya.