Somalia yajiunga Uanachama wa Afrika Mashariki (EAC)

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
1700837419030.png

Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika Jijini Arusha nchini Tanzania, umeridhia Nchi ya Somalia kujiunga na EAC na sasa inakuwa Mwanachama wa nane wa Jumuiya hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba ni miongoni mwa Viongozi waliotoa pongezi za awali kabisa kwa Somalia kuridhiwa kuwa Mwanachama mpya wa EAC ambapo ameitakia kheri Somalia katika kuielewa na kuiishi pamoja na kuitekeleza misingi ya EAC na itifaki zake katika kukuza na kuendeleza Jumuiya hiyo.

Katika hatua nyingine mkutano huo pia umemtangaza Rais wa Sudan, Salva Kiir Mayardit kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Itakumbukwa katika mkutano kama huo mwaka jana aliyekuwa Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo wakati huo, Uhuru Kenyatta alitangaza rasmi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kujiunga na EAC.
 
Watanzania wakijua kuwa uhuru wa nchi yao pamoja na sheria za nchi yao utakuwa chini ya hii jumuia ndipo hapo itakuwa too late.

Na tukipata raisi muelewa kama JPM atatutoa huko kwenye kundi la wasiojitambua. Yani nchi maskini zimejikusanya pamoja kwa amri ya world economic forum Claus shwab ndiyo anawaamrisha tuta toka huko ngoja tupate mwamba
 
Na SADC nako tumtegemee Jambazi gani wa kututoa huko au Makonda?
 
Back
Top Bottom