Igunga OFFICIAL Results: Dr. Kafumu atangazwa mshindi

Igunga OFFICIAL Results: Dr. Kafumu atangazwa mshindi

Kafumu wa ccm ameshnda kwa kura 26484 na chadema wamepata 23260, cuf 2104

Mmhhh!!!!!!!!!!!! Hata kama tumepoteza Jimbo sina shaka kwamba huu ni mtaji mkubwa kwa CDM.

Pia, nimeamini juu ya comment ya mwaJF ambaye asubuhi amesema kuwa CUF wanajua MAPENZI kwa kukubali kugawa kura zao kwa CCM. Hili ni tatizo la kufanya mapenzi kazini!!!
 
Machungu wamenijaa moyoni, ila nashakuru kwa ushindi ambao Cdm imeupata. Igunga ni ngome imara ya Zzm ila tumewakimbiza mbaya. Na hii imetoa fundisho wakome kuvuana magamba wakithubu kulivua kwa Chenge tunachukua kiulaini. Na wazee walio ichagua zzm kwa kupewa kilo moja ya nyama na kanga,skafu na kofia wanaendelee na moyo huo ili yale maji wanayotumia kama chai ya maziwa na Nyumba za full suti wavifaidi. Ndungu zetu wa Bakwata waliokubali kutumika waendelee hivyo ila wajue mwenyezi Mungu atawapunguzia tawabu siku ya kiama kwa kushiriki kukumbatia udhalimu unaofanywa na zzm.
 
nawapongeza wote walioshiriki pale igunga, lakini ni kwa nini wapiga kura hawakufika hata elfu 60???????????????????????:noidea:

Tatizo siyo wapiga kura. Tatizo ni daftari la kudumu la wapiga kura. Hili limekuwa doctored kwa ajili ya kuacha mwanya wa kuingiza majina ya wapiga kura wa uwongo kulingana na mahali na mazingira ya jimbo. Kuna majina mengi kuliko idadi halisi ya wapiga kura. Siyo igunga peke yake bali ni nchi nzima kama tulivyoona 2010.

Vyama vya upnzani lazima vikazane hili daftari liwe audited na watu ambao ni independent ili wadau wote walidhike nalo. Mimi nawapongeza cdm kwa mafanikio waliyoyapata igunga. Ushauri wangu kwa cdm ni kuwa kutoka sasa waangalie vile vile mambo ya nje ya majukwaa ambayo yana athari kwa uchaguzi. Hayo ni pamoja na uandikishaji wa wapiga kura, elimu kwa wapiga kura, kulenga makundi maalum kama wanawake, kuanzisha matawi na mashina, n.k
 
Umasikini wa watanzania ni mtaji wa ccm kwakuwa wanaweza kuwa rubuni kiurahisi kwa rushwa ipo siku mungu atawaumbua la sivyo wabadilike hivi mpaka sasa halimashauri ya wilaya kilombero mishahara haija toka kwanini au ndo zilipelekwa igunga wakapewa wagambo wagawe kwa watu kama yule alie kamatwa jana na laki saba ninakerwa sana na hali hii maana sasa tunaishi kama watumwa ndani ya nchi yetu
 
Kweli hawa ndugu zangu wamenisikitisha sana ,watu tunataka changes wao wanarudisha magamba...
Next time kampeni inabidi zianzie vijijini kwanza maana hawa wazee wana upeo mdogo ,elimu duni ,utandawazi hakuna wanamjua mwalimu Nyerere tu na CCM ....................

Mimi nadhani tatizo kubwa na la msingi ni daftari la wapiga kura. Watu wengi wenye sifa hawapati fursa ya kupiga kura kutokana na aidha majina yao kutoonekana ilihali wao wana shahada, ama majina ya wapiga kura kuhamishwa kwenda vituo vingine vya mbali hivyo watu wengi kushindwa kupiga kura.

Na jambo jingine ni umaskini wa watanzania, na ccm wanatumia vizuri sana mwanya huo kuwarubuni kwa kuwakirimu sana wakati wa kampeni; khanga, tshirts, ubwabwa kwa wingi na posho za kujikimu kwa visiku vichache.

Kama ingelikuwa ni suala la vijijini, basi dar es salaam itakuwa kijijini kuliko kigoma kaskazini!!
 
Igunga wasubiri magufuli akawajengee daraja na barabara! Wajinga ndio waliwao.
 
Yule jamaa wa CUF amezungumza jambo moja la nsingi sana. PESA, siasa za kitanzania na kiafrika kwa ujumla ni pesa tu, wananchi wengi hasa hawa wa vijijini wana uelewa mdogo juu ya katiba na maendeleo kupiga kampeni kazi bure, unaweza kupata kura zao kwa kuwarubuni na vijizawadi vidogo-vidogo, hata buku kumi kumi wanakugaia kura.

Huo ndio ukweli na ndio strategy pekee inayofanya kazi kwa sasa. Hadi pale wananchi walio wengi watakapoelimishwa na wakafahamu sababu za umasikini wao nachelea kusema mambo yatakuwa yanajirudia hivi kila chaguzi.

Itachukua muda zaidi ya tunavyofikiria unless Chadema wakubali falsafa ya if you can't beat them join them nao waanze kampeni ya mapesa ama waanze kufanya kazi ya ziada kupeleka elimu ya maendeleo kwa wananchi wa mikoani na vijijini, venginevo hiyo 2015 mambo yatakuwa ni yale-yale . Money Talk- Hata Rostam akisema arudi kugombea atashinda tena kwa vile ana hela na yuko tayari kuitumia, huo ndio ukweli.

Ulianza vizur lakin ulipofika kwenye cdm kumwaga mapesa ndo nikakuona wa ajabu sn. Kwa mfumo huo utakuwa kenge kwenye msafara wa mamba
 
na haya yanafanana na hayo hii ni blod ya mjengwa toka watu wao wa ccm ,wezi sana hawa jamaa wa magamba

Matokeo Igunga.(Jumla kuu ni CCM 26266. CHADEMA 22443)
Na haya ni kata kwa kata...
Mboto CCM 730- CHADEMA 302
Nguvu moja CCM 694 CHADEMA 284
Nkinga CCM1479. CHADEMA 1085
Itumba CCM1079 CHADEMA 590
Nanga. CCM 897. CHADEMA 645
Igurubi CCM 925 CHADEMA 592
Mwisi CCM 926. CHADEMA 992
Mbutu. CCM 1186. CHADEMA 1426
Kinungu. CCM 505 CHADEMA 268
Ngulu CCM 622 CHADEMA 412
Igunga CCM 3181 CHADEMA 3358
Choma CCM 1227 CHADEMA 918
Kining. CCM 700 CHADEMA 451
Mwashiku. CCM 798 CHADEMA 484
Nsimbo CCM 738 CHADEMA 1016
Itunduru CCM 738 CHADEMA 784
Mwamashimba CCM 1224 CHADEMA 1421
Mbutu CCM 1335 CHADEMA 1427
Bukoko CCM 1136 Chadema 931
Nyandekwa CCM 691 Chadema 631
Ndembezi CCM 866 Chadema 806
Chabutwa CCM 545 Chadema 581
Ziba CCM 1053 Chadema 860
Igoweko CCM 1051 Chadema 880
Sungwizi CCM 1225 Chadema 718
Isakamaliwa CCM 525 Chadema 593

mbona mbutu ziko mbili, angalia kwenye red, au ndo haya sio rasmi ni yale na nape aliyokuwa akijumlishia chumbani?
 
Igunga wasubiri magufuli akawajengee daraja na barabara! Wajinga ndio waliwao.

Na asipojenga daraja la mbutu pamoja na barabara, mwaka 2015 kiulainiiiiiiiiiiiiii kama tunanawa.

Hata wakijenga bado tutawadhibiti, wakati huo kila mtu atakuwa jimboni kwake, hakuna cha mzee wa kusinzia wala magufuli. Kama biharamulo vile.
 
Dalaly Kafumu aliyekuwa katika kinyang'anyiro cha kugombea ubunge wa jimbo la Igunga, Tabora kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, ametangazwa leo na msimamizi wa tume ya uchaguzi ya Taifa kuwa ndiye mbunge mpya wa jimbo hilo baada ya kuwashinda wagombea toka vyama vingine.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 2, 2011 CCM ilipata kura 26,484 wakati CHADEMA ilijizolea kura 23,260 na CUF kura 2104.

Taarifa zaidi za takwimu kamili zitapatikana katika tovuti ya uchaguzi ya Taifa
 
Umasikini wa watanzania ni mtaji wa ccm kwakuwa wanaweza kuwa rubuni kiurahisi kwa rushwa ipo siku mungu atawaumbua la sivyo wabadilike hivi mpaka sasa halimashauri ya wilaya kilombero mishahara haija toka kwanini au ndo zilipelekwa igunga wakapewa wagambo wagawe kwa watu kama yule alie kamatwa jana na laki saba ninakerwa sana na hali hii maana sasa tunaishi kama watumwa ndani ya nchi yetu

pia Same kuna dungu yangu hajapata mshahara wa sept, kisa kuna wafanyakazi hawafanyi kazi ila wanalipwa mpaka wachunguze wafanyakazi wote ndo mishahara itoke. Kweli zimepelekwa Igunga.
 
wana Jf, CCM kimeshinda igunga lakini kwa maoni yangu mimi hali si shwari kwa chama changu hiki cha CCM ambacho ndio kikubwa kuliko vyote nchini. haiwezekani chama cha CHEDEMA ambacho hakikusimamisha mgombea katika uchaguzi mkuu 2010; halafu katika uchaguzi mdogo chama hichohocho tuwe tumekishinda kwa kura ambazo hazizidi hata 3000!!!

kwa wana ccm wote, pamoja na kusherehekea ushindi huo mwembamba bado inabidi tujiulize mara mbilimbili kulikoni; wapinzani wetu hawa katika kipindi kichache tu watoke from zero mpaka wapate kura 23,260?

hii si dalili nzuri katika uchaguzi mkuu wa 2015; hebu tujiulize hapa ni Igunga ambapo palikuwa ni ngome yetu CCM hali iko hivi, je itakuaje maeneo kama Arusha, Mwanza, Kigoma, Mara, Singida kwa Tundu Lissu, Moshi, Iringa kwa mch Msigwa, Dar kwa mjjika na mdee; maeneo ambayo yanawatu wengi na chadema inakubalika mno, hali itakuaje katika chaguzi zijazo kama wanaume hawa watapiga kampeni mpaka vijijini kama walivyofanya Igunga?

Inabidi tutafakari kwa mapana yake kwa wana CCM wote la sivyo 2015 ndiyo utakuwa mwisho wetu wa kutawala nchi hii!!
 
kufumua ni lugha gani??
nikisema kamfumua mama yako na wewe nimekosea??
 
Du mm naona bora mwizi niliyemzoea kuliko aje mwizi mwingine mpya.
Dr Kafumu kazi za madini sasa kazi kwako utudanganye na wewe
 
wana Jf, CCM kimeshinda igunga lakini kwa maoni yangu mimi hali si shwari kwa chama changu hiki cha CCM ambacho ndio kikubwa kuliko vyote nchini. haiwezekani chama cha CHEDEMA ambacho hakikusimamisha mgombea katika uchaguzi mkuu 2010; halafu katika uchaguzi mdogo chama hichohocho tuwe tumekishinda kwa kura ambazo hazizidi hata 3000!!!

kwa wana ccm wote, pamoja na kusherehekea ushindi huo mwembamba bado inabidi tujiulize mara mbilimbili kulikoni; wapinzani wetu hawa katika kipindi kichache tu watoke from zero mpaka wapate kura 23,260?

hii si dalili nzuri katika uchaguzi mkuu wa 2015; hebu tujiulize hapa ni Igunga ambapo palikuwa ni ngome yetu CCM hali iko hivi, je itakuaje maeneo kama Arusha, Mwanza, Kigoma, Mara, Singida kwa Tundu Lissu, Moshi, Iringa kwa mch Msigwa, Dar kwa mjjika na mdee; maeneo ambayo yanawatu wengi na chadema inakubalika mno, hali itakuaje katika chaguzi zijazo kama wanaume hawa watapiga kampeni mpaka vijijini kama walivyofanya Igunga?

Inabidi tutafakari kwa mapana yake kwa wana CCM wote la sivyo 2015 ndiyo utakuwa mwisho wetu wa kutawala nchi hii!!
we waache tu tutawachinjia baharini hawa 2015
 
Awali ya yote nashukuru Uchaguzi Igunga umekwisha na sasa tugange yajayo!
Kwa wanaChadema, matokeo haya niliyasema mapema sana nikisema ndio ukweli na hali halisi ingawa inauma. Sasa swali la kujiuliza sielewi mmejifunza kipi!
Na mkuu wangu, Feedback na Quinine nataka muelewe kwamba watu kama nyie ndio mmechangia sana kuanguka kwa CDM, na CCM wataendelea kutumia jazba zenu kama nyenzo ya kuwapa ushindi mahala popote.
 
Back
Top Bottom