Igunga OFFICIAL Results: Dr. Kafumu atangazwa mshindi

Igunga OFFICIAL Results: Dr. Kafumu atangazwa mshindi

Hongereni wananchi wa Igunga, hapa mshindi ni demokrasia. Vilevile nawpongeza sana wapiganaji wa Chadema, pamoja na kutoshinda, hakika mmepigana kiume!
 
ccm hawana cha kujivunia wanahatari sana mwaka 2015,wanatakiwa wajipange upya maana kwa matokea haya!sijui tusubiri maajabu yanaweze kutokea tanzania,cdm nyota inawaka 2015
 
Hongera chadema. Japo ccm wameshinda.
 
Not bad...good work CHADEMA,kwenda Igunga kwa mara ya kwanza tena ndani ya miezi miwili na kupata kura zaidi ya 20 elfu ni dalili tosha kuwa tukijipanga vyema,twaweza kufanya vyema next time....
 
na haya yanafanana na hayo hii ni blod ya mjengwa toka watu wao wa ccm ,wezi sana hawa jamaa wa magamba

Matokeo Igunga.(Jumla kuu ni CCM 26266. CHADEMA 22443)
Na haya ni kata kwa kata...
Mboto CCM 730- CHADEMA 302
Nguvu moja CCM 694 CHADEMA 284
Nkinga CCM1479. CHADEMA 1085
Itumba CCM1079 CHADEMA 590
Nanga. CCM 897. CHADEMA 645
Igurubi CCM 925 CHADEMA 592
Mwisi CCM 926. CHADEMA 992
Mbutu. CCM 1186. CHADEMA 1426
Kinungu. CCM 505 CHADEMA 268
Ngulu CCM 622 CHADEMA 412
Igunga CCM 3181 CHADEMA 3358
Choma CCM 1227 CHADEMA 918
Kining. CCM 700 CHADEMA 451
Mwashiku. CCM 798 CHADEMA 484
Nsimbo CCM 738 CHADEMA 1016
Itunduru CCM 738 CHADEMA 784
Mwamashimba CCM 1224 CHADEMA 1421
Mbutu CCM 1335 CHADEMA 1427
Bukoko CCM 1136 Chadema 931
Nyandekwa CCM 691 Chadema 631
Ndembezi CCM 866 Chadema 806
Chabutwa CCM 545 Chadema 581
Ziba CCM 1053 Chadema 860
Igoweko CCM 1051 Chadema 880
Sungwizi CCM 1225 Chadema 718
Isakamaliwa CCM 525 Chadema 593

mbona mbutu ziko mbili, angalia kwenye red, au ndo haya sio rasmi ni yale na nape aliyokuwa akijumlishia chumbani?
 
It is quite sad new.....but all in all CHADEMA we have a reason to boost us up!! Igunga kwa CDM ni jaribu la kwanza ambalo limeonesha kuwa kuna kukubalika zaidi as days goes on....

I feel so proud kuwa supporter wa CDM than before has nikiangalia jambajamba waliyooipata CCM pamoja na support kubwa ya serikali na vyombo vyake

Mkuu ni kweli kabisa, kilichotokea ni kwamba tumepoteza kiti cha ubunge igunga lakini tumetoa ushindani wa hali ya juu.

Hatuna sababu ya kuvunjika moyo, tunatakiwa kujipongeza na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wowote unaokuja mbele yetu.

Sasahivi hawathubutu kutuita chama cha msimu, kwakuwa wamelazimika kutumia government machinery zote pamoja na mbinu chafu kushinda.
 
Hongera chadema kwa kuwaonyesha ccm kuwa chadema si lelemama! Jinsi wamelivyovuta kama si tuvyama twingine na usaidizi wa bakwata, serikali, nec, shura ya maimamu, mtaji wa cuf n.k wangeaibika mbaya!

Big up chadema!
 
Of course CCM ni wezi wa kila kitu,kura mpaka rasilimali za watanzania..ila mwisho wenu ni awamu hii tu,2015 mtakaa bench!

ccm wangeweka mgombea muislam wasingeshinda! kwa watu wasomjua kafumu ni mdini sana pamoja na 'kigulu' mchemba na wamewatumia vizuri sana waislam katika suala la hijab!
 
CCM ..lakini joto ya jiwe wameipata serikali yote ilihamia Igunga..
 
Nawapongeza CCM kwa ushindi. Nawaomba mjiandae kwa 2015 kwa sababu matokeo haya ni dalili mbaya kwa chama chenu. Mkiendeleza mtaji wenu wa wazee, 2015 mhesabu maumivu.

Madai ya CHADEMA sasa ni uboreshwaji wa daftari la wapiga kura ili vijana wenye umri stahiki wasikose haki yao.
Nawaomba mjipange tunyang'anyane hao vijana.

In loosing the Igunga elections CHADEMA has no much pain. On the contrary there is much to gain. We have recruited and invested the knowledge of freedom into the younger generation while CCM has continued to boast on the old generation. Psalms 127:3 - 5 says:
[SUP]3[/SUP]Children are a blessing and a gift from the LORD. [SUP]4[/SUP]Having a lot of children to take care of you in your old age is like a warrior with a lot of arrows. [SUP]5[/SUP]The more you have, the better off you will be, because they will protect you when your enemies attack with arguments.

In Igunga: CCM you have just "won a battle but not the war". I am sure you know this one very well. You have the powers (police and the administration) but CHADEMA has the people. See you in 2015!!!

Hapo panawahusu sana CUF, wamebaki wanalia na moyo.
 
Kweli aliye lala amelala tu, sehemu ambazo zinashida sana ndizo ambazo ccm wanashinda, hivi igunga kuna vyombo vya habari? Siamini pamoja na makosa ya wazi yanoyotendwa na serikali ya ccm still watu wanapanga foleni na kuchagua mbunge wa ccm.
 
Ni vema viongozi wa CDM kabla ya kuondoka Igunga wawashukuru wananchi na wapiga kura wa Igunga, mantiki inaontesha kuwa mwendo ni mzuri kwa CDM na wananchi wamejitahidi kuwapa kura. Ikumbukwe mikakati yote ya uchaguzi kwa CDM imeaanza baada ya Rostam kujiuzulu, ingawa inauma kwa wahusika lakini CCM na CUF lazima watatafakari kulikoni? Kwa nguvu iliyotumika na mfumo wa nchi yetu ulivyo leo CDM kupata kura kiasi hicho, wanastahili kupongezwa na ni kiashiria kuwa tuendako mambo yanaenda kubadilika
 
hawa wajinga wa vyama vingine wangeunga cdm vikura vyao vingesaidia. Ccm hawawez kufurahia chama kisichokuwa na mizizi ugunga kimewapeleka hvy
chadema pale imepata ushindi wa kishindo na ile ni ishara mbaya sana kwa kikwete & company!
 
am very sad kwakweli, WanaIgunga hawajawa na uzalendo kabisaaa

Kweli hawa ndugu zangu wamenisikitisha sana ,watu tunataka changes wao wanarudisha magamba...
Next time kampeni inabidi zianzie vijijini kwanza maana hawa wazee wana upeo mdogo ,elimu duni ,utandawazi hakuna wanamjua mwalimu Nyerere tu na CCM ....................
 
Back
Top Bottom