IGP Wambura na Jeshi lako, Kurusha Picha za "Wanawake wafanyabiashara ya Ngono", mitandaoni, ni Uvunjaji wa haki za Mwadamu... hatua zichukuliwe.!!.

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
24,052
71,360
Mimi sitoongea sana, kwakua kilichotokea kinajulikana na tumeona.

Mtuhumiwa lazima Alindwe, kitendo cha Askari wako wajinga wajinga kujichukulia sheria mkononi, kupiga picha hao Wanawake na kuanza kuwasambaza mitandaoni kwa Sura, Majina, na Kabila, ni kitendo cha ajabuu , cha kudhalilisha na kisicho cha kiungwana ambacho lazima tukikemee .

Ni Mara ngapi mnaficha Identity za watuhumiwa ? Hili Leo limewashinda ?

Siku hizi Jeshi la Polisi ndio limekuwa la kuhukumu? Eehhh hii ya kupost hao Wanawake mitandaoni ni sawa na Kuwahukumu .

Watu wapo Dar wanajenga huko makwao vijijini, wanasomesha watoto wao huko vijijini, halafu Leo hiii mnawaweka mitandaoni?

Mimi siungi mkono suala la biashara ya Ngono kwa kuwa sio maadili , lakini ieleweke, hii biashara tangu na tangu ilikuwepo, Yesu mwenyewe alimsamehee yule mwanamke anayejiuza !!.

Mimi naelewa, zinapokaribiaga Sikukuu, Baadhi ya Askari huwa na njaa ya Pesa sana, na Sina shaka hao ni wale Wanawake waloshindwa kutoa Pesa ili picha zao zisimwage.

SASA MIMI NAWAULIZA, SIKU HIZI HUKO VITUONI KWENU, MNAKOPIGA PICHA WATUHUMIWA, MNA KACHUMBA KANAKOJIHUSISHA NA KUTUSHA PICHA ZA WATUHUMIWA MITANDAONI?

KWA HIYO LENGO LA KUPIGA PICHA WATUHUMIWA, NI KUWARUSHA MITANDAONI?

SHAME ON YOU !!.
 
Wafanye kazi kwa kuzingatia maadili, weledi na miiko ya kazi........vinginevyo wanambeep IGP.
 
Back
Top Bottom