Asante sana IGP Wambura kwa Kuufanyia Kazi Uzi wangu kumhusu Mfanyabiashara Katili Bwana Cherehani wa Soko la Kawe

Cognizant

JF-Expert Member
Aug 13, 2022
492
1,056
Asante sana IGP Wambura na Mkuu wa Police Kandaa Maalum ya Dar es Salaam ACP Muliro na Jeshi la Police kwa Ujumla kwa Kufanyia Kazi Uzi wangu niliouanzisha hapa Kumhusu Mfanyabiashara wa Mihogo Soko la Kawe Bwana Cherehani akamatwe kwa Ukatili mbaya na Usiovumilika alioufanya.

Taarifa ambazo Cognizant ( alias ) Adorable Angel nimezipata kutoka Chanzo Mamlaka na Aminika ni kwamba Mkuu wa Police Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Muliro amemuagiza Mkuu wa Police Kituo cha Kawe upesi sana Kumkamata Mfanyabiashara wa Mihogo Soko la Kawe Bwana Cherehani kwa Kosa la Kumjeruhi vibaya kwa Kumkata Sikio na Kidole cha Kati Mwanaume anayedaiwa ni Mgoni wake na Kutembea navyo Sokoni Kawe akivionyesha huku akifurahia na Kutamba.

Na Taarifa imeendelea kusema kuwa hata Mkewe pia nae anatakiwa Kukamatwa kwani alishirikiana na Mfanyabiashara huyu Bwana Cherehani ( ambaye ni Mumewe na Yeye akiwa ni Mke wake wa Tatu ) katika Kumtega hadi Kumfanya Mjeruhiwa afike Nyumbani Kwao waliko na Kumfanyia Ukatili huo Usiovumilika.

Mkiambiwa kuwa Mtandao huu wa JamiiForums una Nguvu sana na Ushawishi mkubwa na ni Mahiri kama Mchezaji Bora wa Argentina na Dunia Lionel Cognizant Messi muwe mnakubali, muuheshimu na muuamini pia.

Hata hivyo IGP Wambura na ACP Muliro nawapeni tu Taarifa za awali kuwa huyu Mfanyabiashara Bwana Cherehani ameshatoroka na nimetaarifiwa kuna baadhi ya Askari wenu Kituo cha Police Kawe ni Marafiki zake, anawamudu kwa Pesa zake za hapa na pale hivyo wamemwambia ajifiche hivyo kusababisha sasa Kutoonekana Sokoni Kawe au hata akija hakai eneo alilozoeleka bali anajificha kwa mbali.

Mwisho IGP Wambura na Kamanda wa Police Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Muliro mkimkamata huyu Mfanyabiashara Katili na Mpumbavu wa Mihogo Soko la la Kawe Bwana Cherehani upesi sana mwambieni awapeleke alipovitupa hivyo Viongo alivyovikata Sikio na Kidole ( ambavyo alikuwa akivionyesha kwa Watu na Wafanyabiashara wenzake Soko la la Kawe huku akitamba na Kufurahi ) amevizika au amevitupia wapi kwani kwa Taarifa zilizoko zinasema atakuwa amezifukia katika Makaburi Jirani na Ukuta wa Chuo cha Tiba cha Kijeshi Kawe ( MCMS ) huku zingine zikisema kuwa amevitupa katika Shimo la Vyoo vya Kulipia katika Soko la Kawe.

Nasisitiza Cognizant Mimi siungi mkono Kitendo alichokifanya Mjeruhiwa cha kuwa na Mahusiano na Mke wa Mfanyabiashara Bwana Cherehani na nimekilaani kwani si Kitendo kizuri ila sijafurahishwa zaidi na Ukatili mkubwa, mbaya na Usiovumilika alioufanya Mfanyabiashara Bwana Cherehani dhidi ya Mgoni wake na hapa ikiwezekana Sheria ziwabane wote Wawili japo najua kuna Mmoja itambana na itamgharimu zaidi.
 
Huyo mwenye mke hajatendewa unyama bwana Mightier, tena ulisema mke ana mimba ya kuzaa...........sidhani kuna poti yoyote anakubali dharau ile.
 
BR HESHIMU IGP
UKO NA KITUO CHA KAWE KWANN USIENDE KUTOA TAARIFA SIO KILA KITU UNAHITAJI IGP...FWATA MKONDO WA SHERIA UTASAIDIAWA TU KAMA NDUGUYO NDIE KAFANYIWA HIVYO NAJUA IMEUMA
 
Mi nilifikiri Kuna fisadi kakamatwa na na meno,au mtu kakutwa na hatia ya kuiba bilioni kadhaa,kumbe mambo ya kiswahili!!sasa hayo si mambo ya kumalizia ofisi ya kata?
 
BR HESHIMU IGP
UKO NA KITUO CHA KAWE KWANN USIENDE KUTOA TAARIFA SIO KILA KITU UNAHITAJI IGP...FWATA MKONDO WA SHERIA UTASAIDIAWA TU KAMA NDUGUYO NDIE KAFANYIWA HIVYO NAJUA IMEUMA
Upo sahihi bwana Pdidy, huyo mtafunaji wa mke wa mtu ndo alitakiwa kwenda polisi au mahakamani kama anahisi ameonewa badala ya kumtegemea bwana Mightier amsemee JF...
 
BR HESHIMU IGP
UKO NA KITUO CHA KAWE KWANN USIENDE KUTOA TAARIFA SIO KILA KITU UNAHITAJI IGP...FWATA MKONDO WA SHERIA UTASAIDIAWA TU KAMA NDUGUYO NDIE KAFANYIWA HIVYO NAJUA IMEUMA
We nawe ushaambiwa anahonga pesa polisi ulitaka Aya seme wapi haya?? Au ndio nyie polisi tajwa kwenye Uzi ?
 
Back
Top Bottom