Wanabodi
Kufuatia mazungumzo ya rais wa TLS juzi kuomba kuonana na Rais Samia,kumuomba pamoja na mambo mengine,ni kuomba Lissu aachiwe,kanuni za uchaguzi zirekebishwe,Chadema ishiriki uchaguzi.
Kiukweli,sijawahi kuona rais msikivu kama Samia!,siku ya Jumanne mtu aombe kumuona rais,kesho yake Jumatano nafasi ikapatikana
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Rais Samia ni msikivu, apewe maua yake. Vipi Serikali yake, Bunge na mahakama ni wasikivu? Kama sio inamanisha
Siku zote nimekuwa nikilalamika humu kuwa wasaidizi wa Rais Samia sheria hawamsaidii,wanamuogopa na kushindwa kumwambia ukweli,hii kesi ya uhaini ya Lissu ni hakuna kitu pale!
Pre GE2025 - Wazalendo Wapenda Haki, Msiwe na Wasiwasi, Uhaini ni Matendo na Mipango Mkakati wa Kuutenda, Sio Maneno!, Maneno ni Sedition tuu na Sio Treason!
TLS ni wasaidizi wa Samia wa sheria,sisi TLS hatumuogopi Samia hivyo nilishauri tumweleze ukweli
Rais Samia Mgeni Rasmi AGM ya TLS: Wanasheria Tumweleze Ukweli Kuhusu Ubatili wa Katiba Yetu na Sheria Zetu, Turudishe Haki Kuu ya Msingi
Jana hili limetokea kama zali, TLS imekutana na Samia,na tumemweleza hili la Lissu
Rais wa TLS: Tumezungumza mengi na Rais Samia
Kama hoja hizi za TLS ni za kweli, na sio Lip Services, then Tundu Lissu anakwenda kuachiwa, kanuni za uchaguzi zinarejewa, Chadema inafuta NRNE ,Inashiriki Uchaguzi, TAL Mgombea Urais wa Chadema, Tunafanya Uchaguzi Mkuu Huru na wa Haki Kweli!
NB:Angalizo,isije kuwa TLS wamepigwa tuu sound,lip services!
Je, kuna uwezekano baadhi ya Viongozi wetu wanatoa baadhi ya Ahadi kwa "Paying lip Services"?
Hili la watu kupigwa sound, niliwahi kumshauri Mama
Mama don't preach. I think we've had enough of Preaching about law, justice & human rights. Would you Please just Practice what you Preach?
Pia tulimsisitiza Mama
Ombi kwa Rais Samia, tunakushukuru kwa mahubiri mazuri kuhusu haki, tunakuomba utende unachohubiri yasibaki kuwa maneno tuu lakini vitendo ni tofauti
Kuhusu kuachiliwa kwa haka ka simba ka Kizimkazi,
Pongezi Rais Samia kwa Tanzania kuwa Kinara Uhuru wa Habari, EAC, Vipi Kale ka 'Simba ka Kizimkazi' Mnaonaje Kaachiwe?, Kanatuvurugia Sana Amani?
Mungu Ibariki Tanzania
Paskal