Huyu Pogba wetu ni hasara tu

Huyu Pogba wetu ni hasara tu

yani bora wangemsajili ngolo kante timu ingelifanya vizur na Mashabiki wake wangefurahi hadi ligi inakwisha.lakini sasa imani juu yake imepotea kabisaaa
 
Kama kuna mchezaji anayejiamini sana ulimwenguni basi ni Pogba. Anaweza kufanya kila kitu peke yake bila ushauri wowote. Mashabiki mkilalamika kuhusu kushuka kiwango cha klabu anawaita ninyi washabiki wa team pinzani. Mkisema mna hali ngumu sana hata mnashindwa kuhudhuria mechi anacheka na kusema "bado hamjaisoma namba vizuri" Anafurahia majonzi ya washabiki.
Kinachonikera ni kwamba uchezaji wake mbovu unauumiza hadi mashabiki wa timu pinzani
POGBA NI NANI NA MAANA YA NENO POGBA NI NINI?
Kwani kwenye google hamna?
 
Kinachonikera ni kwamba uchezaji wake mbovu unauumiza hadi mashabiki wa timu pinzani

Kwani kwenye google hamna?
Sikudhani kuwa naweza lipata kwenye kamusi etc. Neno baya! Silitaki tena
 
POGBA NI NANI NA MAANA YA NENO POGBA NI NINI?
Ni mchezaji wa timu ya Manchester United ya England. Alisajiliwa kimagumashi, kinyume na matarajio ya wengi kwa gharama kubwa, lakini hachezi ipasavyo kwa kadri ya matarajio ya wengi. Soma hii thread kuanzia mwanzo, utaelewa katoka timu gani na sasa yuko timu gani na kwa nini mashabiki mpaka wa timu pinzani wanamlalamikia. Utaelewa tu.
 
Jf chukueni huu Uzi mchapishe kitabu! Hapa nanusa mabilioni ya shilingi! Ila nadhani dakika ya 92 Pogba atapiga hat trick, japo mashabiki wote watakuwa wameondoka uwanjani kwa kukata tamaa! Pogba ni mtaalam wa dakika za majeruhi, iweni wavumilivu!
 
7ce6d6fea54acf4aa34ee4c860d9ae85.jpg
 
Naipenda sana Manchester lakini kama huyu Pogba atabaki msimu ujao nitahama timu isiwe taabu maana sijazaliwa nayo na siwezi kukosa furaha ya moyo wangu kisa Pogba.
Mbwembwe nyingi na hamna kitu...
Umesikia hata mashabiki siku hizi hata hawanunui jezi wala kuingia uwanjani kama ilivyotakiwa sasa timu mapato yameshuka?? mwambie na Lizaboni muungane mtafute timu ya ukweli itakayoleta dira mpya!!
 
FA inampendelea sana Pogba, jamaa anaishindia timu yake kwa kufunga mabao ya mkono.

Halafu hizi timu pinzani hazijiangaishi kupata ile manual yenye sheria 17 za soka.

Nahisi hata msimu ujao Pogba atatwaa kiatu cha dhahabu kwa kufunga magoli ya mkono.

Nikimfikiria huyu Pogba napatwa na hasira..........Kama vipi mashabiki tuingie uwanjani tukakinukishe kama wale mashabiki wa Zamalek ya kule Misri!
Utaanzaje wakati kila shabiki anaogopa tena kuanzia wa chini kabisa mpaka yule mwenye hisa.......labda jaribuni kuingia barabarani ila mkumbuke mnaweza fungiwa kuingia uwanjani pia
Wapi Kiranga haya ndo mambo yako ina maana umesusa jumla.......umeondoka mchambuzi makini kabisa......
 
Ni mchezaji wa timu ya Manchester United ya England. Alisajiliwa kimagumashi, kinyume na matarajio ya wengi kwa gharama kubwa, lakini hachezi ipasavyo kwa kadri ya matarajio ya wengi. Soma hii thread kuanzia mwanzo, utaelewa katoka timu gani na sasa yuko timu gani na kwa nini mashabiki mpaka wa timu pinzani wanamlalamikia. Utaelewa tu.
Asante, kuna muungwana amenijbu na kunielekeza ni google! Lo! Sikuamini! (naishia hapa). Nilidhani mwandishi kakosea spelling alilenga kuandika Drogba! Kumbe NO, !
 
Mi niliomba huyu Pogba tumpe japo miaka miwili cz naamini baada ya miaka hiyo ataleta matunda yaliyotarajiwa. Si mnakumbuka jinsi alivyoikuta Man U ikiwa dhoofu ilhali baada ya uongozi mbaya wa LVG!? Na kwa kitendo cha mleta mada kutumia hela ya usajili wa Pogba kumponda Pogba ni wazi yeye mleta mada na wanaomuunga mkono wamejiandaa kuangukia pua baada ya msimu huu. Hamjiulizi ni kwa nini huyu Pogba ni maarufu sn kwa sasa hadi Forbes wanamwelewa sana na wanaamini haya ni mapito tu,na huyu pogba ana bright future!? Kwa imani yako mleta mada labda ungemtumia Fellaini, ila kwa huyu Pogba naamini wengi tunaamini huko mbeleni atatoa matunda mazuri. Watanzania wanajua,Forbes wanajua na dunia inajua!!
Unadhani anguko hili la uchumi haraka namna hii ndani ya Man linarekebishika ndani ya mwaka mmoja au 2? Kuporomoka ni rahisi ila kuurudisha sasa,mhhhh!! Maana mashabiki sasa hawaingii uwanjani na hata juzi hapa kafukuza bodi ya kukysanya viingili akihisi wanampiga cha juu milangoni,ye haangalii alipojikwaa anaangalia alipoangukia

Endelea kuwa shabiki wa mashetani wekundu!!
 
Umesikia hata mashabiki siku hizi hata hawanunui jezi wala kuingia uwanjani kama ilivyotakiwa sasa timu mapato yameshuka?? mwambie na @Lazaboni muungane mtafute timu ya ukweli itakayoleta dira mpya!!
Kuna mashabiki wengine hata timu ikishuka daraja anashuka nayo kama kaambiwa ndo mama yake mzazi. Hawa ndio wanakufaga na presha majumbani kwao.
 
Nadhani POGBA ana tatizo sio kama wachezaji wenzake waliowahi kununuliwa kwa bei kubwa. wenzake waliacha mbwembwe . lanini pogba bado anamajisifu na kujiona yeye ndio manyuuu, anabadili mikato na rangi za nywele.

ila najiuliza mbona haitaji ile rangi ya team yake? hivi huyu ni manyuu kweli? Kweli POGBA anatuharibia team,....
Sio kwamba tatizo ni timu?
 
hivi hamkujiuliza Juve kwanini ilikubari kumuuza Pogba na kumnunua wachezaji wa maana ?


Hamkujiuliza kwanini Pogba alikubari kutua Manuu bila kujali kutoshiliki CL?

Hivi Pogba alikuwa lini mfungaji bora ?
 
Kuna mashabiki wengine hata timu ikishuka daraja anashuka nayo kama kaambiwa ndo mama yake mzazi. Hawa ndio wanakufaga na presha majumbani kwao.
Umemsikia yule mumiliki wa magazeti ya udaku ya The Sun ana lalama walifanya biashara na Man U ila hawataki kumlipa,sijui akilipwa ataendelea kuwepo huko au ataondoka akili zitakuwa zimemrudia?
Ila ngoja tuone approach aloitumia itamkosti.....haaaa....Twiga Bankork wameanza mufilisi,sasa......Eee Mungu nipe uzima nione mengi!!
 
Back
Top Bottom