more88
JF-Expert Member
- Apr 9, 2016
- 447
- 413
Hahaha
HahahaPOGBA anataka kupiga kona na afunge yeye
HahahaPOGBA anataka kupiga kona na afunge yeye
Wanajamvi mtakumbuka wakati wa usajili tuliambiwa hii timu yetu sasa inasajili bonge la fowadi anayekuja kumaliza matatizo yote.
Hata kuingia kwake ktk timu alikuja na mbwembwe kibao, Mara kufanya mazoezi ya ghafla klabuni usiku au mchana akiwa na waandishi Wa habari ili mradi ajioneshe tuu kwa mashabiki kuwa anauwezo.
Cha kushangaza ligi ilipoanza ameanza kuja na Masharti kibao klabuni eti ili aonekane kuwa yeye ni mchezaji mzuri kuliko Wa timu pinzani tumtimizie mambo yafuatayo.
1. Mabeki wa timu pinzani wote wafungwe miguu na mikono wawapo uwanjani.
2. Timu yetu iwe inapewa penati kila mechi na marefa ili yeye awe mfungaji bora.
3. Timu pinzani zisiruhusiwe kuleta mashabiki uwanjani.
Sasa wenye Akili hapa klabuni tukaanza kuhoji huyu kweli ni fowadi au garasa?
Mbona fowadi tuliye muacha alikuwa anafunga magoli huku mabeki Wa timu pinzani wakicheza japo tulimuona kama kashuka kiwango?
Tena timu pinzani ziliruhusiwa kwenda kwa ndege helcopta au usafiri wowote kokote hapa nchini kuchukua mashabiki na kuwaleta uwanjani katika mashindano mbali mbali.
Uchumi Wa klabu umeshuka ghafla mashabiki hawana imani naye tena kabisa. Wanajiuliza fowadi gani hawezi cheza mechi za kimataifa anag'ang'ania mechi za mchangani tuu.
Huyu Pogba klabu imepata hasara kubwa Sana kwa kusajili mchezaji bila hata kuangalia uzoefu na historia yake hapa klabuni. Anazua hofu ubabe na kushabikia magoli ya mikono eti yawe halali kwa timu yake tuu.
Nadhani POGBA ana tatizo sio kama wachezaji wenzake waliowahi kununuliwa kwa bei kubwa. wenzake waliacha mbwembwe . lanini pogba bado anamajisifu na kujiona yeye ndio manyuuu, anabadili mikato na rangi za nywele.Pogba kwani si ndo kwanza ana msimu wa kwanza katika mkataba wa miaka mitano!!! Slow slow anatupia magoli ya kushtukiza. Japo inaonekana kama uhaba wa magoli kwa mashabiki umeanza kuwa tatizo kwake na kwa team. Mashabiki wanalia sana kwani toka kikosi kilichopita kilivyokuwa kinasuasua kwenye league nyakati za mwisho, afueni ilipatikana wakati wa mechi za majaribio akitupia magoli na pasi za mwisho matata sana. Ooh! Inawezekana kukosekana kwa first eleven ya uhakika ndo tatizo la Pogba ama yeye kama superstar wa team basi anataka kila mafanikio ya team uwanjani asemwe ni yeye. Nadhani Pogba anatakiwa kupata ushauri wa kimchezo toka kwa viungo nguli maana naona ma-legend kama Scholes na Giggs wamempa ushauri ila anaona yeye ndo yeye.
Labda kama alivyosema mwenyewe ngoja ainyooshe klabu.
Siku nyingine soma Kwanzaa uelewe ndio ujibu leo tupo na Paul pogba kule team coach sizonje hatari hatari`bonge la fowadi` Pogba sio fowadi,,, nenda kwa Edo kumwembe akufundishe uchambuzi
ETI APIGE PENATI BILA KIPA KUWEPO!Pogba nasikia anajiapiza kuzinyoosha timu kwa kufunga magoli mengi huku kumbe anatoa kitu kidogo kwa makipa....kama vile 10m ili apewe magoli ya chee
Qwi Qwi Qwi.... Huyu jamaa ni Div V kabisa!! Eti nenda kwa Edo Kumwembe akuelezee kuhusu Pogba wa Man U!!! Fasihi kidogo tu inamshinda?Siku nyingine soma Kwanzaa uelewe ndio ujibu leo tupo na Paul pogba kule team coach sizonje hatari hatari
Mtu mmoja huyo huyo? Kwa mechi moja ama mechi anuwai?Tatizo yeye ni ni kiungo....
Wakati huo anataka kuwa forward.....
Wakati huo anataka kuwa beki........
Sometime anataka awe Goalkeeper...
Na Baadae mtasema miaka miwili ni michache sana kama awali mlivyo sema Siku mia ni chache.HAMNA POGBA YUKO FRESH TU SEMA WABONGO TUNABEBEWA SANA AKILI ZETU NA TUNATUMIKA KWA KUDANGANYWA NA MAKOCHA WA TIMU PINZANI KAMA HATUKO TIMAMU. KWA KIFUPI MAKOCHA NA VIONGOZI WA TIMU PINZANI WAMESHINDWA KUFUNDISHA NA KUENDESHA SOKA LA UKWELI,WAMEBAKI KUFANYA POROJO TU WANAPOKUWA HUKO CNN,SKY NEWS,BBC NK! ILA POGBA KIWANGO BADO KIPO CHA KUELEWEKA TU. HALAFU YATUPASA TUMPE JAPO HATA MIAKA MIWILI HUYU POGBA!!
Kila Mtu Man U anatamani Van Persie asingeuzwa. Van Persie alikua mtu wa majeraha ila alikua akifunga Magoli na hasa magoli Muhimu.Nasikia pogba analalamika hakujua kama hii kazi ya uchezaji ni ngumu,ange-sign mkataba wa miaka miwili tu na siyo mitano
Acha Uchochezi bana!! Sisi tunamzungumzia Pogba na Man U. Qwi Qwi Qwi...Kama wanaompa taarifa wanamdanganya, akipita hapa anaweza kuona wahariri na wanahabari wanamsaidia aelewe hali ya kitaa. Mkulu aliwaomba wahariri na wanahabari waisadie serikali. Hiyo taarifa sikuitayarisha, nimeiwasilisha tu kama ilivyoripotiwa.
Ingawaje viongozi wanajitahidi kutushawishi kwamba uchumi unakua, unapaa lakini hali ya maisha ya kitaa inaonesha kama uchumi umepiga stop. Uchumi gani wa kukusanya mapato tu? (kuwakamua walalahoi). Haya sasa mambo ndio hayo, mfalme amevaa joho linalompendeza sana.
Mtoto ametokea kum-save mfalme ili asitembee bila nguo.
Kwa kweli waandishi na wanahabari wanatakiwa kwenda kitaa kuwahoji wananchi live!
Teh teh teh.... huu uzi umewapiga Chenga watu wengi sana, hasa wale wasomaji wa magazeti ya Ijumaa na kiu bila kuwasahau waangaliaji wa Bongo Muvie.Pogba wa KAUZU FC AU HUYU NINAYEMFAHAMU???
Isee Unataka Pogba apige Chenga uwanja mzima nini kwani anacheza mwenyewe?
Pogba-Herrera-Matta goal
Mtoto anaweza kuongoza mtihani kwa wastani wa 20% jiulize hilo darasa likoje?
POGBA halisi hana shida labda pogba wa Kauzu fc
Weeeh! Kumbe Pogba yuko vizuri!Tuache uongo wakati mwingine.
Ni upepo tu, hata C7 walisema ameisha leo yuko wapi?Weeeh! Kumbe Pogba yuko vizuri!
ah pogbaaaaaa...
pogba nasikia amekuwa mnyang'anyi mtaani,eti mali za washabiki wake zote zinapaswa azimiliki yeye...
na ukitaka kumjua pogba vizuri mwambie hujui kucheza mpira...
hapo mechi utazisikia ukiwa gerezani...
pogbaaaaaaaaaaaaa...
akijibu hoja jiandae kushangaa kwamba ni msomi au kila.za wa mpira.

Lous van gaal alisema tutamkumbuka na tatal footbal yke.
hadi raha dah! Watu mnatisha