Huyu Pogba wetu ni hasara tu

Huyu Pogba wetu ni hasara tu

Wanasema Jezi za Pogba zinauzwa sana,kiasi kwamba klub inapata faida mpaka mashabiki wamenunuliwa ndege kupitia mauzo Ya Jezi za POGBA.Niliskia kipindi Pogba anatafta usajili aliwaahidi mashabiki wake Mill.50 ila tangu aanze kucheza hajatoa hata sh.200.
 
Tatizo ni kochaaaa, alimsifia sana sasa matokeo yake kila mpira anabutua tu hajui kama ni wa kona, faulo, wakurusha au vipi......
Na kila mpira anataka acheze na kupiga yeye tu, ukiuliza utaambiwa et kisa ana ari na kasi ya mchezo,

Sizonje mtoe huyu jamaa tunakusa magoli muhimu bhana
 
tatizo akiwapa pasi mmalizie mnanyang'anywa mipira kirahisi...sasa kama ana uchungu na timu kwa nini asicheze uwanja mzima!? Mwacheni Pogba aisaidie timu!
 
Pogba bwana sasa hiv anadai akicheza na grizman atafanya vizuri. Tumtoen huyu hatufai
 
POGBA anataka kupiga kona na afunge yeye
Hayo mambo ya kichuya, Pogba hana kiwango hicho..
Japo nasikia alienda kwa "Vardy" yule tolu wa ile timu ndogo iliyopanda daraja kwa kasi na kubeba "ndoo" hapo jirani kuchukua maujuzi, sasa sijui kama anatumia mbinu alizopewa ipasavyo? Au kwa kuwa timu yetu ya manyuu ni kongwe sana ukilinganisha na ile reisista ya Vardy, inataka maujuzi mapya na sio C&p? maana kule Vardy nasikia anaheshimiwa wakati Pogba anazomewa
 
Pogba kwani si ndo kwanza ana msimu wa kwanza katika mkataba wa miaka mitano!!! Slow slow anatupia magoli ya kushtukiza. Japo inaonekana kama uhaba wa magoli kwa mashabiki umeanza kuwa tatizo kwake na kwa team. Mashabiki wanalia sana kwani toka kikosi kilichopita kilivyokuwa kinasuasua kwenye league nyakati za mwisho, afueni ilipatikana wakati wa mechi za majaribio akitupia magoli na pasi za mwisho matata sana. Ooh! Inawezekana kukosekana kwa first eleven ya uhakika ndo tatizo la Pogba ama yeye kama superstar wa team basi anataka kila mafanikio ya team uwanjani asemwe ni yeye. Nadhani Pogba anatakiwa kupata ushauri wa kimchezo toka kwa viungo nguli maana naona ma-legend kama Scholes na Giggs wamempa ushauri ila anaona yeye ndo yeye.

Labda kama alivyosema mwenyewe ngoja ainyooshe klabu.
 
Hayo mambo ya kichuya, Pogba hana kiwango hicho..
Japo nasikia alienda kwa "Vardy" yule tolu wa ile timu ndogo iliyopanda daraja kwa kasi na kubeba "ndoo" hapo jirani kuchukua maujuzi, sasa sijui kama anatumia mbinu alizopewa ipasavyo? Au kwa kuwa timu yetu ya manyuu ni kongwe sana ukilinganisha na ile reisista ya Vardy, inataka maujuzi mapya na sio C&p? maana kule Vardy nasikia anaheshimiwa wakati Pogba anazomewa
Vardy hahahahaha
 
Man ya POGBA haiwezi kushuka daraja kwa sababu zifuatazo:-
1.huyu mchezaji amezuia timu washindani wasifanye mazoezi hadi 2020 ila MAN U wanaendelea na mazoezi
2.man u hulazimisha refa achezeshe wanavyotaka wao
,......
.......klabu imefirisika mashabiki wanahama timu
 
POGBA mwenyewe alishajisemea alimbip mwenye timu simu ikanasiamo huko kwa mwenye timu na akamsajili wakati yeye wala hakutaka na hakujipanga basi tu ilitokea.
 
POGBA HONGERA POGBA NASEMA TENA HONGERA ZIKUFIKIE POPOTE ULIPO

Wewe ulitumia usanii kupata usajili Na umefanikiwa.
Cheki wanatimu wakiumia uwanjan Panadol hawapati wakati enzi za HB tulienda tibiwa nje kwa gharama zake

pogba wewe Ni huna mfano umesema eti timu utafungua viwanda Kila Kona cha ajabu wachezeji wamejitahid kusomaa sasa pesa huwapi vyuon wameishia kusoma no ya tshit yako tuu .

Ivi pogba ahad yako ya kuwasaidia wachezaji wanyonge imeishia wapi kwa maana hta sh hawaon tena
 
Kama kuna mchezaji anayejiamini sana ulimwenguni basi ni Pogba. Anaweza kufanya kila kitu peke yake bila ushauri wowote. Mashabiki mkilalamika kuhusu kushuka kiwango cha klabu anawaita ninyi washabiki wa team pinzani. Mkisema mna hali ngumu sana hata mnashindwa kuhudhuria mechi anacheka na kusema "bado hamjaisoma namba vizuri" Anafurahia majonzi ya washabiki.
 
Wanajamvi mtakumbuka wakati wa usajili tuliambiwa hii timu yetu sasa inasajili bonge la fowadi anayekuja kumaliza matatizo yote.

Hata kuingia kwake ktk timu alikuja na mbwembwe kibao, Mara kufanya mazoezi ya ghafla klabuni usiku au mchana akiwa na waandishi Wa habari ili mradi ajioneshe tuu kwa mashabiki kuwa anauwezo.

Cha kushangaza ligi ilipoanza ameanza kuja na Masharti kibao klabuni eti ili aonekane kuwa yeye ni mchezaji mzuri kuliko Wa timu pinzani tumtimizie mambo yafuatayo.

1. Mabeki wa timu pinzani wote wafungwe miguu na mikono wawapo uwanjani.

2. Timu yetu iwe inapewa penati kila mechi na marefa ili yeye awe mfungaji bora.

3. Timu pinzani zisiruhusiwe kuleta mashabiki uwanjani.

Sasa wenye Akili hapa klabuni tukaanza kuhoji huyu kweli ni fowadi au garasa?
Mbona fowadi tuliye muacha alikuwa anafunga magoli huku mabeki Wa timu pinzani wakicheza japo tulimuona kama kashuka kiwango?

Tena timu pinzani ziliruhusiwa kwenda kwa ndege helcopta au usafiri wowote kokote hapa nchini kuchukua mashabiki na kuwaleta uwanjani katika mashindano mbali mbali.

Uchumi Wa klabu umeshuka ghafla mashabiki hawana imani naye tena kabisa. Wanajiuliza fowadi gani hawezi cheza mechi za kimataifa anag'ang'ania mechi za mchangani tuu.

Huyu Pogba klabu imepata hasara kubwa Sana kwa kusajili mchezaji bila hata kuangalia uzoefu na historia yake hapa klabuni. Anazua hofu ubabe na kushabikia magoli ya mikono eti yawe halali kwa timu yake tuu.
huyu pogba ni PIMBI kabisa
 
Mmmmh dua la kuku halimpati mwewe.....Hapa Kazi Tu.
 
au akipiga kona adake yeye maskini pogba.akipiga chenga akabe yeye,akirusha mpira uliotoka nje aupokee yeye, kali kabisa wakati wa penalti akipiga hata goli likwa tupu atapaisha au mpira utatoka nje jamani Pogba
 
Kila nikimtazama Pobga huyu namkumbuka Denis Berkhamp...Huyu jamaa alikua hapandi ndege, sasa sijui POGBA naye kamuiga kutokupanda ndege tu na kusahau kumuiga kufunga mabao?
 
Back
Top Bottom