Huyu Pogba wetu ni hasara tu

Huyu Pogba wetu ni hasara tu

Pogba ana wakala wake ana cheo cha ujaji.......hiyo ndio sitaki kabisa kumsikia maana alimtangaza kwa mbwembwe kweli.
 
Pogba ata bonus kwa mashabiki wake tangu asajiliwe ameshindwa kutoa, nitofauti na Van Nestroy alikuwa anafunga magoli ya off-side lakini yanahesabiwa pamoja na kwamba alikuwa akisaidiwa na refa Howard web.
 
''Wanajamvi mtakumbuka wakati wa usajili tuliambiwa hii timu yetu sasa inasajili bonge la fowadi anayekuja kumaliza matatizo yote.''

ingekua lugha ya mamtoni nisingeelewa,,,,,
Trust me hujamwelewa soma maliza!! Ni kweli pogba halisi ni kiungo japo anatumika sometimes kama namba kumi!! Ila huyu sio pogba huyo unaemzani
 
Pogba baada ya kuona hawezi kufunga magoli upinzani sasa ameamua kujifunga mwenyewe,ili apate sifa aliokujanayo man U.Lakini mambo ni magumu mashabiki wamekasirika sasa hawamtaki lakini wanashindwa kumwambia waziwazi,kisa wanaogopa kufukuzwa uwanjani.
 
Mleta uzi ni zaidi ya Ngugi wa Thiong'o na ile tamthiliya yake ya I Will Marry When I Want (Ngaahika Ndeenda)
 
Pogbaunited na man United wanaisoma namba tuu, na wakitaka wamnunue na pirlo ili awe mfungaji bora kuliko Diego. YNWA
 
Kwani ilienda wapi?
Tumia kichwa kufikiri mambo yanavoenda sio kufugia nywele...we unafikiri kwa threads zenu mlizokuwa mnaandikiana na kujijibu wenyewe kuhusu chama chenu kuna GT angetamani hata kupoteza mda wake kufungua nyuzi,humu mlikuwepo mapoyoyo!watu wenye akili timamu ndo wanao-run hii forum that's why nyuzi makini kama hizi zikiandikwa kuna watu hujawahi kuwaona ila unaona wanachangia.
 
Naipenda sana Manchester lakini kama huyu Pogba atabaki msimu ujao nitahama timu isiwe taabu maana sijazaliwa nayo na siwezi kukosa furaha ya moyo wangu kisa Pogba.
Mbwembwe nyingi na hamna kitu...
 
Tatizo yeye ni ni kiungo....

Wakati huo anataka kuwa forward.....


Wakati huo anataka kuwa beki........

Sometime anataka awe Goalkeeper...
Muda mwingine anangangania kucheza nyuma ya goli akiamini yeye ni mchezaji namba 12.

Kiukweli haeleweki huyu djemba djemba wa man u.
 
ah pogbaaaaaa...
pogba nasikia amekuwa mnyang'anyi mtaani,eti mali za washabiki wake zote zinapaswa azimiliki yeye...
na ukitaka kumjua pogba vizuri mwambie hujui kucheza mpira...
hapo mechi utazisikia ukiwa gerezani...
pogbaaaaaaaaaaaaa...
akijibu hoja jiandae kushangaa kwamba ni msomi au kila.za wa mpira.
Pogba kapiga dongo lake saaafi kichwa alafu katia blichi ili awe kama mkongo.

Sijui anataka kuhamia kwenye kunengua au dansa wa diyamondii.
 
Me nadhani kuna haja ya kubadili sheria za FiFA wachezaji kama hawa ni wa kufungiwa hata kufungwa kabisa maana wanaitia hasara sana club, pesa aliyosajiliwa ni kubwa mno.
Sema Pogba hataki kabisa kusikia maswala ya FIFA na sheria mpya.
 
FA inampendelea sana Pogba, jamaa anaishindia timu yake kwa kufunga mabao ya mkono.

Halafu hizi timu pinzani hazijiangaishi kupata ile manual yenye sheria 17 za soka.

Nahisi hata msimu ujao Pogba atatwaa kiatu cha dhahabu kwa kufunga magoli ya mkono.

Nikimfikiria huyu Pogba napatwa na hasira..........Kama vipi mashabiki tuingie uwanjani tukakinukishe kama wale mashabiki wa Zamalek ya kule Misri!
 
Tatizo kubwa linalonisikitisha kwa pogba akipigiwa zile clear asist yeye hukasirika na kuchukua majukumu ya kocha ya kumpiga sub mido
 
Back
Top Bottom