Huyu Pogba wetu ni hasara tu

Huyu Pogba wetu ni hasara tu

HAMNA POGBA YUKO FRESH TU SEMA WABONGO TUNABEBEWA SANA AKILI ZETU NA TUNATUMIKA KWA KUDANGANYWA NA MAKOCHA WA TIMU PINZANI KAMA HATUKO TIMAMU. KWA KIFUPI MAKOCHA NA VIONGOZI WA TIMU PINZANI WAMESHINDWA KUFUNDISHA NA KUENDESHA SOKA LA UKWELI,WAMEBAKI KUFANYA POROJO TU WANAPOKUWA HUKO CNN,SKY NEWS,BBC NK! ILA POGBA KIWANGO BADO KIPO CHA KUELEWEKA TU. HALAFU YATUPASA TUMPE JAPO HATA MIAKA MIWILI HUYU POGBA!!
Alipewa miaka 20 akashindwa 2 itamtosha?
 
Nasikia pogba analalamika hakujua kama hii kazi ya uchezaji ni ngumu,ange-sign mkataba wa miaka miwili tu na siyo mitano
 
UMEAMUA KUWEKA MAMBO HADHARANI
Kama wanaompa taarifa wanamdanganya, akipita hapa anaweza kuona wahariri na wanahabari wanamsaidia aelewe hali ya kitaa. Mkulu aliwaomba wahariri na wanahabari waisadie serikali. Hiyo taarifa sikuitayarisha, nimeiwasilisha tu kama ilivyoripotiwa.

Ingawaje viongozi wanajitahidi kutushawishi kwamba uchumi unakua, unapaa lakini hali ya maisha ya kitaa inaonesha kama uchumi umepiga stop. Uchumi gani wa kukusanya mapato tu? (kuwakamua walalahoi). Haya sasa mambo ndio hayo, mfalme amevaa joho linalompendeza sana.
Mtoto ametokea kum-save mfalme ili asitembee bila nguo.

Kwa kweli waandishi na wanahabari wanatakiwa kwenda kitaa kuwahoji wananchi live!
 
Pogba nasikia anajiapiza kuzinyoosha timu kwa kufunga magoli mengi huku kumbe anatoa kitu kidogo kwa makipa....kama vile 10m ili apewe magoli ya chee
Halafu huagiza refa atoe kadi ya rangi ya jezi yake kwa kipi na mabeck wa timu pinzan ili apate mteremko
 
Mchezaji gani huyu anapanic akiulizwa maswali magumu?
Afu ni mlagai, alisema amesitisha kutoa pasi kwa mda usiozidi miezi miwili, sasa inaenda kuwa miezi 6 na bado hajatoa pasi kwa wachezaji chipukizi,kazi zake kupiga danadana tu na kupaka mpira rangi, Huyu Pogba hafai kuwa hata mchezaji wa Machame Fc.
 
Hapo mmeuziwa pogba fake
 

Attachments

  • 1479756989784.png
    1479756989784.png
    83.4 KB · Views: 38
Pogba wa KAUZU FC AU HUYU NINAYEMFAHAMU???

Isee Unataka Pogba apige Chenga uwanja mzima nini kwani anacheza mwenyewe?

Pogba-Herrera-Matta goal

Mtoto anaweza kuongoza mtihani kwa wastani wa 20% jiulize hilo darasa likoje?

POGBA halisi hana shida labda pogba wa Kauzu fc
 
Ile sheria mpya ya soka iliyopitishwa juzi huku rais wa chama chetu cha mpira akijinasibu kuisaini mapema imfikiapo nadhani ishaanza kufanya kazi...kujadili uwezo wa mchezaji alievunja rekodi ya mapato ya mauzo ya jezi kila mwezi ni kosa
 
Wanajamvi mtakumbuka wakati wa usajili tuliambiwa hii timu yetu sasa inasajili bonge la fowadi anayekuja kumaliza matatizo yote.

Hata kuingia kwake ktk timu alikuja na mbwembwe kibao, Mara kufanya mazoezi ya ghafla klabuni usiku au mchana akiwa na waandishi Wa habari ili mradi ajioneshe tuu kwa mashabiki kuwa anauwezo.

Cha kushangaza ligi ilipoanza ameanza kuja na Masharti kibao klabuni eti ili aonekane kuwa yeye ni mchezaji mzuri kuliko Wa timu pinzani tumtimizie mambo yafuatayo.

1. Mabeki wa timu pinzani wote wafungwe miguu na mikono wawapo uwanjani.

2. Timu yetu iwe inapewa penati kila mechi na marefa ili yeye awe mfungaji bora.

3. Timu pinzani zisiruhusiwe kuleta mashabiki uwanjani.

Sasa wenye Akili hapa klabuni tukaanza kuhoji huyu kweli ni fowadi au garasa?
Mbona fowadi tuliye muacha alikuwa anafunga magoli huku mabeki Wa timu pinzani wakicheza japo tulimuona kama kashuka kiwango?

Tena timu pinzani ziliruhusiwa kwenda kwa ndege helcopta au usafiri wowote kokote hapa nchini kuchukua mashabiki na kuwaleta uwanjani katika mashindano mbali mbali.

Uchumi Wa klabu umeshuka ghafla mashabiki hawana imani naye tena kabisa. Wanajiuliza fowadi gani hawezi cheza mechi za kimataifa anag'ang'ania mechi za mchangani tuu.

Huyu Pogba klabu imepata hasara kubwa Sana kwa kusajili mchezaji bila hata kuangalia uzoefu na historia yake hapa klabuni. Anazua hofu ubabe na kushabikia magoli ya mikono eti yawe halali kwa timu yake tuu.
!!!!!!!!!!????????????????
 
Ndiyo matatizo ya kocha asiyejitambua siku zote anadhani yeye ni mchezaji na si kocha na kutaka kucheza kila position yeye matokeo yake timu yetu pendwa inafanya vibaya kuliko wakati wowote ule tangu ianzishwe. Tumekuwa timu ya hovyo hovyo hata wacheza wamepoteza ari kabisa.

Tatizo yeye ni ni kiungo....

Wakati huo anataka kuwa forward.....


Wakati huo anataka kuwa beki........

Sometime anataka awe Goalkeeper...
 
Mchezaji gani huyu anapanic akiulizwa maswali magumu?
Afu ni mlagai, alisema amesitisha kutoa pasi kwa mda usiozidi miezi miwili, sasa inaenda kuwa miezi 6 na bado hajatoa pasi kwa wachezaji chipukizi,kazi zake kupiga danadana tu na kupaka mpira rangi, Huyu Pogba hafai kuwa hata mchezaji wa Machame Fc.
Kumbe huyu Pogba ndo ana mambo ya kipuuzi kiasi hiki sijui kamati ya usajili ilijifikiria kusajili mchezaji asiejielewa kiasi hiki mpaka chipukizi hawapati nafasi ya kuonyesha viwango vyao huu ni ujinga sasa.
 
Back
Top Bottom