Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

The problem is, those people who always praise him don't go back and clear their nonsense mistakes. At the end of the day, JK will be responsible with what we have/have-not achieved. It's a game in a political stage b'se these so called ministers and other officials are just trying to protect their status/Ugali.
 
Alaah Mzee ameshtuka,kwa nini anasifiwa sana wakati tuna matatizo kibao!Ni bora anajua hivyo,kwani hakuna sababu yoyote ya kumsifu ikiwa kuna matatizo kibao ambayo yapo kwenye udhaifu wa utendaji!
 
Muungwana JK, tulijua toka wakati wa uchaguzi kuwa yeye na kundi lake la mtandao kisiasa wana tatizo kubwa, maana zile kampeni hazikuwa za kawaida kwa nji yetu masikini. Hela za kampeni zilikuwa nyingi mno, kuharibu majina ya wanasiasa wengine kwa makusudi ili tu wapate power,

Wakaenda mpaka kuiharibu katiba na mwenendo wa uchaguzi wa CCM, wakatishia mpaka kwamba nji haitatawalika iwapo hawatapata, wakawaharibu watu babu kubwa kama kina Salim, maneno mengi, tulijua kuwa ni upepo tu na nguvu ya soda, tuliposema mapema tukatukanwa matusi mazito kule BCS, tulipojaribu kuwasihi wabongo waamuke usingizini, maana they were about to commit the worst political mistake ever, wakatujia juuu, sasa here we are!

One year tayari wananchi wamechoka, tena choka mbaya maana wamepigika ile mbaya na hawana hamu, leo eti Muungwana hataki misiifa, ebo! hataki misifa kwa vipi? Yaani anatuona sisi wabongo wajinga? au? Hebu atuambie zile misifa aliyokuwa akipewa hata kabla ya uchaguzi na kina Kingunge, Tido Mhando mzee wa polls za BBC, watu wa Mlimani, zilikuwa ni sifa za nini? Aliwahi kufanya nini cha maana kabla ya kuwa rais? Hebu kuweni wakweli what didi the man do?

Muungwana toka siku ya kwanza ulipoanza hizi kampeni za urais you were wrong, sina tatizo na Muungwana personally, lakini kiuongozi I do, kwa sababu you just don't have it, kule mwanzoni nilisema kwamba kile tu kitendo cha kuwapa watu 60 uwaziri, mpaka Ikulu viti havikutosha kwenye mkutano wa cabinet, ilikuwa tayari dalili za ku-go home.Mimi ninasema katika awamu nzima ya nne tuliyonayo, ninamuona kiongozi mmoja tu angalau mwenye nafuu naye ni Mama Migiro, wengine wote wanaweza kufunga virago waondoke na taifa letu litakuwa just fine! Yes we will be just fine, I mean what are these people doing? Kuna mliosema tumpe muda, sasa tuambieni tufanye nini sasa?

Eti leo hataki misifa tena? Mzee JK na kundi lako tafuteni njia za kujiondoa kwenye madaraka, kwa sababu hakuna njia nyingine ya kuwaondoeni, na hatuwezi kusema eti mnaweza kuwa rehabilitated kwa sababu mtu anyekuwa rehabed, ni yule ambaye kabla ya kuwa na tatizo alikuwa sawa, sasa nyinyi hamjawahi kuwa sawa, ndio maana hiyo option haipo, nyinyi ni kuondoka au mkiendelea acheni ngebe ngebe,

nyamazeni kuleni mapesa ya kodi zetu wajinga, hakuna hope maana Chadema nayo ndio hivyo tena taifa zima tutaishia kulazimishwa kula kisusio for breakfast na kusikiliza miziki ya Jimmy Reeves na Dolly Parton!
 
The whole thing is NONESENSE, kwani aliyekuwa nataka misifa si yeye mwenyewe, sasa anataka kutudanganya kuwa hapendi misifa na sisi tunakubali?

No ni yeye aliyeanzisha kampeni za misifa, mpaka kutajwa tajwa na Twanga pepeta, kuwa mtu wa watu mbona asiseme then kuwa waache kumpa sifa, why now?

Alipokuwa akipewa zile sifa kule mwanzoni alikuwa amfanya kitu gani cha maana, sasa anchokataa ni nini, mimi ningetegemea angekubali publicly kuwa ametuangusha wabongo maana hana sifa za kuwa rais ana angeomba radhi badala ya kutumia ujanja wa kukaripia watu wanaomsifia, wakati ule Mkapa anamsifia kwenye kampeni alikuwa anasifia nini?

Wakati mtandao wanaiponda serikali ya Mkapa mwanzoni na kujifanya wao ni wajuaji walikuwa wakijisifia kitu gani? Wabongo hebu taumke na tuache kukubali huu usaniii, guys litsen hawa mtandao ahwana lolote ni usaniii tu na hii ya Muungwana kujifanya hataki misifa ndio hasa usaniii wenyewe!

Huwezi kuwandanganya wananchi kwa muda mrefu, sasa ukweli umejitokeza wazi for everybody to see kwamba Awamu ya nne ni wasaniiii watupu, mawaziri 60, hawana jibu la kitu kidogo kama umeme, maneno mengiiiiiiii oooh mimi nimeeenda Wall streeet, rais wa kwanza blah blah blah blah, ooh yea sasa hutaki tena misifa, acheni usaniii mmeshindwa kubalini yaishe!

Alichopaswa kusema kwenye huo mkutano ni kuwaomba radhi wabongo na taifa zima, kwa kuishusha hadhi ya urais, na kutokuwa na uwezo wa uongozi mzito kama huo, nigeeelewa, lakini sio kukataa misifa maana ni tabia aliyoianzisha yeye mwenyewe alipokuwa akiwalipa wapiga muziki wa Twanga wamtaje taje bila sababu!
 
The question is how many fake publicity stunts he has done? That's what he can get for faking. I don't know about you guys, but for this year I can vote JK as the most annoying name in 2006. I feel like to flip my computer table when I log online and read something like "JK boyz". Who cares?
Ninachomshauri rais wetu asichelewe sana, he should start working for the people NOT for Tony Blair. Watu ndiyo waliomuweka madarakani unaposema huwezi kuacha kusafiri kwa sababu ya malalamiko ya watu nashindwa kuelewa ni nini hasa unataka kusema.
Anyway, kitenda cha ku come clean ni cha kishujaa ila lazima ukiri mambo ambayo utaweza kufanya na mambo gani huwezi usiwape watu matumaini ambayo hayapo. Kwa mfano kupambana na madawa ya kulevywa HUWEZI. Kabla ya kufika huko lazima utatue kwanza mambo ya msingi. Pili, ungeanza kufikiria kutogombea tena 2010 kwana kazi huwezi na hicho ni kitu ambacho tutakushukuru sana.
 
you aint see nothin yet

Mimi yaani i dont know what to do with BLAIR hapa UK

Unajua kumlinganisha na JK nadhani JK anafadhali mara mia

ukisikia mtu yuko out of touch with people basi nduguyangu huyu Blair tushamchoka na Huyo jamaa yao CHADEMA {cameron} amejaa spin kwa kila kitu

No wonder JJ 'debatable 'MNYIKA haonekani
 
Jamani,

Angalau JK kasema la maana na tumpe tano kwa hilo. Ni fundisho
kwa magazeti ya IPP na wana CCM ambao kazi zao ni kusifia tu
hata pale ambapo mambo yanaenda mrama
 
The whole thing is NONESENSE, kwani aliyekuwa nataka misifa si yeye mwenyewe, sasa anataka kutudanganya kuwa hapendi misifa na sisi tunakubali?

No ni yeye aliyeanzisha kampeni za misifa, mpaka kutajwa tajwa na Twanga pepeta, kuwa mtu wa watu mbona asiseme then kuwa waache kumpa sifa, why now?

Alipokuwa akipewa zile sifa kule mwanzoni alikuwa amfanya kitu gani cha maana, sasa anchokataa ni nini, mimi ningetegemea angekubali publicly kuwa ametuangusha wabongo maana hana sifa za kuwa rais ana angeomba radhi badala ya kutumia ujanja wa kukaripia watu wanaomsifia, wakati ule Mkapa anamsifia kwenye kampeni alikuwa anasifia nini?

Wakati mtandao wanaiponda serikali ya Mkapa mwanzoni na kujifanya wao ni wajuaji walikuwa wakijisifia kitu gani? Wabongo hebu taumke na tuache kukubali huu usaniii, guys litsen hawa mtandao ahwana lolote ni usaniii tu na hii ya Muungwana kujifanya hataki misifa ndio hasa usaniii wenyewe!

Huwezi kuwandanganya wananchi kwa muda mrefu, sasa ukweli umejitokeza wazi for everybody to see kwamba Awamu ya nne ni wasaniiii watupu, mawaziri 60, hawana jibu la kitu kidogo kama umeme, maneno mengiiiiiiii oooh mimi nimeeenda Wall streeet, rais wa kwanza blah blah blah blah, ooh yea sasa hutaki tena misifa, acheni usaniii mmeshindwa kubalini yaishe!

Alichopaswa kusema kwenye huo mkutano ni kuwaomba radhi wabongo na taifa zima, kwa kuishusha hadhi ya urais, na kutokuwa na uwezo wa uongozi mzito kama huo, nigeeelewa, lakini sio kukataa misifa maana ni tabia aliyoianzisha yeye mwenyewe alipokuwa akiwalipa wapiga muziki wa Twanga wamtaje taje bila sababu!

Mimi ninampenda sana JK kwa sababu zangu mwenyewe ninakumbuka zamani ukiwa na rafiki anaitwa Juma au Shabani KWA UPANDE WA PILI rafiki John au Manka basi inaonekana nikitu cha ajabu sana sijui kwanini, mnisaisidie unajua hawa ndugu zetu walisha onekana hawawezi,

Shule nyingi nzuri zilikuwa za seminari hapo pia mnisaidie,.......

mnisamee kwa fikira zangu za kizamani,au uko niliko toka kijijini,mimi ninapenda watu wa imani zote baada ya kuja mjini na kutembea nchi tofauti, sasa ujio wa muh. huyu kwenye ngazi kubwa namna hii kweli hata mimi unanipa wasiwasi hii nchi ni kubwa kuliko yeye alivyo kuwa

anafikiri,kikwete angelikuwa waziri wa kawaida mimi sina neno naye, kama anajifunza urais basi atuambie tumpe muda, saa nyingine jinsi wanavyo chukulia mambo jamani sisi ni wakada lakini tunaona kama kuchoka choka hivi,
mimi kinacho niuma kila mtu sasa anasema anamjua JKna EL na wao ndiyo

wanaopanga na kuendesha taifa hili, wafanyabiahsara walioisaidia CCM kuingia madarakani sasa wana tia aibu ata mwaka haujaisha. kwakweli rais wetu amefungua mlango wa kila mtu kugombea urais''break record'' kama vile mtoto masikini TIGGER HOOD alivyo vunja record ya kucheza GOLF duniani siyo

mchezo wa matajiri tu. jingine kama ameona sifa za kijinga zina miminika natumaini sasa yuko form two ya urais chama chetu kimezungukwa na watu wengi no elimu sasa tuna tengemea nini kama siyo kumwagia rais sifa ili waendelee kula, wadau wa CCM wakiwa bar wanasema sisi ndiyo tuna ipigania nchi yetu, akuna rais kama JK,

atukatai akuna rais kama JK kama mkono unafika kinywani je walalahoi sauti zao nani atazisikia.
mimi jama sijui hii nchi ni yanani kwa sababu Mkapa alishauza yote hiyo sehemu ndogo iliyo bakia basi afazali hii nchi iuzwe lika mtu apewe chake aondoke mimi nikoteari kwenda Sudan kutafuta maisha

Ikosiku kweli tutaongozwa na BINADAMU na siyo WATU Tanzania?
 
Muungwana JK, tulijua toka wakati wa uchaguzi kuwa yeye na kundi lake la mtandao kisiasa wana tatizo kubwa, maana zile kampeni hazikuwa za kawaida kwa nji yetu masikini. Hela za kampeni zilikuwa nyingi mno, kuharibu majina ya wanasiasa wengine kwa makusudi ili tu wapate power,

Wakaenda mpaka kuiharibu katiba na mwenendo wa uchaguzi wa CCM, wakatishia mpaka kwamba nji haitatawalika iwapo hawatapata, wakawaharibu watu babu kubwa kama kina Salim, maneno mengi, tulijua kuwa ni upepo tu na nguvu ya soda, tuliposema mapema tukatukanwa matusi mazito kule BCS, tulipojaribu kuwasihi wabongo waamuke usingizini, maana they were about to commit the worst political mistake ever, wakatujia juuu, sasa here we are!

One year tayari wananchi wamechoka, tena choka mbaya maana wamepigika ile mbaya na hawana hamu, leo eti Muungwana hataki misiifa, ebo! hataki misifa kwa vipi? Yaani anatuona sisi wabongo wajinga? au? Hebu atuambie zile misifa aliyokuwa akipewa hata kabla ya uchaguzi na kina Kingunge, Tido Mhando mzee wa polls za BBC, watu wa Mlimani, zilikuwa ni sifa za nini? Aliwahi kufanya nini cha maana kabla ya kuwa rais? Hebu kuweni wakweli what didi the man do?

Muungwana toka siku ya kwanza ulipoanza hizi kampeni za urais you were wrong, sina tatizo na Muungwana personally, lakini kiuongozi I do, kwa sababu you just don't have it, kule mwanzoni nilisema kwamba kile tu kitendo cha kuwapa watu 60 uwaziri, mpaka Ikulu viti havikutosha kwenye mkutano wa cabinet, ilikuwa tayari dalili za ku-go home.Mimi ninasema katika awamu nzima ya nne tuliyonayo, ninamuona kiongozi mmoja tu angalau mwenye nafuu naye ni Mama Migiro, wengine wote wanaweza kufunga virago waondoke na taifa letu litakuwa just fine! Yes we will be just fine, I mean what are these people doing? Kuna mliosema tumpe muda, sasa tuambieni tufanye nini sasa?

Eti leo hataki misifa tena? Mzee JK na kundi lako tafuteni njia za kujiondoa kwenye madaraka, kwa sababu hakuna njia nyingine ya kuwaondoeni, na hatuwezi kusema eti mnaweza kuwa rehabilitated kwa sababu mtu anyekuwa rehabed, ni yule ambaye kabla ya kuwa na tatizo alikuwa sawa, sasa nyinyi hamjawahi kuwa sawa, ndio maana hiyo option haipo, nyinyi ni kuondoka au mkiendelea acheni ngebe ngebe,

nyamazeni kuleni mapesa ya kodi zetu wajinga, hakuna hope maana Chadema nayo ndio hivyo tena taifa zima tutaishia kulazimishwa kula kisusio for breakfast na kusikiliza miziki ya Jimmy Reeves na Dolly Parton!

mzee ES

Uko sawa ninakubaliana na wewe 100% kama Tido Mhando mzee wa polls za BBC, watu wa Mlimani, REDET, JE wale wa www.uchaguzitanzania.com mbona hatuwasikii au ndiyo imetoka jamani kumbukumbu tunazo pia magazeti radio,TV Walivyo kuwa yana toa front page JK anaongoza katika kura za maoni.
kwenye mtandao
 
Mzee ES: Ulimsifu sana JK mwanzoni. Ulikuwa na safu yako inaitwa kitu kama: Kikwete Huyoo! Na alipomsimamisha Mahalu, ulilitoa hilo kama mfano wa uchapaji kazi hodari! Naona alikukatisha tamaa baadaye, lakini kwa uzito wako, ilibidi uweze kuona ukweli tangu mwanzoni.

Maji ukishayavulia nguo, sharti uyaoge. JK ndiye Rais wetu sasa, na cha muhimu sana ni kuangalia taifa lisizorote mno kutokana na ukweli huo. Ili kunusuru uchumi wa taifa letu, napenda kushauri yafuatayo yafanyike:

  1. Kuwe na badiliko katika Baraza la Mawaziri, na nafasi hiyo itumike kuwapunguza wabaki si zaidi ya 20.
  2. Arudishwe Dr. Kigoda kwenye ofisi ya Rais kama waziri atakayesimamia uchumi.
  3. Ateuliwe kiongozi wa hali ya juu kushika wadhifa wa Gavana wa BoT, na azingatie kuhakikisha shilingi haishuki thamani yake kiholela.
  4. Upelekwe mswada wa fedha (mini budget) bungeni ambao utaongeza kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya Elimu kwa asilimia 100. Fedha hizo zitoke kwenye karibu shilingi trillion moja zilizoachwa Hazina katika bajeti inayotumika sasa.
  5. Upelekwe mswada bungeni utakaolazimisha mikataba kati ya nchi na wawekezaji kujadiliwa na kupitishwa na bunge kabla haijaweza kuwa sheria.
  6. Miktaba ya madini iliyopo sasa ipitiwe kwa dhati, na tusikubali ruzuku. Kwa mfano, Barrick Gold wanamiliki aslilimia 75 tu ya hisa za mgodi wao wa dhahabu uliopo Papua New Guinea. Zilizobaki ni mali ya Papua New Guinea. Kwa nini watwae asilimia 97 hapa kwetu?
  7. Upitishwe mswada wa kukataza matumizi ya fedha zaidi ya shilingi. Malipo yote mahotelini, vyuoni na kwingineko yafanyike kwa fedha zetu. Iendelee kuwa halali kuwa na fedha nyingine, lakini malipo yote hapa nchini yafanyike kwa shilingi ya Tanzania.
Augustine Moshi
 
Ushauri mwingine kwa JK,

Chukua washauri wa bure iwe openly au kwa siri kutoka Jambo Forum, kwani kuna VICHWA MAKINI SANA HAPA eg Mkandara, Fikiraduni, Mwl Moshi, MM Mwanakijiji, Aljazeera, Mwl Kichuguu, Mlalahoi, Kulikoni, JJ Mnyika, Kyoma (ingawa alipotea) na wengine ambao ni kama hao (Ofcourse DON'T INCLUDE people like Nungwi and Mswahili!!!!). hata ukiangalia post zao hapa utakubaliana nami
 
Mzee Moshi,

Heshima yako mzee, mimi sio closed mind kiasi kwamba wewe yaani Jk was so bad kwamba asingeweza kufanya kitu chochote na wala hakukuwa na a room ya kumpa bafasi angalau kidogo, hapana, I was willing kumpa nafasi angalau kiddogo maana ni bin-adamu, mwenye mapungufu kama mimi,

Issue ya Mahalu, kwangu ilikuwa ndio the turning point ya utawala wake, na ninakumbuka nililia sana na wanaouhusika kwamba waanze kujenga mikakati yao mipya from there on, kwa kuisimamia kesi hiyo mpaka mwisho na kumpeleka mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake, ninakumbuka jinsi viongozi wengi jasho lilivyoanza kuwavuja baada ya ile issue, lakini sielewi kilichotokea tena ila baadaye nilisikia kwamba Mahalu amejitayarisha kupambana nao mahakamni yaani viongozi wezniwe wengi waliokuwa involved na wizi wake na mpaka leo sijui kesi imeishia wapi?

Tatizo la kwanza bongo ni viongozi wabovu, sasa JK alipoanza na Mahalu, nilijua kuwa sasa anaeleke kwenye the right direction, bongo hakuna theory yoyote positive ya reforms ambayo haianzi na kusafisha viongozi wabovu, hata ufanye nini ni kazi bureee, kwanza anza na kusafisha viongozi wabovu maana ndio hasa chanzo cha matatizo ya IPTL na Richmond, ni viongozi wabovu!

Mzee Moshi, katika maisha uungwana ni kuwapa watu nafasi kabla ya kuwahukumu, hata kama unajua toka mwanzoni kuwa hawafai lakini ni lazima wapewe nafasi kwanza, sisi wote ni bin-adamu tuna mapungufu! JK bado ni muungwana kulinganisha na wote waliopita!
 
Mzee ES: Ulimsifu sana JK mwanzoni. Ulikuwa na safu yako inaitwa kitu kama: Kikwete Huyoo! Na alipomsimamisha Mahalu, ulilitoa hilo kama mfano wa uchapaji kazi hodari! Naona alikukatisha tamaa baadaye, lakini kwa uzito wako, ilibidi uweze kuona ukweli tangu mwanzoni.

Maji ukishayavulia nguo, sharti uyaoge. JK ndiye Rais wetu sasa, na cha muhimu sana ni kuangalia taifa lisizorote mno kutokana na ukweli huo. Ili kunusuru uchumi wa taifa letu, napenda kushauri yafuatayo yafanyike:

  1. Kuwe na badiliko katika Baraza la Mawaziri, na nafasi hiyo itumike kuwapunguza wabaki si zaidi ya 20.
  2. Arudishwe Dr. Kigoda kwenye ofisi ya Rais kama waziri atakayesimamia uchumi.
  3. Ateuliwe kiongozi wa hali ya juu kushika wadhifa wa Gavana wa BoT, na azingatie kuhakikisha shilingi haishuki thamani yake kiholela.
  4. Upelekwe mswada wa fedha (mini budget) bungeni ambao utaongeza kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya Elimu kwa asilimia 100. Fedha hizo zitoke kwenye karibu shilingi trillion moja zilizoachwa Hazina katika bajeti inayotumika sasa.
  5. Upelekwe mswada bungeni utakaolazimisha mikataba kati ya nchi na wawekezaji kujadiliwa na kupitishwa na bunge kabla haijaweza kuwa sheria.
  6. Miktaba ya madini iliyopo sasa ipitiwe kwa dhati, na tusikubali ruzuku. Kwa mfano, Barrick Gold wanamiliki aslilimia 75 tu ya hisa za mgodi wao wa dhahabu uliopo Papua New Guinea. Zilizobaki ni mali ya Papua New Guinea. Kwa nini watwae asilimia 97 hapa kwetu?
  7. Upitishwe mswada wa kukataza matumizi ya fedha zaidi ya shilingi. Malipo yote mahotelini, vyuoni na kwingineko yafanyike kwa fedha zetu. Iendelee kuwa halali kuwa na fedha nyingine, lakini malipo yote hapa nchini yafanyike kwa shilingi ya Tanzania.
Augustine Moshi

ushauri mzuri but some of your ideas doesnt reflect the real world

Papua New Guinea technically has been sod o Australia and Indonesia

and I am more scare with your last one can you expand it a little bit in terms of economics

You forgot to mention that we need to have a supreme court
 
Mzee Mtanzania,

Hakuna cha Hi 5, kwenye hili ni yeye JK ndiye aliyekuwa akiwalipa waandishi wa magazeti wamsifie, ni yeye ndiye aliwalipa kina Tido Mhando BBC wamsifie, ni yeye aliyewalipa waaandhi wa IPP na magazeti yote bongo wamsifie, ni yeye aliyetembezwa na Mkapa kwenye kampeni akimsifia, je walikuwa wakkimsifia kitu gani ambacho leo eti hataki?

Wewe umesikia wapi katika demokrasia ya kweli, watu wanaambiwa wachukue fomu za uongozi, halafu kabla ya uchaguzi rais aliyeko madarakani anasema atafanya suprise ya kumpitisha asiyetegemewa kati ya waliochukua fomu, meaning kwamba alishaamua ni advance nani atakuwa rais, sasa why waste our time and money za walipa kodi kufanya uchaguzi? Yeye mwenyewe Mkapa ndiye aliyeanza na misifa kibao, alikuwa akimsifia kitu gani? Mbona wakati ule asikatae misifa isiyokuwa na mpango why now?

Hivi unajua bongo leo tuna marais watatu, JK, Lowassa, na Mama Kikwete, ndio wote ni marais sasa, mimi hata wakumlaumu sielewi ni yupi kati ya watatu, kazi ni kusafiri tu, eti ni nji gani duniani ilifanikiwa kimaendeleo kutokana na rais wao kusafiri constatly, bila ya kupumzika? Halafu hizi safari mbona tunasikia kuwa yeye ndiye huwa anaziomba zitayarishwe? na hata kuwaomba mabalozi wetu wawaombe wenyeji? Sasa hivi ataenda London, akirudi tena atakaa kdiogog na kurudi tena nchi moja ya jirani siiitaji hapo hapao karibu na London, sasa hii ni nini?

Mzee Muungwana, hebu wewee na timu yako kaeni chini mfanye kazi hapa hapa bongo hizo safari waachie wasaaidizi kama ni muhimu, unajua hivi majuzi nilpata nafasi ya kuongea na balozi wa China hapa bongo, sasa anasema sisi wabongo ni watu wa ajabu maana nji zote za Afrika zinaenda China kuomba misaaada ya maendeleo ya bara bara, reli na bandari zao, lakini sisi tunaenda huko kuomba vichwa vya treni ya Tazara na maji ya kumwagilia Chalinze, yaani hata watu wa nje nao wanatucheka mzee JK, aibuuuu mwanangu!

tena nasikia tayari unaaanza mbinu za kampeni ya 2010, ndio maana kina Tido na wengine wanarudi kuianza mapema, mbona kazi mwanangu!
 
Faith yangu kwa JK ilianza kupungua alipofanya reshuffle bubu na kumwacha Msabaha anapeta.Ilimalizika kabisa pale alipoitetea Richmond na kuelezea upuuzi mwingine kuwa Cabinet yake iko makini na itaweza kuleta the so-called "maisha bora kwa kila Mtanzania"

Kuna makala hii nimeona kwenye Tanzania Daima ambayo nadhani imemweleza JK vizuri zaidi hasa baada ya kumaliza mwaka akiwa madarakani huku kukiwa hakuna lolote la maana alilofanya zaidi ya kutoa ahadi mpya kila kukicha.

Juvenalis Ngowi

SALAMU kwako ewe mpendwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Kabla ya kutoa yale niliyokusudia kuyawasilisha kwako ewe kiongozi mkuu kabisa unayekalia ofisi kubwa zaidi katika nchi yetu, nianze kwa kutimiza ile jadi yangu ya kumuomba Manani heri na baraka, kumshukuru kwa yote aliyotujalia kwa wiki nzima, lakini pia kwa namna ya pekee kumshukuru huyo aliye juu ya wote kwa kutuwezesha kuona mwaka mmoja wa uongozi wako. Ashukuriwe Yeye.

Waama baada ya dua hiyo fupi nirudi kwako wewe ndugu rais. Wengi wamesema na kuandika hisia zao wakijaribu kupima mafanikio yako katika kipindi cha mwaka mmoja ulichomaliza ukiwa katika ofisi hiyo kuu. Tathmini za wengi hazitofautiani sana.

Mimi nataka tutete katika waraka huu badala ya kufanya tathmini ambazo wakati mwingine hazina vionjo vya takwimu sahihi.

Kama ujuzi wangu wa hisabati bado ni mzuri, basi ni hakika kwamba umemaliza tayari asilimia ishirini ya muda tuliokuajiri ufanye kazi hii yenye heshima kubwa kabisa.

Ndiyo, zimebaki asilimia tano tu uwe umemaliza robo ya muda wa kukaa ofisini katika ngwe ya kwanza ya utawala wako. Mwaka mmoja kati ya miaka mitano umemalizika.

Katika kipindi hiki umekumbana na mengi magumu. Yapo uliyoyaita majaribu au mitihani ya Mwenyezi Mungu. Pengine mitihani hii kwa namna moja au nyingine yamesababisha iwe vigumu kutimiza walau asilimia ishirini ya ahadi ulizotoa wakati wa mchuano wa kupanga jengo hilo jeupe la Magogoni; Ikulu. Inategemea maoni ya mtu, lakini wapo wanaodhani kwamba ahadi zinapaswa zitekelezwe kwa uwiano wa muda uliokaa ofisini.

Mpendwa rais, ni siku nyingi kiasi zimepita tangu walipokunukuu ukisema wala rushwa wanafahamika na ukaagiza wajirekebishe vinginevyo hatua zitafuata.

Ndugu rais katika muda huu uliokaa ofisini, wala rushwa uliowapa muda wa kujisafisha wamefanya hivyo? Kama bado sasa huna haja tena ya kuwa na subira na watu hao. Wapo wengi wanaoendelea kufanya vitendo ambavyo kwa namna yoyote ile tafsiri yake ni rushwa. Hii ndiyo kero kubwa kabisa kwa raia walio wengi hapa kwetu. Pengine badala ya kutumia rushwa tutumie neno ufisadi. Umekaa ofisini kwa asilimia ishirini ya muda wako wa miaka mitano ya awali, je, vita dhidi ya ufisadi imepata mafanikio kwa asilimia ngapi? Wasaidizi wako wakupe taarifa za kweli tena kweli tupu ili tujue tulipo.

Basi bila shaka katika kipindi hiki cha mwaka mmoja yapo mengi yamesemwa au chini chini au kwa kupaza sauti.

Bila shaka haya ni sehemu ya changamoto kwa utawala wako. Unakumbuka hawa walioanza kuzusha kwamba vyeo vimetolewa katika misingi ya udini? Kuibuka kwa hoja hii ambayo watu kadhaa waliiandikia makala ndefu kila mmoja akiwa na upande wake na vielelezo vyake kuna maanisha kwamba bado una kazi kubwa mbele yako ya kujenga jamii ya Watanzania wasiokuwa na ubaguzi wa kidini.

Hoja kubwa katika mjadala huu ni hivi; Watanzania sasa tumeanza kuulizana nani ameshika nafasi ipi na dini yake ni ipi? Ndugu rais kuna kazi kubwa ya kusonga mbele.

Nakumbuka sijawahi kukupa pongezi kwa kuchaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa chama chetu kigumu na kinachodumu.

Hongera sana. Hili nimelikumbuka kutokana na hili ninalotaka kukunong’oneza sasa. Eti watu wanasema bado kivuli cha wanamtandao kipo na kwa hakika kina nguvu kubwa. Hao wanaotunong’oneza kwamba wanamtandao wapo, wana hofu ya kwamba hao wanamtandao wanajisifu kwa kuwa na ushawishi mkubwa.

Kwamba kama jitihada hazitafanyika chama chetu ambacho ni kigumu na kinadumu kinaweza kuwa na vyama viwili ndani ya kimoja. Ni matumaini yetu kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja uliokaa madarakani kama rais ulikuwa na nafasi kubwa ya kuutokomeza kabisa huo “uanamtandao” ambao wengine hatuujui hasa ni kitu gani.

Labda utakuwa ukinishangaa kuunganisha mwaka mmoja wa wewe kuwa katika madaraka ya serikali na hapa naingilia chama. Ndiyo, ni lazima vyote viwili ni lazima viwe safi. Chama ndio injini ya kuendeshea serikali. Ndicho kinatoa dira. Serikali iliyopo madarakani inatekeleza na kutumikia ilani ya chama. Ubora wa chama ni muhimu kama ndoto ya maisha bora kwa kila Mtanzania inategemewa kuwa kweli.
Inafurahisha kwamba umekemea suala la kutumia fedha kupata uongozi ndani ya chama.

Ukilisimamia hili vyema, Tanzania yenye neema inawezekana. Nimepokea dokezo kwamba mwakani mtafanya uchaguzi wa chama. Wakumbushe watu wako kwamba kuvaa rangi za kijani na njano si lazima kuwa na mapenzi na chama tawala.

Wapo wengi wanavaa hivyo kwa manufaa binafsi. Wengine ni mashabiki wa soka tu ambao wala hawana hili wala lile, si makamaradi wenzetu. Mbaya zaidi wapo wanaojidai makamaradi kumbe wapo pale kwa ajili ya kinga au kwa minajili ya kuchuma. Bila kupata watu wenye ufurukutwa na nchi hii hata tukipigania Tanzania yenye neema kwa miaka mia moja bado itakuwa ndoto.

Mpendwa rais, katika mwaka huu wa kwanza wa utawala wako tumeshtushwa kidogo na sera yetu ya elimu ya juu. Nimeamua kuiita sera kwa kuwa sioni neno jingine jema zaidi.

Hii ni sera ya kukopesha wanafunzzi wa elimu ya juu. Tumeambiwa wavulana watakaobahatika kukopeshwa kodi za wazazi wao ili kugharamia masomo yao ni wale wenye daraja la kwanza pekee kwa wavulana. Pia tumeambiwa wasichana watakuwa wale wenye daraja la kwanza na la pili tu. Jambo la kusikitisha kabisa mpendwa rais.

Hatuna haja ya kusimulia kwamba tuna uhaba wa wataalamu. Kwa mfano nimesoma kwamba tuna madaktari 100,000 tu wa meno nchini. Bado tuna upungufu mkubwa wa walimu, madaktari wa kawaida, madaktari bingwa, mahakimu, polisi taja na kada nyingine yoyote.

Bado licha ya yote hayo tunathubutu kuweka uzio katika njia ya elimu? Mbona hicho ndicho kingekuwa kipaumbele cha kwanza?

Mheshimiwa rais tutawezaje kwenda kwa kasi na nguvu bila akili na utaalamu? Utaalamu utapatikana wapi ikiwa kuingia chuo kikuu sasa ni ndoto kwa watoto wengi wa wakulima na wafanyakazi waliokupigia kura? Mpendwa rais tunaomba serikali yako ifikirie upya hili la elimu. Bila elimu tena elimu bora, maisha yenye neema kwa kila Mtanzania ni ndoto.

Nafahamu yapo mengi mema yaliyotokea katika kipindi hiki cha utawala wako.

Tunakupongeza kwa hayo. Lakini tunataka uyatazame yale ambayo bado yanatutatiza sisi wana wako ili katika tathmini ya miaka miwili ya utawala wako tuwe tumeona walau robo ya neema inayotarajiwa katika Tanzania yenye neema.
Tunakutakia heri na baraka katika siku za utawala wako na hata baada ya kustaafu. Mwenyezi Mungu akupe ujasiri wa kutekeleza kwa vitendo kauli na ahadi zako ambazo zaweza kuwa shubiri kwa wengine pindi utakapozitekeleza, lakini hiyo ndiyo njia ya kufikia Tanzania yenye neema. Nikutakie heri na baraka ya Krismasi hapo kesho. Ndimi raia wako mwaminifu.
 
Mzee ES
Naungana na wewe kwa 100%. Yeye ndiye aliyekuwa mastermind wa hizo fake publicity stunts. Why should we give him hi5? Amesema aliyosema na sisi tumesikia na hao waliokuwa wanafanya inabidi waache. Is Tido Mhando another publicity stunt?
You can fool some of the people all of the time, and all of the people some of the time, but you can not fool all of the people all of the time.
Abraham Lincoln - 16th president of US (1809 - 1865)
 
Back
Top Bottom