Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

dua hiyo picha si mchezo nashangaa kwa nini kina fred maro hawakutuonyesha watanganyika namna sorveignity yetu inavyonyenyekea ,kwa maana rais wetu anabeba utaifa wetu,si busara kumuinamia mkuu mwenzake wa nchi[mfalme akihito] namana ile ...noma.
heko kwa balozi maajar kampa malkia heshima ya kawaida ,angekua jk pale angepiga magoti kabisa,
 
Mi naona JK aliamua kusalimia kwa Kijapani (Ohayo Gozaimasu!) hivyo akainama kama Wajep wenyewe wafanyavyo wanaposalimiana. Lakini si kama alisujudu. Maajar hakuwa na haja ya kupiga magoti (goti) kwani Waingereza hawana mila hiyo! As pure and simple as that.
 
dua ,mwanagenzi ana point hapo ..sasa kama kuna mtu ana picha za akihito alkisalimiana na bush au putin au museveni [jirani yetu]ets atuwekee hapa ,ili tuwe fare ili isijekuwa tunasujudu kwa ajili ya umasikini wetu
 
Mwanagenzi,

Hata kama ni jadi ya Wajapan huwezi kumsalimu mtu kwa ishara zisizofanana. Wajapan wakikutana vigogo wote huinama na sio mmoja wao unless wewe ni mtawaliwa!...
Sasa hapa tunaona hizi heshima za Utumwa zinaendelezwa kwani kama kuinama hata huyu msalimiwa alitakiwa kuinama.
Tukirudi kwa Queen mbona umechukua Utamaduni wetu kuutolea mfano badala ya Utamaduni wa Waingereza kama ulivyofanya kwa Japan?
 
Support Kikwete’s anti-graft war, says Butiku
2006-12-22 09:12:23
By Judica Tarimo

The Director, Mwalimu Nyerere Foundation, Joseph Butiku addresses the press yesterday in Dar es Salaam. He called on members of the public to support President Jakaya Kikwete�s anti-corruption crusade. (Photo:Moshy Kiyungi)

The Executive Director of Mwalimu Nyerere Foundation, Joseph Butiku, has said that the government’s commitment and openness in fighting corruption deserved public praise.

He described President Kikwete as a role model, calling on the public to give him full support in his endeavour to fight the vice.

Butiku, who was speaking at a press conference in Dar es Salaam, said Kikwete is determined to fight the vice.

Speaking to members of the ruling party in Dodoma this week, President Kikwete lashed out at the party members who buy votes saying they would not be accepted.

”To the surprise of most of us, the President openly told CCM leaders and members that the party will not accept corrupt leaders buy leadership posts.

These are strong words from a man who is determined to fight the vice,” Butiku said.

Kikwete was disappointed by rampant corruption within CCM circles and appealed to the party leaders and members to respect code of ethics.

”There are allegations that some of us (CCM leaders) are buying posts�I am saying this from the bottom of my heart�I am angry with these acts,” said Butiku, quoting Kikwete’s speech.

Butiku described the President’s openness as one step towards success in the fight against corruption, deeply-routed in public and private sectors.

He also lauded the government’s initiatives to fight money laundering, drug abuse and other social problems currently on the rise.

Local media once quoted President Kikwete as saying he had names of corrupt officials and drug dealers, but no
tangible efforts have been made to pin down the culprits.


Anti-corruption crusaders have constantly been accusing the government for inaction and lack of seriousness against corrupt elements reported in public institutions.

”There could be some problems with implementation, but as I said before� the government openness and willingness is so important in the whole battle,” said Butiku.



Bahati mbaya au nzuri huyu jamaa yetu ambaye sisi waswahili tunasema alikuwa jikoni kwa muda mrefu ambaye ameanza kupiga debe ati JK ataiweza hii biashara ya kutokomeza rushwa.

Je ni miaka mingapi alikaa serikalini na matokeo yake ni yapi? Butiku huna utajiri wewe wa kutupwa kutokana na kukaa serikalini kwa muda mrefu kwa njia za rushwa?

Sio wewe ambaye unataka watu wakuabudu? Kwa nini hunyamazi na kula pension yako bila kuwabughudhi wanachi ambao uliwasaliti kwa muda mrefu?
 
Wengine nao hawa hapa...

KKKT yaridhishwa na kasi ya Rais Kikwete


2006-12-27
Na Salome Kitomary, PST, Moshi


Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), imesema inaridhishwa na utendaji kazi wa Rais Jakaya Kikwete katika kipindi cha mwaka mmoja alichokaa madarakani, kutokana na jinsi anavyowajali wanyonge na wenye shida mbali mbali.

Hayo yalisemwa juzi na Askofu Martin Shao wa Dayosisi hiyo katika Usharika wa Moshi Mjini.

Alisema hayo wakati akihubiri katika ibada ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo miaka 2000 iliyopita.

Alisema kwa kipindi cha mwaka mmoja ambacho Rais Kikwete amekuwa madarakani, hajakaa Ikulu bali amekuwa akitoka na kwenda katika masoko, magerezani na sehemu mbalimbali, ambako angeweza kuwafikia wananchi wanyonge kiurahisi.

”Kitendo hicho kimeonyesha kuwa anawajali wananchi wake, hasa wa kiwango cha chini, ambao walikuwa hawana mtu wa kusikia kilio chao, lakini yeye alitoka na kwenda kuzungumza nao ana kwa ana na kujua shida zao,” alisema.

Alisema Rais Kikwete ni wa kwanza kufanya hivyo, kwani amejishusha na kuchanganyika na wananchi wa kima cha chini na wenye matatizo mbalimbali, hivyo kusikiliza shida zao ili kuzipatia ufumbuzi kuliko kusubiri kuambiwa na watendaji wake.

”Kwa kipindi kifupi alichokaa madarakani, tumeona akiwatembelea watu kwenye migodi, magerezani, wafanyabiashara ndogo ndogo na hata wauza mchicha na machungwa kule sokoni�ni mfano wa kuigwa kwani ameona badala ya kukaa Ikulu tu na kusubiri taarifa, ni vema akawafikia wananchi moja kwa moja,” alisema Askofu Shao.

Alisema kanisa hilo linampongeza kwa moyo huo na kumtaka aendelee nao ili kutatua matatizo ya wananchi, kiuchumi na kijamii .

Askofu Shao alisema viongozi wengine waliopo wa serikali ya Awamu ya Nne, hapana budi waige mfano huo na kutoka maofisini na kujishusha hadi kuwafikia wananchi na kusikiliza shida zao na kuzipatia ufumbuzi.

”Utaratibu wa Rais kuwatembelea wananchi hasa wanyonge ambao kilio chao kilikuwa hakisikiki, kwani hata wakimwandikia barua hadi imfikie ni muda mrefu na wakati mwingine inaweza isimfikie, ni cha kishujaa sana.

Tumeona matatizo ya wananchi yakitatuliwa kwa haraka sana.

Sisi tunamuomba Mungu amtie nguvu zaidi katika kutatua matatizo ya wanyonge,” alisisitiza.

Aidha, aliwataka waumini wa Kanisa hilo kushikamana katika kuhakikisha amani iliyopo nchini inaendelea kuwepo, kuliko kujiingiza katika uchochezi, ambao husababisha vita.

Alisema dayosisi hiyo inatarajia kutoa sadaka maalum ya kuwasaidia watu wenye shida mbalimbali kama yatima, wajane, walemavu na wasiojiweza wanaohudumiwa katika vituo mbalimbali vya dayosisi hiyo.

SOURCE: Nipashe
 
Dua la kuku halimpati mwewe.
Tupe/tuambie mali/hela alizonazo Butiku.

Tunasubiri.
 
Hao KKT nao ndio wajinga kabisa!!

Hata yeye mwenyewe ashakataa kuabudiwa na kusifiwa, ila watu ndo kwanzaaaa wanaanza!

Tz...
FD
 
Hawa KKKT walipeana cha kuongea nadhani maana Askofu wa Zanzibar alikemea serikali juu ya mkataba wa Richmond, Askofu wa Moshi anamsifu JK na Askofu Malasusa naye anangata na kupuliza kwa kukemea viongozi kujitajirisha.

Pengine huu ndio mwanzo wa mabadiliko na wana dini nao kuaza kuzungumzia hali halisi ya kisiasa moja kwa moja kwa washirika wao.

As far as Butiku; naona ana lake JAMBO ila kwa sasa sina uhakika ni lipi limemfanya kuitisha Press Conference na kuzungumzia hilo. Time will tell...
 
Mzee Mkandara,

Kutokana na tafsiri mbalimbali za picha hiyo ya JK, nadhani JK na timu yake watazidi kumaizi umuhimu wa kuimarisha kitengo chao cha habari/mawasiliano. Wakumbuke kuwa picha za viongozi wakuu wa kitaifa (Rais, VP, PM) zinapaswa kuhaririwa au kuhakikiwa kabla hazijatolewa kwa umma zisije zikaleta utata kama huu ambao umejitokeza hapa.

Niongeze yafuatayo:

1. Kwa ujumla, Watanzania tunafahamika kwa ukarimu na upole, na ni kweli pia kuwa tu wepesi kuiga na kuthamini vya watu na hata mila za wengine, pengine kuliko za kwetu.

2. JK ni mtu wa mzaha mwingi (msanii could have been appropriate but unfortunately of late it has taken a negative connotation!) na huenda alitaka kumwonyesha mwenyeji wake kuwa anafahamu jinsi wanavyosalimiana.

3. Inawezekana wote waliinama, lakini JK kwa kutofahamu vizuri mila hiyo aka-overdo na hasa kwa kuwa yeye ni mrefu zaidi ya Abe, kiasi kwamba wakati picha inachukuliwa mwenzake alishainuka, hivyo yeye ikaonekana kama aliinama sana wakati mwenzake hakuinama!
 
So far .......

"Upitishwe mswada wa kukataza matumizi ya fedha zaidi ya shilingi. Malipo yote mahotelini, vyuoni na kwingineko yafanyike kwa fedha zetu. Iendelee kuwa halali kuwa na fedha nyingine, lakini malipo yote hapa nchini yafanyike kwa shilingi ya Tanzania.
Augustine Moshi."

Now, this is what I call constructive idea. Well done Mwalimu Moshi. Ninaelewa faida ya hii.

FD
 
tTumeshuhudia katika kampeni cha CCM, wakitumia Ari mpya kasi mpya na nguvu mpya.
Watanzania inatakiwa tuamke na tufanye mabadiliko,
Rais Mkapa alitumia sera ya ukweli na uwazi na alikuwa Rais mchapakazi mwenye ahadi za kweli, akisema kitu kipo ni kweli kipo akisema hakipo ni kweli hakipo, Ndivyo alivokuwa, HATUTAPATA RAIS MKWELI KAMA YEYE,
Tumuangalie JK
Sifa hiyo hana,,,
Ari mpya...watanzania tukaanza na janga la njaa,
Kasi mya... Watanzania tunapata matatizo ya Umeme na mahakama za kadhi kuingizwa kwenye ilani ya chama cha mapinduzi, katiba inasema chama chocote cha siasa kitakachojihusisha na maswala ya dini chama hicho kitafutwa, tunashangaa kuiona ccm bado ipo wakati kimevunja katiba ya nchi kwa kuingiza swala la mahakama ya kadhi kwenye katiba....

Hiyo in Ari na Kasi....... TUNASUBURI NGUVU MPYA TUONE ITAKAVYOKUWA,,,,,,WATANZANIA ZINDUKENI.

g2muslims@yahoo.com
 
Butiku hana hela yeyote!
Ni mtu ambaye ana roho mbaya sana,hata ndugu zake wenyewe wanamtenga.

Alikula sana pesa za MNF enzi za Mwalimu.Kuna kipindi MNF ilikuwa na excess of 3 million dollars kwenye accounts zake.Mandela alivyo take over peace talks baada ya Mwl kufariki za Burundi,alilijua hili na alikuwa anatafuta pesa kutoka na specific operations,na alikuwa anataka kupewa gharama halisi za mikutano...sio kama ilivyo kuwa wakati wa Mwalimu ambaye alikuwa anatafuta pesa kijumla,huku Butiku akizila.

Mmoja wa trustees wake pale alikuwa ni Kate Kamba.Huyu mama alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Butiku.Tender zote zinahusiana na MNF,be it kuprint t shirts,kukarabati majengo,alikuwa anapewa mtoto wa Kamba.

Kuna mtoto wa Mwalimu ambaye alisomea mambo ya finance aliomba kazi ya kuwa Finance Director pale,Butiku akakataa,na sababu aliyotoa ni kuwa wafadhili wakiona wanafamilia wa Mwalimu wanafanya kazi MNF,watasita kutoa pesa kwani eti itapoteza maana yake,wakati yeye mwenyewe kajisahau kuwa ni mwanafamilia!

Humo MNF wote wamemchoka ile mbaya,ilikuwa astaafu toka mwaka jana,lakini akifikiria kwenda kuishi kijijini anaona ngumu.

Ninavyoona mimi,hili debe analompigia JK ni kujitafutia ubalozi tu.Maana hawa pamoja na Adam Marwa ndio kati ya waliomweka BM kwenye urais,na baadae wakatibuana,ndio kisa cha kupiga kelele sana kwenye utawala uliopita kuwa wizi ulikuwa umekithiri.Hili debe la sasa ni kujitafutia ulaji tu,hakuna zaidi.

Na kwa kifupi ni kwamba amekula pesa nyingi sana za MNF,akaanzisha miradi kijijini kwao Butiama,huko nako jamaa wakawa wanamlia tu pesa zake....mara kajenga shule,kanunua malori,huku anashamba kubwa na kujenga nyumba nyingine ya kuishi huko,sasa hivi ukienda huko ni kichekesho.
 
JK kumsalimia mtawala wa Japan alivyofanya sio kutudhalilisha.

Nakumbuka Clinton siku moja aliandika jinsi alivyoshauriwa namna ya kumsalimia mfalme wa Japan,na akauliza kama inabidi ainamishe kichwa tu au ajipinde kutoka kwenye kiuno,na alichoambiwa ni kujipinda kiunoni(kitu ambacho kwake kilikuwa ni rahisi sana..LOL!).

Wajapani ni watu wenye heshima ya hali ya juu,na kujali mila zao nji kitu muhimu sana.Hivyo mimi nadhani JK alitimiza tu vile alivyoshauriwa.
 
Actually Butiku was and is against Mkapa. Butiku thought SAS would be President, just to find a bid betrayal from Mkapa. Anataka Kikwete afiche madhambi yake. Mkapa aliwaambia nyie ni wakora wa mali za MNF (wakakasirika)
 
Huyu anajikosha. Ameshakuwa nje ya system kwa muda mrefu, sasa anatafuta namna ya kurudi. Alimkandia sana JK wakati wa kura za maoni in support for SAS. Sasa hii MNF ina hali mbaya kifedha, inabidi aipigie magoti serikali. Yaani huyu, ni yale yale aliyosema Mzee ES-njaaaaaa kali sana tu!
 
Augustino Moshi-great ideas; but I am afraid if they can get a space in JK's agenda becasue as correctly argued by renowned Professor Issa Shivji 'it is not part of CCM political culture to listen to voices other than its own'. Unless you are part of them.
 
Jamani mimi nampa credit yule askofu wa zanzibar kwa sababu amesema kama ilivyo bila kuongeza chumvi . Kwa mtazamo wangu nadhani viongozi wa dini wana nafasi kubwa sana katika kutokomeza maovu katika nchi yetu kama wakitumia nafasi hiyo vizuri.

Butiku nadhani hakuna sababu yoyote ya kumdiscuss hapa kwa sababu hata foundation ya Nyerere inakufa wakati yeye akiongoza. Sijui kwa nini wana familia awamfukuzi huyu mtu kwani hafai .
 
Kumafananisha JK na Idi Amin i think is hitting below the belt! Duh!
JK tumemchagua wenyewe kwa 80%,nchi yenye vyama vingi,hio utaisikia wapi kwingine?JK amekuwa accused of so many things(rightly so kwa mitazamo tofauti) maana ndio bosi wetu,lakini jamani Idi Amin was a dictator,darasa la nne,alipindua nchi yake,akafukuza raia wake(wahindi)...he was a buffoon,murderer,cannibal,daft,na vingine vyingi tu,sioni hapa JK anaingiaje.
Mimi ninachoona unaweza kumfananisha na JK labda kwa sababu wote ni wanajeshi na wote ni watu wa watoto,ambapo kwa hapo basi wako wengi tu,wakina Rawlings,Kabila,Blaise Compaore etc.Yes JK ana mapungufu yake,but i think sometimes we are being a bit too harsh on him.
 
Back
Top Bottom