Damn! I am lost,
yaani Butiku anatokea wapi tena? Butiku na foundation yake walikuwa wakipewa shillingi millioni 300, na Mkapa kila baada ya miezi sita, hela za walipa kodi! Butiku akaanza njama za ktaka kumpitisha Salim kwa kum-blackmail na kumu-intimidate Mkapa, akaenda mikoani kuanzisha ziara ya kuwasikiliza wananchi, akafanya vikao vya public na kuwaita wananchi waanze kuitukana serikali, akaita na waandishi kibao, alipooona Mkapa hashituki,
Yeye na Salim, wakaamua kwa makusudi kufanyia sherehe za kumuadhimisha Mwalimu, kwa kumuomba M7 awafanyie kwenye bunge la Uganda, wakaenda wakafanyia kule, ndipo kwa mara ya kwanza JM akamfuata, Mkapa na kumpa darasa kuhusu Butiku na mipango yake, Mkapa akakata msaada wa miillioni 300 ukawa hakuna tena?
Waliporudi Uganda wakaanza kampeni za chini chini za urais wa Salim, wakamuita Mzee Ndejembi na kumpa gari ya aina double cabin ili aanza kuzunguka mikoani kumfanyia kampeni, but, at the same token huyu mzee naye alikuwa njiani kugombea tena uenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dodoma, ambako JM tayari alikuwa ameshamtayarisha mtu wake, Masima.
Mkapa akasikia kuhusu Ndejembi na kupewa gari na Butiku/Salim, akamtuma mwenyekiti wa CCM Tabora, aende Dodoma na kumpa ujumbe Ndejembi, kwamba "........aache mara moja hizo kampeni zake, maana Mwarabu hatakuja kuiongoza Tanzania........", Mtandao wakaona opportunity, Rostam akampa Mzee Ndajembi, shillingi millioni 10 kwa ajili ya kampeni zake Dodoma za uenyekiti wa CCM, kwa sababu Rostam alijua kuwa JM hana hela za kutosha kumpa mgombea wake, Ndejembi akamshinda mgombea wa JM lakini kwa taabu sana. Huyu mzee akaendelea kumfanyia kampeni Salim anyway, ndipo Rostam akaanza kumtumia wajumbe kwamba arudishe hela zake yeye alikuwa amemkopesha tu, au aache kampeni za Salim. Huyu Mzee akabidi aache kampeni maana hakuwa na hela za kurudisha.
Warioba naye akajiunga na hizi kampeni za Butiku for Salim, ndipo Mkapa akaamua kuwapiga marufuku Ikulu wote wawili, na hata kuonana nao tena mpaka leo hajawahi. Kufika Dodoma Jm akatolewa kwanza mapema na Mkapa, kwa hiyo Warioba na Butiku wakaenda kwa Jm, na kumuomba awasaidie ili wajumbe wake wahamie kwa Salim, Jm akawatukana sana kwamba nyinyi si ndio mlikuwa mnamfurahia Mwalimu alipokuwa akinipiga vita, akakataa kuwasaidia, pamoja na kwamba aliwadanganya atawasaidia, kwa sababu Muuungwana alishawawahi usiku akaonana na Jm na wakaelewana.
Matokeo Muungwana akashinda, Butiku akaondoka na hasira isyokuwa na kifani akamuandikia barua Mkapa na kuwapa copy wajumbe wote wa kamati kuuu, na wenyekiti wa CCM wa mikoa yote, ya kumtukana Mkapa kwa kumpitisha Muungwana, na akataja mpaka kiasi cha hela alizopewa na Muungwana, yaani dola millioni moja na kwamba CCM is dead sivyo kama Mwalimua alivyomuachia, akajaribu kuwa mjanja kwa kumalaumu kutompitisha Jm, badala ya mgombea wake Salim, Warioba kuona mambo yameharibika, naye akawa mjanja, akatukana tukana alip[oona no body is paying attention akajingiza kwenye kampeni ya mtandao dakika za mwisho, MFN ikaachwa ndio mwisho wake kabisaaaa. Sasa since then maisha yamekuwa magumu sana kwa Mzee Butiku, na foundation kwa ujumla.
Sasa with all that said, ninasema kwamba hiii njaa ya bongo itatufikisha mahali tutaanza kulana wenyewe kwa wenyewe, kama mbwa mwitu, no question kwamba huyu Mzee sasa anakuwa motivated na njaaa kali, tena sana, maana hela hana, kama kuna alizochukua kwenye zile enzi zilishaisha maana jamaa ni mjinga sana kwa kinamama, ninajua kuwa ana njaa maana sasa ni karibu mwaka mmoja na nusu hajatoka nje ya nchi kama ilivyokuwa zamani. Barua aliyomuandikia Mkapa ya kumtukana it was a good thing, lakini viongozi wengi nilipowauliza maoni yao, walisema barua should never had came from him, maana hana record nzuri au sio msafi, na mfano mzuri ni jinsi alivyoshirikiana na Nyakyoma, kula Gapex yote mpaka chini.
Butiku, anahitaji kurudi kijijini na kukubali kwamba maisha ya mjini hayawezi, maana sasa anaanza kuwa kichekesho, leo Tanzania hakuna mtu yoyote aliye-serious na rushwa maana inawajumuisha karbu viongozi wote wa nji, na Butiku anapaswa kuwa mtu wa mwisho duniani kuzungumzia rushwa, sheria zilikuwepo siku zote za kuzuia rushwa kuna mpaka tume ya kuzuia rushwa, je haikuwa na sheria? Kwa nini viongozi wa bongo wanapenda kuwachezea wananchi kila wakati na PR za kitoto? Butiku anaongelea nini? Alipokuwa Ikulu kilichomshinda kukomesha rushwa ni nini? Eti rais ameonyesha kusikitishwa na rushwa wakati wa uchaguzi, uchaguzi upi huo? Kwani yeye aliiingiaje kwenye power? Sasa Butiku amesahau zile dola millioni moja? Na mahela yote aliyokuwa akipewa Mzee anayemiliki Ngurudoto kunakofanyia mikutano yote ya serikali, kutengeneza fulana na kofia zilitoka wapi? Hela za kuwapa kina Darwesh na magari mawili mapya kuzunguka bongo nzima kumpaka Salim zilitoka wapi? Mzee Butiku, huu mji una wenyewe ndugu yangu, basi imetosha rudi kijijini maisha ya kuruka kwenye ndege yalishaisha, madaraka ulikuwa nayo for 28 years, sasa leo ni kitu gani tena ambacho hukukifanya then, aibuuu mtu mzima, wewe ni kurudi tu kijijini na kukubali yaishe na ninajua kuwa mtandao sio wajinga hawatakupa kitu, maana wao wenyewe bado wanatafutana vyeo havitoshi.
Jamani huyu mzee ni njaaa tu inamsumbua! Nyie kina Zanaki hebu mwambieni huyu mzee kuwa Mang'ana Gasalikilire, amnga'ang'anie Mama Kamba ili amlishe na ajifunze kuacha kupora wake za watu, ila cheo hamna tena!