Huyu ndiye fisadi hatari zaidi

Huyu ndiye fisadi hatari zaidi

Rais angekuwa dhaifu angemtoa muhongo lakini kwa hili kikwete kaonyesha yeye sio dhaifu anasimamia ukwelii hawezi kumfukuza mtu kazi kwa sababu ya media manipulation
.
.
Tunasubiri bunge likae na tunachotaka kuona kwa wabunge ni kuwakilishwa kwa hoja ya kumfukua waziri mkuu.
Pinda ni sharti atolewe katika wadhifa wake kwa kosa la udhaifu wa rais wake.
Kwa makosa ya JK kudharau maazimio ya bunge kipindi kilichobaki kwa vikao vya bunge mwaka huu litakuwa ni unrest.
.
 
Nimeshakwambia raisi angekuwa dhaifu angekuwa nafanya kazi kwa kufuata majunguu sasa nakuhakikishia aliowatuma lazima aumbukee
 
Pinda hawezi kutolewa ukiona katolewa raisi ndo kataka kutolewaa ,hivi huwa mnafikiria kwa kitumia ninii nyinyi maboya ,raisi ni mwingine kabisaaa hapana chezeaa
 
Hivi nyinyi mngekuwa na ubavuu mngezui katibaa pendekezwa isipitishwe bungeni kama imepitaa gani nyinyi ni walaini sanaaa
 
FISADI ANAYETUMIA KISINGIZIO CHA KUTETEA WANYONGE KUZIFANYA CHUKI ZAKE BINAFSI ZIWE NI UGOMVI WA KITAIFA:
Kwa miaka mingi kumukuwepo na jitihada za makusudi kabisa zinazofanywa na vyombo vya habari vya IPP kuchafua baadhi ya wizara za serikali, watu binafsi na ofisi za taasisi mbalimbali kwa malengo yao binafsi wanayoyajua wao wenyewe. Ni wazi kabisa hakuna asiyejua chuki binafsi alizonazo mmiliki wa vyombo vya habari na baadhi ya waliokuwa viongozi wandamizi wa serikali na baadhi ya mawaziri ambao bado wanaendelea kuhudumu katika serikali. Mmiliki huyu amekuwa akitumia kivuli cha utetezi wa wanyonge kuanzisha vurugu dhidi vya viongozi wa serikali kwa kuaminisha uma kwamba anatetea maslahi ya watanzania. Jambo ambalo hata siku moja halijawahi kuwa na ukweli hata kidogo kwani siku zote amekuwa akitanguliza mbele maslahi yake binafsi kwa kigezo cha uzawa, kisha ya serikali na baadaye wananchi wa mwisho. Sote tunafahamu ufisadi aliokwisha wahi kuufanya kwa kivuli cha uzawa kupitia NBC, NICO, Commodity Import Support (CIS), TANPACK Industries Ltd na mengine mengi.
Kama ambavyo iliwahi kutamkwa huko nyuma, historia ya Mengi inamuonyesha kwamba ni mtu anayependa kuanzisha ugomvi katika mambo yanayohusu maslahi yake binafsi lakini unapopamba moto na kuona anazidiwa, hutafuta hifadhi kwa kulia lia na kutaka aonewe huruma na kutaka kuliingiza Taifa zima. Katika kufanikisha hayo, amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwapotosha wananchi ili waone anaonewa au eti anapigania maslahi yao. Historia inaonyesha amewahi kuanzisha ugomvi na watu wafuatao kwa sababu anazozijua yeye.
a) Alianzisha ugomvi na wamiliki wa vituo vya televisheni vya DTV na CTN mwaka 1994 kwa hofu tu ya kwamba watakuwa washindani wa kituo chake cha ITV na akafika hatua ya kuwazushia kwamba wanataka kumuua, akaufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

b) Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora, Mheshimiwa Wilson Masilingi, baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Katika kudhihirisha jinsi alivyo mtu wa chuki na visasi, kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata hashiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo.

c) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mheshimiwa Shamim Khan, kwa kutakiwa afute maelezo katika maji ya kunywa yanayozalishwa na kampuni yake kwamba yalikuwa ya chemchem wakati hayakuwa hivyo, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

d) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Edward Lowassa, aliyemkanya Mengi asitumie nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira kuwakomoa washindani wake wa biashara kwa kuwazushia tuhuma za kuchafua mazingira na kuvifungia viwanda vyao, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

e) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, baada ya kumnasa akikwepa kodi katika uendeshaji wa biashara yake ya bahati nasibu ya BINGO, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

f) Akaanzisha ugomvi na kampuni ya Habari Corporation iliyokuwa inaongozwa na Jenerali Ulimwengu baada ya kufichua habari za jinsi alivyoifilisi benki ya NBC, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

g) Akaanzisha ugomvi na mfanyabishara Yusuf Manji ambaye kwanza walikuwa wakigombea uendeshaji wa mchezo wa bahati nasibu, na baadaye akajenga chuki naye binafsi kwa sababu tu alifanikiwa kuusuluhisha mgogoro wa Yanga ambao Mengi ulimshinda, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

h) Akaanzisha ugomvi na Mheshimiwa Adam Malima ambaye alihoji Bungeni jinsi Mengi anavyotumia vibaya vyombo vyake vya habari kwa kutangaza habari za kujitukuza binafsi zaidi ya hata vinavyotangaza habari zinazowahusu viongozi wa kitaifa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

i) Akaanzisha ugomvi na mfanyabiashara Tanil Somaiya baada ya kumuona kijana huyo aliyekuwa wakala wa kuuza bidhaa za viwanda vyake Mengi (kabla ya kuviua mwenyewe), ameweza kujiimarisha na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara hata kumshinda yeye Mengi, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

j) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Lawrence Masha, kwa kuja na madai ya kutaka kuhujumiwa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

k) Akaanzisha ugomvi na Ndugu Rostam Azizi, baada ya kuona kwamba amekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, na aka ufanya ni ugomvi wa wa nchi nzima.

l) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Mbarawa Makame baada ya serikali kupitisha azimio la kubadili mfumo wa matangazo kutoka analojia kwenda digitali ambapo alikuwa akishinikiza watanzania wakatae kwa lengo la yeye mwenyewe kujinufaisha binafsi.

m) Ni huyu huyu Reginald Mengi amekuwa akipiga vita ya chini kwa chini kuhakikisha Tanzania haipati katiba bora kwa malengo yake binafsi na huu ni mpango mkakati anao uratibu kwa kushirikiana na UKAWA na baadhi ya balozi za kutoka nchi ya wahisani.

n) Na siku za karibuni kaanzisha ugomvi mkali na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo baada ya kuona harakati zake za kutaka kupewa vitalu vya gesi bure kwa kigezo cha uzawa kugonga mwamba.
Watanzania tuna haja na kila sababu ya kujiuliza mara mbili mbili juu ya uhalali wa mtu huyu kuamua kutumia kigezo cha utetezi wa wanyonge (uzawa) kwa minajili ya kujinufaisha yeye binafsi na familia yake. Kamwe hatuwezi kukubali hili na tunatoa wito sasa ni wakati ambao serikali ina bidi ichekue hatua kali dhidi ya mmiliki huyu ambaye amekuwa akichochea vurugu na kuivuruga serikali pasipo sababu.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

We ni Tanzania kweli?
 
Swali la kuzushii Mzee mengi ametengeneza ajira zaidi ya elfu 10..anasaidia walemavu na watanzania wengine wengii wanaishii..wanasoma wanafurahia maisha kwa sababu ya mengi..huyu professor dalali. Amefanya kipi cha maana?
 
Ajira nchi hii zimetengenezwa na watu wengi sana sio mengi peke yakee kwa taarifa yako karibu robo tatu ya watangazaji wa tv za mengi wamehamia azamtv hivi inaonyesha huyu jamaa anawalipa wafanyakazi wake mishahara mbuzi ndo mana wanahama
 
Angekuwa ni tajiri wa kutu inspire angekuwa anaonyesha everything is possible sio unataka utajirike kwa kutaka favour na kutumia agenda ya uzawa ,compete hawaigi wenzake kama wakina dangote wao wanasema ikifika mwaka 2017 jamaa anataka dongote group iwe inaworth us 100 billion
 
Home plus acha kukurupa uliza ufahamishwe hoja yako mufilisi eti mengi hawalipi vizuri wafanyakazi wake thus way wanahamia azam!!nakujibu kama ifuatavyo..kila company ya mengi ina management yake na utaratibu wake..anaeamua kulipa mishahara sh ngapi si Mzee mengi..Bali ni management ya company husika..watu wana utashi wao wa kuhamia company watakayo ndiyo maana.walipokuja IPP hawakuwatangazia nyie kuwa wanajiunga na IPP....walikuja hawajui kitu..wenyine fresh from school wamefundishwa kazi...wamekuwa maarufu hadi we we mwehu umewajua...na wanaruhusiwa kwenda watakapo...it means ndani ya IPP...demokrasia imejaa.ikutoshe tu kuwa hakuna media house inayolipa vizuri Tanzania kama ippmedia..huu ndiyo ukweli..najua utabisha...kwa sababu kawaida yako kubisha...hata mama yako alipokuthibishia kuwa Mimi "Mzee wakusoma"ndiyo baba yako mzazi ulibisha.Niko hapa kumtetea mwenyekiti wangu hadi tone la mwisho...leta hoja ujibiwe.
 
Mengi anafanya biashara na Watanzania na ameajiri watz.
Wewe Muhongo ni dalali wa nani ?
 
Tunafunga mjadala..bibie alienzisha mada ya kumkashifu mzee mengi..anayejiita "kiboko ya mengi"ameomba poo.amekiri alitumwa kumchafua Mzee mengi.Na amesema ameukubali ukweli kuwa Mzee mengi ni muadilifu...msafi..mwenye huruma...mtetezi wa wanyonge..kimbilio na Tegemeo la sisi wanyonge.tunamuomba mwenyezi mungu ampe Mzee mengi maisha marefuu...afya tele...na ulinzi wa malaika wake.akiibuka mwingine sie Tupi.tutamtetea hadi damu ya mwisho.
 
Swali la kuzushii Mzee mengi ametengeneza ajira zaidi ya elfu 10..anasaidia walemavu na watanzania wengine wengii wanaishii..wanasoma wanafurahia maisha kwa sababu ya mengi..huyu professor dalali. Amefanya kipi cha maana?

Amesomesha watu zaidi ya hao Elfu 10 na hao alosomesha ndio wengine wanasomesha sasa jiulize kupitia yeye ni wangapi wamenufaika? Usimshabikie mpenda bikini wewe boya. Hakuna kampuni isiofanya hayo unafkir Mengi ameajir watu wengi kumshinda Bakhresa? Au anasaidia zaidi ya kumshinda Bakhresa? Bakhresa hata kujisifu ama kujionesha ushawahi kuona hio kitu?
 
Si ni heri Mzee Mengi kafanya unavyosema kafanya lakini kawekeza hapa nchini na kuajiri watanzania wengi kitu ambacho serikali yao imeshindwa kutengeneza ajira. Je analingana na hao wanaoiba na kuweka fedha mabenki ya nje na kunufaisha nchi hizo???
Tumieni akili kidogo mnapokuwa mna- critic. watu kama Mzee Mengi.

#Mbowe ana account nje na amenunua nyumba Dubai kwa pesa ambazo hakuna muamala wa benk yoyote hapa bongo. Ni uhuni na wizi mwingine huu wakuhujumu Taifa & kuwafaidisha diaspora.

Chakushangaza sasa, Mengi anawatumia wapinzani kama huyo bwana kuwasakama wale wanaojitahidi kiuyendaji kama Muhongo. Kina Kafulila e.t.c wanavuta imprest daily kumkazia Muhongo na wengine.

To be honest,Mengi mtu mbaya sana (hata kama na hawa wengine ni wabaya). Mengi cku za usoni ndiye atakayekuwa anafanya deal la siraha na #PANYAROAD kuliunguza Taifa. Maana kwake hakunaga zaid ya #Mpunga (ngawira!!)
 
Thread imeandikwa na Muhongo. Ni ya kipuuzi na uzandiki. Mod, weka kapuni hii.
 
Hana lolote huyo mzee. Ana roho mbaya kupindukia. Kama kweli ni mtu mwema kwa nini kila wakati anagombana na viongozi wa serikali? Ameshawafanyia watu wengi ukatili wa kutisha hadi wengine wamepoteza maisha. Si huyu ndiye aliyetajwa na Mtikila hata kwenye mauaji ya Chacha Wangwe? Siku ile alienda Dodoma kufanya nini? Huyu mtu ni wa kumulikwa.
R.I.P chacha wangwe: Mengi ndiye alifhadhili muvi lote likiwemo kuhakikisha Ukweli hauwekwi Wazi.
 
#Mbowe ana account nje na amenunua nyumba Dubai kwa pesa ambazo hakuna muamala wa benk yoyote hapa bongo. Ni uhuni na wizi mwingine huu wakuhujumu Taifa & kuwafaidisha diaspora.

Chakushangaza sasa, Mengi anawatumia wapinzani kama huyo bwana kuwasakama wale wanaojitahidi kiuyendaji kama Muhongo. Kina Kafulila e.t.c wanavuta imprest daily kumkazia Muhongo na wengine.

To be honest,Mengi mtu mbaya sana (hata kama na hawa wengine ni wabaya). Mengi cku za usoni ndiye atakayekuwa anafanya deal la siraha na #PANYAROAD kuliunguza Taifa. Maana kwake hakunaga zaid ya #Mpunga (ngawira!!)

R.I.P chacha wangwe. Mzimu wake umechauka sasa wale walioshiriki Unyama ulee mwaka 2015 wataumbuka sana, hata Mengi sasa kapoteza Mashabiki wengi kutokana na kiufadhili Unyama huo, huko nyuma Kauli za Mengi zilikuwa na Nguvu na hakukuwa na wa kumpinga Mengi wala kumkosoa hadhalani kama sasa.
 
Thread imeandikwa na Muhongo. Ni ya kipuuzi na uzandiki. Mod, weka kapuni hii.

Nadhani ww ni lazima utakuwa Rais wa JF Duniani kote kutokana na Amri yako. Tunakuomba Mh Rais wa JF uyakubali maoni ya watu iwe ni sehemu ya kujifunza na kutambua mapungufu, maovu na Ufisadi ambao akina Mengi wanadhani wamejificha hawaonekani, Mh Rais wa JF tunaomba kutumia Fursa hii kukuomba umwambie Regnal Mengi atulie aviheshimu na kuviacha vyombo vya Uchunguzi vifanye kazi yake pasipo kuingiliwa na Mengi wala wanasiasa ambao ni Watumishi wa Mengi nyuma ya Pazia.
 
FISADI ANAYETUMIA KISINGIZIO CHA KUTETEA WANYONGE KUZIFANYA CHUKI ZAKE BINAFSI ZIWE NI UGOMVI WA KITAIFA:

Kwa miaka mingi kumukuwepo na jitihada za makusudi kabisa zinazofanywa na vyombo vya habari vya IPP kuchafua baadhi ya wizara za serikali, watu binafsi na ofisi za taasisi mbalimbali kwa malengo yao binafsi wanayoyajua wao wenyewe.

Ni wazi kabisa hakuna asiyejua chuki binafsi alizonazo mmiliki wa vyombo vya habari na baadhi ya waliokuwa viongozi wandamizi wa serikali na baadhi ya mawaziri ambao bado wanaendelea kuhudumu katika serikali.

Mmiliki huyu amekuwa akitumia kivuli cha utetezi wa wanyonge kuanzisha vurugu dhidi vya viongozi wa serikali kwa kuaminisha uma kwamba anatetea maslahi ya watanzania.

Jambo ambalo hata siku moja halijawahi kuwa na ukweli hata kidogo kwani siku zote amekuwa akitanguliza mbele maslahi yake binafsi kwa kigezo cha uzawa, kisha ya serikali na baadaye wananchi wa mwisho.

Sote tunafahamu ufisadi aliokwisha wahi kuufanya kwa kivuli cha uzawa kupitia NBC, NICO, Commodity Import Support (CIS), TANPACK Industries Ltd na mengine mengi.

Kama ambavyo iliwahi kutamkwa huko nyuma, historia ya Mengi inamuonyesha kwamba ni mtu anayependa kuanzisha ugomvi katika mambo yanayohusu maslahi yake binafsi lakini unapopamba moto na kuona anazidiwa, hutafuta hifadhi kwa kulia lia na kutaka aonewe huruma na kutaka kuliingiza Taifa zima.

Katika kufanikisha hayo, amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwapotosha wananchi ili waone anaonewa au eti anapigania maslahi yao. Historia inaonyesha amewahi kuanzisha ugomvi na watu wafuatao kwa sababu anazozijua yeye.

a) Alianzisha ugomvi na wamiliki wa vituo vya televisheni vya DTV na CTN mwaka 1994 kwa hofu tu ya kwamba watakuwa washindani wa kituo chake cha ITV na akafika hatua ya kuwazushia kwamba wanataka kumuua, akaufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

b) Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora, Mheshimiwa Wilson Masilingi, baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Katika kudhihirisha jinsi alivyo mtu wa chuki na visasi, kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata hashiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo.

c) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mheshimiwa Shamim Khan, kwa kutakiwa afute maelezo katika maji ya kunywa yanayozalishwa na kampuni yake kwamba yalikuwa ya chemchem wakati hayakuwa hivyo, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

d) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Edward Lowassa, aliyemkanya Mengi asitumie nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira kuwakomoa washindani wake wa biashara kwa kuwazushia tuhuma za kuchafua mazingira na kuvifungia viwanda vyao, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

e) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, baada ya kumnasa akikwepa kodi katika uendeshaji wa biashara yake ya bahati nasibu ya BINGO, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

f) Akaanzisha ugomvi na kampuni ya Habari Corporation iliyokuwa inaongozwa na Jenerali Ulimwengu baada ya kufichua habari za jinsi alivyoifilisi benki ya NBC, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

g) Akaanzisha ugomvi na mfanyabishara Yusuf Manji ambaye kwanza walikuwa wakigombea uendeshaji wa mchezo wa bahati nasibu, na baadaye akajenga chuki naye binafsi kwa sababu tu alifanikiwa kuusuluhisha mgogoro wa Yanga ambao Mengi ulimshinda, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

h) Akaanzisha ugomvi na Mheshimiwa Adam Malima ambaye alihoji Bungeni jinsi Mengi anavyotumia vibaya vyombo vyake vya habari kwa kutangaza habari za kujitukuza binafsi zaidi ya hata vinavyotangaza habari zinazowahusu viongozi wa kitaifa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

i) Akaanzisha ugomvi na mfanyabiashara Tanil Somaiya baada ya kumuona kijana huyo aliyekuwa wakala wa kuuza bidhaa za viwanda vyake Mengi (kabla ya kuviua mwenyewe), ameweza kujiimarisha na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara hata kumshinda yeye Mengi, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

j) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Lawrence Masha, kwa kuja na madai ya kutaka kuhujumiwa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

k) Akaanzisha ugomvi na Ndugu Rostam Azizi, baada ya kuona kwamba amekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, na aka ufanya ni ugomvi wa wa nchi nzima.

l) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Mbarawa Makame baada ya serikali kupitisha azimio la kubadili mfumo wa matangazo kutoka analojia kwenda digitali ambapo alikuwa akishinikiza watanzania wakatae kwa lengo la yeye mwenyewe kujinufaisha binafsi.

m) Ni huyu huyu Reginald Mengi amekuwa akipiga vita ya chini kwa chini kuhakikisha Tanzania haipati katiba bora kwa malengo yake binafsi na huu ni mpango mkakati anao uratibu kwa kushirikiana na UKAWA na baadhi ya balozi za kutoka nchi ya wahisani.

n) Na siku za karibuni kaanzisha ugomvi mkali na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo baada ya kuona harakati zake za kutaka kupewa vitalu vya gesi bure kwa kigezo cha uzawa kugonga mwamba.

Watanzania tuna haja na kila sababu ya kujiuliza mara mbili mbili juu ya uhalali wa mtu huyu kuamua kutumia kigezo cha utetezi wa wanyonge (uzawa) kwa minajili ya kujinufaisha yeye binafsi na familia yake.

Kamwe hatuwezi kukubali hili na tunatoa wito sasa ni wakati ambao serikali ina bidi ichekue hatua kali dhidi ya mmiliki huyu ambaye amekuwa akichochea vurugu na kuivuruga serikali pasipo sababu.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Nonsense!
 
Back
Top Bottom