Huyu ndiye fisadi hatari zaidi

Huyu ndiye fisadi hatari zaidi

Hajawekeza hapa hapa mbona kanunua nyumba nje hata hv karibuni kanunua nyumba south Africa ya ajili ya mke wake mama wa mapacha.

YEs, kuwa na nyumba nje si tatizo, as long as his primary base ya biashara ipo nyumbani

vipi hao waliobeba escrow money kwa silver boxes?? plus hao wanaoweka offshore??

Lets be objective here, mnampinga Mengi kwasbabu anapinga mafisadi wanouza nchi nje?? would you rather sell vitalu kwa wageni madalali kuliko madalali wa nyumbani???

Kumbukeni, hata Nigeria, peace imerudi kwenye mafuta baada ya wazawa kupewa ruhusa ya exploration na umiliki wa shares kwenye makampuni

uzawa ni peace token

endeleeni kulamba kengele za wageni

Your knowledge must be very limited
 
Nadhani utakua hujui ulichokiandika,unatakiwa kujua yafuatayo.

1. Mengi hapingani na mafisadi wanaouza raslimali nje na wala mengi hajawahi kuwa mtetezi wa watanzania,mengi anajitetea mwenyewe apewe vitalu aviuze.

2.umetoa mfano mzuri,Nigeria wazawa wanamiliki hisa,hapa tz wazawa wamekaribishwa kununua hisa tpdc,mengi hilo hataki anataka apewe vitalu vyake mwenyewe,huo ni wehu gani?

3. Gesi inatakiwa kuwafaidisha watanzania wote sasa kama watapewa madalali wazawa ina maana watakaofaidika ni hao madalali wazawa na sio watanzania wote.

Ndio maana serikali imeteua tpdc iwe dalali kwenye gesi na mafuta maana ni shirika la umma,likipata pesa zitawahusu watu wote tofauti na dalali anaejitegemea akipata pesa ni zake mwenyewe.
 
Pinda hawezi kutolewa ukiona katolewa raisi ndo kataka kutolewaa ,hivi huwa mnafikiria kwa kitumia ninii nyinyi maboya ,raisi ni mwingine kabisaaa hapana chezeaa

Mapenzi aliyokupa unataka watanzania wote tufurahi???? Kamwe haitatokea!!
 
Tatizo lenu watanzania wengi huko home.. Tz mnafikiri kwa kutumia kalio..ndiyo maana akili zenu fupi kama kashata za magomeni!kamati ya bunge PAc inamtaja muongo kama dalali mkuu kwenye dili la escrow.. Kumbukeni kamati ilipewa hadidu za rejea..na kamati ili leta taarifa kutoka kwa CAG na TAKUKURU...ambavyo ni vyombo vilivyoundwa na mheshimiwa rais.Sasa nyie mnaokataa ukweli huu mnataka ukweli gani?au ndiyo kwa vile mke shurti amtetee mume hivyo mnajitoa fahamu mkisimama upande wa ke?? Na ni chombo kipi cha serikali kiliwahi Mtangaza mengi fisadi zaidi ya kumjazia mitunzo kibao??(TRA)wanempa juzi.Nasisitiza muongo ni mpigaji tu na Mzee mengi ni mr.clean!!mtabisha ila kimoyomoyo mnakubali.
 
FISADI ANAYETUMIA KISINGIZIO CHA KUTETEA WANYONGE KUZIFANYA CHUKI ZAKE BINAFSI ZIWE NI UGOMVI WA KITAIFA:

Kwa miaka mingi kumukuwepo na jitihada za makusudi kabisa zinazofanywa na vyombo vya habari vya IPP kuchafua baadhi ya wizara za serikali, watu binafsi na ofisi za taasisi mbalimbali kwa malengo yao binafsi wanayoyajua wao wenyewe.

Ni wazi kabisa hakuna asiyejua chuki binafsi alizonazo mmiliki wa vyombo vya habari na baadhi ya waliokuwa viongozi wandamizi wa serikali na baadhi ya mawaziri ambao bado wanaendelea kuhudumu katika serikali.

Mmiliki huyu amekuwa akitumia kivuli cha utetezi wa wanyonge kuanzisha vurugu dhidi vya viongozi wa serikali kwa kuaminisha uma kwamba anatetea maslahi ya watanzania.

Jambo ambalo hata siku moja halijawahi kuwa na ukweli hata kidogo kwani siku zote amekuwa akitanguliza mbele maslahi yake binafsi kwa kigezo cha uzawa, kisha ya serikali na baadaye wananchi wa mwisho.

Sote tunafahamu ufisadi aliokwisha wahi kuufanya kwa kivuli cha uzawa kupitia NBC, NICO, Commodity Import Support (CIS), TANPACK Industries Ltd na mengine mengi.

Kama ambavyo iliwahi kutamkwa huko nyuma, historia ya Mengi inamuonyesha kwamba ni mtu anayependa kuanzisha ugomvi katika mambo yanayohusu maslahi yake binafsi lakini unapopamba moto na kuona anazidiwa, hutafuta hifadhi kwa kulia lia na kutaka aonewe huruma na kutaka kuliingiza Taifa zima.

Katika kufanikisha hayo, amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwapotosha wananchi ili waone anaonewa au eti anapigania maslahi yao. Historia inaonyesha amewahi kuanzisha ugomvi na watu wafuatao kwa sababu anazozijua yeye.

a) Alianzisha ugomvi na wamiliki wa vituo vya televisheni vya DTV na CTN mwaka 1994 kwa hofu tu ya kwamba watakuwa washindani wa kituo chake cha ITV na akafika hatua ya kuwazushia kwamba wanataka kumuua, akaufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

b) Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora, Mheshimiwa Wilson Masilingi, baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Katika kudhihirisha jinsi alivyo mtu wa chuki na visasi, kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata hashiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo.

c) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mheshimiwa Shamim Khan, kwa kutakiwa afute maelezo katika maji ya kunywa yanayozalishwa na kampuni yake kwamba yalikuwa ya chemchem wakati hayakuwa hivyo, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

d) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Edward Lowassa, aliyemkanya Mengi asitumie nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira kuwakomoa washindani wake wa biashara kwa kuwazushia tuhuma za kuchafua mazingira na kuvifungia viwanda vyao, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

e) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, baada ya kumnasa akikwepa kodi katika uendeshaji wa biashara yake ya bahati nasibu ya BINGO, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

f) Akaanzisha ugomvi na kampuni ya Habari Corporation iliyokuwa inaongozwa na Jenerali Ulimwengu baada ya kufichua habari za jinsi alivyoifilisi benki ya NBC, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

g) Akaanzisha ugomvi na mfanyabishara Yusuf Manji ambaye kwanza walikuwa wakigombea uendeshaji wa mchezo wa bahati nasibu, na baadaye akajenga chuki naye binafsi kwa sababu tu alifanikiwa kuusuluhisha mgogoro wa Yanga ambao Mengi ulimshinda, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

h) Akaanzisha ugomvi na Mheshimiwa Adam Malima ambaye alihoji Bungeni jinsi Mengi anavyotumia vibaya vyombo vyake vya habari kwa kutangaza habari za kujitukuza binafsi zaidi ya hata vinavyotangaza habari zinazowahusu viongozi wa kitaifa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

i) Akaanzisha ugomvi na mfanyabiashara Tanil Somaiya baada ya kumuona kijana huyo aliyekuwa wakala wa kuuza bidhaa za viwanda vyake Mengi (kabla ya kuviua mwenyewe), ameweza kujiimarisha na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara hata kumshinda yeye Mengi, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

j) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Lawrence Masha, kwa kuja na madai ya kutaka kuhujumiwa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

k) Akaanzisha ugomvi na Ndugu Rostam Azizi, baada ya kuona kwamba amekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, na aka ufanya ni ugomvi wa wa nchi nzima.

l) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Mbarawa Makame baada ya serikali kupitisha azimio la kubadili mfumo wa matangazo kutoka analojia kwenda digitali ambapo alikuwa akishinikiza watanzania wakatae kwa lengo la yeye mwenyewe kujinufaisha binafsi.

m) Ni huyu huyu Reginald Mengi amekuwa akipiga vita ya chini kwa chini kuhakikisha Tanzania haipati katiba bora kwa malengo yake binafsi na huu ni mpango mkakati anao uratibu kwa kushirikiana na UKAWA na baadhi ya balozi za kutoka nchi ya wahisani.

n) Na siku za karibuni kaanzisha ugomvi mkali na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo baada ya kuona harakati zake za kutaka kupewa vitalu vya gesi bure kwa kigezo cha uzawa kugonga mwamba.

Watanzania tuna haja na kila sababu ya kujiuliza mara mbili mbili juu ya uhalali wa mtu huyu kuamua kutumia kigezo cha utetezi wa wanyonge (uzawa) kwa minajili ya kujinufaisha yeye binafsi na familia yake.

Kamwe hatuwezi kukubali hili na tunatoa wito sasa ni wakati ambao serikali ina bidi ichekue hatua kali dhidi ya mmiliki huyu ambaye amekuwa akichochea vurugu na kuivuruga serikali pasipo sababu.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Kwa mwenendo huu na nada yako hii, hakuna sababu ya kumtaka Mungu aibariki Tanzania!! Haya yanayofanywa na hao uliowataja kuwa wana ugomvi na Mengi ndo unataka Mungu ayabariki?!
Hebu jaribu kuwa na akili mkuu, manake nikiangalia mchango wa Mengi kwa watanzania ni mkubwa sana ukilinganisha na hao mbwa uliowataja kuwa wana ugomvi na Mengi!
Kejeli na Majigambo ya prof Muhongo, unamwomba Mungu azibariki!!!!? Wewe ni mfu usiejitambua kamwe!
 
Nadhani utakua hujui ulichokiandika,unatakiwa kujua yafuatayo.

1. Mengi hapingani na mafisadi wanaouza raslimali nje na wala mengi hajawahi kuwa mtetezi wa watanzania,mengi anajitetea mwenyewe apewe vitalu aviuze.

2.umetoa mfano mzuri,Nigeria wazawa wanamiliki hisa,hapa tz wazawa wamekaribishwa kununua hisa tpdc,mengi hilo hataki anataka apewe vitalu vyake mwenyewe,huo ni wehu gani?

3. Gesi inatakiwa kuwafaidisha watanzania wote sasa kama watapewa madalali wazawa ina maana watakaofaidika ni hao madalali wazawa na sio watanzania wote.

Ndio maana serikali imeteua tpdc iwe dalali kwenye gesi na mafuta maana ni shirika la umma,likipata pesa zitawahusu watu wote tofauti na dalali anaejitegemea akipata pesa ni zake mwenyewe.

na akina Muhongo, na wenzake wanapigania maslahi ya watanzania sio??

Like i sadi before, Mengi ni fisadi na mwizi pia, but sio mnafiki, anapiga kibiashara, wengine ni wanafiki wanatudanganya kwenye majukwaa
 
YEs, kuwa na nyumba nje si tatizo, as long as his primary base ya biashara ipo nyumbani

vipi hao waliobeba escrow money kwa silver boxes?? plus hao wanaoweka offshore??

Lets be objective here, mnampinga Mengi kwasbabu anapinga mafisadi wanouza nchi nje?? would you rather sell vitalu kwa wageni madalali kuliko madalali wa nyumbani???

Kumbukeni, hata Nigeria, peace imerudi kwenye mafuta baada ya wazawa kupewa ruhusa ya exploration na umiliki wa shares kwenye makampuni

uzawa ni peace token

endeleeni kulamba kengele za wageni

Your knowledge must be very limited

Unabishana na hawa kaka!Mbona ni wale wale tu!Marafiki wa MAFISADI na mali za umma ndiyo maana wanachuki zao binafsi kwa Mengi.

Wala usipoteze muda wako,ukiona hoja kama hizo ujue:
1.Ni mtoto wa Waziri au mzazi aliyewahi kuwa waziri na mfaidikaji wa madeal yote.
2.Familia,ndugu au marafiki wa mtoto wa waziri wau aliyekuwa waziri na ni mnufaikaji wa madeal ya kuuza nchi.
3.Marafiki wa Mtoto wa Rais wetu mpendwa ambao kwa namna moja ama nyingine wanafaidika na wizi wa mali za umma ama kwa kutetea ujinga huu wataikwaa ukuu wa wilaya au mkoa.
4.WanaCCM ambao ni walaji na wafaidikaji wakubwa wa wizi wa mali za umma.

Hivyo usishangae sana,ndiyo maisha ya bongo
 
Naweza kuwa ninabishana na mtu aliyerudia LA 7mara nne kama huyo mnae mshabikia...
 
Mtamsema sana Mengi, main reason ni kwamba anajua kujisimamia, sasa anawakera kwa kujisimamia... as a business man he has to stand his ground na ni dalali fisadi etc, but he stands his ground kwa uwazi, tatizo la Muhongo team ni kujifanya wasafi wakati wanataka sana kupiga wawe na net worth ya 600M USD

Mwisho unafika
 
Nimeshakwambia raisi angekuwa dhaifu angekuwa nafanya kazi kwa kufuata majunguu sasa nakuhakikishia aliowatuma lazima aumbukee

Hebu tuambie wewe, Tibaijuka kafukuzwa kwa kosa lipi? Manake kama ni uadilifu, serikali yote ingetakiwa iachie ngazi!! Mkuu usitetee uozo kisa unakunufaisha wewe na familia yako!!
 
Mtoa mada sijui km alijipanga na kujua atakachokiandika au ameshinikizwa kwa ujira
 
Mtoa mada chizi...hoja zake mufilisii tunazipangua moja moja..naona amekimbia kwenda kuogesha watoto wa boss!!tunasisitiza mengi ni muadilifu....msafi..hata na kamwe hatakuwa fisadi.
 
Angekuwa ni tajiri wa kutu inspire angekuwa anaonyesha everything is possible sio unataka utajirike kwa kutaka favour na kutumia agenda ya uzawa ,compete hawaigi wenzake kama wakina dangote wao wanasema ikifika mwaka 2017 jamaa anataka dongote group iwe inaworth us 100 billion

Yaani wewe ni mfu usiyejitambua!! Wewe unapepeta mdomo, eti ikifika 2017 worth usd 100 bn. Safi kabisa, wewe mpango wako huo wakati utakua umepiga umbea kiasi gani....! Nahisi ikifika huo wakati hutaweza kuiona hata keyboard! Laana za Watanzania lazima zitawafikia ninyi mnaonufaika na mfumo!
 
Leta hoja ya kwa nini kikwete hataki kimfukuza fisadi muhongo? Zaid ya hapo ni walewale
 
na akina Muhongo, na wenzake wanapigania maslahi ya watanzania sio??

Like i sadi before, Mengi ni fisadi na mwizi pia, but sio mnafiki, anapiga kibiashara, wengine ni wanafiki wanatudanganya kwenye majukwaa

Ni mahala gani muhongo kawatetea wageni na kuwaacha watanzania?.

Kama ni escrow rais kam clear muhongo,kasema wazi zile zio pesa za umma,kwa hiyo hapo mhongo hahusiki,muulizeni rais.

Mi nashangaa,watu kumtuhumu muhongo kuwatetea wageni,wapi?au kwenye sekta gani?[gesi na mafuta iko wazi hakuna mtanzania anaeweza kuchimba]

sio kwamba natetea wizi au wezi,nataka facts zilizo wazi za kumtuhumu mtu na sio maneno ya kuambiwa.

Kama mhongo kadalalia watu kwa nini facts zisianikwe?imebaki kua ni tuhuma bila ushahidi.

Kusema mengi sio mnafiki unakorea,mengi ni mnafiki mkubwa,akikosa anachokitaka hujifanya ku-team up na wananchi na kujifanya kuwatetea,akipata humsikii akilalamika. Hana wema wowote mkuu.
 
Kwa mwenendo huu na nada yako hii, hakuna sababu ya kumtaka Mungu aibariki Tanzania!! Haya yanayofanywa na hao uliowataja kuwa wana ugomvi na Mengi ndo unataka Mungu ayabariki?!
Hebu jaribu kuwa na akili mkuu, manake nikiangalia mchango wa Mengi kwa watanzania ni mkubwa sana ukilinganisha na hao mbwa uliowataja kuwa wana ugomvi na Mengi!
Kejeli na Majigambo ya prof Muhongo, unamwomba Mungu azibariki!!!!? Wewe ni mfu usiejitambua kamwe!

Hivi unaweza kutuambia mengi ana mchango gani kwa watanzania?
Hivi maendeleo ya mtu binafsi ndio yanahakisi watu 45mln? Duh kwa akili hizi maendeleo hadi karne ya 30.
 
Kaka m...tumia ubongo kufikiri..usitumie kalio.nenda TAKUKURU na kwa CAG kaulize.Halafu ujibu hivyo ni vyombo ya Nani?
 
Tatizo lenu watanzania wengi huko home.. Tz mnafikiri kwa kutumia kalio..ndiyo maana akili zenu fupi kama kashata za magomeni!kamati ya bunge PAc inamtaja muongo kama dalali mkuu kwenye dili la escrow.. Kumbukeni kamati ilipewa hadidu za rejea..na kamati ili leta taarifa kutoka kwa CAG na TAKUKURU...ambavyo ni vyombo vilivyoundwa na mheshimiwa rais.Sasa nyie mnaokataa ukweli huu mnataka ukweli gani?au ndiyo kwa vile mke shurti amtetee mume hivyo mnajitoa fahamu mkisimama upande wa ke?? Na ni chombo kipi cha serikali kiliwahi Mtangaza mengi fisadi zaidi ya kumjazia mitunzo kibao??(TRA)wanempa juzi.Nasisitiza muongo ni mpigaji tu na Mzee mengi ni mr.clean!!mtabisha ila kimoyomoyo mnakubali.
Kwa Mtizamo wako peke yako na wenzake wachache mnamwona Mengi ni Mtu Saafi,Hao TRA na vyombo vya Serikali hawamgusi kwani kawanunua tayari na ana Mtandao wake humo, Watu pekee wa kumsomea Mashitaka Mengi ni Wana JF tu ambao wengi wapo wakini na hawakubali kuburuzwa kirahisi pasipo kujua undani wa kila Jambo.
 
Back
Top Bottom