wajibu wake wa kwanza ni kutetea mali zetu (uma) ambao hakutekeleza na badala yake akawatetea wanaotudhulumu kwa uzembe au makusudi. Pesa zilizokuwa kwenye account ya escrow zilikuwa na sehemu ambayo ni kodi ya wananchi, na hata sehemu ya TANESCO ambayo yeye hakuitetea na zaidi sana alikuwa anatetea upande wa pili. Hili tu linathibitisha yeye kuwa adui wa uma.
Kibaya zaidi ali alishiriki kubariki ulipwaji wa fedha hizo kwa kampuni ambayo inaelezwa kwamba haikuwa na uhalali wa kisheria kulipwa wakati huo.
Mwisho kabisa ana mawazo ya kitumwa na yaliyokosa uzalendo ya kuwasujudia wageni wazi wazi kwa kutamka kuwa watanzania hawawezi kuwekeza katika uchumi wa gesi bali kwenye kusindika juice! Kauli hii haitakiwi kutolewa na kiongozi anayeishi kwa kutegemea kodi za hao anaowadharau.
Ok,alitetea wezi wapi?kama ni hela za escrow kikwete ambae ndie bosi wa watu wote kasema sio za umma,kosa la mhongo ni lipi,kwa nini msimuulize kikwete na mbaki kumuandama muhongo?
Pesa zilihusisha wizara nyingi ikiwemo ya fedha,hakuna hela kubwa kiasi hicho kutoka bila waziri wa fedha kujua,mbona haulizwi?ni muhongo,muhongo,muhongo!
Watanzania tunapenda sifa za kijinga,tunapenda kupewa sifa ambazo hatuna,wewe uwezo wako ni wa kula mihogo na chai unataka uambiwe unakula baga,kahawa ya kapchino,maziwa nk,huo ni ujinga,hatupendi kuambiwa ukweli,ukweli tunauita matusi. Mengi & wazawa wameambiwa hawana hela ya kuchimba gesi,wengine wameelewa,mzawa mengi haelewi,analazimisha.
Kama kuna mtu wa kulaumu kuhusu escrow mlaumuni kikwete,juzi kawaambia watanzania kua hakuna hela za umma pale,kwa nini aandamwe muhongo?muhongo na kikwete nani msemaji wa mwisho?