Huyu ndiye fisadi hatari zaidi

Huyu ndiye fisadi hatari zaidi

Mzee wa miaka 80 eti kaoa BINTI sawa na Mjukuu wake huku akiwa na rekodi na Utitiri wa michepuko na Utata juu ya nani alisaidia kumzalia hao mapacha, Mengi anapaswa atambue kuwa watanzania wa sasa wapo macho hawadanganyiki kirahisi kama zamani alivyokuwa amezoea.
Anafahamu kwamba bado wapo misukule... thanks God, am not one of them!
 
Biashara zote zimemshinda Mengi,imebaki majungu.Hamuoni hata maji ya kilimanjaro sasa yapo ktk cartons za viroba badala ya boxes.Azam ndiye kiboko yake
 
FISADI ANAYETUMIA KISINGIZIO CHA KUTETEA WANYONGE KUZIFANYA CHUKI ZAKE BINAFSI ZIWE NI UGOMVI WA KITAIFA: Watanzania tuna haja na kila sababu ya kujiuliza mara mbili mbili juu ya uhalali wa mtu huyu kuamua kutumia kigezo cha utetezi wa wanyonge (uzawa) kwa minajili ya kujinufaisha yeye binafsi na familia yake. Kamwe hatuwezi kukubali hili na tunatoa wito sasa ni wakati ambao serikali ina bidi ichekue hatua kali dhidi ya mmiliki huyu ambaye amekuwa akichochea vurugu na kuivuruga serikali pasipo sababu.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Inawezekana haya madai ni kweli, ila mbona wote uliowataja wanakabiliwa au kweli walikabiliwa na TUHUMA ZA KIFISADI?!
Hatujaona majina masafi au ambayo hayana dosari hapo, ya akina JAN MAKAMBA, ZITTO, SLAA, MWAKYEMBE, MAGUFULI, MWIGULU NCHEMBA, MNYIKA, WASSIRA, MWANDOSYA, Saada Mkuya Salum n.k. n.k.
Inawezekana hao wote either ni mafisadi wenzake au kawaumbuwa..
 
Mengi ana Madhambi mengi kama lilivyo jina lake, kwanza Wafanyakazi wake Anawaibia sana kwa kuwalipa mishahara Mibovu, Rostam Azizi aliuza hiza zake za Voda kwa dola million 300 akaondoka Nchini pasipo kulipa kodi baada ya kumugawia mengi Mabilioni kwa ajili yakumaliza Ugonvi wao na pia Mengi kamsaida kukwepa kodi.

Unaonyesha unaujua,udhaifu wa Selikari any way hiyo ni kesi ya jinai ambayo inatosha kumfukuzisha kazi hata waziri wa fedha tupe ushahidi tuupeleke bungeni,alafu huyu Rostam si yule wa CCM aliyeleta sera ya kujivua Gamba mmh hapa ipo namna,mtu anajivua gamba alafu halipi kodi.
 
Mengi uwa ananifurahisha sana anavyowakusanya vilema anawapa pombe na pilao huku waandishi wa habari wanachukuwa picha.
 
FISADI ANAYETUMIA KISINGIZIO CHA KUTETEA WANYONGE KUZIFANYA CHUKI ZAKE BINAFSI ZIWE NI UGOMVI WA KITAIFA:
Kwa miaka mingi kumukuwepo na jitihada za makusudi kabisa zinazofanywa na vyombo vya habari vya IPP kuchafua baadhi ya wizara za serikali, watu binafsi na ofisi za taasisi mbalimbali kwa malengo yao binafsi wanayoyajua wao wenyewe. Ni wazi kabisa hakuna asiyejua chuki binafsi alizonazo mmiliki wa vyombo vya habari na baadhi ya waliokuwa viongozi wandamizi wa serikali na baadhi ya mawaziri ambao bado wanaendelea kuhudumu katika serikali. Mmiliki huyu amekuwa akitumia kivuli cha utetezi wa wanyonge kuanzisha vurugu dhidi vya viongozi wa serikali kwa kuaminisha uma kwamba anatetea maslahi ya watanzania. Jambo ambalo hata siku moja halijawahi kuwa na ukweli hata kidogo kwani siku zote amekuwa akitanguliza mbele maslahi yake binafsi kwa kigezo cha uzawa, kisha ya serikali na baadaye wananchi wa mwisho. Sote tunafahamu ufisadi aliokwisha wahi kuufanya kwa kivuli cha uzawa kupitia NBC, NICO, Commodity Import Support (CIS), TANPACK Industries Ltd na mengine mengi.
Kama ambavyo iliwahi kutamkwa huko nyuma, historia ya Mengi inamuonyesha kwamba ni mtu anayependa kuanzisha ugomvi katika mambo yanayohusu maslahi yake binafsi lakini unapopamba moto na kuona anazidiwa, hutafuta hifadhi kwa kulia lia na kutaka aonewe huruma na kutaka kuliingiza Taifa zima. Katika kufanikisha hayo, amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwapotosha wananchi ili waone anaonewa au eti anapigania maslahi yao. Historia inaonyesha amewahi kuanzisha ugomvi na watu wafuatao kwa sababu anazozijua yeye.
a) Alianzisha ugomvi na wamiliki wa vituo vya televisheni vya DTV na CTN mwaka 1994 kwa hofu tu ya kwamba watakuwa washindani wa kituo chake cha ITV na akafika hatua ya kuwazushia kwamba wanataka kumuua, akaufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

b) Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora, Mheshimiwa Wilson Masilingi, baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Katika kudhihirisha jinsi alivyo mtu wa chuki na visasi, kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata hashiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo.

c) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mheshimiwa Shamim Khan, kwa kutakiwa afute maelezo katika maji ya kunywa yanayozalishwa na kampuni yake kwamba yalikuwa ya chemchem wakati hayakuwa hivyo, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

d) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Edward Lowassa, aliyemkanya Mengi asitumie nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira kuwakomoa washindani wake wa biashara kwa kuwazushia tuhuma za kuchafua mazingira na kuvifungia viwanda vyao, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

e) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, baada ya kumnasa akikwepa kodi katika uendeshaji wa biashara yake ya bahati nasibu ya BINGO, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

f) Akaanzisha ugomvi na kampuni ya Habari Corporation iliyokuwa inaongozwa na Jenerali Ulimwengu baada ya kufichua habari za jinsi alivyoifilisi benki ya NBC, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

g) Akaanzisha ugomvi na mfanyabishara Yusuf Manji ambaye kwanza walikuwa wakigombea uendeshaji wa mchezo wa bahati nasibu, na baadaye akajenga chuki naye binafsi kwa sababu tu alifanikiwa kuusuluhisha mgogoro wa Yanga ambao Mengi ulimshinda, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

h) Akaanzisha ugomvi na Mheshimiwa Adam Malima ambaye alihoji Bungeni jinsi Mengi anavyotumia vibaya vyombo vyake vya habari kwa kutangaza habari za kujitukuza binafsi zaidi ya hata vinavyotangaza habari zinazowahusu viongozi wa kitaifa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

i) Akaanzisha ugomvi na mfanyabiashara Tanil Somaiya baada ya kumuona kijana huyo aliyekuwa wakala wa kuuza bidhaa za viwanda vyake Mengi (kabla ya kuviua mwenyewe), ameweza kujiimarisha na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara hata kumshinda yeye Mengi, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

j) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Lawrence Masha, kwa kuja na madai ya kutaka kuhujumiwa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

k) Akaanzisha ugomvi na Ndugu Rostam Azizi, baada ya kuona kwamba amekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, na aka ufanya ni ugomvi wa wa nchi nzima.

l) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Mbarawa Makame baada ya serikali kupitisha azimio la kubadili mfumo wa matangazo kutoka analojia kwenda digitali ambapo alikuwa akishinikiza watanzania wakatae kwa lengo la yeye mwenyewe kujinufaisha binafsi.

m) Ni huyu huyu Reginald Mengi amekuwa akipiga vita ya chini kwa chini kuhakikisha Tanzania haipati katiba bora kwa malengo yake binafsi na huu ni mpango mkakati anao uratibu kwa kushirikiana na UKAWA na baadhi ya balozi za kutoka nchi ya wahisani.

n) Na siku za karibuni kaanzisha ugomvi mkali na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo baada ya kuona harakati zake za kutaka kupewa vitalu vya gesi bure kwa kigezo cha uzawa kugonga mwamba.
Watanzania tuna haja na kila sababu ya kujiuliza mara mbili mbili juu ya uhalali wa mtu huyu kuamua kutumia kigezo cha utetezi wa wanyonge (uzawa) kwa minajili ya kujinufaisha yeye binafsi na familia yake. Kamwe hatuwezi kukubali hili na tunatoa wito sasa ni wakati ambao serikali ina bidi ichekue hatua kali dhidi ya mmiliki huyu ambaye amekuwa akichochea vurugu na kuivuruga serikali pasipo sababu.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Mtoa mada yuko sahihi na mkweli.Ukitaka kumjua Mengi vilivyo nenda pale Tanzanite Africa Mirerani uone anacyowanyanyasa wachimbaji wake.Ni halali kumlipa kibarua sh 10800 kwa juma??Je ni halali kibarua kufanya kazi kwako bila ya mkataba?? Mengi kama mwekezaji aufahamishe umma ni msaada upi aloutoa kwa jamii iliko migodi yake zaidi ya kuwalaghai kwa kujiita ole mengi.Ile taasisi ya magonjwa ya moyo aliokuwa anajenga pale mnadani maili sita (HAI) iliishia wapi?? Watanzania kuweni makini na huyu jamaa misaada anayotoa ni ya kujisifu tu .Hatufai.
 
Mengi "U DR" aliupatia wapi au siku hizi ni sangoma?

Je naye Mkuu wa Kaya ni sangoma? Kukurupuka bhana!

Hongera Mengi kwa kufanya restitution. Restitution is allowed ethically. Mmeiba za EPA, tunataka za Escrow. Nasikia kuna zaidi ya trilioni moja umeshirikiana na wenzako kuiba kwenye gesi ya Mtwara.
 
Ndio maana Taifa letu haliendelei, mtu ukikomalia maslahi yako unaambiwa kwamba wewe ni mgomvi, ifike mahala watu tubadilike na kufanya kile unachoamini hata kama ni mmoja katika wengi mpaka pale utakapopata maelezo ya kutosha. Kiukweli imekuwa kitu cha kawaida kwetu kwamba mtu akiwa against na watu either walio wengi au mmoja anapewa majina ya MBISHI KWELI HUYU JAMAA kisa wengi wamekubaliana na hoja
 
Familia ipi ya Mengi unayoiongelea wewe aliyoidhulumu? Hebu nenda kamuangalie au kumuulize mdogo wake Mengi pale moshi Benjamin walivyonufaika na matunda ya utajiri ya kaka yao pamoja na watanzania waliomzunguka.

Ka Mengi,pia kanatajwatajwa kuhusika na uchomwaji moto wa benki kuu miaka ya nyuma kuharibu nyaraka za siri zilizomuhusisha na ufisadi.
 
Mengi kamuumbua nani kwenye ufisadi gani acha kupotosha na akili yako mkuu,

mengi amekuwa mtu wa kutaka kupewa bure hata bila kufuata sheria halafu unasema aumbua mafisadi,

juzi tumeona mengi akitaka kupewa kitaru cha gesi bure ndipo muhongo kamwambia no akaanza kulia kama kafiwa mtoto na kuanza kupanda chuki kwa muhongo kupitia gazeti lake na nipashe.

Hvi unajua ni watanzania wangapi wanafaidika na utajiri wa Mengi theni unijulishe wanaofaidika na ufisadi wa Muhongo kwa hela alizozipata Escrow?
 
SERGIO,

Ukija na hoja kuwa UKAWA inalenga kuhakikisha Tanzania haipati Katiba bora huwezi kueleweka, at least kwenye jukwaa hili la watu werevu. Wengi hapa tunafahamu ni CCM, Chenge and company walio/wanaokwamisha upatikanaji Wa Katiba Bora kama ilivyopendekezwa na Tume ya Warioba. Kipengele (m) & (n) kwenye post yako kinanifanya niamini kuwa wewe ni mtu Wa kutunga mambo na ninawajibika kukudharau.
 
Tibaijuka aliojiwa Star tv pamoja na kafulila,kingine kama mengi anaudhaifu mfano halipi kodi kwanini selikari isichukue hatua au inamuogopa na kama ndiyo basi hii si selikari.Kama wana ushahidi juu ya Uchafu wa Mengi kwa nini wasimshitaki mahakamani na kesi ikaonyeshwa live TBC ili kila mtu aone,ki ualisia Mengi anatake advantage ya Udhaifu wao na makosa yao.TBC ingefanya vizuri lakini Walimtoa Tido Muhando ambae alifanya watu waanze kuipenda wakateua mtu ovyo asiye na weledi wa kazi sasa watu,hawaipendi kuntu.
Ni vema ukajikagua kabla ujakaguliwa any way tuambieni je na Mwingulu alihongwa na Mengi pale bungeni?

Kama ni kwenda Mahakamani angeanza huyo Mengi kwani ndiye anahaha kumung'oa Muhongo na ndiye anajidai kuwanyoishea wengine vidole kuliko kutumia TV zake kusaka huruma za Wananchi na Kuufanya Ugonvi wake Binafsi na Muhongo kuwa Ugonvi wa kitaifa.

Mengi yy ana Mapungufu kibao anapaswa kujitizama kabla ya kuwakomalia wengine.
 
Hakuna sehemu yoyote wezi wamewahi kushinda watu wema tupo na mzee mengi bega kwa bega adi siku tutakayo tokomeza wezi!
Na kifo chochote cha utata dhidi ya mzee mengi.............!
 
Muhongo ang'oke tu ndo habari ya escrow mengine kuhusu fedha zake nyie kuleni tu
 
Rostam sasa ni marafiki sana na Mengi baada ya kuuza hisa za voda kwa Dola milion 300 kisha akatimuka pasipo kulipa Kodi kwa msaada wa Regnal mengi ambaye alipewa Mabilioni kama njia ya kumaliza Ugonvi wao na kumsaidia Rostam kukwepa kodi.

Mengi amsaidie kada wa CCM kukwepa kodi?haya mamlaka husika ziko wapi au TRA ni ya Mengi,Takukuru ilikuwa wapi au kwa kuwa ni Rostam mfadhili wa CCM ndo maana ilishindwa kufanya kazi yake.
 
Sawa, lakini hilo halina uhusiano na hoja za SERGIO. Labda tu niweke nyama kwenye hoja yake kwamba alitaka kuanzisha bifu na watu wa TCRA/Wizara ya Mawasiliano pale ilipotangazwa kuzimwa mitambo ya analogy!!

Ni Mheshimiwa Mengi huyu huyu ambae alipinga wazi wazi suala la kuzima mitambo kwa kisingizio kwamba, mitambo ya analogy ikizimwa, basi wananchi wanyonge wasio na uwezo wa kununua ving'amuzi watanyimwa haki yao ya kupata habari! Kama kawaida yetu, wakajitokeza wa kumshangilia na kumuita ni mtetezi wa kweli wa wanyonge! Maskini ya Mungu, Watanzania hawakufahamu kwamba Mengi alipinga uzimwaji wa analogy kwa kuwa alikuwa na mpango wa kuleta ving'amuzi vyake vya Digitek kwahiyo aliogopa endapo mitambo ingezimwa mapema kabla Digitek haijaingia sokoni, basi Watanzania wasingekuwa na option zaidi ya kununua ving'amuzi vya Startimes na hivyo kufanya ving'amuzi vyake vikose soko pindi vitakavyoingia sokoni!!

Kusoma hatujui, hata picha ukutani hatuzioni?! Tangu Digitek viingie sokoni, hatujamsikia tena Mzee Mengi akiwatetea wanyonge katika suala zima la kunyimwa uhuru wa habari!

Lakini hili bila shaka ndilo linaweza kukufungua macho zaidi na kuona unafiki wa huyu Mzee wa kututumia walalahoi kama ngao yake! Wakati wa kuanzishwa suala la kuingia digitali, ikatungwa sheria kwamba all stations with national coverage ambazo hazikuwa za kulipia; zitaendelea kuwa free tutakapoingia digitali! Baada ya ving'amuzi vya Digitek kuingia sokoni, IPP Media (Mengi) wakaiondoa ITV kutoka Startimes ambako WALALAHOI anaotutetea tulikua tunaangalia bure hata tusipokuwa na malipo ya mwezi... walalahoi wale wale ambao alidai tunakoseshwa uhuru wa kupata habari!!

Thanks to Professor Mkoma... the guy stood firm na IPP wakalazimishwa kuirejesha ITV hewani....

Inakwaje Mengi ambaye ni mfanyabiashara tu aitingishe wizara au serikali?hiyo wizara ya nishati Mhungo anatikisikaje kama yupo salama?hana mistake halafu asumbuliwe na mengi kiasi hicho?bila shaka Mengi amembinya sehemu
 
Mzee wa miaka 80 eti kaoa BINTI sawa na Mjukuu wake huku akiwa na rekodi na Utitiri wa michepuko na Utata juu ya nani alisaidia kumzalia hao mapacha, Mengi anapaswa atambue kuwa watanzania wa sasa wapo macho hawadanganyiki kirahisi kama zamani alivyokuwa amezoea.

Hivi kiafya hua anajali kweli huyu Mengi!? i mean anatumia zana?
 
Wewe SERGIO, yote uliyoeleza hata kama yalikuwa na mantiki kwa namna moja au nyingine, sura yako kamili imeonekana kwenye kifungu(m). Mtahangaika sana ila wananchi wameshaamka.
 
Kwa watanzania wapenda maendeleo na wenye akili timamu wenye kujua madhara ya ufisadi lazima waungane na Mengi kwenye haya mapambano dhidi ya haya majambazi ya nchi.
Ufisadi anaoupigia kelele Mengi ni dhidi ya wafanyabiashara wenzake... hali inayowafanya wengine waamini kwamba anatumia gia hiyo dhidi ya mahasimu wake kibiashara! Mtu haihitaji kuwa na shahada kufahamu kwamba, kila alipo fisadi mfanyabishara, mkono wake wa kuume kuna fisadi mwanasiasa, ama kiongozi wa serikali au kiongozi wa umma! Mengi aliwachana wazi wazi Rostam Aziz na Yusuf Manji kwamba ni mafisadi... nisaidia wewe sasa! Je, Mengi hadi leo ametutajia ufisadi wa Manji na Rostam Aziz ulihusisha wanasiasa gani?

Haya huyu Muhongo, ugomvi dhidi yake wala sio ufisadi per se bali hatua ya Muhongo kuwaambia akina Mengi kwamba hakuna preferential treatment kwenye suala la vitalu vya gesi! Sasa ni ufisadi gani huu wa kila siku kuusema pindi tu anapogambana na watu?
 
Mengi huwa ni mkwepaji mzuri wa kodi huko TRA huwa ana Mtandao wake na kama Rostam asingempooza leo Hii hilo sakata lingekuwa kubwa sana.

Nashukuru kwa kututhibishia kuwa system ime corrupt kama Mengi ana mtandao selikarini maana yake selikari ni wala rushwa haifai ndio maana tunai delete CCM kwani ndio source ya selikari mbovu.
 
Back
Top Bottom