Huyu Issa Bin Mariamu ni nani? Uhusika wake ukoje?

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
3,261
2,000
Tahadhari: huu si mjadala wa mashambulizi ya Kidini. Ni mjadala wa kisomi wa kujenga Hoja. Kelele za Dini zenu pelekeni kwingine. Hapa tunataka hoja na uelewa. Sisi wengine hatuna Dini.

1. Nimekuwa nikijiuliza kwa nini huyu Nabii kwenye Quran anatambulika kama Issa Bin Mariam. Kwa jina la Mama yake ni si ukoo wa Baba yake kama wengine wote waliosalia.

2. Je wenye Quran wanamwamini katika namna gani? Kuwa ni mtume. Je ni mtume kama Mtume mwingine?

3. Je wasiotumia Quran wanamfaham na wanamkubali kuwa ni mmoja ya manabii?

Naomba tujadiliane kwa utulivu kwa nia ya kujifunza. Mimi naifaham Quran na ninaifahamu Biblia. Kwa kuwa nmekulia katika mazingira yote mawili.
 
Chemical Engineer

JF-Expert Member
Dec 29, 2017
239
500
1. Nimekuwa nikijiuliza kwa nini huyu Nabii kwenye Quran anatambulika kama Issa Bin Mariam. Kwa jina la Mama yake ni si ukoo wa Baba yake kama wengine wote waliosalia.
Hana Baba.
2. Je wenye Quran wanamwamini ktk namna gani? Kuwa ni mtume. Je ni mtume kama Mtume mwingine?
Ni mtume kama mitume wengine.... Ni mtume wa mwisho wapili kabla ya mtume Muhammad SAW
3. Je wasiotumia Quran wanamfaham na wanamkubali kuwa ni mmoja ya manabii?
Watakuja kujibu wenyewe..
Naomba tujadiliane kwa utulivu kwa nia ya kujifunza. Mimi naifaham Quran na ninaifahamu Biblia. Kwa kuwa nmekulia katika mazingira yote mawili.
Naaam....
 
olando da costa

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
262
500
Tahadhali : huu si mjadala wa mashambulizi ya Kidini. Ni mjadala qwa kisomi wa kujenga Hoja. Kelele za Dini zenu pelekeni kwingine. Hapa tunataka hoja na uelewa. Sisi wengine hatuna Dini.

1. Nimekuwa nikijiuliza kwa nini huyu Nabii kwenye Quran anatambulika kama Issa Bin Mariam. Kwa jina la Mama yake ni si ukoo wa Baba yake kama wengine wote waliosalia.

2. Je wenye Quran wanamwamini ktk namna gani? Kuwa ni mtume. Je ni mtume kama Mtume mwingine?

3. Je wasiotumia Quran wanamfaham na wanamkubali kuwa ni mmoja ya manabii?

Naomba tujadiliane kwa utulivu kwa nia ya kujifunza. Mimi naifaham Quran na ninaifahamu Biblia. Kwa kuwa nmekulia katika mazingira yote mawili.
Unaifahamu Quran na biblia alafu bado unakuja kuuliza?
 
grand millenial

JF-Expert Member
Jul 29, 2018
1,955
2,000
Hakuna mtu asiye na baba. Anakosaje baba?
Kuna watu wasio na baba labda kwa kuwa hauna ufahamu wa hayo mambo ipo hivi kuna genetic dissoder moja inajulikana kama turners syndrome ni pale mtoto anapozaliwa bila mbegu Ya mwanaume kuungana na ya mwanamke.

Hii inamaanisha atakuwa na chromosomes 45 kati ya zile 46 anazotakiwa kuwa nazo , na mtoto huyo atakuwa wa kike. ila kuna vitu baadhi atakuwa kapungukiwa mfano atakuwa na webbed neck , pia hatoweza kupata mazazi na pia baadhi yao huwa na upungufu wa akili.

Kwa case ya issa bin maryam ni tofauti sana maana Mungu ndo aliamua azaliwe bila baba kivipi? Mimi sijui anajua Mungu pekee maana kidogo mfano wake unafanana na wa adamu.

Hope umepata kitu.
 
safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
8,491
2,000
Nimekuwa nikijiuliza kwa nini huyu Nabii kwenye Quran anatambulika kama Issa Bin Mariam.
Hii ni sawa na kuuliza kwa nini yesu atambulika kama yesu ndani ya bibilia.

Yani anatambulika hivyo kwa sababu ndo aliitwa hivyo,hilo sio jina la utani alilopewa na Qurani ni jina halisi ambalo Qurani imenukuu na kutusimulia visa vyake.
Kwa jina la Mama yake ni si ukoo wa Baba yake kama wengine wote waliosalia.
Yeye hakua na baba kwa maana Allah alijaalia mariam apate mimba bila ya mume.

Na hiki kitendo cha kuwa hana baba ndio maana akaitwa issa bin maryan.

Bin ni mtoto wa kiume.
Binti ni mtoto wa kike

Kwa hivyo ukiambiwa john bin magufuli hii bin inamhusu aliyetangulia kutajwa na sie anaefuata kutajwa.

Mfano.

Samia bint hassa. Manake unajua binti inamhusu samia kwa maana hapa samia ndio binti mwenyewe.

Hii bin na binti sana ipo katika lugha ya kiarabu ambayo ina utajiri wake wa maneno kama lugha zingine.
2. Je wenye Quran wanamwamini ktk namna gani? Kuwa ni mtume. Je ni mtume kama Mtume mwingine
Yule ni mtume mkuu kwa mujibu wa Qurani.lakini Qurani haikuishia hapo tu kutambua kwamba ni mtume bali iendelea kuonesha kwamba inatambua kuna watu wanamtukuza kinyume na alivyo.

Mfano ukiangia aya hii..

ูˆุฅุฐ ู‚ุงู„ ุงู„ู„ู‡ ูŠุง ุนูŠุณู‰ ุงุจู† ู…ุฑูŠู… ุฃุฃู†ุช ู‚ู„ุช ู„ู„ู†ุงุณ ุงุชุฎุฐูˆู†ูŠ ูˆุฃู…ูŠ ุฅู„ู‡ูŠู† ู…ู† ุฏูˆู† ุงู„ู„ู‡ ู‚ุงู„ ุณุจุญุงู†ูƒ ู…ุง ูŠูƒูˆู† ู„ูŠ ุฃู† ุฃู‚ูˆู„ ู…ุง ู„ูŠุณ ู„ูŠ ุจุญู‚ ุฅู† ูƒู†ุช ู‚ู„ุชู‡ ูู‚ุฏ ุนู„ู…ุชู‡ ุชุนู„ู… ู…ุง ููŠ ู†ูุณูŠ ูˆู„ุง ุฃุนู„ู… ู…ุง ููŠ ู†ูุณูƒ ุฅู†ูƒ ุฃู†ุช ุนู„ุงู… ุงู„ุบูŠูˆุจ [ AL - MAIDA - 116 ] Na pale Mwenyezi Mungu atakapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwisha yajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyo fichikana.

Hii aya inaelezea future time yaani kana kwamba imefanya time travelling na kujua kitakachotokea siku ya kiama.3. Je wasiotumia Quran wanamfaham na wanamkubali kuwa ni mmoja ya manabii?
Hili ni swala ambalo wanatakiwa wajibu hao watu ambao hawatumii Qurani

Kuwajibia suala kama hili hatutafanya haki.
 
Johnny Impact

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
2,678
2,000
Issa siyo Yesu
1. Yesu alizaliwa kwenye holi la ng'ombe wakati Issa alizaliwa chini mtende
2. Yesu alisurubiwa, akafa na siku ya 3 akafufuka wakati Issa hakusurubiwa, hakufa wala kufufuka.
3. Yesu alitumia Biblia. Alipewa kusoma kitabu cha Isaya na alibatizwa wakati Issa alitumia Quran na hakubatizwa.
Kwanini huwa mnang'ang'ania Yesu ni Issa? Siyo kosa lako sbb huwa mnakaririshwa.
Baba yake ni nani ?

Moja ya maajabu ya Mola Muumba ndo hayo... Mariam alipandikiziwa mimba bila kuingiliwa na mwanaume yoyote... Hivyo, logically, Issa ( Yesu) hana baba....
 
Salumu45

Member
Mar 10, 2020
43
125
Issa siyo Yesu
1. Yesu alizaliwa kwenye holi la ng'ombe wakati Issa alizaliwa chini mtende
2. Yesu alisurubiwa, akafa na siku ya 3 akafufuka wakati Issa hakusurubiwa, hakufa wala kufufuka.
3. Yesu alitumia Biblia. Alipewa kusoma kitabu cha Isaya na alibatizwa wakati Issa alitumia Quran na hakubatizwa.
Kwanini huwa mnang'ang'ania Yesu ni Issa? Siyo kosa lako sbb huwa mnakaririshwa.
We mwamba acha uongo,wakati wa nabii issa quraan haikuwepo
 
Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,732
2,000
Mohamad siyo mtume wa Mungu. ni mjanjamjanja fulani hivi
Na wayahudi wanasema hivyo hivyo Yesu alikuwa muhubiri mzuri tu mjanja lakini hakuwa Mesiah kwao Mesiah bado hajaja hao Jews na wanasema wazi kabisa yesu alikuwa jew na mama yake myahudi alitembea nje ya ndoa akazaliwa ila hawamtambui kabisa tena wameenda mbali kusema dini ya kikristo muanzilishi ni Paul sio yesu.
 
Jackwillpower

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
693
1,000
Na wayahudi wanasema hivyo hivyo Yesu alikuwa muhubiri mzuri tu mjanja lakini hakuwa Mesiah kwao Mesiah bado hajaja hao Jews na wanasema wazi kabisa yesu alikuwa jew na mama yake myahudi alitembea nje ya ndoa akazaliwa ila hawamtambui kabisa tena wameenda mbali kusema dini ya kikristo muanzilishi ni Paul sio yesu.

WARUMI 3​

1Basi Myahudi ana nini zaidi? Na kutahiriwa kwafaa nini? 2 Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu. 3 Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutoamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu? 4 La hasha! Mungu aonekane kuwa kweli japo kila mtu ni mwongo; kama ilivyoandikwa,
Ili ujulikane kuwa una haki katika maneno yako,
Ukashinde uingiapo katika hukumu.
 
Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,732
2,000
We mwamba acha uongo,wakati wa nabii issa quraan haikuwepo
Huyu jamaa kapotosha hapo sasa sijui kusudi au kutokujuwa. Yesu( Issa) alifwata injili ya hebrew mengi mafundisho ya torat inaitwa agano la kale hii injili agano jipya lilikuwa baada ya zaidi miaka 400 Paul alichiandika kuchanganya ya zamani na mpya ndio maana wayahudi wanasema dini ya Paul ila yesu alikuwa muhubiri mzuri mjanja akajitenga kidogo katika jews na kuanza harakazi zake wanamchukulia kama mwana mpotevu tu ila ukisikiliza sana wayahudi wanawadharau sana wakristo sababu yesu kwao hana nafasi yoyote ukija kwa Mohammed wanasema mwarabu na dini yake islam ila wote wamechukuwa kwetu Torah, kuna ukweli fulani quraan imethibitisha yote mitume wote na vitabu vyote tofauti kuu hapa. Jews wanamuamini Mussa tu na kitabu chao Torah, Yesu hawamtambui kabisa sio Mesiah. Wakristo hawamtambui Mohammed ila waislamu wanawatambua wote ziko tofauti baina yao. Ila katika dini hizi 3 zipi wanakaribiana kidogo kwa mujibu wa Jews. Ni Jews na Islam ila wa kristo wanasema no hakuna Messiah bado hajaja.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom