KERO Huu utaratibu wa Shule za Sekondari za kutwa kugeuzwa kuwa za Bweni (Kambi) ni kero kubwa. Serikali iko kimya hadi pale madhara makubwa yatakopotokea

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

digba sowey

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
10,141
Reaction score
22,022
Serikali Ipige Marufuku Shule za Serikali za Kutwa Kugeuzwa Mabweni ya Kambi za Mitihani,

Katika miaka ya karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la shule za serikali za kutwa kugeuzwa kuwa kama shule za bweni kwa wanafunzi wa madarasa ya mitihani yaani kidato cha pili na cha nne. Mabadiliko haya hufanyika kwa kisingizio cha kuongeza ufaulu na kupunguza daraja sifuri. Hata hivyo, hatua hii imegeuka kuwa mzigo mkubwa kwa wazazi na hatari kwa wanafunzi, na pia inakiuka utaratibu wa serikali kuhusu uendeshaji wa shule kwa Tanzania.

Serikali imeweka wazi kuwa kuna aina mbili za shule: shule za kutwa na shule za bweni.
  • Kugeuza shule ya kutwa kuwa ya bweni bila taratibu, vibali, wala maandalizi ya miundombinu ni uvunjaji wa sheria na kanuni za elimu.
  • Walimu na baadhi ya maafisa elimu wamekuwa wakitumia hoja ya “kutokomeza daraja sifuri” kama kisingizio cha kulazimisha kambi, bila kuzingatia madhara makubwa yanayowapata wanafunzi na wazazi.
Baadhi ya madhara au Changamoto za shule za kutwa kugeuzwa kuwa Kambi ni Miundombinu na Usalama,
Shule nyingi za kutwa hazina miundombinu ya mabweni,
hivyo wanafunzi hulazimika kulala kwenye madarasa. Hili linaibua matatizo makubwa:
  • Madarasa hayana faragha, hasa kwa wasichana.
  • Madarasa yako wazi na watu hupita karibu muda wote, hivyo usalama wa wanafunzi unakuwa mdogo.
  • Endapo msichana anaumwa usiku, hakuna mazingira salama ya kumhudumia au kumstiri.
  • Hakuna uzio, walinzi wa kutosha, wala vifaa vya dharura vinavyotakiwa kwa mazingira ya bweni.
Lakini pia inapelekea Mzigo Mkubwa wa Kifedha kwa Wazazi
  • Wazazi vijijini tayari wanahangaika na hali ngumu ya maisha.
  • Kambi hizi zinawalazimisha kulipa michango mikubwa kwa chakula, ulinzi, usafi, na vifaa vingine—michango ambayo haipo kwenye mwongozo wa serikali.
Hatari ya Usalama kwa Wanafunzi Usiku
  • Shule za kutwa hazina walinzi wa kutosha wala uzio madhubuti.
  • Wanafunzi wako hatarini kuvamiwa, kujeruhiwa, au kukumbana na matukio ya ukatili wa kijinsia.
Athari za Kisaikolojia kwa Wanafunzi
  • Kulazimishwa kuishi mazingira yasiyo rafiki huongeza msongo wa mawazo.
  • Wanafunzi hukosa usingizi wa kutosha kutokana na kelele, baridi, au hofu ya usalama.
Hatari ya Magonjwa na Uchafuzi
  • Madarasa hayajatengenezwa kwa ajili ya kulala: hakuna vitanda, hewa ya kutosha, wala sehemu za kuoga.
  • Hali hii huongeza uwezekano wa magonjwa ya ngozi, mafua, na maambukizi mengine kama kipindupindu nk
.Kukosekana kwa Faragha na Heshima kwa Wasichana
  • Wasichana hulala kwenye madarasa yasiyo na milango imara wala pazia.
  • Wanapopata hedhi au kuumwa, wanakosa mazingira ya kujisitiri na kupata huduma kwa usalama.
Ushauri kwa Serikali
Serikali inapaswa kupiga marufuku mara moja tabia ya kugeuza shule za kutwa kuwa mabweni ya muda kwa sababu zifuatazo:

  • Inakiuka taratibu rasmi za uendeshaji wa shule.
  • Inaweka maisha ya wanafunzi hatarini, hasa usiku.
  • Inawaongezea wazazi mzigo wa kifedha usio wa lazima.
  • Inadhalilisha na kuhatarisha usalama wa wasichana.
  • Inaharibu malengo ya elimu kwa kugeuza shule kuwa maeneo yasiyo na hadhi ya kibinadamu.

Badala yake, serikali inaweza:
Kuimarisha ufundishaji wakati wa mchana.
  • Kuongeza walimu wa ziada kwa masomo ya mitihani.
  • Kutoa mwongozo wa kitaifa wa namna ya kufanya maandalizi ya mitihani bila kambi za kulazimisha.
  • Kufanya ukaguzi mkali kwa shule zinazokiuka taratibu.

Hitimisho
Kambi za kulazimisha katika shule za kutwa si suluhisho la ufaulu. Zinavunja sheria, zinawaumiza wanafunzi, na zinawaumiza wazazi. Serikali ikichukua hatua sasa, italinda usalama, utu, na haki za watoto wetu—na kurejesha nidhamu katika mfumo wa elimu.
 
Hiki kitu nilikiwaza jana usiku wakati nafikiria watoto wangu hawatosoma bweni.
Nitaonekana tu mkorofi ila mtoto wangu sitoruhusu akakae shule kwa kisingizio cha darasa la mtihani.
 
Nikajua madogo wanafanyana michezo michafu ambayo sio na haina afya kwa jamii kumbe ni hayo matatizo madogo tu yanayotatulika kwa muda na maamuzi, oya kuna kitu nilitaka niseme hapa ila ngoja nipite kimya
 
Ndalichako aliwahi kupiga marufuku hizo kambi akamuibua RC Anthony Mtaka na povu la kutakatisha kaniki.

NB:Serikali imeshindwa kuchukua hatua kwa shule zinazobakiza watoto nyakati za likizo na hili pia haitoboi.
 
Huu ni ulimbukeni wa wakuu shule kutaka sifa kuwa wanafundisha sana. Mi kama mwalimu ujinga huo huwa siutekelezi kwa kuwa haupo kwenye azimio la kazi na wakaguzi hawana muongozo wa kukagua ujinga huo. Muda wa kozi nzima kwa mihula yote umepangwa tangu mwanzo hadi mwisho wa kozi, kwenda kupiga kambi eti kusoma kwa bidii huko ni kuchosha wanafunzi na walimu kufanya kazi nje ya utaratibu maalumu wa kitaalamu kwa mujibu wa kanuni za ufundishaji
 
Naunga mkono hoja hii kwa nguvu! Hii yote inasababishwa na siasa mbovu za hii nchi.

Too risk, na inatweza utu wa watoto na walimu pia.
 
Hata hawa watoto wadogo wa msingi siku hizi hawapumziki ku fresh mind. Watoto wanasoma mwaka mzima bila mapumziko ya mihula mpaka jumamosi watoto wapo shule. Mpaka la saba nao wanakuwa kambini muda mrefu mpaka mtihani. Ukiona wanachofundishwa si kivile sana useme kwa kuwa wako kambini basi wanasoma sana kumbe hakuna kitu! Watoto wanabanwa sana kiasi kwamba wanakosa kufanya mambo ya elimu huria wakati wa likizo za wanafunzi
 
Kama mfumo wa Elimu ya Tza usipofanyiwa total overhaul basi wan dei uta collapse na red flag zishajionesha.....
NB: THREAD HII AIONE WANU HAFIDH AMEIR PALE MASJALA MAKAO MAKUU
 
Duuh, umeeleza kwa undani sana na kihisia zaidi
 
Nimeangalia uandishi wako nikagundua wewe ni msomi haswa kwa sababu umepangilia vyema andiko lako na point nyingi pia inaonesha umefanya uchunguzi mzuri hongera saana

Lakini nikagundua kitu wewe ni mwalimu MWENYE WIVU WA MAENDELEO YA WENZAKO
kilikubwa kilichokuleta hapa ni matokeo ya wivu baada ya kuona walimu wenzako wamefanikiwa maisha kupitia hizo program

HIZI KAMBI ZINAPANDISHA UFAULU SAANA NGOJA nikupe mifano hai

KIGOMA Kuna shule mbili zipo jirani
Mlole secondari
Masanga secondary
Nenda kuangalia matokeo yao utaona utafauti mkubwa Wa kimatokeo kati ya mlole secondari ambayo Ina hizo Kambi na masanga secondary ambayo haina hizo Kambi

MOROGORO
Toka hapo nenda mkoani morogoro wilaya ya Milmba katika Kijiji Cha Mbingu utakuwa Kuna shule mbili pale
Londo secondary
Mbingu (ngajengwa) secondary
Utaona utafauti mkubwa Wa kimatokeo kati ya Londo secondary shule ambayo haina Kambi dhidi ya Ngajengwa secondary shule yenye Kambi

Nimewai kuishi mbingu kwa miaka 7
Kuna mwalimu alijenga bweni kubwa ngajengwa kantini kwa pesa zake mwenyewe ndani ya eneo la shule
Huwa anawapa walimu chakula Cha mchana na asubuhi plus usiku Bure lkn walimu hao hao ndio wanaongoza kumpiga majungu aliyakuwa kiuhalisia wanaona kabisa matokeo yanapanda na ufaulu unaongezeka

Ukiuliza watoto wanakwambia mmiliki Wa bweni ukiwa hauna hela ya chakula unamwambia tu anakusaidia free
50% ya wanafunzi wanakula Bure

HIVYO BASI NDUGU MWALIMU ACHA ROHO MBAYA NA WIVU KWA WENZIO BHANA UNATIA AIBU

FANYA KAZI WIVU SIO MZURI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…