Sina uhakika na kitu kilocho anza kujadiliwa hapa, ila maoni yangu ni kuwa; (tukichukulia kama yaliyosemwa yote ni ya kweli), cha kujiuliza hapa ni kuwa: Je, alitubu? Je, alizilipa hizo pesa? Je,hajarudia kosa kama hilo tena? Je, sasa hivi anasaidia vipi jamii? n.k.
Nimeuliza maswali hayo kwani mimi naona ndiyo msingi mzuri wa maendeleo, kama mtu kafanya kosa ambalo tunaweza kusema ni la kiwango cha kawaida katika jamii (kwani makosa yapo tu nyakati zote), yanini kuendelea kumshutumu mtu huyo kama atakuwa amejirekebisha na ametubu makosa yake..
Kuna mifano mingi inaweza kutolewa hapa, lakini nitakao toa ni ule wa David Cameron, Kiongozi wa upinzani Uingereza. Huyu alishutumiwa kuwa alivuta bangi akiwa chuoni, walipo muhoji wakati wa kuchaguliwa kwake hakujibu swali hata kidogo kama kweli alifanya hivyo.
Muhimu sasa, huyo Cameron alichaguliwa kuwa kiongozi bila kujali yaliyo pita au yanayosadikiwa kuwa ni makosa ya kawaida katika jamii hata kama mtu huyo hakukiri au kutubu makosa yake ya awali, kwani uwezo wake wa kuwa kiongozi kwa wakati huu ndiyo uliotiliwa maanani zaidi.
Nakubali kuwa kuna makosa fulani fulani ambayo mtu ukitenda katika jamii haya sahuliki na pengine hayasameheki kabisa. Ndiyo maana nimesema kuwa msingi wa maendeleo kama wananchi watautambua ni hayo maswali, kwani yakijibiwa, swali la mwisho likawa kuwa huyo Dr. Slaa anaendeleza demokrasia na kusukuma gurudumu la maendeleo kwa kuhoji wabadilifu katika jamii, basi makosa yake yanaweza kusahaulika na kusameheka kama hayo maswali mengine hapo juu atakuwa ameyatekeleza ipasavyo.
SteveD.