SoC03 Huu ndio mwarobaini (Suluhu) dhidi ya mimba kwa watoto wa kike mashuleni na majumbani

Stories of Change - 2023 Competition

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
7,905
14,376
Karibuni katika kuchangia mawazo ili kuweza kupata mbinu zitakazo wezesha kumnusuru mtoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni na ukatili wa kingono,mara nyingi naweza sema kuwa serikali imekuwa nyuma sana katika kuhakikisha kuwa inazuia na inaweka mazingira ambayo mtoto wa kike anakuwa katika hali salama katika swala la mahusiano ya kimapenzi na ukatili wa kingono, kwani mara nyingi mbinu za serikali kwa jinsi nionavyo mimi hazilengi katika kuzuia mambo haya yasiwepo tena na kubaki historia,kwani serikali hutokea pale tu jambo linapotokea Kama kutoa hukumu na wala haitoi suruhu kwa mwathirika baada ya kuwa amebebeshwa mimba au kufanyiwa ukatili wa kingono,kwani huishia kutoa kifungo kwa mkosaji huku ikishindwa kutoa suruhu kwa mwathirika.

Mara nyingi watoto wa kike katika nchi yetu wamekuwa wakikatishwa ndoto zao za kufikia pale wanapohitaji kielimu, changamoto kubwa ikiwa ni mimba za utotoni ambazo mara nyingi katika utafiti wangu usio rasmi wahanga wa tatizo hili wengi wao huwa ni watoto kutoka familia zenye kipato duni,Ni nadra sana kukuta mtoto anayetoka katika familia inayojimudu kiuchumi binti kapewa ujauzito katika umri mdogo na ikitokea kuna uwezekano mkubwa sana wa mhusika wa tukio hilo kuwajibishwa kisheria kwa sababu katika familia hizi zinazo jimudu kiuchumi ni nadra kufanikisha makubaliano ya kifedha nje ya vyombo vya sheria . Mara nyingi watoto kutoka familia zenye kipato duni hujihusisha na mapenzi kama njia moja wapo ya kujipatia mahitaji madogo madogo na mwisho wa siku huishia kupata mimba na kupelekea kushindwa kufikia ndoto zao kielimu .

Cha kustaajabisha hadi karne hii mambo ya mtoto wa kike kupata mimba katika umri mdogo yameshindwa kupewa suruhu kwa miaka na miaka kutoka na hali mbili ambazo ni,Moja umasikini wa familia husika ambayo binti anatoka na pili kutokuwajibika kwa serikali katika kuweka mazingira rafiki ambayo yatatoa suruhu kwa mwathirika pindi mkosaji anapo tiwa hatiani, je kwanini nimechaguwa sehemu mbili ambazo ni umasikini wa familia husika pamoja na kutokuwajibika kwa serikali katika kuweka mazingira ambayo yatatoa suruhu kwa mwathirika pindi mkosaji anapotiwa hatiani !? Fuatana nami hapa chini.

Nikianza na Umasikini wa familia ni kwamba mtoto huyu baada ya kupewa mimba,familia ya mhusika wa kosa au hata familia ya binti (mwathirika) hukimbilia kufanya makubaliano ya kulipana fedha kidogo ili jambo hili lisifike kwenye vyombo vya kisheri, hivyo kutokana hali duni ya familia atokayo binti(mwathirika) kuwa na hali duni hukubali malipo ili kutoruhusu mambo haya yasifike mbele ya vyombo vya sheria, hali hii imepelekea swala la watoto wadogo kubebeshwa mimba kuonekanakama kama jambo la kawaida katika jamii zetu kwani ni mara chache sana kuona wahusika wa matukio haya wakifikishwa mbele ya sheria,na pengine wale wachache wanao fikishwa mbele ya sheria hutokana na kushindwa kuafikiana katika malipo ya nayofanyika nje ya vyombo vya sheria. Mfano ;Ukitembelea mashuleni kwa shule moja kwa mwaka waweza kuta watoto zaidi ya kumi waliacha(walikatiswa) masono yao kwa kubebeshwa mimba lakini huwezi kukuta hata kesi moja iliyofikishwa mahakamani na wahusika wakatiwa hatiani,sasa unabaki kujiuliza je hawa watia mimba wa hawa watoto wanatoka sayari gani ambako hakuna sheria au wasimamizi wa sheria zetu wamehindwa kuwafiia,!!?, Lakini yote kwa yote hii inathibisha kuwa kuna maelewano yanayofanyika nyuma ya pazia ili kuzia kesi hizi zisifike mbele ya vyombo vya sheria na matokeo yake hali hii imepelekea kuwepo ugumu katika kutokomeza na kumkomboa mtoto wa kike ili aweze. kufikia ndoto zake katika nyanja ya elimu na pia jambo hili linakwamisha juhudi za kukomesha mimba kwa watoto wa kike kwani hakuna matokeo ya moja kwa moja ambayo kwayo watu watajifunza na kujua kuwa kujihusisha kimapenzi na mtoto wa shule au mtoto chini ya umri wa miaka 18 ni hatari,pengine jamii ingeweza kuona moja kwa moja hatua kali wanazopata wahusika wa mambo haya kwani wahenga walisema kusikia kwa kenge hadi damu zimtoke masikioni ,huenda ingesaidia kutokomeza jambo hili lenye athari kubwa kwa mtoto wetu wa kike .

Pili, Kutokuwajibika kwa serikali katika kuweka mazingira rafiki ambayo yatatoa suruhu kwa mwathirika pindi mkosaji anapo tiwa hatia na pia kuhakikisha kuwa mtoto(mwathirika)huyu anakuwa katika mazingira salama pamoja na kiumbe kilichoko tumboni ,hii inamaanisha kuwa licha ya uwepo wa sheria kali ndani ya nchi yetu dhidi ya ukatili wa kingono kwa watoto hasa wa kike ambao ndio wahanga,bado sheria zetu zinatoa mwanya wa watu kufanya mambo haya bila hofu, kwani kwa wale wachache wanaofikishwa mahakamani baada yakubainika kuwa wamehusika katika matukio hayo huishia kufungwa kifungo bila kutoa suruhisho kwa mwathirika(mtoto wa kike),yaani unakuta mzazi kapoteza muda ba pesa kwenda mahakamani kutoa ushahidi mwisho wa siku kweli mhusika ana hukumiwa kifungo cha miaka 30,je baada ya hukumu hiyo,mwathirika (mtoto) anabaki vipi na anaishije ukizingatia wengi ya hawa wathirika ni watoto wanaotoka katika familia zenye kipato duni,sasa wengi wao kutokana na kuhofia mtoto kukosa malezi ya pande mbili( Yaani baba na mama) pia hofu ya mtoto kukosa huduma japo kidogo, hupelekea kuyamaliza mambo haya kinyemela,kwani sheria zetu hazitoi suruhu juu ya nini kinafuata kwa Mwathirika(binti) baada ya mkosaji utiwa hatiani.

Nini kifanyike ili kusiwepo na maswala/mazingira yatakayopelekea watu kufanya maelewano kabla ya jambo kufikishwa mahakamani ,kwanza kabisa naomba nikiri kuwa sheria zetu zina nguvu sana na ni kali ila kuna jambo moja linalopelekea Kuwepo kwa mwanya wa wakosaji kupenya na hivyo kupelekea jambo la ukatili na mimba kwa mtoto wa kike liendelee kuwepo jambo hili ni serikali kutowajibika au kutoweka mazingira mazuri kwa mwathirika kupata matunzo mara baada ya mhusika kutiwa hatiani( kuhukumiwa)hivyo serikali pamoja mashirika yanayopinga unyanyasaji pamoja na mimba za utotoni bila kusahau ukatili wa kingono, waje na kifurushi (pesa) ambayo italipwa kwa mwathitika ili isaidie malezi ya mtoto,mfano kila tukio la mtoto wa kike kupigwa mimba angali mwanafunzi au kupigwa mimba chini ya umri wa mika 18,mwathirika(Mtoto) alipwe angalau shilingi milioni 3 kwa ajili ya matunzo yake mara baada ya mhusika kuhukumiwa( kutiwa hatiani),hii itapunguza kwa namna fulani tatizo hili na pia italeta usawa kwa mwathirika pamoja na mtoto atakayezaliwa na hivyo kupunguza au kuondoa kabisa kwa kiasi fulani mazingira ya watu kuelewana nje ya mahakama pindi matukio haya yanapotokea,hii itamaanisha kuwa ili mhusika wa ukatili akubali kuelewana na familia ya mhanga itampasa kuwa na zaidi shilingi milioni tatu ili jambo liishe bila kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria kwani mara nyingi mambo haya yamekuwa yakimalizwa nyuma ya pazia kwa pesa kiasi kidogo sana huku ukiangalia sababu huwa ni uduni wa maisha kwa familia ya binti(mwathirika).

Mwisho serikali pia iwezeshe upatikaji wa elimu Kuhusu madhara ya mapenzi na mimba chini ya umri wa miaka 18 ambayo kwa ufupi ni :- matatizo wakati wa kujifungua kwa mtoto wa kike kutokana na via vya uzazi kutokuwa tayari kubeba mimba, pia vifo vingi vimekuwa vikiripotiwa kwa watoto wadogo waliobeba mimba wakiwa chini ya miaka 18, lakini pia serikali itilie mkazo juu ya upatikanaji wa elimu ya kijinsia na mahusiano kwa watoto wa kike ambapo elimu hii itamsaidia mtoto kutambua madhara ya kujihusisha na mapenzi katika umri mdogo sio hivyo tu bali pia jamii nayo ipate elimu juu ya namna ya kupambana na mambo haya na hata namna ya kushughulika na wahusika wa ukatili kwa watoto,kwani unaweza kuta mtoto kapewa mimba lakini mzazi hajui ni wapi apeleke swala lake ili lishughulikiwe.Hivyo kama jamii tunapaswa kuungana kwa pamoja katika swala hili ili mwisho wa siku swala la mimba za utotoni liwe historia katika nchi yetu kwani limekuwa kikwazo katika kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu ,kwani wahenga walisema "ukimwelimisha mwanamke ,umeielimisha jamii nzima"
 
asante kwa andiko lenye kufirikisha,kwa upande wangu nakubaliana na wewe juu ya swala la watu kumalizana kinyemela pale maswala ya ukatili na unyanyasaji kwa watoto wa kike yanapotokea,kuhusu suruhu panahitaji mjadala mpana sana ili kuweza kukomesha jambo hili
 
asante kwa andiko lenye kufirikisha,kwa upande wangu nakubaliana na wewe juu ya swala la watu kumalizana kinyemela pale maswala ya ukatili na unyanyasaji kwa watoto wa kike yanapotokea,kuhusu suruhu panahitaji mjadala mpana sana ili kuweza kukomesha jambo hili
Ahsante Sana Mkuu, usisahau kunipa kura yako
 
umeeleza nyema,ni muda muafaka sasa kwa serikali kuja na sheria ambayo itazingatia mambo haya lengo likiwa ni kukomesha ukatili wa kingono kwa watoto wetu
 
Mkuu Nini kifanyike ili kumkomboa mtoto wa kike dhidi ya hali hivi!?
Tubadili malezi, tupunguze uzungu uzungu.. tuwape watoto maadili mema.. lia tuwe tuna waeleza hali halisi, dunia ilivyo.
Kuna nyakati mzazi kuwa mkoloni kiasi chake.. waoneshe watoto njia sahihi.

Unakuta tangazo la salama kondom, mzazi anatizama na mwanae.. mtoto apigwe pumbu, ila atumie kinga🤣

Kuna lile tangazo, eti shangazi mtu kawakuta vijana(wanafunzi) wameenda zahanati ya mbaali kabisa, kuepuka kuonekana, wameenda kupata elimu ya uzazi wa mpango, shangazi akuhamaki wala nini, akafurahia, kwa kuwa wanajitambua, wameenda kupata elimu, wagegedane kiusalama kuepuka mimba, ili watimize ndoto zao.. nikatiza.a nikaona ujinga huu.. hapo mnaruhusu mabinti waujue mkuyenge mapema na tunajua unavyowavuruga hata wavulana pia, huwa inavuruga kwa baadhi ya vijana.
 
Uko sawa mkuu mtu akipiga pumbu akabidhiwe mzigo asomeshe mpaka chuo, apo mzazi wala mtoto hawapati hasara
 
Back
Top Bottom