SoC03 Kumaliza tatizo la mimba na ndoa za utotoni tuondoe Umasikini kwanza

Stories of Change - 2023 Competition

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,712
6,508
Tuondoea umasikini wa Vipato ili kumaliza tatizo la Ndoa za utotoni na wanafunzi kupewa Mimba.

Ukijaribu Kusoma Historia ya wazungu hasa maisha yao ya miaka ya 1800 huko hadi 1930 huko utagundua kwamba haya yanayo tokea huku kwetu sasa pia na kwao yalikuwepo, Wazungu walikuwa na Ndoa za utotoni sana, wanafunzi kupata kupigwa mimba yote haya yalilisha watokea na kadri maisha yao yalivyo kuwa yanabadilika haya matatizo yalipungua au kuisha kabisa.

Ukiangalia Marekani maeneo ya watu masikin hasa Wamarekani weusi haya mambo bado yangalipo ila kwa kiwango cha chini sana.

kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya ndoa za utotoni, wasichana kuozwa mapema na swala la umasikini.

Juzi niliona kule Tundulu Mkuu wa wilaya akivamia na kuivunja ndoa ya mwanafunzi wa kidato nazani cha Tano sikumbuki, na pia kule Shinyanga ilitokea hivi karibuni na haya matukio yapo sana maeneo mengi.

Je tusha wahi kufanya utafiti wa maeneo yanako tokea haya matatizo na hali za kimaisha za maeneo husika?

Mimba za utotoni, wanafunzi kupewa ujauzito, wanafunzi kuacha masomo, haya matatizo ni sugu kabisa kwa baadhi ya maeneo hapa Tanzania, na hayo maeneo yote ukiangalia kuna shida sana za umasikini, hali za kimaisha za maeneo husika ni ngumu sana, mikoa yote inayo tajwa kuwa sugu wa haya matatzio ni mikoa ambayo ina shida pia ya umasikini mkuwa sana.

Mwa mujibu wa report ya shirika la Save the Children, wasichana kutoka familia masikini wako katika hatari ya kuolewa mapema mara 4 zaidi ya wasichana kutoka familia zinazo jiweza kipato, hii ni picha tosha ya nini sababu kuu ya hili tatizo.

Kuna uhusiaano mkubwa sana wa umasikini wa vipato na mimba za wanafunzi, ndoa za utotoni, wanafunzi kuozwa, kuacha masomo na kadhalika, haya matukio huwezi yakuta kwenye maeneo au familia zenye vipato vizuri, huwezi sikia kwenye Familia zenye viapato vizuri kwamba Binti mdogo anaozeshwa, haya yako kwenye Familia zenye umasikini na kuozeshwa mabinti wa dogo ni moja ya njia za kujipatia kipato.

Haya matatzio hayawezi isha kwa Sheria kari sana na kuvamia kuvunja hizo ndoa hapana kuna ambao hawafanyi hata hizo ndoa za wazi watoto wanaolewa juu kwa juu tu watu wanakuja kujua baadae sana kwamba Fulani au mtoto Fulani kaolewa.

NJia za kupambana na haya matatizo ni kwa Serikali kuwekeza sana kwenye kumaliza tatizo la umasilini wa vipato, umasikini ndio sabbau ya haya yote yanayo tokea, hakuna familia au mazazi mwenye kipato atamuoza Binti yake mwanafunzi au binti kuacha shule ili aolewa na hata pia wanafunzi kupewa mimba.

Ukiangalia hata swala la wanafunzi kupewa mimba liko sana connected na umasikini, kiwango ni kikubwa sana kwenye maeneo ya masikini na unakuta sana binti alidanganywa kwa hata Chips Mayai au Chips kuku.

Miradi ambayo inaweza wasaidia wananchi kuondokana na umasiini wa vipato itasaidia sana kumaliza kupunguza haya matatzio kama sio kuyamaliza kabisa. Serikali iache kuamini kwamba itamaliza haya matatzio kwa sheria kari sana na kukemea bali iwekeze sana kwenye maisha ya wananchi, wnanachi wanapo kuwa na vipato moja kwa moja haya matatizo yatapungua.

Serikali inapaswa kuwekeza sana kwenye miradi ya kuondoa umasikini moja kwa moja badala ya kuwa na miradi mikubwa mikubwa ambayo sana inawanufaisha watu wachache.Miradi ya kilimo, miradi ya ufugaji ni moja ya miradi ambayo inawa saidia kutomoeza hii tatizo, na katika maeneo haya yote wananchi wanalima ndio lakini kilimo chao na ufugaji ni haujasaidia kuondoa umasikini wa vipato hivyo jitihada zinahitajika sana hapa ili kumaliza tatizo.
 
Back
Top Bottom