Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,568
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema katika Mikoa ya Dar es salaam, Njombe na Ruvuma viwango vya mimba za utotoni vimeongezeka, huku mapambano ya kupunguza idadi ya mimba hizo yakirudi nyuma ambapo amewataka Wazazi waendelee kuwalinda Watoto wetu dhidi ya mimba za utotoni.
Rais Samia amesema hayo wakati akizindua Ripoti hiyo ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania ya Mwaka 2022 na Ugawaji wa Magari ya Kubebea Wagonjwa na Vifaa Tiba Jijini Dar es salaam.
Rais Samia amenukuliwa akisema “Mkoa wa Dar es salaam, Chalamila uko wapi?, upo?, kwa Mkoa wako wa Dar es salaam mmerudi nyuma kutoka 11.9% sasa mko 18.1% mmelegeza wapi sijui kajiangalieni”
“Njombe wametoka 19.7% wamepanda mpaka 25.5% kuna nini kajiangalieni, Ruvuma mmetoka 32% mmekwenda 37.2% kaangalieni sababu za hili mzifanyie kazi, nitoe wito kwa Wazazi tuendelee kuwalinda Watoto wetu dhidi ya mimba za utotoni”